Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha Ema kichwa maji sana anajua kujikausha
Ngoja tusibili show ya teacherTulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 19.
Safari ikazidi kusonga kuelekea kusiko julikana.Ilikuwa muda wa usiku sana na giza lilikuwepo kiasi,kiasi fulani kulikuwa na nuru ya mbala mwezi.Tulitembea tukiwafuata wale watu ambao mpaka wakati huo hawakufahamu kama tulikuwa nyuma yao!.
Sasa kuna mahali walifika yule wa mbele akampatia mwenzie aliyekuwa nyuma ishara ya kwamba inapaswa wasimame,waliposimama pale kwa muda ndipo kuna watu wengine ambao nilipowahesabu walikuwa ishirini,sasa ukijumlisha na wale wa lile kundi la kwanza ambao walikuwa wa tano akiwemo Headmaster pamoja na Ema,jumla yao ilifanya kundi lote la watu kuwa ishirini na tano.Basi ndipo nikamuona yule mzee Makono akiwa kwa mblele akiongoza jahazi huku akiendelea kuimba nyimba za kisukuma na wenzie kuitikia.
Baada ya safari ya muda mrefu ndipo sasa tukafika kulipokuwa na mashamba yaliyokuwa yamepandwa mtama,ule ulikuwa mtama kwasababu nilikuwa ninafahamu namna mahindi yalivyo na mtama ulivyo hata ukiwa bado haujakomaa,kwahiyo sikuwa na shaka kabisa kwamba lile lilikuwa shamba la mtama kwasababu pia lilikuwa shaghala baghala,tofauti na mahindi yanayopandwa kwa kuacha nafasi na kwa mstari!.Walipofika hapo mzee makono alipiga mruzi kama vile anachunga ng'ombe.
Basi wale jamaa waliokuwa wakimsaidia ile kazi walikimbia kuelekea mbele ambapo walianza kuwapanga wale watu na kuwapa majembe,majembe yale hayakuwa kama haya ambayo sisi tunalimia kawaida,yale yalikuwa kwa mbele yamechongoka kama Mundu!.Baada ya kukabidhiwa yale majembe kila mtu alikuwa akipewa ishara na kuanza kulima kwa spidi kali mno!.
Hakuna jambo ambalo mpaka leo siwezi kusahau kama lile la watu kulimishwa kichawi huku nikiwa nashuhudia kwa macho yangu,miaka ya nyuma kwa stori za vijiweni nilidhani yawezekana ikawa tu stori watu wanajitungia lakini baada ya kushudia mimi mwenyewe ndipo nikaamini kwa hakika uchawi upo na unafanya kazi kubwa mno!.Kwa spidi ile waliyokuwa wanatumia wale watu kiukweli haikuwa ya kawaida!.Niliendelea kumtazama Headmaster na Ema wanavyohenyeshwa kuna muda huruma iliniingia sana lakini sikuwa na nmna!.
Kutokana na ule udharirishaji wa Ba'mdogo mbele ya wanafunzi niliona kabisa anachokipata ndicho anachokistahili,ningeweza kumwambia Monica amwambie mama yao awasaidie lakini niliona ngoja wapitie shubiri,kwa upande wa Ema sikuwa kabisa na huruma nae na nilitaka amenyeke kishenzi maana alikuwa na mdomo mrefu sana!.
Monica "Huyo ndugu yako juzi nilimwambia akajifanya mjanja,ngoja wamfundishe adabu"
Mimi niliendelea kutulia na kujionea mwenyewe huku moyoni nikifurahia kupendwa na Monica maana isingekuwa hivyo na mimi uenda ningekuwa ni miongoni mwa wahenyeshwaji!.Wale watu walipalilia lile shamba bila kupumzika hata kidogo!.
Mimi "Hivi hawachoki?"
Monica "Unataka ukajaribu?"
Mimi "Hapana,mi nimeuliza tu!"
Monica "Hapo hakuna kuchoka,utaenda kuchoka huko kwako lakini hapo hauchoki"
Basi tuliendelea kutazama lile shuruba walilopata wale watu na kiukweli hakukuwa na huruma hata punje!.
