Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Kwanza kabisa nawashukuru sana ndugu zangu wote mnaopongeza uzi huu na kutoa shukurani kedekede!,ningependa mtambue ya kwamba kwangu pesa si kipaumbele ingawaje nazihitaji pesa ili kufikia vipaumbele vyangu!.Wengi walitaka angalau nitoze kiasi cha fedha,ndugu zangu sijaja hapa JF kwa ajili ya fedha,ingawa fedha ikinifuata siwezi kuikataa kwasababu pia tunakesha tukiitafuta!,Lengo la huu uzi ni kukufunza,kukuburudisha na kukuelimisha!.Nilihitaji watu wapate shule kwa yale wengine tuliyopitia huko vijijini!.

Sasa Kuna mambo baadhi naona yamewatatanisha watu au wamesshindwa kuelewa!.

1.Kulipia kiasi cha Tsh 100 kwenye banda,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani.

2.Monica kutembea usiku ingawaje ni mtoto wa kike.

3.Msukuma kumiliki Ng'ombe zaidi ya elfu 10,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.

4.Kucharazwa viboko mbele ya wanafunzi kwa kosa la nyumbani,pia vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.

NAOMBA KABLA SIJAJIBU NITOE KISA KIFUPI!.

Mwaka 2000 kuna kaka yangu mtoto wa baba mkubwa kazi yake ilikuwa kuzibua vyoo(mzibua vyoo)Ingawa sikuhizi ameacha,kazi hii ilimpatia pesa za kutosha kwa miaka hiyo kwasababu pale wilayani ni kampuni yao ndiyo ilikuwa ikifahamika kwa shughuli hiyo!.
Sasa nakumbuka siku moja Mzee wangu alimuita yeye na watu wa kampuni yake pale nyumbani kuja kuzibua chemba ambayo ilikuwa kwa ajili ya nyumba ya wapangaji!,pamoja na kuja kuzibua ile chemba lakini pia walitakiwa kuchora ramani kwa ajili ya kujenga chemba(shimo)nyingine!..Mzee alitaka yale mashimo yawe na uwezo wa kupokea mzigo mkubwa na ndiyo maana akataka shimo lingine liongezwe!.

Basi kazi ya kuchora ramani ikaanza,ilikuwa mida ya saa 1 asubuhi!,walikamilisha kuchora ramani saa 1:20 Asubuhi,sasa kazi rasmi ya kuchoronga na kuchimba shimo jipya ikaanza!.Sasa wakati shimo linachimbwa nakumbuka tukawa tunapiga stori za kufa mtu!,wakati wao wanachimba mimi kazi yangu ilikuwa ni kutizama na kuchangia kwenye stori walizokuwa wakipiga!,ilikuwa wakihamia kwenye mademu na mimi najifanya kuchangia kana kwamba hao mademu hata ninaweza kuwamudu!,walikuwa wakihamia kwenye siasa na mimi nimo!,wakienda kwenye habari za magari na mimi nimo!.

Sasa kuna muda mada za kaka yangu huyo na wale jamaa wenzie zikaamia kwenye vyakula,na mimi nikawa mchangiaji!.

Brother "Yanii muda huu nikipata donati 10 na vikombe angalau vitatu vya chai ya maziwa ndipo moyo wangu utasuuzika"

Basi baada ya kusikia ile kauli umughaka mimi nikaanza kumzodoa brother huku nikibisha,sasa kiukweli kukawa na ubishani mkubwa mno!.

Brother alikuwa akisema kwamba anao uwezo wa kumaliza Donati 10 na vikombe 3 vya chai ya maziwa!,mimi nilikuwa ninabisha,wale wenzie wakanitaka tusiandikie mate wakati wino upo!.wakapendekeza tuweke dau la kila mmoja shilingi elfu 2,kwa mwaka huo nadhani ndugu zangu mtaelewa namna shilingi elfu 2 ilivyokuwa na thamani!.

Sasa tukakubaliana ya kwamba,ikifika saa 5 asubuhi tuelekee mjini kwa ajili ya kumnunulia brother donati 10 na vikombe vitatu vya chai ya maziwa,donati wakati huo kwa moja ilikuwa inauzwa Tsh 200,na chai ya maziwa kikombe ilikuwa inauzwa Tsh 100,na endapo asipoweza kumaliza basi angelipia hela niliyokuwa nimenunulia vitafunwa vile pale mgahawani na angenipatia Tsh elfu 2 kama tulivyokubaliana!.

