DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 41,728
- 103,997
Duh!, Kilugha gani hicho[emoji848]Muhogo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh!, Kilugha gani hicho[emoji848]Muhogo.
Tangu uishi nao hadi leo umekaa.. yeye ndio akutafutie kazi na akili yako haijiongezi.. Pole kwako.. mitandao haikufahi kabisa.. ni vizuri akusome humu akutimue kabisa..
Mimi mwenyewe niliacha kazi mwezi wa sita Leo hii nimempigia mwajiri wangu wa zamani kama Kuna nafasi za kujitolea pale kazini
Lugha ya kanda ya ziwa.Duh!, Kilugha gani hicho[emoji848]
HatarDebe la mahindi Tsh 22,000
Debe la udaga 12,000
Dagaa kisado 7,000
Lita 3 mafuta ya kupikia Tsh 21,000
Mchele Kilo 1 Tsh2,600
Nyama kilo 1 Tsh 8,000
Mkaa gunia Tsh 40,000
Sukari kilo 1 Tsh 3,000
Kipande cha sabuni Tsh 500 unafua jeans 3 kimeisha (za sasa sjui wamezifanyaje)
Kilo ya mahrage Tsh 3,000
Pakti ya chumvi Tsh 500
Kodi ya chumba na sebule
Bill ya maji
Bill ya umeme
King'amuzi 23,000
Bando la simu (GB 1) ni Tsh 2,000
Mke hajavaa
Watoto hawajavaa
Mafuta ya kujipakaa
Ndugu, jamaa na marafiki
Sadaka
Mengineyo
Akiba
Mshahara 370,000/=
CCM imeshindwa kuboresha maisha ya watu wake. Hiki ni chama mfu, kimekosa ubunifu.
Wachumi wake kanjanja wamo bungeni kusema yah yah yah yah yah yah trab trat utumbavu getteh.
Tunahitaji serikali ijitafakari ikubali katiba mpya ya Warioba irasimishwe. Pili twende kwenye serikali ya mseto, na covid 19 watolewe bungeni, wapelekwe mahakamani hadi warudishe mishahara na posho your waliyochukua kwa miaka sita
Udaga ni ndugu wa matobolwaUdaga Ndo Nini[emoji848]
Ukiingia porini uanze kilimo, watakuja watu wa CCM, wanajiita wenyeviti wa kijiji na watendaji wa kijiji watakusakama kwamba umevamia uoto wa asili, hii mijitu mipumbavu kabisaNchi inaardhi kubwa yenye rutuba, Moto, maziwa na mabwawa lakini ati chakula ni Ghali. Ajabu Sana hii
Ukiingia porini uanze kilimo, watakuja watu wa CCM, wanajiita wenyeviti wa kijiji na watendaji wa kijiji watakusakama kwamba umevamia uoto wa asili, hii mijitu mipumbavu kabisa
Tozo, ushuru wa mazao, vizuizi vipi kila kijiji, na inatakiwa uulipie huo mzigo. Hadi unafika sokoni umeshaishiwa kabisa, na unapokelewa na madalali wenye kiu na njaa.😀😀
Kama utabahatika kuruka kigingi hiko, ukijaaliwa ukalima ukapata mazao unakavuna, utakutana na Vyama za ushirika Kama sio bei ya hovyo
Ngano na mafuta ya kura tunategemea Urusi na Ukraine.Nchi inaardhi kubwa yenye rutuba, Moto, maziwa na mabwawa lakini ati chakula ni Ghali. Ajabu Sana hii
Niliacha ili nifanye biasharaUliacha Kwa Sababu gani?
Na unarudi Kwa sababu gani?
Mimi nipo kwa shemeji huku dar halo ya mwaka jana na mwaka huu hali tofauti siamini kwa jinsi shemeji anvyopenda wali uliokolea nazi na mboga nzuri ilikuwa kwa wiki lakima kitu kitolewe hata mara tano sasa nipo hapa mwezi umeisha nimekula wali siku mbili tena kwa papatupapatu na mchicha .
Ugali na mboga za majani imekuwa kama ada natauta sasa hivi hata harufu ya wali tu nakutafuta kwa tochi .
#MamaAnafunguaNchi
Ngano na mafuta ya kura tunategemea Urusi na Ukraine.
Mpaka Sasa hakuna effort zozote za maana kuzalisha ngano yetu wenyewe ya kutosha na kujitosheleza na uzalishaji wa mafuta ya kura.
Tozo, ushuru wa mazao, vizuizi vipi kila kijiji, na inatakiwa uulipie huo mzigo. Hadi unafika sokoni umeshaishiwa kabisa, na unapokelewa na madalali wenye kiu na njaa.
Wao wanapata kikubwa, wewe kiduchu
Tatizo la watanzania tunachagua na kubagua vyakula.TULIANZA NA MILO MITATU, TUKAJA MILO MIWILI. SASA TUPO MLO MMOJA. NIMEITISHA KIKAO CHA DHARURA.
Anaandika, Robert Heriel
Sio kama nina Parkinson Disease Kwa jinsi ninavyotetemeka hapa. Hata nikikosea maandishi hapa msinitukane ndugu zanguni. Eleweni njaa haina mbabe. Nina ubao hapa siiiioo mcgezo.
Wengi humu wanajua ninaishi Kwa Shemeji yangu, aliyemuoa Dada yangu kipenzi, Naelijwa, labda mtajiuliza naanika mambo ya familia ya dadaangu Mtandaoni, lakini sina jinsi, hata hivyo dada na Shemeji hawatumii mitandao ya kijamii ingawaje rafiki zao wanaweza kuwa humu. Lakini Mimi sijali wala nini.