Baada ya muda mrefu kupita,ndipo nikasikia tena mruzi unapigwa kwa nguvu!,alikuwa ni yuleyule mzee makono akatoa ishara ya kwamba wamemaliza lile eneo na kilichofuata ni kuhamia eneo jingine ili kazi ya kulima iendelee!.Lile zoezi lilimaliza kukiwa kunakaribia mapambazuko kabisa!.
Monica "Tuondoke"
Mimi "Nyumbani?"
Monica "Nikurudishe kwenu niwahi kwenda kulala".
Mimi "Wamemaliza"
Monica "Pakishapambazuka kama hivi hakuna ujanja,watawarudisha tu"
Basi tukaondoka lile eneo mpaka nyumbani,tulipofika nyumbani Monica hakutaka kuondoka na akanitaka kile kibuyu nilichokuwa nimekishika nikiweke pale pembezoni ya mlango kama ilivyokuwa mwanzo na akanitaka nisimame nae pale ukutani mpaka Ema na Ba'mdogo watakaporejeshwa!.
Basi haukupita muda kuna jamaa aliingia na Ema mpaka ndani akawa amemlaza pale kitandani!,sasa ile jamaa anataka kutoka ni kama alikuwa na mashaka sana akaanza kuangaza chumba kizima lakini hakuona chochote!,ndipo akawa ametoka nje!.Sasa wakati Monica anataka kutoka pale tulipokuwa akanibana tena na kunitaka nitulie kimya kabisa!,mara ghafla aliingia mle chumbani mzee makono na yule jamaa aliyemlaza Ema pale kitandani!,walijaribu kuangaza chumba kizima lakini mzee makono nikaona ni kama alikuwa na mashaka!,basi wakazungumza na yule jamaa kisukuma kisha wakawa wametoka nje!.Kiukweli niliingiwa uoga na hofu kubwa mno!.
Mimi "Hawajatuona kweli?"
Monica "Hivi unamjua mama yangu au unamsikia?"
Aliendelea "Mama ndiye mkubwa hata huyo mzee haoni ndani,mama hajawahi kushindwa!"
Monica "Hivi Umughaka huwa huniamini ninapokwambia nitakulinda?,wala hakuna anayeweza kutuona hapo,hao ni wadogo sana mbele ya mama"
Baada ya kunihakikishia hivyo kiukweli sasa moyo wangu ulipata amani!.
Monica "Mimi naondoka,nikuombe usimuamshe huyo ndugu yako mpaka atakapoamka mwenyewe"
Aliendelea "Jioni nitakuja kukuchukua,Bibi yangu aliyemzaa mama anakuja na mama alisema nije kukuchukua nikakutambulishe".
Mimi "Sawa"
Baada ya kuniambia hivyo akawa ametoweka,nilimuitikia kishingo upande nilakini moyoni sikutaka kabisa kwenda kwao maana niliogopa viboko na adhabu ya Ba'mdogo,sikuwa na namna ilibidi niwe mtumwa wa penzi la Monica,ingawaje kuna muda niliona kabisa ananipenda na ndiyo maana mimi sikupata taabu na shuruba za wachawi pale kijijini,zile feva zilifanya nikampenda sana Monica!.
Baada ya Monica kuondoka na kile kibuyu ndipo nilivua zile nguo nilizokuwa nimevaa nikaavaa nguo nyingine na kupanda kitandani!,sasa nilipopanda kitandani ndipo kumuangalia Ema miguuni nikakuta bado anatope la shambani!,sasa sikufahamu ndiyo ulikuwa utaratibu wao au walijisahau kuwaosha au waliwaacha vile kwa kusudi la kuwakomoa,nilipanga lile swali ningeonana na Monica nimuulize!.Muda huo ilikuwa saa 11 alfajiri,sikuweza kabisa kulala niliamua kushuka kwenye kitanda na kwenda kukaa kwenye kiti.
Siku hiyo sikuwa na haraka kabisa ya kwenda kufata miwa nilitaka Ema aamke nione ataniambia nini!.Sasa ilipofika saa 12 asubuhi jamaa bado alikuwa amekala huku akiendelea kujigeuza geuza kitandani akichafua shuka na yale matope!.
Nilichukua mswaki nikaanza kusukua na kunawa uso hapo kando ya bafu!,sasa wakati nikiwa ndani nilimsikia Maza mdogo akiita "Emaaaa....." wewe Emaaaaa".