Ilipofika mida hiyo kweli tukaelekea mjini kwa ajili ya kuupa muda na nafasi kwa ajili ya ule ubishi wangu kwa brother!.Niliagiza vile vitafunwa kama tulivyokuwa tumekubaliana!.
Ilikuwa ni ajabu kumuona brother akimaliza zile donati ndani ya muda mfupi kuliko nilivyodhani!,vile vikombe vya chai ya maziwa vilimpungua ikabidi nimuongezee vingine vitatu!,wakati huo kamaliza zile donati 10 ambazo mle kwenye mgahawa kila mtu alibaki kumshangaa kama ni binadamu wa kawaida au alikuwa kiumbe wa ajabu,cha kushangaza pamoja na kumaliza lakini alidai bado hajashiba hivyo alisema atangojea nyumbania ugali uive ili ajazilizie mapengo ya nafasi tumboni!.

Pamoja na yote lakini pia nilimpatia Tsh elfu 2 kama ilivyokuwa ahadi yetu.

SASA NILICHOTAKA KUSEMA NI NINI?

Tangu siku hiyo huwa sibishi ovyo ovyo tu kama punguani!.Yaani tumbo lako halafu nikubishie?,yaani mimi kama nakula robo wali nianze kubisha wewe kumaliza Nusu wali?,uenda nitakuwa mwendawazimu!.

Sasa nimeamua kuutoa huo mfano ili watu wajifunze jambo,usibishe jambo lolote kama hujawahi kupitia!,yaani wewe uzaliwe Magomeni ambako unashindia kutwa dagaa mchele halafu unambishia mtu aliyekulia huko UKILI GURU anayeshindia mihogo kwamba hawezi kuilima!.

Ikiwa kuna maisha hujawahi kuyaishi nikutaadharishe usije kubisha kwasababu watu watabaki kukushangaa na utaoneka Kituko mbele ya wanaume!.

1.Mimi binafsi nimeanza kushangilia mpira kwenye TV mnamo mwaka 1996 tena wakati huo nilikuwa naipenda sana Liverpool,ila ilipofika mwaka 1998 nikaanza kushabikia timu ya Arsenal!.Sasa mwaka 2004 ninaposema bandani nilikuwa nalipa Tsh 100 naamanisha!,siyo kwamba naigiza ndugu zangu!,na ndiyo maana nikamuomba huyo jamaa anayebisha yeye aje atuambie huo mwaka huko alikokuwa alikuwa analipa kiasi gani?,kama hana majibu basi atulie aache ubishi!,haiwezekani wewe uje uanze kuangalia mpira mwaka 2013 halafu ubishie watu tulioanza kuingia mabandani mwaka 1996!.

2.Suala la Monica kutembea usiku eti mtu anashangaa!,yaani leo mabinti kulala nje na kukesha kwa wanaume unadhani ni jambo jipya?,yaani binti ambaye kwao walikuwa washirikina na hakuwa na baba,yeye kutembea usiku unaona kuna uongo?,watanzania ni nani katuroga?,Mbona alivyolala na Ema pale kwa rafiki yake Jack usiku kucha mpaka kupelekea ugomvi na Deborah hamkuhoji?,mmeona muhoji mimi kukutana naye usiku kule mnadani!,Aiseee kuna sehemu vijana wa hili taifa wanapaswa kurekebisha ili mambo yaende sawa!.

3 Suala la Msukuma kumiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10 mwaka 2003-2004 mtu anabisha,huyohuyo mtu ukimuuliza kwamba amewahi kufika Tabora au sehemu nyingine ya usukumani atakwambia bado,halafu anabisha!,na huyu ni msomi mzima anashangaa kabisa!.Atahoji hadi sisi kupewa lita 5 za maziwa bure kila siku pale kwa Headmaster atakwambia ni uongo!,Kama hujawahi kutembea kwenye hii nchi nikuombe usije nyanyua mdomo wako ukabisha!.Kuna mtu ukimwambia pale Geita na Mwanza kuna watu wanahela chafu kuliko huyo anayejiita Mo Dewji bado watakuja hapa kubisha kana kwamba huyo Mo ni baba yake!.

4.Kwamba mimi kuchwapwa mbele ya wanafunzi ilikuwa ni stori ya kutunga!,Hii nchi kuna watu wanashida kubwa mno!,kwamba unataka kusema kwakuwa wewe umekulia na kusomea mjini unadhani watu wote tumesomea mjini?,Kuchwapwa mbele ya kadamnasi haikuwa mjadala!,na wala si mbele ya wanafunzi tu!,yaani stiki ulikuwa unakung'utwa hata sokoni kama ukileleta ukora!,Vijana kama hamjui vitu tuambieni tuwaelekeze muweze kuvifahamu.

Mimi nimesoma shule ya kata isiyokuwa na maabara(laboratory)masomo ya sayansi (pcb) na nilifaulu ufaulu mzuri tu wa dvs 2 sema baadae nilifeli form 6 kwasababu ya mapenzi ya mwanamke wa kitanga.Sasa hivi vijana nyie hamuwezi kufaulu masomo ya sayansi bila maabara!.

