Tulifika Pabaya: Mwenyekiti Ulinzi na Usalama Wilaya eti ni Jambazi?

Tulifika Pabaya: Mwenyekiti Ulinzi na Usalama Wilaya eti ni Jambazi?

Nimeiona hiyo Mkuu, tunapigwa changa la macho. Mpaka tukae sawa movie imekwisha.

akiwa RPC arusha,mkurugenzi wa PCCB kwa sasa aliwahi kumpa mtuhumiwa cheti cha kutambua mchango wake kwenye maswala ya kiusalama.

lakini sasa anatakiwa akawe miongoni mwa mashahidi akiwa RPC kwa kama ripoti za uhalifu wa jamaa yetu zilifika kwake.

wiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Hili la sabaya kwa sasa ni tuhuma ambazo msingi wake kwa wengi ni kisasi tu. Na hapo ndio tunaona mama ni msaliti wa magufuli kwa kumtupa lupango kada wa ccm aliyetimiza wajibu wake hadi kuking'oa chama cha upinzani kwenye jimbo. Wana ccm kiitikadi wana shaka na samia. Hawana imani nae.
Wewe ni mwanaCCM au jambazi kama Sabaya?

Uliambiwa wapi kwamba kazi ya mkuu wa wilaya ni kung'oa wapinzani kwa kutumia njia haramu? Wapinzani walikuwa wanaongoza hai tu nchi hii? Huko kwingine mbona wakuu wa wilaya hawakufanya ujambazi na uhuni wa Sabaya?

Endeleeni kudemka tu nyinyi wapambe wa Sabaya. Tutawadaka mmojammoja mpaka mnyooke.

Tunataka nchi inayoongozwa kwa misingi ya haki na sheria. Period.
 
Halafu kila J2 siku ya Ibada atalazimisha kuhutubia na kuomba mniombee!!!
Siasa za nyumba za ibada sijui hata waliwezaje kumkubalia.
Afadhali sasa hivi wengine watarudi kushiriki ibada..
 
Matajiri wapo Wilaya ya Hai tu hapa Tanzania? Mbona Wakuu wengine wa Wilaya hatukuwasikia wakipambana na Matajiri walipe kodi? Kwa nini Sabaya peke yake? Au yeye ndiye Magufuli ajaye?
kweni unadhani utendaji kazi wako ni sawa na wafanyakazi wenzio au wafanya biashara wenzio mtaani?unaweza ukawa ni kilaza na wenzio ni mahili wa kupambana na maisha
 
Wewe ni mchaga pumbavu kuliko wapumbavu
Mimi ni mmakonde, uchaga umetoka wapi wewe msukuma usiyetahiriwa?
Bwana wenu ashaoza analiwa na mafunza mwaka huu tunauza korosho kiroho safi. Manina.
 
Naomba tukubaliane wote, kwamba nchi hii katika awamu ya tano tulifika pabaya sana chini ya Amirijeshi mkuu Magufuli.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa au wilaya (RC or DC) ni mtu muhimu sana katika eneo husika kwa ajili ya usalama na ulinzi.

Sasa tulifikaje hapa ambapo mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya anafikia hatua ya kushtakiwa kwa unyang'anyi wa kutumia silaha (ujambazi)?

Inamaana serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli ilikuwa haijajui haya aliyokuwa anatenda DC huyu? Au ilijuwa ikanyamaza kwa vile ni DC wa Hai? na ndio maana watetezi wa Sabaya makada wa CCM, walimtetea sana?

Mnaona uchama CCM ulivyokuwa umeifikisha mahali pabaya nchi?

Hii maana yake ni kuwa, kama ya sirini ya Sabaya yanajulikana basi walio mpiga risasi Lissu na kumuua Akwilina mchana wanajulikana, walioteka watu mchana wanajulikana nk.

Sasa ili nchi isafishike walio tenda maovu wote kwa kutumia kivuli cha serikali ya Jamhuri ya Tanzania washughulikiwe bila aibu ili kuliondolea balaa taifa (hii Mshana Jr ) anaweza kuielezea vizuri zaidi maana pengine inahitaji maombi au kafara ya kitaifa.

