Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niliwahi kushuhudia miaka ya nyuma Geita huko vijijini kuna mwanamke alipambana na majambazi wenye silaha na yakatelekeza bundukiUkizaliwa na kukulia dar utakua sahihi , tembea huko vijijini kuna wanawake majasiri kuliko wanaume. Acha kabisa kuna experience zinapatikana huko bush huwezi amini. Kwa watu waliozaliwa dar ni ngumu sana kuelewa . Pia miaka hii wazazi hawana utamaduni kuwapeleka watoto mikoani ndio tatizo . Ungekua kila mwaka likizo unaenda kijijini ungeamini
Daah stori tamu sana, ila hapo kwa Monika bado sijaamini km umeachana nae kirahiv hivyo wakati ni wachawi wa kiwango cha SGRTulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 25.
Baada ya Headmaster kutoka kuwasindikiza wageni,tuliamua kukaa kikao cha kifamilia na kuzungumza mambo kadhaa yaliyotuweka sawa.Sasa kila mtu alielekea chumbani kulala,baba mdogo na mkewe waliingia chumbani kwao,mimi na Ema pia tuliingia chumbani kwetu kulala.
Siku hiyo mle chumbani hakuna aliyepata usingizi kabisa,kabla ya kulala nakumbuka tulipakaa usoni dawa aliyokuwa ametupatia mama yake Monica,pia tukashikiria na zile hirizi mkononi kama alivyokuwa ameagiza tufanye!.Kadri muda ulivyokuwa ukisonga tuliona kimya,mimi nilianza kupitiwa na usingizi maana nilikuwa nimechoka sana!,kumbe wakati mimi napitiwa na usingizi,Ema yeye alikuwa macho kabisa na jamaa alikuwa na shauku ya kuona ni kitu gani kingetokea!.
Sasa ilipofika mida ya saa 8 usiku,nilishitushwa na Ema akiniamsha!.
Ema "Umesikia hicho kishindo?".
Mimi "Hapana,kishindo cha kitu gani?"
Ema "Kutakuwa na kitu nadhani!"
Ema alikuwa akiniambia kwa sauti ndogo kabisa na yenye uoga ndani yake!.
Mimi "Nyamaza"
Niliamka kitandani nikaenda kuwasha taa,nilifahamu kabisa kile kishindo Ema alichosikia hakikuwa cha kawaida na uenda wale jamaa wakawa wamekuja kama kawaida yao,kiukweli mimi kwa upande wangu sikuwa kabisa na hofu kwasababu kwa siku chache nilikuwa nimeshazoea yale mazingira ya kuwaona wachwawi laivu!.Nilimwambia na kumbusha Ema ya kwamba chochote atakachokiona asipige kelele wala kushituka!.
Haukupita muda,mara ghafla wakaonekana watu watatu wakiwa wamesimama mle chumbani huki wakiwa uchi kama walivyozaliwa,watu wale safari hii walikuja wawili wanaume na mmoja akiwa mwanamke!.Niliwaangalia kwa kuibia kama vile sielewi chochote!,Ema alikuwa akitetemeka sana na nilimpatia ishara ya kwamba atulie kabisa!.Basi nadhani yule mwanamke alihisi jambo maana niliona anamsogelea Ema akawa kama anamtisha aone kama amemuona,sasa alipoendelea kumtisha Ema nikaona anaweza kupiga kelele,nikaanza kumpigisha Ema stori ili kupotezea ile hali!.
Mimi "Mwanangu wewe piga kimya kabisa wala usimfanye chochote yule demu"
Ema "Yule demu mwanangu anazingua kinoma"
Mimi "Halafu Headmaster alisema ukamuamshe aandae yale masomo"
Ema "Halafu kweli umenikumbusha,ngoja nikamuamshe!"
Sasa wakati tunaongea yule mwanamke alirudi kwa wenzie na wakaendelea kushangaa shangaa,tulichokifanya na Ema pale kwa ule muda mfupi ni hakika walidhani hatuwaoni kumbe lengo lilikuwa ni kumuondolea Ema uoga na kuwapoteza maboya!.
Ema aliamka akatoka kwenda kumgongea Headmaster chumbani kwake ili aje ajionee!,sasa wakati Ema ameondoka,nilianza kujipigisha mruzi wa uongo na kweli ili kuikabili ile hali kwasababu ilikuwa inatisha si kitoto!..
Headmaster "Umughaka tacho omahe"
Baba alipotoka nje aliniita kwa kilugha nikawa nimetoka nje,sasa alianza kutueleza ya kwamba tusishituke na tuendelee kuwa watulivu,alitwambia Ema achukue madaftari tuelekee wote sebuleni ili iwe rahisi kuwakabili,mimi nilimwambia wao wakae sebuleni na mimi nirudi chumbani kukaa karibu na kibuyu kwa kazi maalumu!.
Basi wale watu wakawa wamepotea ghafla mle chumbani!,nilitoka nje kwenda kumwambia Headmaster.
Headmaster "Ngoja tusubiri,yawezekana wakawa wameshituka"
Mimi "Lazima warudi"
Headmaster "Halafu mbona yule mzee hayupo?"
Mimi "Uenda leo kawaagiza hawa"
Wakati tukiwa tunaendelea kuongea pale,Maza mdogo akamwambia Headmaster kwa kikurya kwamba,wale watu wako kule chumbani kwake na anawaona,Headmaster akamwambia atulie na asipige kelele!.Sasa tukiwa tunaendelea kuongea pale sebuleni huku Headmaster akijifanya kumpigisha Ema pindi,tukasikia kishindo kikubwa tena pale uani!.
Haukupita muda akawa ametokea yule mzee makono akiwa na usinga mkononi huku akiwa uchi kama wenzie!,akaja mpaka pale sebuleni huku tukiendelea kumpimia tu!,aliendelea kuangaza huku na huko na hatimaye akawa ameingia mle chumbani kwa Headmaster.Basi baada ya kuingia chumba cha Headmaster,Headmaster aliinuka kwa ghadhabu huku akisema "Lero n'uramanye uwe tombanyoko" (Leo utanitambua).
Sasa Headmaster alipoingia chumbani alijifanya kuongea na mkewe huku wakiwatazama,sasa nadhani mzee makono aliwaambia wale watu waende wakawalete watu wa kwenda kulima ili wakifika watuunganishe na sisi tuondoke!,wale watu watatu walitoweka wakamuacha mzee makono mle chumbani akitaka kufanya mambo yake ili amchukue Headmaster kama kawaida aje atuunganishe na sisi tuelekee kwenye kilimo cha usiku kisichokuwa na tija!.
Wale watu walipotoweka tu na mzee makono kubaki mwenyewe,Headmaster alichukua kile kibuyu alichopewa na mama yake Monica akakifungua,alipokifungua tu!,yule mzee akaanza kucheza kwa kuzunguka mle chumbani kama mwendawazimu!.Headmaster alituita tukaingia kumtazama,yaani kuna muda nilianza kumuonea huruma maana alikuwa kama amepagawa kwa kushikwa ugoni.
Kadiri muda ulivyokuwa ukienda,wale watu waliotumwa na mzee makono hawakurudi kabisa na nadhani watakuwa walishituka mapema!.Ile hali ilifanya maza mdogo kutoka kule chumbani akabaki mzee makono akizunguka chumba kizima kama mwendawazimu.Usiku huko hakuna mtu aliyepata usingizi kabisa,tumekuja kushangaa imefika saa 11 alfajiri bila kujua!.
Sasa ilipofika saa 12 asubuhi,Mama yake Monica alikuja akiwa na wale kina mama,alihuzunika sana kwanini tuliamua kuwaachia wale watu watatu wakaondoka!.
Mama Monica "Mwalimu nilikwambia,nadhani sasa unaniamini"
Headmaster "Sikuzote Msukuma nakuamini,si leo tu!".
Mama Monica "Kwanini mmewaachia wale washenzi?"