KAMA HUJAPITIA MAISHA FULANI USISIMAME NA TUMBO LAKO UKAANZA KUBISHA MBELE YA WANAUME,UTATIA AIBU!.

NI HAYO TU.
 
Kuna fisi huwa wanaishia njiani humu ,ila bwana umughaka ni muungwana sana kamalizia yote asee..licha ya ujuaji wa wana jf ,nadhani ndo mana wengine huwa wanatokomea kwa kukatishwa tamaa na wajuaji wa jf
 
Heko mleta story... Kwa kweli nilikuwa kwenye stress Kali sana umenisaidia kupunguza stress sana... Ubarikiwe sana

Mkuu stress hazina budi kuja!! Humu jf huwa zinapata dawa kwa kiasi fulani..POLE KWA UNACHOPITIA MKUU,MUNGU AKUONGOZE UVUKE SALAMA[emoji1488]
 
Baada ya lile tukio si badae ba Mdogo mtu alihamia Biharamulo au?? Nani wa kubaki huko Kijijini weeeee!! Anyways majibu kamili anayo Umughaka!

Yupo shule gan hapa Biharamulo mie mwenyeji sana naweza kumcheki
 
Mkuu UMUGHAKA unaweza ukatenga muda ukatusimulia hicho kisa cha wewe kufeli form 6 kwa sababu ya mapenzi kwa huyo mwanamke wa kitanga... naamini kuna funzo kubwa sana humo maana watu wengi wamefeli vitu vingi maishani baada ya kukolea na mapenzi nje ya mfumo wake wa kawaida... Mkuu nikuombe ukipata muda utusimulie... Ukorye bhuya mura weito... tabhatigha abhachabhani bhano
 
Halafu kuna mahali ma Monica alimwambia UMUGHAKA kuwa karibuni watapata mtoto hivyo amlinde mwanae,sio kwamba monica alipataga ujauzito kweli. Najiuliza naomba jibu lako mkuu umughaka
@UMUGHAKA tafadhali jibu hii basi [emoji3516]
 
Halafu kuna mahali ma Monica alimwambia UMUGHAKA kuwa karibuni watapata mtoto hivyo amlinde mwanae,sio kwamba monica alipataga ujauzito kweli. Najiuliza naomba jibu lako mkuu umughaka
Mkuu Kalpana wala hakupata mimba,pale mama yake alikuwa tu anasema mimi na Monica tayari ni wapenzi na alikuwa anachukia mtu yeyote kutufanyia vimbwanga kwasababu aliamini tungemletea mjukuu,hivyo alisema angetulinda kwa gharama yeyote,Lakini Monica wala hakuwa na ujauzito wangu!.
 
Mkuu Impimpi Mbona nimeeleza vizuri kuhusu wale wachawi wengine!,baada ya wale waliokuwa wameingia ndani kushituka na kuondoka aliyeshughulikiwa ni mzee makono,ndiyo maana hata mama yake Monica alisema watapata habari huko waliko,yaani watasimuliana!,sasa unadhani kwa tukio lile lililokuwa gumzo pale kijijini kuna mchawi alirudi?,nilisema kuanzia hapo Headmaster na nyumba yake viliogopwa na mpaka anahama hakuwahi kuona tena viroja!.

Kuhusu mimi na Monica,nimeeleza vizuri ya kwamba niliondoka hapo kijijini kwenda shule advance na Monica nikamuacha kwao,sikufahamu maisha yake yaliendelea vipi kwa wakati huo huko kwao kwasababu sikuwa hata na simu,ila nikasema kuna mwaka nilikutana na mtu mmoja tuliyekuwa tukifahamiana pale kijijini na akaniambia Monica sikuhizi anaishi Mwanza ila sijajua ni sehemu gani maana hata aliyeniambia aliishia tu kusema anaishi Mwanza,maisha ya mimi na Monica yalikuwa niyale ya ujana lakini baada ya hapo hatujawahi kuonana!
UMUGHAKA hapo bunju Upo kijiwe kipi, nataka nije tuonane
 
Anyway, Mwenye chombo (pikipiki)ambayo anatumia tu na hajui cha kufanyia hebu anipatie nipigie kazi ili kwa siku au wiki niwe nampelekea hesabu yake,hii chombo ninayotumia ishachoka na inanisumbua sana lakini sema na mimi ni mbishi tu!,nilipopata ajali siku ile natoka kusuruhisha ugomvi wa bro na mkewe ilipata shida kidogo!.

Hivyo kama unachombo nipe nipigie kazi usikae kizembe ili ikulipe kwa siku au wiki.

