Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi?

Kaulimbao ya CCM ilitakiwa isiwe 'Ari Mpya na Kasi Mpya' au 'Kilimo kwanza' bali ilipaswa iwe 'Tupishe mwekezaji maana sisi ni apes'..lolz
 
Kaazi kwelikweli ngoja nami nikajichukulie kibali cha kumiliki ardhi nijiambiwa mie na familia yangu ni wakimbizi hivyo tupishe mwekezaji
 
Nice work Mlenge, I am always asking myself do we have opposition parties to take this information as a fuel in their campeigns??
 
Heshima Mbele,

Nina Habari hapa,ila nashindwa kuthibitisha.Naoma tusaidiane ku connect to the dot..

1.Kwanini huo mradi mipango yote imeanzia marekani?

2.Kwanini iwe haraka hivyo na lazima mradi uanze 2011

3.Kwanini kuna baadhi ya watu ,wafanyabiashara maarufu ndiyo wameuziwa badhi ya viwanja huko?

4.Hivi ni kwanini George alikaa muda mrefu hapa Tanzania?

Kuna habari nimepewa muda huu,bado nazifanyia utafiti ila am speechless
Hivi hii project inaanza 2011?

Basi kwisha kazi...!
 
Bob

Nakubaliana na mtazamo wako kuhusu hili tamko la serikali (sijui limetolewa lini).

Kinachonishangaza kidogo ni kuwa Kigamboni ilishagawiwa tangu Makamba alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dsm. Ninachojuwa ni kuwa hakuna kiwanja "kinacholipa" kigamboni ambacho hakimilikiwi na Kigogo. Pia, Hati za Kumiliki Viwanja za Muda mrefu (miaka 66) zimeshatolewa chini ya mradi ule wa Makamba.

Sasa sina uhakika Mbunge anaposema Serikali imesitisha kutoa hati za arthi kigamboni anamaanisha viwanja ambavyo "havijapimwa" au vile vya mradi lakini yeye/wao bado hawajachukua hati zao?

Mbunge, tafadhali fafanua kidogo au tunaomba link ya hilo tamko ili tujisomee wenyewe kabla hatujaanza kupaniki..!!

mimi nina shamba pake kibada, km 5 tu toka feli, nimenunua 2006 kabla hata ya tamko hili, cha ajabu nilipotaka kulipima ili nipate offer ya kumiliki nikaambia kuna zuio, ni kweli kibada yate tunaambiwa huwezi pima kiwanja.

mimi sikatai mji mpya kujengwa lakini sasa je haki yangu kweli nitapata? kwa sasa eneo langu ni heka tatu sasa wakija hawa jamaa naona nitapata bei ya mimea tu na sidhani kama itafika laki saba, manake as of now sina karatasi yoyote inayoonyesha mimi ni mmiliki wa eneo hilo.

jamani haki ya mlalahoi ipo kweli? tuliambiwa we are going to be part of the project - lakini utaingiaje kwenye project wakati hata karatasi ya utambulisho kwamba hilo eneo ni lako huna?

ndugu zangu inafika pahara mtu unajiona kama mkimbizi usiye na haki ya kumiliki chochote ndani ya nchi yako.

Pembeni kwangu kuna mchina - kapewa eneo kama heka 100, alipata kwa bei ya kutupwa kabisa na tayari ana umiliki - mimi mzawa bado nahangaika - kweli kazi ipo.
 
Hey jamani, mji mwema napo ni sehemu ya huu mradi? nina mradi wa kujenga nyumba unalioanza mwezi uliopita.
 
inaelekea wewe bado umelala

huna habari kuwa masterplan ishakamilika?

ongea na Chiligati atakupa copy au CD

Mimi nimebahatika kuiona hiyo Masterplan,lakini kinachonishangaza ni kwanini huu mradi umechelea kwani tofauti na muda wa TANGAZO lao la NOTICE ambayo inaishia Tarehe 30 /10/2010????
 
mimi nina shamba pake kibada, km 5 tu toka feli, nimenunua 2006 kabla hata ya tamko hili, cha ajabu nilipotaka kulipima ili nipate offer ya kumiliki nikaambia kuna zuio, ni kweli kibada yate tunaambiwa huwezi pima kiwanja.

mimi sikatai mji mpya kujengwa lakini sasa je haki yangu kweli nitapata? kwa sasa eneo langu ni heka tatu sasa wakija hawa jamaa naona nitapata bei ya mimea tu na sidhani kama itafika laki saba, manake as of now sina karatasi yoyote inayoonyesha mimi ni mmiliki wa eneo hilo.

jamani haki ya mlalahoi ipo kweli? tuliambiwa we are going to be part of the project - lakini utaingiaje kwenye project wakati hata karatasi ya utambulisho kwamba hilo eneo ni lako huna?

ndugu zangu inafika pahara mtu unajiona kama mkimbizi usiye na haki ya kumiliki chochote ndani ya nchi yako.

Pembeni kwangu kuna mchina - kapewa eneo kama heka 100, alipata kwa bei ya kutupwa kabisa na tayari ana umiliki - mimi mzawa bado nahangaika - kweli kazi ipo.

