Tulikuwa tunaambiwa USA inaendeshwa kitaasisi na si maamuzi ya mtu mmoja. Mbona sasa tunashuhudia vituko?

Nyumbu hawajawahi kujitambua hata kwa dakika moja tu
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja.
. Kwamba katiba yao ndio inaamua,
Kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?
 
Yani USA sasa haina tofauti na nchi za kiafrika maamuzi yanatolewa na mtu mmoja tu
Miaka yote waafrika tunafanya Hivyo hivyo, kwahiyo jambo baya sisi tunataka tunaona sawa, Leo kafanya Trump tunahoji!
Shithole countries.
 
Kwahiyo pale alipo anaweza hata kuamuru kubonyezwa kitufe cha nyukilia kulipua nchi flani bila kuingiliwa na yeyote
Hapana, kuanzisha vita lazima bunge lihusike ila haya mengine yapo ndani ya uwezo wake, kusimamisha misaada kisa watu wanatumia misaada hiyo vibaya sio hata complicated sana
 
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja. Kwamba katiba yao ndio inaamua, kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?
Trump is running America like it's his own house. Those who used to say America has strong institutions should come here and tell us what we're witnessing under Donald Trump's leadership. It's a total disaster for a nation that calls itself a first-world country.
 
Sasa si ndio "one man show" yenyewe kama ilivyo huku afrika tu.

Kumbe katiba yao haina tofauti na zetu.
Sio one man show, mambo mengi anayoyafanya aliahidi kwenye kampeni; nashangaa wanaomlalamikia aidha ni wapinzani wake (wako nje ya utekelezaji) au raia ambao hawajampigia kura, sidhani kwamba anakaa na kuamka tu na kuamua, cabinet yake nayo inapenda mshike mshike wa aina hiyo....... makosa ya kutumia diplomasia kama muhula wake wa kwanza harudii
 
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja. Kwamba katiba yao ndio inaamua, kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?
Nimeshaawahi kuuliza hili swala kwa wale mahbuuba wa usa .. nimegundua rais wa usa ni mtu mwenye nguvu sana
 
Sio one man show, mambo mengi anayoyafanya aliahidi kwenye kampeni; nashangaa wanaomlalamikia aidha ni wapinzani wake (wako nje ya utekelezaji) au raia ambao hawajampigia kura, sidhani kwamba anakaa na kuamka tu na kuamua, cabinet yake nayo inapenda mshike mshike wa aina hiyo....... makosa ya kutumia diplomasia kama muhula wake wa kwanza harudii
Kumbe na kwenyewe US unaweza usitumie diplomasia na ikawa poa tu?
 
Maamuzi anayofanya Trump YAPO ndani ya mamlaka yake kama Rais, mimi na wewe pamoja na wamarekani Gen Z tunaona ajabu kwasababu ni kwa muda mrefu rais hajawahi kutumia mamlaka yake namna hii
Si Kweli kavunja Katiba na sheria mara kibao, kuna kesi za kutosha tu ila hazina nguvu sababu yupo kwenye power.

Mfano
Kwenye Katiba ya Marekani Congress wana uwezo wa kulimit spending za Government, serikali hairuhusiwi kutumia ama kuzuia matumizi ambayo yamepitishwa na Bunge

Trump alivyoingia Madarakani kuna vitu kibao vilivyopitishwa na Bunge amevikataa kwa kisingizio haviendi na will of America

Mfano wa kesi

Sasa hivi Usa kuna Constitutional crisis
 
Trump sasa hivi anaangalia maslahi ya America kwanza yaani akikusaidia wenyewe wanafaidika nini?
Maslahi ya matajiri kama Musk, siku akitoa huduma za Afya, Elimu na vitu vingine vya msingi bure nishtue, Ulaya, Middle East na karibia Nchi zote Tajiri Duniani vitu kama Afya na Elimu si tatizo tena ila Nchi kubwa kama Usa bado wanajadili Bima za Afya kama Tanzania tu. Kupata Degree unaingia Deni unalolipa karibia maisha yote.
 
Trump anadai mifumo ilimkwamisha sana muhula ya kwanza. Muhula huu walikuja na kitu wanaita project 2025. Moja ya malengo ni kutimua wafanyakazi wa mfumo, na kufanya wengi kuwa wateuliwa wa rais ili kuweka wapambe kama huku kwetu.
 
Trump alivyoingia Madarakani kuna vitu kibao vilivyopitishwa na Bunge amevikataa kwa kisingizio haviendi na will of America
Kavizuia kwasababu katiba inamruhusu kuvizuia , angekuwa kavunja sheria kwa kufanya hivyo tayari wapinzani wangeanza zengwe la impeachment ili aondolewe
 
Umesoma hio kesi? Wameshinda vipi hao jamaa kama Katiba inaruhusu?