Tushikane mikono na kusaidiana panapobidi,sisi ni vijana na tunapambana!..
 
Na mimi niseme Umughaka umetisha sana na hii story. Tafadhali elekea Kwa printer iingie kwenye vitabu na wewe upate chochote. Pia ukifanikiwa kuitafsiri kwa kingereza ukampata publisher wa Ulaya kuichapa hela itakufuata
 
Ila hii story ni uongo mtupu, kuna mtoto wa kike atajiamini kutembea usiku ivo?, na anatokaje nyumbani kwao bila wazazi kuskia?
Ukizaliwa na kukulia dar utakua sahihi , tembea huko vijijini kuna wanawake majasiri kuliko wanaume. Acha kabisa kuna experience zinapatikana huko bush huwezi amini. Kwa watu waliozaliwa dar ni ngumu sana kuelewa . Pia miaka hii wazazi hawana utamaduni kuwapeleka watoto mikoani ndio tatizo . Ungekua kila mwaka likizo unaenda kijijini ungeamini
 
Kwanza kabisa nawashukuru sana ndugu zangu wote mnaopongeza uzi huu na kutoa shukurani kedekede!,ningependa mtambue ya kwamba kwangu pesa si kipaumbele ingawaje nazihitaji pesa ili kufikia vipaumbele vyangu!.Wengi walitaka angalau nitoze kiasi cha fedha,ndugu zangu sijaja hapa JF kwa ajili ya fedha,ingawa fedha ikinifuata siwezi kuikataa kwasababu pia tunakesha tukiitafuta!,Lengo la huu uzi ni kukufunza,kukuburudisha na kukuelimisha!.Nilihitaji watu wapate shule kwa yale wengine tuliyopitia huko vijijini!.

Sasa Kuna mambo baadhi naona yamewatatanisha watu au wamesshindwa kuelewa!.

1.Kulipia kiasi cha Tsh 100 kwenye banda,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani.

2.Monica kutembea usiku ingawaje ni mtoto wa kike.

3.Msukuma kumiliki Ng'ombe zaidi ya elfu 10,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.

4.Kucharazwa viboko mbele ya wanafunzi kwa kosa la nyumbani,pia vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.

NAOMBA KABLA SIJAJIBU NITOE KISA KIFUPI!.

Mwaka 2000 kuna kaka yangu mtoto wa baba mkubwa kazi yake ilikuwa kuzibua vyoo(mzibua vyoo)Ingawa sikuhizi ameacha,kazi hii ilimpatia pesa za kutosha kwa miaka hiyo kwasababu pale wilayani ni kampuni yao ndiyo ilikuwa ikifahamika kwa shughuli hiyo!.
Sasa nakumbuka siku moja Mzee wangu alimuita yeye na watu wa kampuni yake pale nyumbani kuja kuzibua chemba ambayo ilikuwa kwa ajili ya nyumba ya wapangaji!,pamoja na kuja kuzibua ile chemba lakini pia walitakiwa kuchora ramani kwa ajili ya kujenga chemba(shimo)nyingine!..Mzee alitaka yale mashimo yawe na uwezo wa kupokea mzigo mkubwa na ndiyo maana akataka shimo lingine liongezwe!.

Basi kazi ya kuchora ramani ikaanza,ilikuwa mida ya saa 1 asubuhi!,walikamilisha kuchora ramani saa 1:20 Asubuhi,sasa kazi rasmi ya kuchoronga na kuchimba shimo jipya ikaanza!.Sasa wakati shimo linachimbwa nakumbuka tukawa tunapiga stori za kufa mtu!,wakati wao wanachimba mimi kazi yangu ilikuwa ni kutizama na kuchangia kwenye stori walizokuwa wakipiga!,ilikuwa wakihamia kwenye mademu na mimi najifanya kuchangia kana kwamba hao mademu hata ninaweza kuwamudu!,walikuwa wakihamia kwenye siasa na mimi nimo!,wakienda kwenye habari za magari na mimi nimo!.

Sasa kuna muda mada za kaka yangu huyo na wale jamaa wenzie zikaamia kwenye vyakula,na mimi nikawa mchangiaji!.

Brother "Yanii muda huu nikipata donati 10 na vikombe angalau vitatu vya chai ya maziwa ndipo moyo wangu utasuuzika"

Basi baada ya kusikia ile kauli umughaka mimi nikaanza kumzodoa brother huku nikibisha,sasa kiukweli kukawa na ubishani mkubwa mno!.

Brother alikuwa akisema kwamba anao uwezo wa kumaliza Donati 10 na vikombe 3 vya chai ya maziwa!,mimi nilikuwa ninabisha,wale wenzie wakanitaka tusiandikie mate wakati wino upo!.wakapendekeza tuweke dau la kila mmoja shilingi elfu 2,kwa mwaka huo nadhani ndugu zangu mtaelewa namna shilingi elfu 2 ilivyokuwa na thamani!.