Headmaster "Wameondoka wenyewe"
Mama Monica "Nilikwambia wakifika tu,ungefungua kibuyu"
Headmaster "Nilipoingia chumbani kufungua kibuyu wakawa wameondoka akabaki mzee lameki"
Mama Monica "watasimuliana,hakuna kilichoharibika"
Aliendelea "Haya sema,unataka tumfanye nini huyu mzee"
Headmaster "Nadhani kama kuna uwezo muondolee uwezo wake asije akaponyoka halafu mengine utaniachia mimi"
Mama Monica "Huyu ameshakwisha,hapa hawezi kukuponyoka kamwe"
Aliendelea "Mimi namshughurikia halafu nakuachia wewe utajua cha kumfanya".
Basi mama yake Monica alimsogelea yule mzee akachukua ule usinga kisha akamvua shanga alizokuwa amejivika kuanzia begani kuteremkia kiunoni!,baada ya hapo kuna dawa alimpatia Headmaster akamwambia kukishapambazuka vizuri atampaka ile dawa na kisha atamuondoa mle ndani!.Mama yake Monica na wale kina mama waliondoka wakawa wamemuacha mzee makono humo ndani akizinguka kama mwehu!.
Kulipopambazuka,Headmaster alielekea kwa mwenyekiti wa kijiji na kutaka yowe ipigwe karibia kijiji kizima ili wananzengo wahalifiwe ya kwamba kulikuwa kuna tukio kubwa la kushangaza!,Basi yowe ilipigwa na watu wakawa wanakuja pale nyumbani huku wengine mikoni wakiwa wameshika mapanga na mafimbo!.Haukupita muda mrefu watu wakawa wamejazana pale nyumbani huku wengine wakichungulia dirishani wakishangaa lile tukio!.
Ilipofika mida ya saa 3 Asubuhi baada ya watu kujazana pale nyumbani,Headmaster alifanya kama alivyoambiwa afanye na mama yake Monica,baada ya kupakwa dawa yule mzee alikurupuka akawa anashangaa sana!,alikuwa akizunguka kitafuta usinga wake lakini hakuuona,ndipo Headmaster aliamrishwa na wananzengo ya kwamba amtoe yule mzee nje ya nyumba ili akapambane na viboko vilivyokosa huruma!.
Yule mwenyekiti aliamuru yule mzee avishwe nguo hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji lakini wananzengo wakagoma,walisema inapaswa atembezwe kijiji kizima huku akila mboko na inapaswa siku hiyo hiyo ahame kijiji!.
Basi nakumbuka Headmaster alimuagiza Ema akalete viboko ili aanze nae mle ndani kwasababu alikuwa akimtafuta sana,viboko vilipoletwa kiukweli yule mzee alichezea kiasi kwamba sikutaka hata kuangalia,viboko vilipozidi aliamua kutoka ndani spidi akikimbilia nje,kufika nje wananzengo wakamdaka nako wakaanza kumsulubisha!.
Alitembezwa kijiji kizima huku akiwa uchi kama alivyozaliwa,kiukweli lilikuwa ni tukio la aibu mno!,sasa walipomfikisha kwake wananzengo hawakutaka mjadala,walimwambia avae nguo kisha atoke,alipotoka waliwasha moto nyumba yake na kila kitu kiliteketea kwa moto!.
Baada ya pale alirudishwa serikali ya kijiji na kutakiwa apotee kwenye kile kijiji ndani ya masaa 2!,hakutakiwa kubaki pale na wananzengo walimwambia watamuua endapo angebaki kwa siku hiyo!.
Lile tukio lilivuta hisia kubwa sana pale kijijini na kiukweli lilimpatia Headmaster ujiko na heshima sana ingawaje mimi ndiye niliyepambana sana mpaka kufikia ile hali.Headmaster aliogopeka sana tangu siku ile lile tukio litokee na hakukuwahi tena kuwa na mambo ya ajabu pale nyumbani.
Headmaster kwa baadae alihama ile shule na kuhamia huko Biharamulo ambako amejenga na anaishi hadi leo,mimi niliondoka na kurudi nyumbani kisha kuelekea shuleni Advance!.
Ema yupo hapo Shinyanga anauza duka la vipuri vya magari,amejenga na anaishi hapo hapo shinyanga.
Monica kuna wakati niliambiwa yupo Mwanza ila sijajua ni Mwanza sehemu gani!,kuna mtu nilikutana nae wa pale kijijini akawa ameniambia hivyo,kwasababu baada ya mimi kuondoka pale kijijini sikurudi tena hivyo tukawa tumepotezana na mpenzi wangu huyo!.
Mimi kwasasa nipo Dar es salaam napambana na maisha ya kukimbizana!,nina kiboda boda changu japo kimekwisha lakini tunapambana na maisha!.Kijiwe changu huwa ni hapo Bunju ndugu zangu!.
MWISHO.
Weka no ya simu sasa tukutafuteTulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 25.

Kuna mdingi home alikuwa anakula embe dodo 60, Tena sio mashindano. Anaokota anakaa chini anayalaka Kisha anaendelea na shughuli zake.Kwanza kabisa nawashukuru sana ndugu zangu wote mnaopongeza uzi huu na kutoa shukurani kedekede!,ningependa mtambue ya kwamba kwangu pesa si kipaumbele ingawaje nazihitaji pesa ili kufikia vipaumbele vyangu!.Wengi walitaka angalau nitoze kiasi cha fedha,ndugu zangu sijaja hapa JF kwa ajili ya fedha,ingawa fedha ikinifuata siwezi kuikataa kwasababu pia tunakesha tukiitafuta!,Lengo la huu uzi ni kukufunza,kukuburudisha na kukuelimisha!.Nilihitaji watu wapate shule kwa yale wengine tuliyopitia huko vijijini!.
Sasa Kuna mambo baadhi naona yamewatatanisha watu au wamesshindwa kuelewa!.
1.Kulipia kiasi cha Tsh 100 kwenye banda,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani.
2.Monica kutembea usiku ingawaje ni mtoto wa kike.
3.Msukuma kumiliki Ng'ombe zaidi ya elfu 10,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.
4.Kucharazwa viboko mbele ya wanafunzi kwa kosa la nyumbani,pia vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.
NAOMBA KABLA SIJAJIBU NITOE KISA KIFUPI!.
Mwaka 2000 kuna kaka yangu mtoto wa baba mkubwa kazi yake ilikuwa kuzibua vyoo(mzibua vyoo)Ingawa sikuhizi ameacha,kazi hii ilimpatia pesa za kutosha kwa miaka hiyo kwasababu pale wilayani ni kampuni yao ndiyo ilikuwa ikifahamika kwa shughuli hiyo!.
Sasa nakumbuka siku moja Mzee wangu alimuita yeye na watu wa kampuni yake pale nyumbani kuja kuzibua chemba ambayo ilikuwa kwa ajili ya nyumba ya wapangaji!,pamoja na kuja kuzibua ile chemba lakini pia walitakiwa kuchora ramani kwa ajili ya kujenga chemba(shimo)nyingine!..Mzee alitaka yale mashimo yawe na uwezo wa kupokea mzigo mkubwa na ndiyo maana akataka shimo lingine liongezwe!.
Basi kazi ya kuchora ramani ikaanza,ilikuwa mida ya saa 1 asubuhi!,walikamilisha kuchora ramani saa 1:20 Asubuhi,sasa kazi rasmi ya kuchoronga na kuchimba shimo jipya ikaanza!.Sasa wakati shimo linachimbwa nakumbuka tukawa tunapiga stori za kufa mtu!,wakati wao wanachimba mimi kazi yangu ilikuwa ni kutizama na kuchangia kwenye stori walizokuwa wakipiga!,ilikuwa wakihamia kwenye mademu na mimi najifanya kuchangia kana kwamba hao mademu hata ninaweza kuwamudu!,walikuwa wakihamia kwenye siasa na mimi nimo!,wakienda kwenye habari za magari na mimi nimo!.
Sasa kuna muda mada za kaka yangu huyo na wale jamaa wenzie zikaamia kwenye vyakula,na mimi nikawa mchangiaji!.
Brother "Yanii muda huu nikipata donati 10 na vikombe angalau vitatu vya chai ya maziwa ndipo moyo wangu utasuuzika"
Basi baada ya kusikia ile kauli umughaka mimi nikaanza kumzodoa brother huku nikibisha,sasa kiukweli kukawa na ubishani mkubwa mno!.
Brother alikuwa akisema kwamba anao uwezo wa kumaliza Donati 10 na vikombe 3 vya chai ya maziwa!,mimi nilikuwa ninabisha,wale wenzie wakanitaka tusiandikie mate wakati wino upo!.wakapendekeza tuweke dau la kila mmoja shilingi elfu 2,kwa mwaka huo nadhani ndugu zangu mtaelewa namna shilingi elfu 2 ilivyokuwa na thamani!.
Sasa tukakubaliana ya kwamba,ikifika saa 5 asubuhi tuelekee mjini kwa ajili ya kumnunulia brother donati 10 na vikombe vitatu vya chai ya maziwa,donati wakati huo kwa moja ilikuwa inauzwa Tsh 200,na chai ya maziwa kikombe ilikuwa inauzwa Tsh 100,na endapo asipoweza kumaliza basi angelipia hela niliyokuwa nimenunulia vitafunwa vile pale mgahawani na angenipatia Tsh elfu 2 kama tulivyokubaliana!.
Ilipofika mida hiyo kweli tukaelekea mjini kwa ajili ya kuupa muda na nafasi kwa ajili ya ule ubishi wangu kwa brother!.Niliagiza vile vitafunwa kama tulivyokuwa tumekubaliana!.
Ilikuwa ni ajabu kumuona brother akimaliza zile donati ndani ya muda mfupi kuliko nilivyodhani!,vile vikombe vya chai ya maziwa vilimpungua ikabidi nimuongezee vingine vitatu!,wakati huo kamaliza zile donati 10 ambazo mle kwenye mgahawa kila mtu alibaki kumshangaa kama ni binadamu wa kawaida au alikuwa kiumbe wa ajabu,cha kushangaza pamoja na kumaliza lakini alidai bado hajashiba hivyo alisema atangojea nyumbania ugali uive ili ajazilizie mapengo ya nafasi tumboni!.
Pamoja na yote lakini pia nilimpatia Tsh elfu 2 kama ilivyokuwa ahadi yetu.
SASA NILICHOTAKA KUSEMA NI NINI?
Tangu siku hiyo huwa sibishi ovyo ovyo tu kama punguani!.Yaani tumbo lako halafu nikubishie?,yaani mimi kama nakula robo wali nianze kubisha wewe kumaliza Nusu wali?,uenda nitakuwa mwendawazimu!.
Sasa nimeamua kuutoa huo mfano ili watu wajifunze jambo,usibishe jambo lolote kama hujawahi kupitia!,yaani wewe uzaliwe Magomeni ambako unashindia kutwa dagaa mchele halafu unambishia mtu aliyekulia huko UKILI GURU anayeshindia mihogo kwamba hawezi kuilima!.
Ikiwa kuna maisha hujawahi kuyaishi nikutaadharishe usije kubisha kwasababu watu watabaki kukushangaa na utaoneka Kituko mbele ya wanaume!.
1.Mimi binafsi nimeanza kushangilia mpira kwenye TV mnamo mwaka 1996 tena wakati huo nilikuwa naipenda sana Liverpool,ila ilipofika mwaka 1998 nikaanza kushabikia timu ya Arsenal!.Sasa mwaka 2004 ninaposema bandani nilikuwa nalipa Tsh 100 naamanisha!,siyo kwamba naigiza ndugu zangu!,na ndiyo maana nikamuomba huyo jamaa anayebisha yeye aje atuambie huo mwaka huko alikokuwa alikuwa analipa kiasi gani?,kama hana majibu basi atulie aache ubishi!,haiwezekani wewe uje uanze kuangalia mpira mwaka 2013 halafu ubishie watu tulioanza kuingia mabandani mwaka 1996!.
2.Suala la Monica kutembea usiku eti mtu anashangaa!,yaani leo mabinti kulala nje na kukesha kwa wanaume unadhani ni jambo jipya?,yaani binti ambaye kwao walikuwa washirikina na hakuwa na baba,yeye kutembea usiku unaona kuna uongo?,watanzania ni nani katuroga?,Mbona alivyolala na Ema pale kwa rafiki yake Jack usiku kucha mpaka kupelekea ugomvi na Deborah hamkuhoji?,mmeona muhoji mimi kukutana naye usiku kule mnadani!,Aiseee kuna sehemu vijana wa hili taifa wanapaswa kurekebisha ili mambo yaende sawa!.
3 Suala la Msukuma kumiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10 mwaka 2003-2004 mtu anabisha,huyohuyo mtu ukimuuliza kwamba amewahi kufika Tabora au sehemu nyingine ya usukumani atakwambia bado,halafu anabisha!,na huyu ni msomi mzima anashangaa kabisa!.Atahoji hadi sisi kupewa lita 5 za maziwa bure kila siku pale kwa Headmaster atakwambia ni uongo!,Kama hujawahi kutembea kwenye hii nchi nikuombe usije nyanyua mdomo wako ukabisha!.Kuna mtu ukimwambia pale Geita na Mwanza kuna watu wanahela chafu kuliko huyo anayejiita Mo Dewji bado watakuja hapa kubisha kana kwamba huyo Mo ni baba yake!.
4.Kwamba mimi kuchwapwa mbele ya wanafunzi ilikuwa ni stori ya kutunga!,Hii nchi kuna watu wanashida kubwa mno!,kwamba unataka kusema kwakuwa wewe umekulia na kusomea mjini unadhani watu wote tumesomea mjini?,Kuchwapwa mbele ya kadamnasi haikuwa mjadala!,na wala si mbele ya wanafunzi tu!,yaani stiki ulikuwa unakung'utwa hata sokoni kama ukileleta ukora!,Vijana kama hamjui vitu tuambieni tuwaelekeze muweze kuvifahamu.
Mimi nimesoma shule ya kata isiyokuwa na maabara(laboratory)masomo ya sayansi (pcb) na nilifaulu ufaulu mzuri tu wa dvs 2 sema baadae nilifeli form 6 kwasababu ya mapenzi ya mwanamke wa kitanga.Sasa hivi vijana nyie hamuwezi kufaulu masomo ya sayansi bila maabara!.
KAMA HUJAPITIA MAISHA FULANI USISIMAME NA TUMBO LAKO UKAANZA KUBISHA MBELE YA WANAUME,UTATIA AIBU!.
NI HAYO TU.
Thanx mkuu kwa kunijibu kwa ufasahaMkuu Kalpana wala hakupata mimba,pale mama yake alikuwa tu anasema mimi na Monica tayari ni wapenzi na alikuwa anachukia mtu yeyote kutufanyia vimbwanga kwasababu aliamini tungemletea mjukuu,hivyo alisema angetulinda kwa gharama yeyote,Lakini Monica wala hakuwa na ujauzito wangu!.
mwaka 2003 wilaya ya kasulu mkoani kigoma kiingilio cha mpira kwa mechi za ulaya ilikuwa shilingi 100 za kitanzaniaKwanza kabisa nawashukuru sana ndugu zangu wote mnaopongeza uzi huu na kutoa shukurani kedekede!,ningependa mtambue ya kwamba kwangu pesa si kipaumbele ingawaje nazihitaji pesa ili kufikia vipaumbele vyangu!.Wengi walitaka angalau nitoze kiasi cha fedha,ndugu zangu sijaja hapa JF kwa ajili ya fedha,ingawa fedha ikinifuata siwezi kuikataa kwasababu pia tunakesha tukiitafuta!,Lengo la huu uzi ni kukufunza,kukuburudisha na kukuelimisha!.Nilihitaji watu wapate shule kwa yale wengine tuliyopitia huko vijijini!.