TULIFIKA PABAYA KAMA TAIFA
Majambazi yalikuwa (yapo) mengi sana kuanzia
1. Uvccm. 2. Hai. 3. Rorya. 4. Arumeru 5. Arusha Mjini 6. Bashite 7. Dotto 8. DPP 9. Musiba n.k
 
kweni unadhani utendaji kazi wako ni sawa na wafanyakazi wenzio au wafanya biashara wenzio mtaani?unaweza ukawa ni kilaza na wenzio ni mahili wa kupambana na maisha
nadhani issue hapa ni why him? nakubali utendaj haufanani yes. but why him?
wako wenzake walikuwa stationed mikoa hatari.. kanda maalum lakin mpaka mama samia anaapa hawana allegation chafu.

why yeye? why si wenzake?
 
Kuna uongo mwingi hapa kwa sababu sasa liko kundi lenye uoga kwa matajiri wakwepa kodi na wazungu washenzi wezi wa Mali za umma.

Sabaya katolewa Kafara tu kwa kumtungia kesi za uongo kwa sababu ya wenye pesa kuweka nguvu ktk kila sehemu panapo mshutumu Sabaya ili aangamizwe,kwa ninavyo wajua waTanzania matajiri ni kweli wakati Sabaya akiwawajibisha kulipa kodi siamini kama aliwaonea,hao hua ni wakwepa kodi wakubwa kwa nguvu za pesa wanahonga kuvusha mizigo yao ya kibiashara

Swala la Hayati JPM linaendelea kushutumiwa kwa uongo na nina hakika 90% ya wanaozusha haya ni watu wa Kaskazini wabinafsi na wapigaji...ni ngumu sana kuondoa upendo wa JPM kwa watu zaidi ya 85% hapa nchini isipokua ni watu wasio sema sema wala hawaingii mitandaoni.

Nchi hii mtu ukiwa mkali na kutetea wengi wasinyonywe na wachache unaitwa dikteta,ukiwa mpole na watu wanaiba wanafurahi na wale wasio na mianya ya kuiba wanakuita dhaifu

Tanzania ni nchi yenye watu wasiojua wanatakaga nini.
Kwanini alichukua jukum la tra?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
HAAAAAAAA wewe naona ni jambazi wenza wa ole saa baya na wenda zake, sasa unajaribu kumutetea muuaji, mwizi na sijui niseme nini, wataka kusema jiwe hahusiki na kupotea kwa azory gwada, ben saa nane, kupigwa risasi 37 mhe tundu lissu, kuiba uchanguzi mchana kweupe hapo 2020, sasa pale dodoma ni makofi tu kwa serikali, mr or mrs you must be suffering from a very seriuos mental illness, see a doc as soon as possible, kuwa na akili sio fermented porridge in your head pls, kapelekee saa baya sabuni na dawa ya meno pale remand home arusha
 
Matajiri wapo Wilaya ya Hai tu hapa Tanzania? Mbona Wakuu wengine wa Wilaya hatukuwasikia wakipambana na Matajiri walipe kodi? Kwa nini Sabaya peke yake? Au yeye ndiye Magufuli ajaye?
Nashangaa....
 
Kuna uongo mwingi hapa kwa sababu sasa liko kundi lenye uoga kwa matajiri wakwepa kodi na wazungu washenzi wezi wa Mali za umma.

Sabaya katolewa Kafara tu kwa kumtungia kesi za uongo kwa sababu ya wenye pesa kuweka nguvu ktk kila sehemu panapo mshutumu Sabaya ili aangamizwe,kwa ninavyo wajua waTanzania matajiri ni kweli wakati Sabaya akiwawajibisha kulipa kodi siamini kama aliwaonea,hao hua ni wakwepa kodi wakubwa kwa nguvu za pesa wanahonga kuvusha mizigo yao ya kibiashara

Swala la Hayati JPM linaendelea kushutumiwa kwa uongo na nina hakika 90% ya wanaozusha haya ni watu wa Kaskazini wabinafsi na wapigaji...ni ngumu sana kuondoa upendo wa JPM kwa watu zaidi ya 85% hapa nchini isipokua ni watu wasio sema sema wala hawaingii mitandaoni.