Sasa tukakubaliana ya kwamba,ikifika saa 5 asubuhi tuelekee mjini kwa ajili ya kumnunulia brother donati 10 na vikombe vitatu vya chai ya maziwa,donati wakati huo kwa moja ilikuwa inauzwa Tsh 200,na chai ya maziwa kikombe ilikuwa inauzwa Tsh 100,na endapo asipoweza kumaliza basi angelipia hela niliyokuwa nimenunulia vitafunwa vile pale mgahawani na angenipatia Tsh elfu 2 kama tulivyokubaliana!.

Ilipofika mida hiyo kweli tukaelekea mjini kwa ajili ya kuupa muda na nafasi kwa ajili ya ule ubishi wangu kwa brother!.Niliagiza vile vitafunwa kama tulivyokuwa tumekubaliana!.
Ilikuwa ni ajabu kumuona brother akimaliza zile donati ndani ya muda mfupi kuliko nilivyodhani!,vile vikombe vya chai ya maziwa vilimpungua ikabidi nimuongezee vingine vitatu!,wakati huo kamaliza zile donati 10 ambazo mle kwenye mgahawa kila mtu alibaki kumshangaa kama ni binadamu wa kawaida au alikuwa kiumbe wa ajabu,cha kushangaza pamoja na kumaliza lakini alidai bado hajashiba hivyo alisema atangojea nyumbania ugali uive ili ajazilizie mapengo ya nafasi tumboni!.

Pamoja na yote lakini pia nilimpatia Tsh elfu 2 kama ilivyokuwa ahadi yetu.

SASA NILICHOTAKA KUSEMA NI NINI?

Tangu siku hiyo huwa sibishi ovyo ovyo tu kama punguani!.Yaani tumbo lako halafu nikubishie?,yaani mimi kama nakula robo wali nianze kubisha wewe kumaliza Nusu wali?,uenda nitakuwa mwendawazimu!.

Sasa nimeamua kuutoa huo mfano ili watu wajifunze jambo,usibishe jambo lolote kama hujawahi kupitia!,yaani wewe uzaliwe Magomeni ambako unashindia kutwa dagaa mchele halafu unambishia mtu aliyekulia huko UKILI GURU anayeshindia mihogo kwamba hawezi kuilima!.

Ikiwa kuna maisha hujawahi kuyaishi nikutaadharishe usije kubisha kwasababu watu watabaki kukushangaa na utaoneka Kituko mbele ya wanaume!.

1.Mimi binafsi nimeanza kushangilia mpira kwenye TV mnamo mwaka 1996 tena wakati huo nilikuwa naipenda sana Liverpool,ila ilipofika mwaka 1998 nikaanza kushabikia timu ya Arsenal!.Sasa mwaka 2004 ninaposema bandani nilikuwa nalipa Tsh 100 naamanisha!,siyo kwamba naigiza ndugu zangu!,na ndiyo maana nikamuomba huyo jamaa anayebisha yeye aje atuambie huo mwaka huko alikokuwa alikuwa analipa kiasi gani?,kama hana majibu basi atulie aache ubishi!,haiwezekani wewe uje uanze kuangalia mpira mwaka 2013 halafu ubishie watu tulioanza kuingia mabandani mwaka 1996!.

2.Suala la Monica kutembea usiku eti mtu anashangaa!,yaani leo mabinti kulala nje na kukesha kwa wanaume unadhani ni jambo jipya?,yaani binti ambaye kwao walikuwa washirikina na hakuwa na baba,yeye kutembea usiku unaona kuna uongo?,watanzania ni nani katuroga?,Mbona alivyolala na Ema pale kwa rafiki yake Jack usiku kucha mpaka kupelekea ugomvi na Deborah hamkuhoji?,mmeona muhoji mimi kukutana naye usiku kule mnadani!,Aiseee kuna sehemu vijana wa hili taifa wanapaswa kurekebisha ili mambo yaende sawa!.

3 Suala la Msukuma kumiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10 mwaka 2003-2004 mtu anabisha,huyohuyo mtu ukimuuliza kwamba amewahi kufika Tabora au sehemu nyingine ya usukumani atakwambia bado,halafu anabisha!,na huyu ni msomi mzima anashangaa kabisa!.Atahoji hadi sisi kupewa lita 5 za maziwa bure kila siku pale kwa Headmaster atakwambia ni uongo!,Kama hujawahi kutembea kwenye hii nchi nikuombe usije nyanyua mdomo wako ukabisha!.Kuna mtu ukimwambia pale Geita na Mwanza kuna watu wanahela chafu kuliko huyo anayejiita Mo Dewji bado watakuja hapa kubisha kana kwamba huyo Mo ni baba yake!.