Sasa Kuna mambo baadhi naona yamewatatanisha watu au wamesshindwa kuelewa!.
1.Kulipia kiasi cha Tsh 100 kwenye banda,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani.
2.Monica kutembea usiku ingawaje ni mtoto wa kike.
3.Msukuma kumiliki Ng'ombe zaidi ya elfu 10,vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.
4.Kucharazwa viboko mbele ya wanafunzi kwa kosa la nyumbani,pia vijana wa 2000 wanasema haiwezekani!.
NAOMBA KABLA SIJAJIBU NITOE KISA KIFUPI!.
Mwaka 2000 kuna kaka yangu mtoto wa baba mkubwa kazi yake ilikuwa kuzibua vyoo(mzibua vyoo)Ingawa sikuhizi ameacha,kazi hii ilimpatia pesa za kutosha kwa miaka hiyo kwasababu pale wilayani ni kampuni yao ndiyo ilikuwa ikifahamika kwa shughuli hiyo!.
Sasa nakumbuka siku moja Mzee wangu alimuita yeye na watu wa kampuni yake pale nyumbani kuja kuzibua chemba ambayo ilikuwa kwa ajili ya nyumba ya wapangaji!,pamoja na kuja kuzibua ile chemba lakini pia walitakiwa kuchora ramani kwa ajili ya kujenga chemba(shimo)nyingine!..Mzee alitaka yale mashimo yawe na uwezo wa kupokea mzigo mkubwa na ndiyo maana akataka shimo lingine liongezwe!.
Basi kazi ya kuchora ramani ikaanza,ilikuwa mida ya saa 1 asubuhi!,walikamilisha kuchora ramani saa 1:20 Asubuhi,sasa kazi rasmi ya kuchoronga na kuchimba shimo jipya ikaanza!.Sasa wakati shimo linachimbwa nakumbuka tukawa tunapiga stori za kufa mtu!,wakati wao wanachimba mimi kazi yangu ilikuwa ni kutizama na kuchangia kwenye stori walizokuwa wakipiga!,ilikuwa wakihamia kwenye mademu na mimi najifanya kuchangia kana kwamba hao mademu hata ninaweza kuwamudu!,walikuwa wakihamia kwenye siasa na mimi nimo!,wakienda kwenye habari za magari na mimi nimo!.
Sasa kuna muda mada za kaka yangu huyo na wale jamaa wenzie zikaamia kwenye vyakula,na mimi nikawa mchangiaji!.
Brother "Yanii muda huu nikipata donati 10 na vikombe angalau vitatu vya chai ya maziwa ndipo moyo wangu utasuuzika"
Basi baada ya kusikia ile kauli umughaka mimi nikaanza kumzodoa brother huku nikibisha,sasa kiukweli kukawa na ubishani mkubwa mno!.
Brother alikuwa akisema kwamba anao uwezo wa kumaliza Donati 10 na vikombe 3 vya chai ya maziwa!,mimi nilikuwa ninabisha,wale wenzie wakanitaka tusiandikie mate wakati wino upo!.wakapendekeza tuweke dau la kila mmoja shilingi elfu 2,kwa mwaka huo nadhani ndugu zangu mtaelewa namna shilingi elfu 2 ilivyokuwa na thamani!.
Sasa tukakubaliana ya kwamba,ikifika saa 5 asubuhi tuelekee mjini kwa ajili ya kumnunulia brother donati 10 na vikombe vitatu vya chai ya maziwa,donati wakati huo kwa moja ilikuwa inauzwa Tsh 200,na chai ya maziwa kikombe ilikuwa inauzwa Tsh 100,na endapo asipoweza kumaliza basi angelipia hela niliyokuwa nimenunulia vitafunwa vile pale mgahawani na angenipatia Tsh elfu 2 kama tulivyokubaliana!.
Ilipofika mida hiyo kweli tukaelekea mjini kwa ajili ya kuupa muda na nafasi kwa ajili ya ule ubishi wangu kwa brother!.Niliagiza vile vitafunwa kama tulivyokuwa tumekubaliana!.
Ilikuwa ni ajabu kumuona brother akimaliza zile donati ndani ya muda mfupi kuliko nilivyodhani!,vile vikombe vya chai ya maziwa vilimpungua ikabidi nimuongezee vingine vitatu!,wakati huo kamaliza zile donati 10 ambazo mle kwenye mgahawa kila mtu alibaki kumshangaa kama ni binadamu wa kawaida au alikuwa kiumbe wa ajabu,cha kushangaza pamoja na kumaliza lakini alidai bado hajashiba hivyo alisema atangojea nyumbania ugali uive ili ajazilizie mapengo ya nafasi tumboni!.
Pamoja na yote lakini pia nilimpatia Tsh elfu 2 kama ilivyokuwa ahadi yetu.
SASA NILICHOTAKA KUSEMA NI NINI?
Tangu siku hiyo huwa sibishi ovyo ovyo tu kama punguani!.Yaani tumbo lako halafu nikubishie?,yaani mimi kama nakula robo wali nianze kubisha wewe kumaliza Nusu wali?,uenda nitakuwa mwendawazimu!.
Sasa nimeamua kuutoa huo mfano ili watu wajifunze jambo,usibishe jambo lolote kama hujawahi kupitia!,yaani wewe uzaliwe Magomeni ambako unashindia kutwa dagaa mchele halafu unambishia mtu aliyekulia huko UKILI GURU anayeshindia mihogo kwamba hawezi kuilima!.
Ikiwa kuna maisha hujawahi kuyaishi nikutaadharishe usije kubisha kwasababu watu watabaki kukushangaa na utaoneka Kituko mbele ya wanaume!.
1.Mimi binafsi nimeanza kushangilia mpira kwenye TV mnamo mwaka 1996 tena wakati huo nilikuwa naipenda sana Liverpool,ila ilipofika mwaka 1998 nikaanza kushabikia timu ya Arsenal!.Sasa mwaka 2004 ninaposema bandani nilikuwa nalipa Tsh 100 naamanisha!,siyo kwamba naigiza ndugu zangu!,na ndiyo maana nikamuomba huyo jamaa anayebisha yeye aje atuambie huo mwaka huko alikokuwa alikuwa analipa kiasi gani?,kama hana majibu basi atulie aache ubishi!,haiwezekani wewe uje uanze kuangalia mpira mwaka 2013 halafu ubishie watu tulioanza kuingia mabandani mwaka 1996!.
2.Suala la Monica kutembea usiku eti mtu anashangaa!,yaani leo mabinti kulala nje na kukesha kwa wanaume unadhani ni jambo jipya?,yaani binti ambaye kwao walikuwa washirikina na hakuwa na baba,yeye kutembea usiku unaona kuna uongo?,watanzania ni nani katuroga?,Mbona alivyolala na Ema pale kwa rafiki yake Jack usiku kucha mpaka kupelekea ugomvi na Deborah hamkuhoji?,mmeona muhoji mimi kukutana naye usiku kule mnadani!,Aiseee kuna sehemu vijana wa hili taifa wanapaswa kurekebisha ili mambo yaende sawa!.
3 Suala la Msukuma kumiliki ng'ombe zaidi ya elfu 10 mwaka 2003-2004 mtu anabisha,huyohuyo mtu ukimuuliza kwamba amewahi kufika Tabora au sehemu nyingine ya usukumani atakwambia bado,halafu anabisha!,na huyu ni msomi mzima anashangaa kabisa!.Atahoji hadi sisi kupewa lita 5 za maziwa bure kila siku pale kwa Headmaster atakwambia ni uongo!,Kama hujawahi kutembea kwenye hii nchi nikuombe usije nyanyua mdomo wako ukabisha!.Kuna mtu ukimwambia pale Geita na Mwanza kuna watu wanahela chafu kuliko huyo anayejiita Mo Dewji bado watakuja hapa kubisha kana kwamba huyo Mo ni baba yake!.