Nipe ushahidi wa Katiba ya Marekani kwamba Anaruhusiwa ku overrule spending alizoekewa na Bunge.
 
Anatumia Executive Orders na huwa zinapingwa mahakamani, mahakama inaweza kuzipindua au kuacha zifange kazi. Je tanzania mnaweza hivyo
 
Trump anadai mifumo ilimkwamisha sana muhula ya kwanza. Muhula huu walikuja na kitu wanaita project 2025. Moja ya malengo ni kutimua wafanyakazi wa mfumo, na kufanya wengi kuwa wateuliwa wa rais ili kuweka wapambe kama huku kwetu.
This makes sense, utafanyaje kazi na watu wanaokupinga every step of the way? Una ajenda na maono basi wapinzani katika utekelezaji wako weka mbali
 
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja. Kwamba katiba yao ndio inaamua, kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?

Inashangaza sana, Trump kamchukua mshkaji wake mr Elon Musk ambaye sio raia wa Marekani na kumpa wizara mpya.

Kumbe hata marekani Rais ndie muamuzi mkuu
 
Umesoma hio kesi? Wameshinda vipi hao jamaa kama Katiba inaruhusu?

Nipe ushahidi wa Katiba ya Marekani kwamba Anaruhusiwa ku overrule spending alizoekewa na Bunge.
Rais wa Marekani hawezi kubatilisha au kukataa moja kwa moja matumizi ya bajeti yaliyoidhinishwa na Kongresi. Hata hivyo, Rais ana mamlaka fulani yanayoweza kuathiri matumizi ya fedha:

1. Mamlaka ya Veto – Rais anaweza kuweka veto kwenye mswada wa matumizi uliopitishwa na Kongresi, lakini Kongresi inaweza kubatilisha veto hiyo kwa kura ya theluthi mbili katika Baraza la Wawakilishi na Seneti.

2. Kuzuia Matumizi (Impoundment) – Rais anaweza kupendekeza kuchelewesha au kuzuia matumizi ya fedha fulani kupitia impoundment, lakini tangu kupitishwa kwa Sheria ya Udhibiti wa Impoundment ya 1974, Kongresi lazima iidhinishe kufutwa kabisa kwa fedha hizo.

3. Uhuru wa Utendaji – Kupitia mashirika ya serikali, Rais ana uhuru fulani wa kusimamia jinsi fedha zinavyotumika ndani ya mipaka ya bajeti, lakini hawezi kupuuza au kupingana na matumizi yaliyoidhinishwa na Kongresi.

Kwa ufupi, ingawa Rais ana njia kadhaa za kushawishi matumizi ya bajeti, hawezi kufuta au kukataa kutumia fedha zilizoidhinishwa na Kongresi bila athari za kisheria (na mpaka Sasa hajatoka nje ya mipaka hii, angekua ametoka wangekuwa washaitisha mswada wa "kukosa Imani na Rais"
 
Sijakuuliza opinion yako, nimetaka ushahidi, najua na wewe pia una opinion zako
 
Wakuu, kwa miaka mingi tuliambiwa maamuzi yoyote pale USA ni ya taasisi na si mtu mmoja. Kwamba katiba yao ndio inaamua, kwamba hata akija Rais kichaa anaongoza maana yeye si mtoa maamuzi pekeake.

Lakini hiki tunachoshuhudia sasa hivi mbona ni kama Afrika tu?

Yani Trump sasa hivi anaweza kuamka tu na kutoa tamko kwamba toa hiki weka pale, kile leta hapa.

Mfano mzuri ni ishu misaada kwa Afrika, na hili la kujitoa WHO na sasa eti anapanga kujitoa UN.

Mbona mimi naona kama US mfumo wao wa uongozi ni mbovu kuliko Afrika?
We unadhani ni maamuzi ya mtu 1?,mi naona ni maamuzi ya wazungu wa marekani wengi ila walikuwa wanatafuta mtu sahihi wa kuimplement.
 
Sijakuuliza opinion yako, nimetaka ushahidi, najua na wewe pia una opinion zako
Huo hapo ndio ushahidi wenyewe , nimefanya inquiry juu ya sheria za Marekani na muktadha ambao Rais anakuwa kavunja sheria
Loophole anayotumia Trump ni hiyo ya kuwa na wabunge wengi ndani ya congress, tangu ameanza mpaka Sasa mambo yote ambayo ameruhusiwa kufanya kafanya kisheri na lolote lenye ukakasi au liko nje ya mipaka yake kama ulivyoona hapo congress imelipinga
 
Back
Top Bottom