4.Kwamba mimi kuchwapwa mbele ya wanafunzi ilikuwa ni stori ya kutunga!,Hii nchi kuna watu wanashida kubwa mno!,kwamba unataka kusema kwakuwa wewe umekulia na kusomea mjini unadhani watu wote tumesomea mjini?,Kuchwapwa mbele ya kadamnasi haikuwa mjadala!,na wala si mbele ya wanafunzi tu!,yaani stiki ulikuwa unakung'utwa hata sokoni kama ukileleta ukora!,Vijana kama hamjui vitu tuambieni tuwaelekeze muweze kuvifahamu.

Mimi nimesoma shule ya kata isiyokuwa na maabara(laboratory)masomo ya sayansi (pcb) na nilifaulu ufaulu mzuri tu wa dvs 2 sema baadae nilifeli form 6 kwasababu ya mapenzi ya mwanamke wa kitanga.Sasa hivi vijana nyie hamuwezi kufaulu masomo ya sayansi bila maabara!.

KAMA HUJAPITIA MAISHA FULANI USISIMAME NA TUMBO LAKO UKAANZA KUBISHA MBELE YA WANAUME,UTATIA AIBU!.

NI HAYO TU.
Mkuu wewe ni Tarime moja nini
 
Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 25.

Baada ya Headmaster kutoka kuwasindikiza wageni,tuliamua kukaa kikao cha kifamilia na kuzungumza mambo kadhaa yaliyotuweka sawa.Sasa kila mtu alielekea chumbani kulala,baba mdogo na mkewe waliingia chumbani kwao,mimi na Ema pia tuliingia chumbani kwetu kulala.

Siku hiyo mle chumbani hakuna aliyepata usingizi kabisa,kabla ya kulala nakumbuka tulipakaa usoni dawa aliyokuwa ametupatia mama yake Monica,pia tukashikiria na zile hirizi mkononi kama alivyokuwa ameagiza tufanye!.Kadri muda ulivyokuwa ukisonga tuliona kimya,mimi nilianza kupitiwa na usingizi maana nilikuwa nimechoka sana!,kumbe wakati mimi napitiwa na usingizi,Ema yeye alikuwa macho kabisa na jamaa alikuwa na shauku ya kuona ni kitu gani kingetokea!.

Sasa ilipofika mida ya saa 8 usiku,nilishitushwa na Ema akiniamsha!.

Ema "Umesikia hicho kishindo?".

Mimi "Hapana,kishindo cha kitu gani?"

Ema "Kutakuwa na kitu nadhani!"

Ema alikuwa akiniambia kwa sauti ndogo kabisa na yenye uoga ndani yake!.

Mimi "Nyamaza"

Niliamka kitandani nikaenda kuwasha taa,nilifahamu kabisa kile kishindo Ema alichosikia hakikuwa cha kawaida na uenda wale jamaa wakawa wamekuja kama kawaida yao,kiukweli mimi kwa upande wangu sikuwa kabisa na hofu kwasababu kwa siku chache nilikuwa nimeshazoea yale mazingira ya kuwaona wachwawi laivu!.Nilimwambia na kumbusha Ema ya kwamba chochote atakachokiona asipige kelele wala kushituka!.

Haukupita muda,mara ghafla wakaonekana watu watatu wakiwa wamesimama mle chumbani huki wakiwa uchi kama walivyozaliwa,watu wale safari hii walikuja wawili wanaume na mmoja akiwa mwanamke!.Niliwaangalia kwa kuibia kama vile sielewi chochote!,Ema alikuwa akitetemeka sana na nilimpatia ishara ya kwamba atulie kabisa!.Basi nadhani yule mwanamke alihisi jambo maana niliona anamsogelea Ema akawa kama anamtisha aone kama amemuona,sasa alipoendelea kumtisha Ema nikaona anaweza kupiga kelele,nikaanza kumpigisha Ema stori ili kupotezea ile hali!.

Mimi "Mwanangu wewe piga kimya kabisa wala usimfanye chochote yule demu"

Ema "Yule demu mwanangu anazingua kinoma"

Mimi "Halafu Headmaster alisema ukamuamshe aandae yale masomo"

Ema "Halafu kweli umenikumbusha,ngoja nikamuamshe!"

Sasa wakati tunaongea yule mwanamke alirudi kwa wenzie na wakaendelea kushangaa shangaa,tulichokifanya na Ema pale kwa ule muda mfupi ni hakika walidhani hatuwaoni kumbe lengo lilikuwa ni kumuondolea Ema uoga na kuwapoteza maboya!.
Ema aliamka akatoka kwenda kumgongea Headmaster chumbani kwake ili aje ajionee!,sasa wakati Ema ameondoka,nilianza kujipigisha mruzi wa uongo na kweli ili kuikabili ile hali kwasababu ilikuwa inatisha si kitoto!..

