Atuulize sie watoto wa waalimu wakuu wa Kijijini enzi hizo.
Kwanza Mzee akikuta umejihusisha na ugomvi wa aina yeyote ile, haulizi umeonewa au nani anamakosa, lazima uchezee fimbo zisizo na idadi. Hata kama tayari umeshapewa adhabu na mwalimu mwingine. Na siku hiyo ukifika nyumbani, una kamisheni ya adhabu Kwa kosa lilelile la shule ambalo tayari umeshatumikia adhabu. Hapo anakuadhibu kama Baba Mzazi mbele ya wadogo zako iwe fundisho kwao.
Kuna siku tunalima shambani, akatokeza mjusi, dogo anaenifuatia akajipendekeza kuinama wakati nimeinua Jembe kumkata mjusi, si likatua kichwani kwake! Damu zinamwagika USO mzima, tukaenda nyumbani mbio, Ile amefika tu, akadakwa na fimbo za rasharasha mwili mzima...hapo nikasema kama wanaufanyia hivi mti mbichi, mkavu itakuwaje? Piga picha huyo anatembezewa kipigo ni mtu aliyekatwa Jembe, Sasa mwenye kumkata itakuwaje?