4.Kwamba mimi kuchwapwa mbele ya wanafunzi ilikuwa ni stori ya kutunga!,Hii nchi kuna watu wanashida kubwa mno!,kwamba unataka kusema kwakuwa wewe umekulia na kusomea mjini unadhani watu wote tumesomea mjini?,Kuchwapwa mbele ya kadamnasi haikuwa mjadala!,na wala si mbele ya wanafunzi tu!,yaani stiki ulikuwa unakung'utwa hata sokoni kama ukileleta ukora!,Vijana kama hamjui vitu tuambieni tuwaelekeze muweze kuvifahamu.
Mimi nimesoma shule ya kata isiyokuwa na maabara(laboratory)masomo ya sayansi (pcb) na nilifaulu ufaulu mzuri tu wa dvs 2 sema baadae nilifeli form 6 kwasababu ya mapenzi ya mwanamke wa kitanga.Sasa hivi vijana nyie hamuwezi kufaulu masomo ya sayansi bila maabara!.
KAMA HUJAPITIA MAISHA FULANI USISIMAME NA TUMBO LAKO UKAANZA KUBISHA MBELE YA WANAUME,UTATIA AIBU!.
NI HAYO TU.
Akipost 25 niite…Sawa Cha utundu...
Alfu Kama utataka pikpiki used nzuri njoo keko matunda pale sheli zinauzwa pikipiki nzuri San kwa Bei POA kbsa kwa milion 1 utapata chombo Safi tvs au boxer nzuri [emoji16]Anyway, Mwenye chombo (pikipiki)ambayo anatumia tu na hajui cha kufanyia hebu anipatie nipigie kazi ili kwa siku au wiki niwe nampelekea hesabu yake,hii chombo ninayotumia ishachoka na inanisumbua sana lakini sema na mimi ni mbishi tu!,nilipopata ajali siku ile natoka kusuruhisha ugomvi wa bro na mkewe ilipata shida kidogo!.
Hivyo kama unachombo nipe nipigie kazi usikae kizembe ili ikulipe kwa siku au wiki.
Tushikane mikono na kusaidiana panapobidi,sisi ni vijana na tunapambana!..
Kuna maneno yamenifurahisha sana humu.....Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane.
Miaka ya fulani baada ya kumaliza shule ya sekondari,niliamua kwenda kumsalimia Ba'mdogo aliyekuwa mkuu wa shule fulani ya sekondari hapo kwenye hicho kijijini.
Wana kijiji walikuwa wakimpa heshima kubwa Ba'mdogo kwasababu wanafunzi wote waliosoma kwenye ile shule walifaulu kuendelea na elimu ya Sekondari ya upili(Advance),japo shule ile ilikuwa ya kata na kwa mwaka ule nilienda mimi ilikuwa imefaulisha kwa awamu ya kwanza,yaani toka hiyo shule ianzishwe wanafunzi waliokuwa wamefika kidato cha ilikuwa tayari ni mara moja,hivyo nilipofika mimi wale nilowakuta ndo walikuwa wa awamu ya pili.
Sasa kwa mwaka ule wa kwanza wanafunzi wa kidato cha nne walimaliza 12 na wote walifaulu kuendelea Advance tena walienda kwenye shule za vipaji maalumu ikiwemo Ilboru.Sasa wanakijiji kiukweli walimpenda sana Dingi mdogo kwa kujitolea kuwaleta waalimu wa ziada ambao kile kijiji kilikuwa kinawalipa.
Nilipofika nilikuta pale kwa Ba'mdogo kila siku iendayo kwa Mungu ilikuwa inakuja Galoni ya maziwa fresh lita 5, kile kijiji kilikuwa na wafugaji wengi sana wa mifugo ya kila aina! Yaani kumuona mwanakijiji anamiliki ng'ombe elfu 10 ilikuwa kitu cha kawaida,sasa mbali na maziwa, kila Jumapili alikuwa analetewa kuku jogoo mmoja na mwanakijiji.
Ba'mdogo aliwahi kuniambia waliwahi kukaa kikao na wana kijiji wakakubali kila kaya kuwa wanakamua maziwa kulingana na zamu walizokuwa wamewekeana kwa ajili ya mwalimu mkuu ikiwemo kitoweo hicho cha kuku.
Nilipofika mara ya kwanza kwa sababu ya uroho na ulafi, nilikuwa nakunywa yale maziwa kwa wingi kana kwamba kesho hayatokuja mengine,yaani kila niliposikia kiu ya maji mimi nilitwanga maziwa, baadae sasa baada ya kuzoea ilifika sehemu tukawa tunayaangalia na tunaishia kuyamwaga tu maana hakukuwa na wakumpa.
Pale kwa Ba'mdogo baada ya mimi kufika,ni kama nilifanya wapumue maana kazi za hapa na pale nilikuwa nikizifanya mimi, ilikuwa ikifika ijumaa dingi mdogo alikuwa akiondoka kuelekea mjini kwa familia yake na ikifika jumapili jioni alikuwa akilejea.
Sasa kwa wakati huo dingi mdogo alikuwa akiishi na bwana mdogo mmoja alikuwa wa rafiki yake ambaye baada ya kufeli shule mahali fulani alimpatia namba na jina akawa amerudia pale kidato cha pili,hivyo nilipofika mimi tukawa watu watatu.
Japo kulikuwa ni kijijini lakini kulikuwa na maisha fulani ya amani sana,kulikuwa na Lambo kubwa ambalo wanakijiji walikuwa wakijipatia maji ya mahitaji yao hapo. Kwa upande wa umeme ulikuwa bado haujafika na wana kijiji walitumia Solar na Majenereta.
Ilipokuwa ikifika wikiendi nilikuwa ninashuka senta kwa ajili ya kuangalia mpira,wakati huo nilikuwa shabiki wa kutupwa wa Arsenal, ingawaje hivi leo sina mahaba kama hapo zamani kwasababu timu haieleweki nini inafanya. Yaani ilikuwa ni bora nilale na njaa kuliko kwenda kuitazama timu yangu pendwa ya Arsenal.
Kwenye ule ukumbi jamaa alikuwa anatumia jenereta na malipo ilikuwa Tsh 100 kwa wakati ule, sasa lile jenereta lilikuwa likiwashwa wakati wa mechi inapoanza tu ili kuokoa mafuta, yale mambo ya kuangalia uchambuzi wa kina Thomas Mlambo na Robert Marawa yalikuwa hayapo.
Sasa nilikuwaga nikimaliza shughuli zangu hapo nyumbani ikifika saa nane mchana,huyoooo naondoka zangu na kurudi mpaka gemu nihakikishe zimeisha ndo narudi nyumbani. Yule jamaa aliyekuwa hapo nyumbani hakuwa mpenzi wa mpira ila alikuwa mpenzi wa papuchi, yaani alikuwa anatembeza stiki si kwa wanafunzi wenzie tu, hadi wanakijiji.
Kutoka hapo nyumbani hadi ufike senta ilikuwa kilomita 3, kwenda na kurudi inakubidi utembee kilomita sita. Kiukweli kile kijiji hakikuwa na ujambazi wala vibaka, shida ya pale ilikuwa Uchawi!
Aiseeee sijawahi kuona asikwambie mtu.
Inaendelea...
- SEHEMU YA PILI (2)
Man UMUGHAKA pongezi mkuu Kwa uandishi wa 1990s nakupongezaMkuu dagii njoo Pm kama unataka mawasiliano yangu
Tumebakiwa na episode moja ya mwisho ambayo itapatikana whatsapp kwa kuchangia 2000 utaadiwa kwenye group. Ili kujua tulichomfanyia mchawi yule njoo whatsapp haraka kwa 2000 tuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mpwanyungu alizingua sana asee.mpwayungu village falasi tuu anakua mwepesi tuu anakasirika kama Debora na Emma
Wabeja sana.Tulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 23.