Headmaster "Umughaka tacho omahe"

Baba alipotoka nje aliniita kwa kilugha nikawa nimetoka nje,sasa alianza kutueleza ya kwamba tusishituke na tuendelee kuwa watulivu,alitwambia Ema achukue madaftari tuelekee wote sebuleni ili iwe rahisi kuwakabili,mimi nilimwambia wao wakae sebuleni na mimi nirudi chumbani kukaa karibu na kibuyu kwa kazi maalumu!.
Basi wale watu wakawa wamepotea ghafla mle chumbani!,nilitoka nje kwenda kumwambia Headmaster.

Headmaster "Ngoja tusubiri,yawezekana wakawa wameshituka"

Mimi "Lazima warudi"

Headmaster "Halafu mbona yule mzee hayupo?"

Mimi "Uenda leo kawaagiza hawa"

Wakati tukiwa tunaendelea kuongea pale,Maza mdogo akamwambia Headmaster kwa kikurya kwamba,wale watu wako kule chumbani kwake na anawaona,Headmaster akamwambia atulie na asipige kelele!.Sasa tukiwa tunaendelea kuongea pale sebuleni huku Headmaster akijifanya kumpigisha Ema pindi,tukasikia kishindo kikubwa tena pale uani!.

Haukupita muda akawa ametokea yule mzee makono akiwa na usinga mkononi huku akiwa uchi kama wenzie!,akaja mpaka pale sebuleni huku tukiendelea kumpimia tu!,aliendelea kuangaza huku na huko na hatimaye akawa ameingia mle chumbani kwa Headmaster.Basi baada ya kuingia chumba cha Headmaster,Headmaster aliinuka kwa ghadhabu huku akisema "Lero n'uramanye uwe tombanyoko" (Leo utanitambua).

Sasa Headmaster alipoingia chumbani alijifanya kuongea na mkewe huku wakiwatazama,sasa nadhani mzee makono aliwaambia wale watu waende wakawalete watu wa kwenda kulima ili wakifika watuunganishe na sisi tuondoke!,wale watu watatu walitoweka wakamuacha mzee makono mle chumbani akitaka kufanya mambo yake ili amchukue Headmaster kama kawaida aje atuunganishe na sisi tuelekee kwenye kilimo cha usiku kisichokuwa na tija!.

Wale watu walipotoweka tu na mzee makono kubaki mwenyewe,Headmaster alichukua kile kibuyu alichopewa na mama yake Monica akakifungua,alipokifungua tu!,yule mzee akaanza kucheza kwa kuzunguka mle chumbani kama mwendawazimu!.Headmaster alituita tukaingia kumtazama,yaani kuna muda nilianza kumuonea huruma maana alikuwa kama amepagawa kwa kushikwa ugoni.

Kadiri muda ulivyokuwa ukienda,wale watu waliotumwa na mzee makono hawakurudi kabisa na nadhani watakuwa walishituka mapema!.Ile hali ilifanya maza mdogo kutoka kule chumbani akabaki mzee makono akizunguka chumba kizima kama mwendawazimu.Usiku huko hakuna mtu aliyepata usingizi kabisa,tumekuja kushangaa imefika saa 11 alfajiri bila kujua!.
Sasa ilipofika saa 12 asubuhi,Mama yake Monica alikuja akiwa na wale kina mama,alihuzunika sana kwanini tuliamua kuwaachia wale watu watatu wakaondoka!.

Mama Monica "Mwalimu nilikwambia,nadhani sasa unaniamini"

Headmaster "Sikuzote Msukuma nakuamini,si leo tu!".

Mama Monica "Kwanini mmewaachia wale washenzi?"

Headmaster "Wameondoka wenyewe"

Mama Monica "Nilikwambia wakifika tu,ungefungua kibuyu"

Headmaster "Nilipoingia chumbani kufungua kibuyu wakawa wameondoka akabaki mzee lameki"

Mama Monica "watasimuliana,hakuna kilichoharibika"

Aliendelea "Haya sema,unataka tumfanye nini huyu mzee"

Headmaster "Nadhani kama kuna uwezo muondolee uwezo wake asije akaponyoka halafu mengine utaniachia mimi"

Mama Monica "Huyu ameshakwisha,hapa hawezi kukuponyoka kamwe"

Aliendelea "Mimi namshughurikia halafu nakuachia wewe utajua cha kumfanya".

