Kigamboni hatunayo tena. Nimeona picha kwa shushushu mmoja ni video kabisa. Pia inapatikana kwenye chuo cha ardhi ambako wameipata kujifunzia planners. Ile video inasema 'kigamboni the new city' iko kwa kiingereza,ni mpango wa marekani,inaitwa intensive investment na inasema utakuwa mji wa kwanza wa kifahari Africa,ukifuatiwa na S.Africa,ama kweli ukiona picha utaipenda. Pia kutakuwa na kambi mbili za majeshi. Mpango uu una unaanza rasmi mwakani,utaanza na ujenzi wa daraja la kigamboni,ukivuka tu unakutana na majengo ya ghorofa na hotel na parking za kumwaga. Phase ya kwanza inaisha 2025 phase II itaanza 2025-2035. Du ukiangalia utalia,mwisho kuna picha ya dr. JEYKEy kavaa suti nyeusi,tai nyekundu. Kumbuka yaliyoipata Misri ya Suez Canal ndo naisi itaikuta Tz,yani payback kwa large investment ni ngumu,mwisho wake ni kuingia kwenye mikataba ya kikoloni, ya madini na majeshi. Mie simo.