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu pale nje,mama yake Monica alituaga akawa ameingia ndani kwa ajili ya kulala,basi na sisi hatukutaka kupoteza muda kabisa tukawa tumeingia ndani ya kwa ajili ya kulala.Ilipofika asubuhi niliamaka mapema nikawa nimemwambia Monica inapaswa nielekee nyumbani!,siku hiyo nakumbuka ilikuwa jumamosi.
Monica "Subiri basi mama aamke kwanza"
Basi Monica alinipatia maji nikanawa uso kisha nikarudi ndani kusubiri hadi mama yake aamke maana alikuwa ameniambia usiku ya kwamba angenipatia kitu ambacho ningeenda nacho nyumbani ili kitusaidie!.
Ilipofika mida ya saa 1 asubuhi mama yake Monica alikuwa ameshaamka na alikuja kugonga mle ndani nilimo lala ili atusalimie,wakati huo nilikuwepo mimi peke yangu na Monica alikuwa yupo jikoni akiandaa uji kwa ajili ya mlo wa asubuhi!.
Mama Monica "Hujambo baba"
Mimi "Sijambo mama,shikamoo!"
Mama Monica "Marhaba,baba yangu"
Aliendelea "Mbona mapema yote hii,unawahi wapi?"
Mimi "Nilitaka kuwahi nyumbani mama nikaendelee na shughuli zangu,siunajua tena ninapaswa kuelekea senta"
Mama Monica "Ni kweli baba"
Aliendelea "Basi njoo umsalimie bibi yako"
Basi nilitoka mle chumbani nikaelekea mpaka nje ya mlango wa ile nyumba aliyokuwa amelala bibi yake Monica!.Kwakuwa kisukuma changu kilikuwa cha salamu tu na kuombea maji ilibidi mama yake Monica niwe naongea halafu na yeye anamtafusiria bibi maana alikuwa hakijui kiswahili hata tone!.
Baada ya salamu na mazungumzo mafupi,mama yake Monica akawa amenitolea kiti nje akanitaka nikae nisubiri uje uive ninywe wakati ambao yeye ananiandalia mitishamba na dawa aliyokuwa ameniambia angenipatia.Kiukweli niseme tu ukweli,mama yake Monica alitokea kunipenda sana na kuna muda nilikuwa nikifika pale kwa Monica najihisi niko kwenye dunia nyingine,mara kwanza nilikuwa naogopaga sana,lakini baada ya kuhakikishiwa usalama wangu,kwakweli sikuwa naogopa tena!.Yule mama alikuwa yuko radhi afanye jambo lolote ili mimi na mwanaye tusalimike!.
Basi haukupita muda Monica akawa ameivisha uji na maboga akatenga kwenye jamvi!,nilishuka kutoka kwenye kiti na kukaa kwenye jamvi kwa ajili ya kupata brekifasti!,kama ambavyo nilisema hapo awali,ile familia haikuwa na hela ila ilikuwa na uchawi wa kutosha!,kunywa uji usiyokuwa na sukari halikuwa jambo la mjadala na kiukweli japo sikuwahi kunywa uji wa sukari hapo kwa Monica lakini uji ulikuwaga mtamu sana kwasababu walikuwa wakiweka maziwa!,hivyo kuufanya kuwa mtamu sana!.Nilipomaliza kupata ile brekifasti,mama yake Monica aliniita ndani ya nyumba kubwa kule alikokuwa amelala bibi yake Monica.
Mama Monica "Mwanangu nisikilize kwa makini!"
Aliendelea "Najua wewe na mwanangu mtakwenda kuniletea mjukuu hivi karibuni,hivyo wewe ni mtu muhimu sana kwasasa katika familia hii"
Mama Monica "Najua Mwalimu Wambura ni Mkurya wa Musoma huko na ndiyo maana ni mjeuri,ila wewe nimekupenda kwakuwa unanisikiliza sana mwanangu,nakuomba usije ukachukua roho ya mwalimu Wambura!"
Aliendelea "Naamini hautanitesea mwanangu pekee Monica"
Mama Monica "Baba yake alikufa angali bado mdogo,hivyo nimemlea kwa matatizo makubwa mno!"
Aliendelea "Tulihamia huku baada ya kufukuzwa huko Ilungu-Magu,na hii yote ni kwasababu ya baba yake Monica"
Mama Monica "Haya yote unayoyaona tumerithishwa na huyu bibi yako unayemuona ningali binti mdogo"
Aliendelea "Kwakuwa baba yake Monica alitaka kuniulia mwanangu wa pekee kwenye michezo yao,ndipo huyu bibi yako tukasaidiana kummaliza kabla hajafanya jambo baya".
Aliendelea kusema "Baada ya mambo kuharibika ndipo tukahamia hapa,kutoka huko Ilungu".
Aliendelea kusema "Hivyo nikuombe mwanangu,hata nikifa leo,nakuomba umtunze mwenzio kwa gharama kubwa maana aliniambia anakupenda sana".
Aliendelea kusema "Mwanangu hajasoma,lakini ni mwerevu na anajua mambo mengi,hivyo na wewe nakuomba umpende!.
Kiukweli siku hiyo mama yake Monica aliamua kunipasulia ukweli kuhusu mwananye na familia yake kwa ujumla, ndipo nikaona kabisa nilikuwa nimethaminiwa kwa kiasi kikubwa na ile familia.
Mimi "Mimi nampenda sana Monica mama na sitaki kumpoteza na yote uliyoongea nimekusikia!".
Mama Monica "Sawa nisubiri nakuja".
Mama yake Monica aliingia chumbani akawa anazungumza na bibi yake Monica kisukuma.Sasa wakati nikiwa nasubiri mama atoke chumbani,ndipo Monica naye akawa ameingia ndani!.Haukupita muda mama yake Monica alitoka ndani akiwa amebeba furushi la mfuko wa rambo la blue!.
Alianza kuufungua ule mfuko kisha kutoa vitu ambavyo sikuvielewa.
Mama Monica "Kamata hii"
Aliendelea "Hiyo niliyokupa ukifika pale nyumbani kwenu,nenda kule nyuma lilipo dirisha la chumba cha Mwalimu na uhakikishe unachimbia chini usawa wa dirisha!".
Mimi "Sawa mama"
Aliendelea "Kamata na hii"
Alisema " Hii naomba umwambie mwalimu aogee yeye na mkewe,halafu wakimaliza kuoga wajipake hii hapa".
Aliendelea kusema "Wewe na mwenzio pia mfanye hivyo hivyo,baadae nitakuja mimi mwenyewe na nitakupatia maelekezo namna ya kufanya"
Mama Monica "Nataka kumsaidia mwalimu ili aepukane na hii fedheha ya yule mpumbavu na wenzie"
Aliendelea "Mwalimu amewahi kunitusi na tulikuwa hatusalimiani,ila inapaswa akushukuru sana wewe".
Mimi "Mwalimu hatakataa nikimwambia?"
Mama Monica "Wewe mwambie,akikataa shauri yake"
Aliendelea "Kama anataka kuondoa fedheha na kumuahibisha mbaya wake mwambie atumie,akikataa usimlazimishe muache".
Mimi "Nashukuru sana mama"
Mama Monica "Andaeni sherehe kesho mtafurahi na itakuwa fedheha hapa kijijini"
Basi baada ya mama yake Monica kunikabidhi zile dawa nikawa nimeaga na kuondoka kurudi nyumbani.Muda huo ilikuwa yapata saa 3 asubuhi.
Baada ya kutembea kwa muda namshukuru Mungu nikawa nimefika nyumbani salama,nilipofika mida hiyo bado sikumkuta mtu yeyote pale nyumbani!.Basi niliingia stoo nikachukua jembe nikazunguka kule nyuma ya nyumba ambako kulikuwa na dirisha la chumba alichokuwa analala Ba'mdogo.Nilichimba haraka haraka na kufukia ile dawa kama ambavyo mama yake Monica alikuwa amenielekeza.
Nilipomaliza nilirudisha jembe stoo kama kawaida,nilichukua dumu la maji nikaelekea lamboni kuchota maji ili nije nikaoge ile dawa ambayo alinipatia maelekezo na kututaka wote tuoge kama tunataka kuwa salama ikiwemo Headmaster na mkewe!.Basi baada ya kumaliza kuoga nilianza zoezi la kuosha vyombo na kumwaga ule ugali nikiyokuwa nimeupika jana na ukakosa walaji!.
Baada ya ile kazi iliyochukua muda wangu mwingi,niliingia ndani kulala!.Nilishituka nikiwa naamshwa na Ema mida ya Saa 7 mchana,wakati huu jamaa alikuwa akijechekelesha chekelesha na nikajua kutakuwa na kitu lazima kwasababu haikuwa kawaida yake,mara nyingi alikuwaga akiharibu mahali basi alikuwa akinichangamkia sana kwakuwa mimi nilikuwa mtetezi wake!.
Mimi "Vipi".
Ema "Mwanangu si Headmaster amenifuma nampiga Deborah mate"
Mimi "Amekufuma wapi"
Ema "Situlikuwa tumesimama pale karibu na ule muale".
Mimi "Sasa amewaona vipi"
Ema "Yaani mwanangu na mimi sifahamu,nimeshituka namuona huyu hapa"
Mimi "Amekwambia nini"
Ema "Ametuchora tu,hajaniambia chochote"
Nilijua tu atakuwa ameharibu mahali na ndiyo maana akajifanya kuja kwangu na kuanza kujichekesha!,kimoyo moyo nilimuhurumia maana nilijua fika stiki atakazokutana nazo si za kitoto!.
Sasa ilipofika mida ya saa 9 alasiri nilitoka zangu ndani na kwenda kumsalimia Headmaster ambaye alikuwa amesharudi,lakini haikuwa kawaida yake nilivyomuona,kiukweli alio alionekana kama mtu aliyekata tamaa na kuchoka kwingi,sasa sikufahamu huko alipokuwa ameenda kilikuwa kimemkuta nini!.
Headmaster "Hivi mwalimu Dani huwa unafahamu anapokaa"
Mimi "Hapana,sijawahi kufika kwake"
Headmaster "Hebu mwambie huyo mjinga aje nimuagize"
Basi nilitoka kwenda kumuita Ema.
Headmaster "Wewe mwalimu Dani siunapafahamu anapokaa?"
Ema "Eeenh,napajua"
Headmaster "Nenda ukimkuta umwambie akupatie mzigo wangu,na uwahi kurudi".
Basi baada ya Ema kuondoka,nilimwambia baba nilikuwa nina mazungumzo nae yeye pamoja na mama.
Headmaster "Kwani huwezi kuniambia mimi mpaka awepo mama yako mdogo?"
Mimi "Ni vizuri akiwepo na mama baba"
Headmaster "Sawa,nilimuacha kwa mama Salome,ngoja tumsubiri arudi".
Nilitaka awepo Maza mdogo maana nilifahamu ningemwambia Headmaster angeweza kukataa,ila Maza mdogo akiwepo isingekuwa rahisi yeye kukataa!.
Bro why imeisha mapema hii ilitakiwa kua isifingoTulichomfanya Yule Mchawi hatokuja kusahau kamwe! - 25.
Baada ya Headmaster kutoka kuwasindikiza wageni,tuliamua kukaa kikao cha kifamilia na kuzungumza mambo kadhaa yaliyotuweka sawa.Sasa kila mtu alielekea chumbani kulala,baba mdogo na mkewe waliingia chumbani kwao,mimi na Ema pia tuliingia chumbani kwetu kulala.
Siku hiyo mle chumbani hakuna aliyepata usingizi kabisa,kabla ya kulala nakumbuka tulipakaa usoni dawa aliyokuwa ametupatia mama yake Monica,pia tukashikiria na zile hirizi mkononi kama alivyokuwa ameagiza tufanye!.Kadri muda ulivyokuwa ukisonga tuliona kimya,mimi nilianza kupitiwa na usingizi maana nilikuwa nimechoka sana!,kumbe wakati mimi napitiwa na usingizi,Ema yeye alikuwa macho kabisa na jamaa alikuwa na shauku ya kuona ni kitu gani kingetokea!.
Sasa ilipofika mida ya saa 8 usiku,nilishitushwa na Ema akiniamsha!.
Ema "Umesikia hicho kishindo?".
Mimi "Hapana,kishindo cha kitu gani?"
Ema "Kutakuwa na kitu nadhani!"
Ema alikuwa akiniambia kwa sauti ndogo kabisa na yenye uoga ndani yake!.
Mimi "Nyamaza"
Niliamka kitandani nikaenda kuwasha taa,nilifahamu kabisa kile kishindo Ema alichosikia hakikuwa cha kawaida na uenda wale jamaa wakawa wamekuja kama kawaida yao,kiukweli mimi kwa upande wangu sikuwa kabisa na hofu kwasababu kwa siku chache nilikuwa nimeshazoea yale mazingira ya kuwaona wachwawi laivu!.Nilimwambia na kumbusha Ema ya kwamba chochote atakachokiona asipige kelele wala kushituka!.
Haukupita muda,mara ghafla wakaonekana watu watatu wakiwa wamesimama mle chumbani huki wakiwa uchi kama walivyozaliwa,watu wale safari hii walikuja wawili wanaume na mmoja akiwa mwanamke!.Niliwaangalia kwa kuibia kama vile sielewi chochote!,Ema alikuwa akitetemeka sana na nilimpatia ishara ya kwamba atulie kabisa!.Basi nadhani yule mwanamke alihisi jambo maana niliona anamsogelea Ema akawa kama anamtisha aone kama amemuona,sasa alipoendelea kumtisha Ema nikaona anaweza kupiga kelele,nikaanza kumpigisha Ema stori ili kupotezea ile hali!.
Mimi "Mwanangu wewe piga kimya kabisa wala usimfanye chochote yule demu"
Ema "Yule demu mwanangu anazingua kinoma"
Mimi "Halafu Headmaster alisema ukamuamshe aandae yale masomo"
Ema "Halafu kweli umenikumbusha,ngoja nikamuamshe!"
Sasa wakati tunaongea yule mwanamke alirudi kwa wenzie na wakaendelea kushangaa shangaa,tulichokifanya na Ema pale kwa ule muda mfupi ni hakika walidhani hatuwaoni kumbe lengo lilikuwa ni kumuondolea Ema uoga na kuwapoteza maboya!.
Ema aliamka akatoka kwenda kumgongea Headmaster chumbani kwake ili aje ajionee!,sasa wakati Ema ameondoka,nilianza kujipigisha mruzi wa uongo na kweli ili kuikabili ile hali kwasababu ilikuwa inatisha si kitoto!..
Headmaster "Umughaka tacho omahe"
Baba alipotoka nje aliniita kwa kilugha nikawa nimetoka nje,sasa alianza kutueleza ya kwamba tusishituke na tuendelee kuwa watulivu,alitwambia Ema achukue madaftari tuelekee wote sebuleni ili iwe rahisi kuwakabili,mimi nilimwambia wao wakae sebuleni na mimi nirudi chumbani kukaa karibu na kibuyu kwa kazi maalumu!.
Basi wale watu wakawa wamepotea ghafla mle chumbani!,nilitoka nje kwenda kumwambia Headmaster.
Headmaster "Ngoja tusubiri,yawezekana wakawa wameshituka"
Mimi "Lazima warudi"
Headmaster "Halafu mbona yule mzee hayupo?"