Baada ya kuona aliyekuwa anamuita haitikii akaanza kuniita "Umughaka!"
Mimi "Naaam"
Basi nikaenda nikafungua mlango wa sebuleni ambao mara zote ulikuwaga unarudishiwa tu kwakuwa haukuwa na komeo!.
Mimi "Mama shikamoo"
Maza mdogo "Marhaba"
Aliendelea "Hebu ingia"
Mimi "Wapi mama,huko?"
Maza mdogo "Ndiyo,njoo"
Basi nikausogelea mlango nikagonga ndipo mama mdogo akaja kunifungulia!.
Maza mdogo "Hebu muangalie baba yako mdogo"
Basi nilipomtazama dingi mdogo miguuni pia alikuwa na tope la kufa mtu!.
Mimi "Amelitolea wapi?"
Maza mdogo "Mi sijui kwakweli,hii nyumba mbona kila siku maajabu hayaishi!".
Mimi " Kwani Ba'mdogo hakutoka kweli?"
Maza mdogo "Huyu usiku kucha nimelala nae hapa,atoke usiku aende wapi?"
Niliamua kukausha na sikutaka kabisa kufungua domo langu na kumueleza mtu jambo lolote!.,Pengine ningewaambia kwa makusudi mema tu lakini nikaogopa wasije kunituhumu na mimi ni mshirikina!.
Maza mdogo "Baba Mary......wewe baba mary"
Maza mdogo "Amka basi"
Ba'mdogo aliendelea kujigeuza kana kwamba yuko kwenye godoro la sita kwa sita kumbe kigodoro chenyewe kilikuwa kidogo tu cha kusukimia maisha pale kijijini!.
Basi mimi ilibidi nitoke nje ili niwache wao humo ndani wakiendelea kuamshana!.Sasa nilipoingia chumbani kwetu nilikuta Ema akiwa ameshaamka na miguuni hakuwa na tope,inaonekana wakati mimi nikiwa kule chumbani kwa Headmaster yeye baada ya kuamka alienda kunawa,hata lile shuka lililokuwa limechafuka alikuwa amelitoa na ametandika shuka jingine!.
Sasa nikasubiri aongee jambo lolote lakini jamaa akapiga kimya,pengine alidhani uenda sifahamu chochote,kimoyo moyo niliona kabisa hata ile adhabu aliyokuwa amepewa ilikuwa ndogo kutokana na namna alivyokuwa na kiburi!.
Haukupita muda ba'mdogo naye akawa ameamka kutoka chumbani kwake akawa ametoka nje!.
Ba'mdogo "We Umughaka"
Mimi "Ndiyo ba'mdogo"
Nilitoka nje kuona alichokuwa ameniitia.
Ba'mdogo "Huyo yuko wapi?"
Mimi "Yupo chumbani Baba"
Mimi "Ema"
Ema "Eeenh"
Mimi "Njoo unaitwa"
Ba'mdogo "Hivi na nyie mmefanywa hivi kama mimi?"
Wakati Ba'mdogo anazungumza alikuwa akizuonyesha miguu yake iliyokuwa imejaa matope.
Mimi "Hapana baba mimi kwangu sijaona"
Ema "Hata mi kwangu sijaona"
Hapo ndipo nikajua Ema anaweza asiwe na akili timamu,yaani alidhani mimi sijamuona miguuni akiwa na matope!,sasa nilishindwa kuelewa kwanini alikuwa akificha,hiyo yote ni kwamba alidhani mimi nitamcheka na kwenda kumtangaza!,kiukweli nilibaki namshangaa!.Sasa nikawa najiuliza lile shuka atalifuaje?,nilibaki kumshangaa tu kiukweli!.
Ba'mdogo "Haya mambo hapa kijijini yameshakuwa ya kawaida na tukijaribu kuyasema hatueleweki"
Aliendelea "Yule mzee nae akaja hapa nikampatia mpaka hela lakini hamna alichokifanya"
Sikutaka kabisa kusema jambo lolote,mzee aliyekuwa akimsema ni yule ambaye wakati wa kuchezwa ngoma pale kwao Monica alishapewa adhabu na kuliwa kabisa!.