Nchi hii mtu ukiwa mkali na kutetea wengi wasinyonywe na wachache unaitwa dikteta,ukiwa mpole na watu wanaiba wanafurahi na wale wasio na mianya ya kuiba wanakuita dhaifu

Tanzania ni nchi yenye watu wasiojua wanatakaga nini.
Km ww ulivyo na uhakika kuwa hayo yote yanazushwa na watu wa kaskazini basi ndivyo ilivyo kwenu pia,tunawatambua wote mnao mtetea aliekuwa dikteta kuwa mnatokea kanda ya ziwa,...hivi Tanzania kuna wakuu wa wilaya wangapi?...INA maana hao wote waliobakia hawakuwa wakisimamia ukusanyaji wa kodi kwnye wilaya zao?...na kimsingi mkuu wa wilaya sio mkusanya kodi na wala hahusiki kuingia dukani kwa mfanya biashara na kuanza kuhoji na kukagua,hio ni kazi ya afisa wa tra,unless mkuu wa wilaya aongozane na afisa wa tra maana ndio mwenye uelewa wa masuala ya kodi na sio DC,lkn mpuuzi yule wa Hai alikua anaingia kwenye maduka akiwa na kundi lake LA mtaani,akijitahidi sana bac anachukua na askari wawili washkaji zake ambao baadae atawapa mgao wao,huyo jamaa ni jambazi linalotakiwa kwenda jela miaka mingi sana,litoke limezeeka.yaani kwa kua kwako ni arusha basis ndio atoke hai kuja kupambana na wafanyabiashara wa arusha kimabavu kweli???....INA maana viongozi wa arusha hawawezi kufanya hio kazi hadi waje wasaidiwe na DC wa hai,semeni yote mtakayosema,lkn lijamaa ni jambazi sugu,na liliwekwa madarakani makusudi na kwa lengo maalum na jambazi kuu mwendazake wenu huyo,alijua kabisa hai ni pagumu kwa MTU asie mbabe na jambazi,na alijua yote yanayotendeka pale ila alifumba macho ili lengo LA kunyoosha viongozi wa hai kuanzia mbunge,madiwani,wenyeviti na wajumbe ambao kwa asilimia krb zote walikua CHADEMA litimie,na pia alijua kuwa bila kuweka jambazi wale wachaga hawatawezekana,na ninakuhakikishia km jambazi kuu lisingekufa basi sabaya angepanda cheo na kwa RC mwaka huu huu au mwakani,hio inakuwa ni kama shukrani kwa kazi kubwa alioifanya hai,na lazime angeletwa dar aje kutesa watu km yule jambazi mwingine aliekuwepo dar,....wajinga hawawezi kuelewa Bali wataona jambazi kaonewa,......time will tell,just be patient na tumuombe Mungu atupe umri tutayaona mengi,usidhani mashtaka ya huyo jambazi yameisha,hayo yaliopelekwa kwa hakimu ni machachr sana ambayo uchunguzi wake umekamilika,lakini subir miezi miwili au mitatu utashangaa jambazi lina kesi 60 pumbavu zake
 
Hii nimeitoa humu Jf,...kuna mwamba kaipandisha km uzi kbs,........

=Mwaka jana mwishoni mfanyabiashara na mbunifu wa mavazi Jeffery Mmbungu maarufu kama @Speshoz alifungua kiwanda cha vinywaji vikali, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Kiwanda hicho kinaitwa Daren Fabrics Industries Ltd kinazalisha kinywaji chenye jina Faru John.

Mwezi February mwaka huu, aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alimpigia Jeff na kumwambia kuwa CCM itafanya maadhimisho ya miaka 44 tangu kuanzishwa, na yeye ni miongoni mwa wanakamati wanaoandaa maadhimisho hayo.

Akataka kiwanda hicho kichangie TZS 10M kufanikisha maadhimisho hayo. Jeff akamwambia hana uwezo wa kuchangia 10M, lakini akaahidi kuchangia 1M. Sabaya akamnanga kwamba serikali ya CCM ndiyo iliyomuwekea mazingira mazuri ya kibiashara hadi akaweza kufungua kiwanda, kwahiyo kuchangia 1M ni dharau kwa chama, anatakiwa achangie kiasi kisichopungua 10M.

Jeff akamwambia hana pesa hiyo. Sabaya akamwambia nimepitia transaction zako TRA najua unafanya mauzo ya mamilioni ya shilingi. Jeff akamwambia bado kiwanda ni kichanga na hakijaanza kujiendesha kwa faida kiasi cha kumpa Sabaya 10M.