Kuhusu Ile kesi niliyompeleka Mahakamani, Taikon niliangukia Pua. Yule Hakimu ni mjinga Sana, tuachaneni na hayo.
Nilipofika hapa kwa Shemeji yangu kipindi kile nilikuta wanakula Milo mitatu. Tulikula Milo mitatu weee mpaka Taikon nikaota shavu. Mboga Saba zilinifanya ninawiri,
Kwa msiojua faida za Kula Milo mitatu na mboga Saba huku juisi embe na mapasheni zikiwa zimesheheni mezani, faida ni hizi;
i. Kunawiri na kuwa na mwili wenye Rutuba
ii. Ngozi kuwa laini
iii. Kuwa na nguvu za kiume
iv. Kuvutia Warembo
Hivyo miezi sita ilinitosha kuwa na mwili wa kushawishi Pisikali za Mjini. Ndipo nikampata huyu mchumba wangu ambaye wote tunakaa Kwa Shemeji.
Nataka nikuambie na wala usije kumuambia mtu, hii ni Siri yetu Mimi na Wewe, chakula kinaleta uzuri Kwa mtu.
Nakumbuka nilipokuja kutoka kijijini Kwetu huko Makanya, nilikuja nikiwa nimezeeka, nilikuwa Sura personal, nilikuwa nimefubaa kama baa za Wanywa mataputapu.
Hivi unajua Kwa nini sipendi uone picha zangu za zamani, ni Kwa sababu nilikuwa kama kioja, kituko kitakachokupa cheko.
Chakula ukila vizuri lazima uzuri uje tu.Hapa asubuhi tulikuwa tunaamkia maziwa na mayai, pamoja na matunda, Mchana tunapiga ugali, Samaki, mboga za majani, maharage, na kajuisi kabariidi. Jioni tunamalizia na chakula laini Kama ndizi au viazi, zilizochanganywa na Nyama au nyama choma na juisi laini.
Taikon Rutuba ikavuta huba, mademu wakaniganda kama Ruba. Nikajisahau kuwa nipo kwa Shemeji, sikukumbuka mambo ya kutafuta kazi mpaka siku nilipoona Mlo mmoja umeondolewa kwenye Ratiba. Mlo wa Asubuhi. Ikabaki Milo miwili. Sasa nikawa sielewi nini kinaendelea. Nikavunga, Tukaanza kupiga Hesabu za Pasi ndefu hapo tungekula chakula saa tano Asubuhi, alafu inapigwa Counterattack ndefu mpaka kumi na moja au kumi na mbili jioni. Hata hivyo Pasi hizo nilishajifunziaga Chuoni Kule Ujerumani kwenye Bundasiliga. Hivyo nikaona It's Okay.
Sijakaa kidogo nashangaa Shemeji amebadilisha mfumo kutoka Counterattack mpaka "One touch" kama mnakumbuka ule mchezo wa mpira WA miguu wa 'one touch' kugusa mara moja. Sasa nikaona application ya mchezo Ile kwenye Really Life.
One touch fomula ilianza Last week. Shemeji nakumbuka weeki mbili zilizopita alituuliza ni saa gani ni katikati ya siku Kwa upande wa mchana, nakumbuka nilitopoka saa sita mchana, aliponiuliza Kwa nini nikamjibu ni Kwa sababu jua lipo utosini. Katikati. Akanisifu Kwa jibu langu.
Sasa nashangaa wiki iliyoanza naamka Asubuhi hola, nahesabu masaa hola, mpaka saa tano ndio namuona Dada anaingia jikoni, anafanya vitu saa sita tukawa mezani, nakumbuka siku ya Kwanza tulikula kimyakimya bila kuongeleshana ungedhani tunakula chakula cha tambiko la mizimu. Sio Shemeji, sio Dada wala sio Mimi. Watoto wapo boarding.
Kesho yake, hivyohivyo, siku ya tatu nako hivyohivyo. Mpaka nikahisi wanataka kunitoa Kafara. Unajua Shemeji yangu ni mtu anayependa Sana kuongelea mambo ya waganga Sana. Sasa kuishi na watu wa namna hii unatakiwa uwe kimachale machale.
Jana nimewaweka kikao cha dharura, kujua Yale yanayoendelea mule ndani, nikamuambia Shemeji yangu imekuwaje tunakula Kama tupo kwenye Meza ya mizimu, pia mbona tunakula mlo mmoja. Shemeji akachukua simu yake akapiga Kwa Mama yake, kisha akaweka Loud;
" Marhàba mwanangu tunakufa njaa, leo hatujala kabisa. Nasubiria ahadi yako. Akiba ya chakula nilikuambia imeisha, mwaka huu mvua hazikunyesha vizuri hivyo hatukuvuna, wala nisingekusumbua mwanangu"
Ilikuwa sauti ya Mamaake na Shemeji yangu. Nilijikuta nipo kimya.
Habari nilizonazo hapa naambiwa Kwa sasa ukila Milo miwili hapo mtaani watu wanakupigia makofi kutokana na Hali kuwa ngumu. Na hao wanaofanya hivyo ni Wale wenye vipato vya Kati na vipato vikubwa.
Wale wenzangu na Taikon Mlo mmoja ukicheza unaweza kuukosa ukalala njaa.
Acha nipumzike,
Ni Yule mpiga One Touch
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam,