Tuliambiwa Magufuli kajenga vituo vya afya kila kata, hivi tunavyoambiwa vinajengwa sasa ni vipi?

ryan riz

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
423
Reaction score
683
Maana inashangaza, pale tulipoambiwa vituo vimejengwa kila kata na mwaziri na wabunge hawa hawa.

Sasa tena mawaziri na wabunge hawa hawa wanasema vituo vya afya vinajengwa kila kata, ina maana vile vya awali vimebomoka ama?

Hebu watuambie wanajenga nini (kama wanafanya ukarabati, wanaongeza majengo labda yale ya awali hayatoshi, ila sio kusema wanajenga vituo vipya wakat tayari wameshatuambia kila kata inakituo cha afya.
 
Kule wilaya ya Chamwino,Jimbo la Mvumi Kata zifuatazo hazina vituo vya Afya:-
Igandu, Nghahelezi, Idifu, Mvumi Misheni, Mvumi Makulu, Makang'wa, Fufu, Loje na Nhinhi

Kata zenye Vituo vya Afya katika Jimbo Hilo ni Handali, Mpwayungu na Mlowa, basi!
Hii nchi imejaa maigizo tupu
 
Kule wilaya ya Chamwino,Jimbo la Mvumi Kata zifuatazo hazina vituo vya Afya:-
Igandu, Nghahelezi, Idifu, Mvumi Misheni, Mvumi Makulu, Makang'wa, Fufu, Loje na Nhinhi

Kata zenye Vituo vya Afya katika Jimbo Hilo ni Handali, Mpwayungu na Mlowa, basi!
Sasa kwa nini awali kipindi cha Magufuli tulikuwa tunaambiwa kila kata kumejengwa kituo cha afya na walikuwa wasema mara nyingi mno...
 
Zipo nyingi tu. Halafu ni kupe siri moja kipindi covid imeingia na kutuambia magufuli kafukuza covid kwa maombi ni kwamba kama ingekamata sana basi wizara ya afya ilikuwa inavuliwa nguo tungejua mapungufu ya nchi kuwa huduma ya afya ni mbovu na vifaa kama oxygen machine unaweza kuta tanzania zipo 100 tu
 
zipo nyingi tu.! alafu ni kupe siri moja kipindi covid imeingia na kutuambia magufuli kafukuza covid kwa maombi ni kwamba kama ingekamata sana basi wizara ya afya ilikuwa inavuliwa nguo tungejua mapungufu ya nchi kuwa huduma ya afya ni mbovu na vifaa kama oxygen machine unaweza kuta tanzania zipo 100 tu
Ndio nawe sasa ujiulize km tuna viongozi au tuna watu wasiojielewa...!

Yaan Rais akisema na wao wanaanza kuimba nchi nzima kwamba rais kafanya hivi mara vile bila hata kuchunguza au hata km wanajua ukweli.

Ni unafki mkubwa sana na nchi kuendelea kwa mtindo huu sahau.

Hiv patia picha kila mbunge akipewa nafasi ya kuongea awe anaeleza changamoto katika jimbo lake za ukweli na pia akaeleza changamoto zilizotatuliwa na kushauri namna ya kutatua zngine labda kwa zile ambazo haziitaji pesa mfano za kisheria tu..

Unafikiri watu hawatarudi kuliheshimu BUNGE..?
 
Maana inashangaza, pale tulipoambiwa vituo vimejengwa kila kata na mwaziri na wabunge hawa hawa.
Sasa tena mawaziri na wabunge hawa hawa wanasema vituo vya afya vinajengwa kila kata, ina maana vile vya awali vimebomoka ama?

Hebu watuambie wanajenga nini (kama wanafanya ukarabati, wanaongeza majengo labda yale ya awali hayatoshi, ila sio kusema wanajenga vituo vipya wakat tayari wameshatuambia kila kata inakituo cha afya.
Kila kata ina vituo double sasa. Kituo JPM na kituo SSH. Tozo hoyee!
 
Maana inashangaza, pale tulipoambiwa vituo vimejengwa kila kata na mwaziri na wabunge hawa hawa.