Pole Mkulu,

Nataka nikuambie kwa maneno mengi zaidi lakini yote yameniisha
 
Mkuu,

Pole sana..ila labda ungefafanua. Unaposema huna karatasi yoyote inayokuonyesha wewe kama mmiliki wa eneo hilo una maana gani??

Iwapo ulinunua hilo Shamba mwaka 2006 ilikuwa ni wajibu wako kuwaita Serikali ya eneo hilo Mjumbe, Mwenyekiti wa Mtaa na Jirani ili wawe mashahidi wako kwamba:

1. Unanunua shamba kutoka kwa mmiliki halali.
2. Wewe ndiye mmiliki mpya wa halali.
3. Anakuuzia shamba lenye mipaka inayoeleweka.

Sasa ina maana wewe hukuweka hao mashahidi au una maana gani?

Swali la pili linajitokeza pia; unasema ulipotaka kupima ili upewe Offer ya kumili, ulitaka kutumia documents gani kuwathibitishia Manispaa ya Temeke kuwa eneo unalotaka kupimiwa ni la kwako??

Kisheria shamba/kiwanja hakiwezi kupimwa bila Mashahidi (Mjumbe na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa) kuweka Sahihi kutbitisha kuwa

1. Unapima shamba/kiwanja chako.
2. Unapima kwenye mipaka yako.

Sasa Mkuu...inakuwaje wewe huna uthibitisho kwamba eneo ni la kwako?

YY
 
Hey jamani, mji mwema napo ni sehemu ya huu mradi? nina mradi wa kujenga nyumba unalioanza mwezi uliopita.

muda wa kufuatilia haupo sababu hutasikilizwa hata ukishinda pale ardhi, cha msingi kama umekaribia kumaliza - endelea uhamie la kama bado upo initial stages - achana na mladi wako ili upime upepo kwanza usije kulia bila kupigwa
 
Mkuu,

Pole sana..ila labda ungefafanua. Unaposema huna karatasi yoyote inayokuonyesha wewe kama mmiliki wa eneo hilo una maana gani??

Iwapo ulinunua hilo Shamba mwaka 2006 ilikuwa ni wajibu wako kuwaita Serikali ya eneo hilo Mjumbe, Mwenyekiti wa Mtaa na Jirani ili wawe mashahidi wako kwamba:

1. Unanunua shamba kutoka kwa mmiliki halali.
2. Wewe ndiye mmiliki mpya wa halali.
3. Anakuuzia shamba lenye mipaka inayoeleweka.

Sasa ina maana wewe hukuweka hao mashahidi au una maana gani?

Swali la pili linajitokeza pia; unasema ulipotaka kupima ili upewe Offer ya kumili, ulitaka kutumia documents gani kuwathibitishia Manispaa ya Temeke kuwa eneo unalotaka kupimiwa ni la kwako??

Kisheria shamba/kiwanja hakiwezi kupimwa bila Mashahidi (Mjumbe na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa) kuweka Sahihi kutbitisha kuwa

1. Unapima shamba/kiwanja chako.
2. Unapima kwenye mipaka yako.

Sasa Mkuu...inakuwaje wewe huna uthibitisho kwamba eneo ni la kwako?

YY

kaka karatasi nazosema mimi si zile zinazotambuliwa na ardhi (offer), hii ni karatasi ya kuuziana tu na inatambuliwa na serikali ya mtaa, ila sidhani itanisaidia sana siku hawa mafisadi wakubwa watakapokuja kuchukua eneo lao (maana si langu tena).

nilivyoenda kupima mwaka 2008, nikiwa na hizo karatasi zangu za ununuzi wakaniambia kuna stop order toka serikali kuu kwamba eneo lote up to 10km toka feli limo kwenye mradi mpya - kwa hiyo upimaji umesimama.

napenda mradi uje lakini jee tutalipwa bei ya soko au ndiyo yaleyele ya ngombe wa maskini?

Kuna majirani zangu kule wanajenga na hawajali - mimi nimeogopa kabisa kutia vijicenti vyangu zaidi viliwe - may be kama kuna mtu ana more information about the project atufafanulie if we should continue to invest ama?
 
kaka karatasi nazosema mimi si zile zinazotambuliwa na ardhi (offer), hii ni karatasi ya kuuziana tu na inatambuliwa na serikali ya mtaa, ila sidhani itanisaidia sana siku hawa mafisadi wakubwa watakapokuja kuchukua eneo lao (maana yake si langu tena).

nilivyoenda kupima mwaka 2008, nikiwa na hizo karatasi zangu za ununuzi wakaniambia kuna stop order toka serikali kuu kwamba eneo lote up to 10km toka feli limo kwenye mradi mpya - kwa hiyo upimaji umesimama.

napenda mradi uje lakini jee tutalipwa bei ya soko au ndiyo yaleyele ya ngombe wa maskini?

Kuna majirani zangu kule wanajenga na hawajali - mimi nimeogopa kabisa kutia vijicenti vyangu zaidi viliwe - may be kama kuna mtu ana more information about the project atufafanulie if we should continue to invest ama?

