Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi?

Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi?

MKUU HAIJAUZWA ..! ni mpango wa jiji kujenga jiji la kisasa..! ila ni possible yakawepo majengo ya raia wa kimarekana..!

ILA JPILI CHAGUA CHADEMA..! PLZZZZ
 
thibitisha sio unakuja na umbea wako hapa then tukuamini
 
Kigamboni hatunayo tena. Nimeona picha kwa shushushu mmoja ni video kabisa. Pia inapatikana kwenye chuo cha ardhi ambako wameipata kujifunzia planners. Ile video inasema 'kigamboni the new city' iko kwa kiingereza,ni mpango wa marekani,inaitwa intensive investment na inasema utakuwa mji wa kwanza wa kifahari Africa,ukifuatiwa na S.Africa,ama kweli ukiona picha utaipenda. Pia kutakuwa na kambi mbili za majeshi. Mpango uu una unaanza rasmi mwakani,utaanza na ujenzi wa daraja la kigamboni,ukivuka tu unakutana na majengo ya ghorofa na hotel na parking za kumwaga. Phase ya kwanza inaisha 2025 phase II itaanza 2025-2035. Du ukiangalia utalia,mwisho kuna picha ya dr. JEYKEy kavaa suti nyeusi,tai nyekundu. Kumbuka yaliyoipata Misri ya Suez Canal ndo naisi itaikuta Tz,yani payback kwa large investment ni ngumu,mwisho wake ni kuingia kwenye mikataba ya kikoloni, ya madini na majeshi. Mie simo.
 
wana JF ndugu zangu mie nimekuja habari mpya ya jinsi JK alivyouza kigamboni yote kwa bush. naomba mjionee wenyewe.
nawatumia pia program ya kuwezesha kutazama picha hiyo kama utakwama.
AMKA NCHI INAUZWA NA CCM

Kigamboni hatunayo tena. Nimeona picha kwa shushushu mmoja ni video kabisa. Pia inapatikana kwenye chuo cha ardhi ambako wameipata kujifunzia planners. Ile video inasema 'kigamboni the new city' iko kwa kiingereza,ni mpango wa marekani,inaitwa intensive investment na inasema utakuwa mji wa kwanza wa kifahari Africa,ukifuatiwa na S.Africa,ama kweli ukiona picha utaipenda. Pia kutakuwa na kambi mbili za majeshi. Mpango uu una unaanza rasmi mwakani,utaanza na ujenzi wa daraja la kigamboni,ukivuka tu unakutana na majengo ya ghorofa na hotel na parking za kumwaga. Phase ya kwanza inaisha 2025 phase II itaanza 2025-2035. Du ukiangalia utalia,mwisho kuna picha ya dr. JEYKEy kavaa suti nyeusi,tai nyekundu. Kumbuka yaliyoipata Misri ya Suez Canal ndo naisi itaikuta Tz,yani payback kwa large investment ni ngumu,mwisho wake ni kuingia kwenye mikataba ya kikoloni, ya madini na majeshi. Mie simo.

Jamani si iko hata kwenye Youtube au ni tofauti? Mimi naona kama ni mipango mizuri ya jiji ya kuboresha jiji la Dar es Salaam. Angalia hii hapa

YouTube - Kigamboni New Dar City Center
 
Jamani si iko hata kwenye Youtube au ni tofauti? Mimi naona kama ni mipango mizuri ya jiji ya kuboresha jiji la Dar es Salaam. Angalia hii hapa

YouTube - Kigamboni New Dar City Center

Mimi nimeiangalia na kulia machozi. Hiyo mnayoita plan si lolote wala chochote. Mnazugwa na flyovers na maupuuzi mengine kiasi mnashindwa kumsikia narrator akisema patakuwa na chuo kwa ajili ya wanafunzi wa kigeni peke yao. Michoro imetayarishwa na kampuni ya Korea Kusini ambayo imetujua udhaifu wetu. Tukiambiwa kuwa utakuwa kama Dubai tunafurahi bila kujiuliza kama utawezaje ku/manage katika nchi isiyo na infrastructure ya aina yeyote! Mradi huu ni matusi kwetu na yeyote anayeipenda nchi yake. Ni yale yale y John Nolan na Msimbazi. Ni hayo hayo tunayoyaona Dar Village. Ni hayo hayo tunayoyaona Mlimani City. Kupenda mteremko kutatuua.

Amandla....
 
Ndugu kama ungekuwa na uwezo na kampuni yako ungeweza kupewa eneo lile na kuliendeleza kama huna uwezo basi achia wengine waendeleze na kulipa kodi , hata dubai iko hivyo na nchi nyingi ziliachia maeneo yao kuendelezwa leo tunaona faida zake
 
Mpaka hapo miaka itapopita na kukuta hakuna kitu ndipo mtakapotambua mmeliwa tena. Sisi sio Dubai wala Singapore. Dubai wana ndugu zao wenye mafuta na bandari iliyo strategically located lakini pamoja na yote hayo sasa hivi wako taabani. Singapore nao bandari yao ni strategic na waliwekeza mno kwenye elimu, matunda yake tunayaona. Sisi walikuja wakina John Nolan na mpango wa kujenga kwenye bonde la Msimbazi, tukapiga vigelegele na hamna lilotokea. Hivi na wale waliosema kuwa watajaza bahari mchanga ili wajenge mji mpya wameishia wapi? Nani atawekeza katika mji ambao hauna umeme au maji ya uhakika, hauna usalama wa raia wa uhakika, hauna njia za mawasiliano za uhakika ..........?

Hapa si suala la uwezo, hao jamaa watawafukuza wananchi, watakata miti na kuharibu mandhari na kutuachia deni sisi! Hakuna free lunches duniani hata tutake vipi.