Mwezi May mwaka huu Sabaya akavamia kiwanda hicho akiwa na mabaunsa wake. Wakawa-harass sana wafanyakazi waliokuwepo. Sabaya akiongozana na waandishi wa vyombo 11 vya habari akatangaza kukifunga kiwanda hicho kwa madai kinajiendesha bila vibali.

Vyombo vya habari vikaripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa kwa kufanya uzalishaji wa vinywaji vikali bila kuwa na kibali. Jeff akashangaa kwa sababu alikua na vibali vyote.

Ana leseni ya BRELA nambari 142255766 iliyotolewa July mwaka 2020. Ana leseni ya TRA nambari 142255766 iliyolewa July 2020. Ana leseni ya biashara nambari 03356294 iliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Hai tarehe 25 September 2020.

Ana Leseni ya mkemia mkuu wa serikali nambari B002C000255 iliyotolewa October mwaka 2020, pia ana Leseni ya TBS nambari 3082 iliyotolewa December 2020. Pia kabla ya kuanza uzalishaji alipewa barua ya ruhusa kutoka TBS yenye Kumbukumbu nambari QA/QCCA/3215/17.

Sasa akashangaa imekuaje kiwanda kifungwe kwa kukosa vibali wakati vibali vyote anavyo? Akampigia Sabaya kumuuliza. Akamwambia aende ofisini.

Alipofika ofisini, wakaongea na akamuonesha nakala za vibali. Sabaya akatoka ofisini na kumuacha ndani. Aliporudi akamnyang'anya simu zote, na kumuamuru akae chini. Akaita mabaunsa wake, wakamvua viatu na mkanda na kumpeleka rumande.

Taarifa za kukamatwa kwake zikafika kwa viongozi mbalimbali wa serikali. Wizara ya ya viwanda na biashara ikatoa tamko kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kwa mujibu wa sheria. Wizara ya uwekezaje, ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali, Shirika la viwango (TBS), pamoja na ofisi ya BRELA wakaingilia kati na kueleza kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kihalali.

Kesho yake Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro akafanya press na kutoa ufafanuzi kuwa kiwanda hicho kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa hiyo ikaeleza kuwa mwezi April kiwanda hicho kilipewa stika za 200M na kiliweza kuhuisha stika za 93M. Pia kwa siku chache za mwezi May (kabla hakijafungwa) kilikua kimehuisha stika za 13M.

Taarifa ya TRA ikaeleza kuwa kiwanda hicho hakijawahi kuwa na mgogoro wowote na serikali wala hakijawahi kujiendesha bila kuwa na vibali. Ikatangaza kukifungulia kiwanda hicho na kukiruhusu kiendelee na uzalishaji.

Media zote zilizoripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa zilialikwa kwenye Press ya TRA ili ziujulishe umma kwamba taarifa ya Sabaya haikua sahihi, na kwamba kiwanda hicho kimeruhusiwa kuendelea na uzalishaji.

Lakini Sabaya akazuia media hizo zisiripoti taarifa hiyo ya TRA. Ni ITV pekee walioamua kusimama katika misingi ya taaluma na kutoa ufafanuzi kwa umma. Media nyingine ziliamua kusimama na Sabaya. What a shame?

Tayari Jeff ameshaenda TAKUKURU kuwasilisha ushahidi wake. Pia atawasilisha malalamiko Baraza la habari nchini (MCT) ili media zilizomchafua na zikakataa kumsafisha zichukuliwe hatua, kwa sababu habari ya kiwanda hicho kufungwa imeathiri mauzo kwa kiasi kikubwa.!
 
Katika kadhia ya bwana mdogo huyu najaribu kuishawishi akili yangu ikubaliane nami kuwa ya hadharani aliyafanya hadharani na ya kizani aliyafanya kizani kisha mengine ya hadharani aliyahamishia kizani.
 
ati kuna nyumba ya mateso aliita -GOLGOTHA. - ha ha ha ha
 
Alitumwa kuuwa upinzani matokeo kafa yeye kisiasa na upinzani still ungalipo
 
Kumtumikia shetani akujawahi kuwa na faida kabaki mwenyewe na Zigo lake acheze nalo
 
Back
Top Bottom