Mimi "Uenda leo kawaagiza hawa"
Wakati tukiwa tunaendelea kuongea pale,Maza mdogo akamwambia Headmaster kwa kikurya kwamba,wale watu wako kule chumbani kwake na anawaona,Headmaster akamwambia atulie na asipige kelele!.Sasa tukiwa tunaendelea kuongea pale sebuleni huku Headmaster akijifanya kumpigisha Ema pindi,tukasikia kishindo kikubwa tena pale uani!.
Haukupita muda akawa ametokea yule mzee makono akiwa na usinga mkononi huku akiwa uchi kama wenzie!,akaja mpaka pale sebuleni huku tukiendelea kumpimia tu!,aliendelea kuangaza huku na huko na hatimaye akawa ameingia mle chumbani kwa Headmaster.Basi baada ya kuingia chumba cha Headmaster,Headmaster aliinuka kwa ghadhabu huku akisema "Lero n'uramanye uwe tombanyoko" (Leo utanitambua).
Sasa Headmaster alipoingia chumbani alijifanya kuongea na mkewe huku wakiwatazama,sasa nadhani mzee makono aliwaambia wale watu waende wakawalete watu wa kwenda kulima ili wakifika watuunganishe na sisi tuondoke!,wale watu watatu walitoweka wakamuacha mzee makono mle chumbani akitaka kufanya mambo yake ili amchukue Headmaster kama kawaida aje atuunganishe na sisi tuelekee kwenye kilimo cha usiku kisichokuwa na tija!.
Wale watu walipotoweka tu na mzee makono kubaki mwenyewe,Headmaster alichukua kile kibuyu alichopewa na mama yake Monica akakifungua,alipokifungua tu!,yule mzee akaanza kucheza kwa kuzunguka mle chumbani kama mwendawazimu!.Headmaster alituita tukaingia kumtazama,yaani kuna muda nilianza kumuonea huruma maana alikuwa kama amepagawa kwa kushikwa ugoni.
Kadiri muda ulivyokuwa ukienda,wale watu waliotumwa na mzee makono hawakurudi kabisa na nadhani watakuwa walishituka mapema!.Ile hali ilifanya maza mdogo kutoka kule chumbani akabaki mzee makono akizunguka chumba kizima kama mwendawazimu.Usiku huko hakuna mtu aliyepata usingizi kabisa,tumekuja kushangaa imefika saa 11 alfajiri bila kujua!.
Sasa ilipofika saa 12 asubuhi,Mama yake Monica alikuja akiwa na wale kina mama,alihuzunika sana kwanini tuliamua kuwaachia wale watu watatu wakaondoka!.
Mama Monica "Mwalimu nilikwambia,nadhani sasa unaniamini"
Headmaster "Sikuzote Msukuma nakuamini,si leo tu!".
Mama Monica "Kwanini mmewaachia wale washenzi?"
Headmaster "Wameondoka wenyewe"
Mama Monica "Nilikwambia wakifika tu,ungefungua kibuyu"
Headmaster "Nilipoingia chumbani kufungua kibuyu wakawa wameondoka akabaki mzee lameki"
Mama Monica "watasimuliana,hakuna kilichoharibika"
Aliendelea "Haya sema,unataka tumfanye nini huyu mzee"
Headmaster "Nadhani kama kuna uwezo muondolee uwezo wake asije akaponyoka halafu mengine utaniachia mimi"
Mama Monica "Huyu ameshakwisha,hapa hawezi kukuponyoka kamwe"
Aliendelea "Mimi namshughurikia halafu nakuachia wewe utajua cha kumfanya".
Basi mama yake Monica alimsogelea yule mzee akachukua ule usinga kisha akamvua shanga alizokuwa amejivika kuanzia begani kuteremkia kiunoni!,baada ya hapo kuna dawa alimpatia Headmaster akamwambia kukishapambazuka vizuri atampaka ile dawa na kisha atamuondoa mle ndani!.Mama yake Monica na wale kina mama waliondoka wakawa wamemuacha mzee makono humo ndani akizinguka kama mwehu!.
Kulipopambazuka,Headmaster alielekea kwa mwenyekiti wa kijiji na kutaka yowe ipigwe karibia kijiji kizima ili wananzengo wahalifiwe ya kwamba kulikuwa kuna tukio kubwa la kushangaza!,Basi yowe ilipigwa na watu wakawa wanakuja pale nyumbani huku wengine mikoni wakiwa wameshika mapanga na mafimbo!.Haukupita muda mrefu watu wakawa wamejazana pale nyumbani huku wengine wakichungulia dirishani wakishangaa lile tukio!.
Ilipofika mida ya saa 3 Asubuhi baada ya watu kujazana pale nyumbani,Headmaster alifanya kama alivyoambiwa afanye na mama yake Monica,baada ya kupakwa dawa yule mzee alikurupuka akawa anashangaa sana!,alikuwa akizunguka kitafuta usinga wake lakini hakuuona,ndipo Headmaster aliamrishwa na wananzengo ya kwamba amtoe yule mzee nje ya nyumba ili akapambane na viboko vilivyokosa huruma!.
Yule mwenyekiti aliamuru yule mzee avishwe nguo hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji lakini wananzengo wakagoma,walisema inapaswa atembezwe kijiji kizima huku akila mboko na inapaswa siku hiyo hiyo ahame kijiji!.
Basi nakumbuka Headmaster alimuagiza Ema akalete viboko ili aanze nae mle ndani kwasababu alikuwa akimtafuta sana,viboko vilipoletwa kiukweli yule mzee alichezea kiasi kwamba sikutaka hata kuangalia,viboko vilipozidi aliamua kutoka ndani spidi akikimbilia nje,kufika nje wananzengo wakamdaka nako wakaanza kumsulubisha!.
Alitembezwa kijiji kizima huku akiwa uchi kama alivyozaliwa,kiukweli lilikuwa ni tukio la aibu mno!,sasa walipomfikisha kwake wananzengo hawakutaka mjadala,walimwambia avae nguo kisha atoke,alipotoka waliwasha moto nyumba yake na kila kitu kiliteketea kwa moto!.
Baada ya pale alirudishwa serikali ya kijiji na kutakiwa apotee kwenye kile kijiji ndani ya masaa 2!,hakutakiwa kubaki pale na wananzengo walimwambia watamuua endapo angebaki kwa siku hiyo!.
Lile tukio lilivuta hisia kubwa sana pale kijijini na kiukweli lilimpatia Headmaster ujiko na heshima sana ingawaje mimi ndiye niliyepambana sana mpaka kufikia ile hali.Headmaster aliogopeka sana tangu siku ile lile tukio litokee na hakukuwahi tena kuwa na mambo ya ajabu pale nyumbani.
Headmaster kwa baadae alihama ile shule na kuhamia huko Biharamulo ambako amejenga na anaishi hadi leo,mimi niliondoka na kurudi nyumbani kisha kuelekea shuleni Advance!.
Ema yupo hapo Shinyanga anauza duka la vipuri vya magari,amejenga na anaishi hapo hapo shinyanga.
Monica kuna wakati niliambiwa yupo Mwanza ila sijajua ni Mwanza sehemu gani!,kuna mtu nilikutana nae wa pale kijijini akawa ameniambia hivyo,kwasababu baada ya mimi kuondoka pale kijijini sikurudi tena hivyo tukawa tumepotezana na mpenzi wangu huyo!.
Mimi kwasasa nipo Dar es salaam napambana na maisha ya kukimbizana!,nina kiboda boda changu japo kimekwisha lakini tunapambana na maisha!.Kijiwe changu huwa ni hapo Bunju ndugu zangu!.
MWISHO.
Ukianza nitag mkuuKesho na Mimi nitaanza kusimulia kisa changu cha kukutana na SHAN bint SADIKI (Jini lenye uzuri wa ajabu) hii ni story ya kweli ilinitokea mwishoni mwa miaka ya tisini na nikawa huru 2006
Nawahaidi kuimaliza yote ndani ya siku nne tu
Asanteni