Amandla......
 
Hapa si suala la uwezo, hao jamaa watawafukuza wananchi, watakata miti na kuharibu mandhari na kutuachia deni sisi! Hakuna free lunches duniani hata tutake vipi.

Amandla......
halafu wao watafaidika nini kwa kuwafukuza wananchi na kuharibu mazingira
 
TUMEPOKEA kwa masikitiko makubwa amri ya serikali kusimamisha utoaji hati za ardhi kwa wote wenye nyumba na viwanja huko Kigamboni. Kwa kifupi kulingana na sheria mpya ya ardhi inayotka kumpa uwezo mwananchi kuitumia ardhi kama njia ya kujikwamua na umasikini huu ni uonevu na mauaji ya kiuchumi.

Ni haki kwa kila mtu hata kama ananunua ardhi leo huko Kigamboni kupewa hati ya ardhi ili hao wenye matrilioni ya halali na ufisadi wanapotaka kuja kujenga wanunue ardhi hiyo toka kwa wananchi na sio kwa wajanja wachache serikalini.

Inavyoonekana ni kwamba Wizara ya Ardhi inataka wao na wanasiasa waliowaweka hapo wafaidike pale ardhi hiyo itakapopaa bei na wananchi wa kawaida Kigamboni waendelee kula kisamvu, dagaa na ugali wa bada. Hilo hatulikubali.

Tunaomba serikali itengue uamuzi huo na kama wizara hiyo haina fedha ya kutengeneza hati za umiliki viwanja na ardhi basi wapewe wakala watu au makampuni yenye uwezo kufanya kazi hiyo. Inatuuma sana maana wizara hii ndiyo inachoyachangia kwa kiasi kikubwa umasikini wetu na matatizo yanayotukabili sisi wananchi wa kawaida hapa Tanzania.

Haya ndiyo matunda ya kuichagua CCM! Endeleeni tu. Mnalalamika nini? Si mmeyataka wenyewe? Na wala hamkulazimishwa. Bado hamjapata uchungu wa kutosha. Siku mkiupata, ndio mtafanya mabadiliko, lakini kwa sasa, HAMJAKAMULIWA DAMU vya kutosha. Bado iko nyingi.

Jenerali Ulimwengu alisema: Ukichagua hovyo, ukatendewa hovyo, usiseme hovyo!

Nafasi ya kufanya mabadiliko bado ipo. Oktoba 31, 2010. Ukiichagua tena CCM, HUNA HAKI ya kulalamika UKITENDWA!
 
Kwanza kabisa huo ni mpango wa serikali kuu na sio mpango wa jiji, DCC haikuhusishwa na hayo matangazo wala michoro inayowavutia watu wengi kiasi cha kupoteza mwelekeo.

Huo mji mpya aka Dubai ya bongo haistaili kujengwa Kigamboni. Historia itakuja kutuhukumu. Hakuna sababu yoyote ya kufukuza watu na kuporomosha magorofa makubwa hata kama watajenga pia taasisi za elimu kama vyuo vikuu n.k. Swali ambalo Watanzania wengi inabidi tujiulize ni kuwa kwanini Kigamboni?
Kwa kuwa kijiografia Kigamboni ina pitika kupitia eneo la biashara la Dar, hilo tatizo la misururu ya magari itaongezeka mara 10. Na ninaweza kuhakikisha hii kwa urahisi sana. Sasa kama watu wanapigana na foleni sasa hivi, fikiria itakuwaje wakati hayo magorofa yamejengwa (sijui lini?). Wanasema kuwa watajenga madaraja 3 na tunnel 1 kutoka Old Dar kwenda New Dar (K'mboni) bado kula walakini kwa barabara za sasa za Old Dar kuhimili ongezeko la watumiaji. Hapa ni kama hesabu za 1+1=2 lakini wao wanafikiri tunawaza 1x1=1.
Ushauri wa bure kama kweli wanafikiria kujenga Dubai fulani hivi Tanzania (kwa sababu ya utalii n.k), basi waijenge maeneo ya mwambao kati ya Bagamoyo na Tanga ama Kati ya Kisarawe na Mtwara. Na hayo matrilioni wanayopanga kuwalipa wahamishwaji na kujenga madaraja na mahandaki wajenge barabara za lami nzuri tu ziunganishe Dar na hio Dubai ya Bongo. Wasitudanganye kuwa eneo la bichi limebakia moja tu na ni K'mboni). Serikali makini haiweze kufanya kitu kama hiki hata siku moja.
IT IS TIME TO KILL THIS PROJECT ANYWAY, SOONER THAN LATER
 
Lets be serious unajua nina plot kule niliinunua kama 1.5mil niko karibu na ile Zoo ni kama 15 km toka ferry sidhani kama tunausika
 
Lets be serious unajua nina plot kule niliinunua kama 1.5mil niko karibu na ile Zoo ni kama 15 km toka ferry sidhani kama tunausika

Kwa sasa unaweza kuiuza kwa 20 mil kama unataka, bei imepanda mara kumi almost...
 
kuna yeyote mwenye taarifa latest kuhusu hii stop order na maendeleo ya Mradi huu? 2011 ndo hii inakatika!
 
Ningefurahi kama wangechukua bomu mpja kubwaaaaa, wakatumalizia mbali huko tukapumzike halafu wao waendelee kufaidi maana inaonekana kama vile tunawawekea kiwingu hapa....yaani inaonekana kama vile kuna wengine wana haki zaidi ya wengine..................
 
Hii ni kwa waathirika wa Mradi huu.Kutakuwa na Mjadala kwenye Tv kuhusu Mradi wa Kigamboni kama si kosei Star Tv saa tatu na Nusu hivi.
 
Back
Top Bottom