Mkulu,

Mimi na wewe tuko kwenye meli mmoja.
Ninacho kushauri usijenge kwani serikali ilishaleta watu wao kufanya assessment toka mwezi wa kumi na moja (11) mwaka jana,kama walikuta eneo lako halina kitu alafu wewe ukajenga sasa hivi basi uwezekano wa kulipwa hicho ulichowekeza kwenye ujenzi ni mdogo sana,ni bora wakulipe hiyo laki saba kwa ardhi yao (ingawa umenunua wewe kwa pesa yako) kuliko wakulipe laki tatu wakati umeshajenga nyumba.
 
Mimi nimebahatika kuiona hiyo Masterplan,lakini kinachonishangaza ni kwanini huu mradi umechelea kwani tofauti na muda wa TANGAZO lao la NOTICE ambayo inaishia Tarehe 30 /10/2010????

JK alishakuja kule alipoulizwa swali akasema - hana uhakika kwamba mradi unaanza lini - kuna miradi mingi tu serikali huwa ina masterplan zake, akasema tunaweza kuutekeleza katika kipindi changu au isiwe hivyo - ila akatuambia tujenge kwa mpangilio.

Sasa hapa mimi ndiyo nabakia hoi kabisa - its too political sababu hata shilling ya kuwekeza kwenye mradi huo hatujui itatoka wapi, wengine wanasema Marekani ila hakuna mwenye ushahidi.

Daraja pia bado kitendawili - miundombinu ndiyo usiseme maanayake maji tunaambiwa lazima yatoke mto rufiji - ndugu zangu .....
 
kaka karatasi nazosema mimi si zile zinazotambuliwa na ardhi (offer), hii ni karatasi ya kuuziana tu na inatambuliwa na serikali ya mtaa, ila sidhani itanisaidia sana siku hawa mafisadi wakubwa watakapokuja kuchukua eneo lao (maana si langu tena).

nilivyoenda kupima mwaka 2008, nikiwa na hizo karatasi zangu za ununuzi wakaniambia kuna stop order toka serikali kuu kwamba eneo lote up to 10km toka feli limo kwenye mradi mpya - kwa hiyo upimaji umesimama.

napenda mradi uje lakini jee tutalipwa bei ya soko au ndiyo yaleyele ya ngombe wa maskini?

Kuna majirani zangu kule wanajenga na hawajali - mimi nimeogopa kabisa kutia vijicenti vyangu zaidi viliwe - may be kama kuna mtu ana more information about the project atufafanulie if we should continue to invest ama?

Aisee jamaa wewe sio entrepreneur uoga wako ndio umaskini wako, jenga fasta fasta malipo ni pale pale, court is there to protect you.
 
Njoo tubanane Shungubweni,kama una hela zako njoo ujikatie huku pande la nguvu,serikali bado haijafika.

Mitaa yote kuanzia kibada mpaka Tundwi songani kupitia Kisarawe II na Dsm zoo ni maeneo hatari kwa sasa,nunua au jenga kwa uangalifu
 
kaka karatasi nazosema mimi si zile zinazotambuliwa na ardhi (offer), hii ni karatasi ya kuuziana tu na inatambuliwa na serikali ya mtaa, ila sidhani itanisaidia sana siku hawa mafisadi wakubwa watakapokuja kuchukua eneo lao (maana si langu tena).

nilivyoenda kupima mwaka 2008, nikiwa na hizo karatasi zangu za ununuzi wakaniambia kuna stop order toka serikali kuu kwamba eneo lote up to 10km toka feli limo kwenye mradi mpya - kwa hiyo upimaji umesimama.

napenda mradi uje lakini jee tutalipwa bei ya soko au ndiyo yaleyele ya ngombe wa maskini?

Kuna majirani zangu kule wanajenga na hawajali - mimi nimeogopa kabisa kutia vijicenti vyangu zaidi viliwe - may be kama kuna mtu ana more information about the project atufafanulie if we should continue to invest ama?

ELNIN0

Endelea kujenga kama hawajafika hapo shambani kwako, mimi nilipoipata habari hii nilianza kujenga kama ninakimbizwa siku waliopita hapa kwangu tayari bati lilikuwa limegongwa , wakanipa ile karatasi yao na kuniambia nisianzishe jengo jipya,
ila hili ninaweza kumalizia na nikaishi.
 
Njoo tubanane Shungubweni,kama una hela zako njoo ujikatie huku pande la nguvu,serikali bado haijafika.

Mitaa yote kuanzia kibada mpaka Tundwi songani kupitia Kisarawe II na Dsm zoo ni maeneo hatari kwa sasa,nunua au jenga kwa uangalifu

Malila;

Hayo si kweli ndg yangu Malila; kwani hata mimi nimebahatika kupata kiwanja cha mradi pale Mikwambe na tayari nimepewa ofa, ninategemea kwenda kuchukua hati yangu kesho asubuhi, sasa unaposema 11 km from Fell ni hatari unamaanisha viwanja ganiMkuu Malila!, usichanganye kuna ule mradi unaochukuwa zile kata 4, lakini kuanzia Kibada na kuendelea viwanja hivyo havina shida.
 
Back
Top Bottom