Ba'mdogo "Nataka nifanye tukio kubwa hapa kijijini kwa hawa washenzi ndipo niondoke"
Ba'mdogo "wao si wanajifanya wajanja!,ngoja uone"
Basi baada ya tafakari na kushangaana pale kila mtu aliendelea na mambo yake,mimi kama kawaida sikutaka kupoteza muda nilielekea kuchukua miwa.
... sasa nilipopanda kitandani ndipo kumuangalia Ema miguuni nikakuta bado anatope la shambani!
GgWewe utakuwa umepita Iyunga Tech wewe maana sio kwa kunikumbusha viunga hivyo.
Aise baba mdogo kayakanyaga kumpa adhabu ya kujaza pipa, Monica aje ampige na kitu kizitoNgoma unogile,masharti ya dawa usiguse maji wala kuoga,Headmaster katoa adhabu ya kujaza pipa maji,hapa lazima uligusa maji,nahisi dawa itaharibika,ngoma bado nzito naamini
Umughaka= Kijana ambaye hajabalehe.
London toilet unavua nguo mbali kisha unaenda uchi, ukienda na nguo unatoka unanuka mzigo siku nzima...nimepita hapo early 2000Wewe utakuwa umepita Iyunga Tech wewe maana sio kwa kunikumbusha viunga hivyo.
Bhalipo bhingi fijhoMkuu....kwani manyamanyafu wakali bhalipo mpaka ulu .....au bhamalike????
Na nine, natighi bhamalike!Bhalipo bhingi fijho
Buji naona upo na hukuAbhalosi bhalipo posa nkisu iki. Kumyitu bhalipo abha Manyamanyafu, bhikulya bhandu. Bhali balosi fijo. Bhalyagha na ama bututu, ughamenye?
Daaah ngupilika bhalosi fijo....Bhalipo bhingi fijho
Nawapilike ijolo fijoNa nine, natighi bhamalike!
Hii ya kuamka tope nimewahi kushuhudia wakati nasoma Karagwe Secondary, kuna jamaa nilikuwa nalala jirani naye bweni moja linaitwa Rumanyika, ile kaamka asubuhi kwanza kwa kukurupuka, miguu imejaa tope sana, mashuka yamechafuka halafu akiwa mchovu. Jamaa alichomoka spidi akaruka fensi akatokomea porini. Hakuwahi kurudi tena shuleni hapo mpaka namaliza.
Nilikuja kusikia alikuwa akifanyiwa hivyo na nduguze wa karibu mara kwa mara.
😅😅😅 jamaa alitokomea kihanga, hivi rumanyika ndiyo bweni lile kama hall, wameweka vitanda? Afu kwa pembeni kushoto kuna vibweni vingine vidogo vidogo?Hii ya kuamka tope nimewahi kushuhudia wakati nasoma Karagwe Secondary, kuna jamaa nilikuwa nalala jirani naye bweni moja linaitwa Rumanyika, ile kaamka asubuhi kwanza kwa kukurupuka, miguu imejaa tope sana, mashuka yamechafuka halafu akiwa mchovu. Jamaa alichomoka spidi akaruka fensi akatokomea porini. Hakuwahi kurudi tena shuleni hapo mpaka namaliza.
Nilikuja kusikia alikuwa akifanyiwa hivyo na nduguze wa karibu mara kwa mara.
Ulikula tunda kimasihalaIvi kuna jamaa wanabisha kuhusu mwalimu kumchapa mwanae shuleni mnashangaza mtakua mmelelewa na wazee warembo sana mimi na chama langu nakumbuka tulipigwa fimbo za kutosha na baba wa rafiki angu mmoja na hatukua wanafunzi yani chai ilitembea siku ile tunaulizwa tuwapeleke polisi au tumalizane apa apa? Watu tukaona tumalizane tu pale school na msala ulikua wakitaa
Mmenikumbusha mbali sana aise tulichezea fimbo mpaka kuna time unaona haziumi ilikua ni mbele ya wanafunzi wote
Uzuri wa lile tukio nilitafuna mabinti wawili kwa huruma zao kuja kunipa pole... Ujanja wote tulishindwa kukimbia lile tukio sijui yule headmaster alituroga
..R.I.P teacher tumebaki tukisimuliana tu lile tukio