Tulifika Pabaya: Mwenyekiti Ulinzi na Usalama Wilaya eti ni Jambazi?

Wakwepa Kodi nchi nzima walikuwa Hai tu
 
Hayo makosa ni Yale yanayodhaniwa kufanyika miezi michache iliyopita.
No, kuna makosa ya rushwa yametajwa ni ya miaka mingi kulingana na ushahidi uliopelekwa PCCCB
 
Usimuite jambazi subiri mahakama imtie hatiani kwanza
 
CCM haiwezi kumtupa Ole Sabaya, alipelekwa Hai kuhakikisha Mbowe harudi bungeni. Amelitekeleza vyema jukumu lake.

Usishangae kuwa sasa hivi Ole Sabaya ana cell yake na chakula anakula cha nyumbani. Wewe ulisikia wapi mahabusu anamvimbia mkuu wa gereza.

Jiandaeni kumlipa Sabaya gharama za usumbufu kupitia kodi yenu.
 
JPM alifanya Sana Mambo ya kihuni kwenye uteuzi, aliongoza kwenye utumishi wa umma vibaka na wahuniwahuni wengi Sana serikalini.Mambo yaliyofanywa na sabaya ni zaidi ya uhuni...
 
Wewe ni kenge mweusi
 
Ogopa sana watu waliopewa madaraka hao ndio wanakuwa more than majambazi.

Polisi amepewa haki ya kulinda raia na mali zao ni kama fisi kumkabidhi bucha ukipata polisi asiye na maadili anakuwa zaidi ya jambazi maana atatumia sheria vibaya.

Sabaya alitumia loop hole hiyo.
 
Miaka yote Mbowe ana shinda Hai, na hakujawahi kufanyika yaliyofanyika na Sabaya,
 
Unashangaa la mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya!!
Hushangai kuwa na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama jambazi na muuaji!!??
 
Pia naomba tupaze sauti kwa pamoja ili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda aweze kushitakiwa kwa makosa aliyoyatenda akiwa mkuu wa mkoa. Ushahidi upo wa kujitosheleza kabisa. Mfano mzuri ni lile tukio la uvamizi na unyang'anyi wa kutumia silaha(Armed Robbery) katika sehemu ya kazi ya radio ya Mawingu.

Matukio mengine anayohusishwa nayo ni ni pamoja na suala la utekaji wa raia wa Tanzania mfano Roma, Mo.

Tupaze sauti kwa pamoja ili haki itendeke.
 
Pia naomba tupaze sauti kwa pamoja ili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda aweze kushitakiwa kwa makosa aliyoyatenda akiwa mkuu wa mkoa. Ushahidi upo wa kujitosheleza kabisa. Mfano mzuri ni lile tukio la uvamizi na unyang'anyi wa kutumia silaha(Armed Robbery) katika sehemu ya kazi ya radio ya Mawingu.

Matukio mengine anayohusishwa nayo ni ni pamoja na suala la utekaji wa raia wa Tanzania mfano Roma, Mo.

Tupaze sauti kwa pamoja ili haki itendeke.
 
Kwa akili yako unataka tuamini Hai ndo wilaya yenye matajiri kuliko wilaya zote nchini! Na kwamba matajiri wa Hai wanafanya biashara haramu zisizoweza kukamatwa na vyombo halali vya ulinzi na usalama mpaka DC aingilie kati na kuingia front mwenyewe.
1.Kwamba Momba yenye mpaka wa Tunduma ambako tulisikia wafanyabiashara wanakimbilia upande wa pili DC wake hakuwa na akili nzuri za kizalendo kama Sabaya akachukua SMG na kuvamia maduka yao ili kuchukua kodi? Ni sheria ipi inayomruhusu DC kukusanya kodi kwa mtutu wa Bunduki?
2.Kwamba Tarime yenye Mpaka wa Silari hakuna matajiri ambao wangeweza kutekwa na DC wa huko ili kuwatia adabu walipe kodi?
3.Kwamba wilaya zote nchini zilikuwa na ma DC wasiojua wajibu wao isipokuwa Hai?

Mapenzi ya kitoto raha sana, mnapendana kitotototo, mwenzio akichukuliwa na wazazi wake akaoge wewe unabaki unalia umeonewa!!
 
Aliyoyafanya Sabaya hayakuwa siri na alisaidiwa na systemen. Mlimsikia RPC anamwambia Mbowe hatashinda uchaguzi 2020. Nilifikia sehemu ya kuichukia Tanzania.
 
Chini ya Marehemu sote tunajua yaliyotokea. Na kuna mengi sana ndani Mkuu, basi tu mengine hayatamkiki lakini kila kitu kilitoka juu kwa Mtu mmoja tushukuru Mungu alipanga yake. Sote hatukuwa na fahari ya Utanzania
CCM bado ni ile ile, kuna waliomsaidia Sabaya ku facilitate aliyoyafanya na bado wana nguvu ndani ya chama na serikalini.
Muda utatuambia. Lakini ninaona tunapigwa changa la macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…