Basi mama yake Monica alimsogelea yule mzee akachukua ule usinga kisha akamvua shanga alizokuwa amejivika kuanzia begani kuteremkia kiunoni!,baada ya hapo kuna dawa alimpatia Headmaster akamwambia kukishapambazuka vizuri atampaka ile dawa na kisha atamuondoa mle ndani!.Mama yake Monica na wale kina mama waliondoka wakawa wamemuacha mzee makono humo ndani akizinguka kama mwehu!.

Kulipopambazuka,Headmaster alielekea kwa mwenyekiti wa kijiji na kutaka yowe ipigwe karibia kijiji kizima ili wananzengo wahalifiwe ya kwamba kulikuwa kuna tukio kubwa la kushangaza!,Basi yowe ilipigwa na watu wakawa wanakuja pale nyumbani huku wengine mikoni wakiwa wameshika mapanga na mafimbo!.Haukupita muda mrefu watu wakawa wamejazana pale nyumbani huku wengine wakichungulia dirishani wakishangaa lile tukio!.

Ilipofika mida ya saa 3 Asubuhi baada ya watu kujazana pale nyumbani,Headmaster alifanya kama alivyoambiwa afanye na mama yake Monica,baada ya kupakwa dawa yule mzee alikurupuka akawa anashangaa sana!,alikuwa akizunguka kitafuta usinga wake lakini hakuuona,ndipo Headmaster aliamrishwa na wananzengo ya kwamba amtoe yule mzee nje ya nyumba ili akapambane na viboko vilivyokosa huruma!.

Yule mwenyekiti aliamuru yule mzee avishwe nguo hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji lakini wananzengo wakagoma,walisema inapaswa atembezwe kijiji kizima huku akila mboko na inapaswa siku hiyo hiyo ahame kijiji!.

Basi nakumbuka Headmaster alimuagiza Ema akalete viboko ili aanze nae mle ndani kwasababu alikuwa akimtafuta sana,viboko vilipoletwa kiukweli yule mzee alichezea kiasi kwamba sikutaka hata kuangalia,viboko vilipozidi aliamua kutoka ndani spidi akikimbilia nje,kufika nje wananzengo wakamdaka nako wakaanza kumsulubisha!.
Alitembezwa kijiji kizima huku akiwa uchi kama alivyozaliwa,kiukweli lilikuwa ni tukio la aibu mno!,sasa walipomfikisha kwake wananzengo hawakutaka mjadala,walimwambia avae nguo kisha atoke,alipotoka waliwasha moto nyumba yake na kila kitu kiliteketea kwa moto!.

Baada ya pale alirudishwa serikali ya kijiji na kutakiwa apotee kwenye kile kijiji ndani ya masaa 2!,hakutakiwa kubaki pale na wananzengo walimwambia watamuua endapo angebaki kwa siku hiyo!.

Lile tukio lilivuta hisia kubwa sana pale kijijini na kiukweli lilimpatia Headmaster ujiko na heshima sana ingawaje mimi ndiye niliyepambana sana mpaka kufikia ile hali.Headmaster aliogopeka sana tangu siku ile lile tukio litokee na hakukuwahi tena kuwa na mambo ya ajabu pale nyumbani.

Headmaster kwa baadae alihama ile shule na kuhamia huko Biharamulo ambako amejenga na anaishi hadi leo,mimi niliondoka na kurudi nyumbani kisha kuelekea shuleni Advance!.

Ema yupo hapo Shinyanga anauza duka la vipuri vya magari,amejenga na anaishi hapo hapo shinyanga.

Monica kuna wakati niliambiwa yupo Mwanza ila sijajua ni Mwanza sehemu gani!,kuna mtu nilikutana nae wa pale kijijini akawa ameniambia hivyo,kwasababu baada ya mimi kuondoka pale kijijini sikurudi tena hivyo tukawa tumepotezana na mpenzi wangu huyo!.

Mimi kwasasa nipo Dar es salaam napambana na maisha ya kukimbizana!,nina kiboda boda changu japo kimekwisha lakini tunapambana na maisha!.Kijiwe changu huwa ni hapo Bunju ndugu zangu!.

MWISHO.
Mungu akubariki sana damu yangu akuzidishie ridhki halali
You made my day
 
Ila hii story ni uongo mtupu, kuna mtoto wa kike atajiamini kutembea usiku ivo?, na anatokaje nyumbani kwao bila wazazi kuskia?
Nyie wototo mliozaliwa na kukulia mjini nyie mnatabu sana dogo ipo siku utatoka mjin alaf utakuja kutubu hapa wee acha tu mim mwenyew nilitoka sinza nikaendaga kusoma shinyanga vijijin huko nikakubali mim ni kama dem wa mjin mbele ya wanawake wa kule asee
 
Back
Top Bottom