Sasa tena mawaziri na wabunge hawa hawa wanasema vituo vya afya vinajengwa kila kata, ina maana vile vya awali vimebomoka ama?

Hebu watuambie wanajenga nini (kama wanafanya ukarabati, wanaongeza majengo labda yale ya awali hayatoshi, ila sio kusema wanajenga vituo vipya wakat tayari wameshatuambia kila kata inakituo cha afya.
Hili la kwako Tisa, kumi je kweli tunataka vituo kila kata??? au watu wanataka huduma bora na sio majengo. Yaani hawa wanasiasa wa sasa hivi walichojifunza kutoka kwa mkoloni ni sheria kandamizi tu.

Wangetumia akili zao japo kidogo tu, ni hospital chache na bora sana ndio watanzania wanataka, sasa kuna mrasimu mmoja yeye akiona majengo na kutafuta mkandarasi kesho anapita kukagua basi kazi nzuri. Huyu wanayempunguzia mwendo wa kufata huduma ndio anafika kituoni hakuna dawa wala mganga.

Kuliko kutawanya rasilimali chache kwa kila kata, wangekuwa na centre of excellence chache bila ubaguzi wangewekeza katika huduma bora.
 
Maana inashangaza, pale tulipoambiwa vituo vimejengwa kila kata na mwaziri na wabunge hawa hawa.

Sasa tena mawaziri na wabunge hawa hawa wanasema vituo vya afya vinajengwa kila kata, ina maana vile vya awali vimebomoka ama?

Hebu watuambie wanajenga nini (kama wanafanya ukarabati, wanaongeza majengo labda yale ya awali hayatoshi, ila sio kusema wanajenga vituo vipya wakat tayari wameshatuambia kila kata inakituo cha afya.
CCM hawakuanza leo na ujenzi wa kituo cha afya kila kata. Kauli mbiu hii ni ya CCM toka enzi na enzi kwani waligundua siku nyingi kuwa ni mradi wa mkakati. Hebu shuhudia hapa...

1662120030242.png

13/10/2014

1662118670098.png

15/11/2016

1662119707020.png

Kwa sasa ni wimbo wa CCM kila awamu toka ya Jakaya Kikwete kabla ya tozo!
Halafu jana tu...

1662119464404.png
 
Maana inashangaza, pale tulipoambiwa vituo vimejengwa kila kata na mwaziri na wabunge hawa hawa.

Sasa tena mawaziri na wabunge hawa hawa wanasema vituo vya afya vinajengwa kila kata, ina maana vile vya awali vimebomoka ama?

Hebu watuambie wanajenga nini (kama wanafanya ukarabati, wanaongeza majengo labda yale ya awali hayatoshi, ila sio kusema wanajenga vituo vipya wakat tayari wameshatuambia kila kata inakituo cha afya.
Inaijua VIEITE wewe ?
 
Ni kweli walijenga Kila kata,na sasa hivi wanajenga juu yake ya yake majengo ya awali ili zibebane ziwe mbili mbili Kama gholofa.
 
Naombi nitoa ufafanuzi kwa niaba ya Mwana wa Mama mpendwa na mpakwa mafuta Migulubaja Chemba;
Mchanganuo:
1.Fedha za tozo tumeagiza Magari ya serikali VIETE na zingine tumemkopesha Waziri wa Shekeli akanunulie mabasi,Watanganyika muendelee kuwa wavumilivu, Waziri ni mtu mwaminifu sana,atarejesha tu.

2.Fedha za COVID-19 tulinunulia Barakoa za Bunge, Serikali na Mahakama na zilizobaki tuligawana sisi viongozi Kama posho ya kuimarisha upendo na mshikamo

3.Fedha za IMF/ Benki ya Dunia, zingine Mama alitumia kwenye ziara Marekani na posho ya wapambe.
4.Ujenzi wa vituo vya Afya ,madarasa na nyumba za waalimu tutaendelea nao mara baada ya Waziri kurekesha mkopo wa mabasi.
Asanteni kwa kunisikiliza!!
 
Back
Top Bottom