Tulikuwa tunaambiwa USA inaendeshwa kitaasisi na si maamuzi ya mtu mmoja. Mbona sasa tunashuhudia vituko?

Chadomo huwaga ni roporopo wanaweza kudanganya wajinga tuu.

Rais ndio Kila kitu kwenye Nchi yeyote hakuna Cha Katiba Mpya Wala ya zamani.
ChoiceVariable "take zako" huwa ni vihoja na mihemko sana kwa sababu ya uelewa wako finyu wa mambo, nikikumbuka ulivyoandika uzi mrefu kuwazodoa "machedema" kwamba Tanzania ina sheria nzuri za Madini kuliko Botswana nacheka sana.
 
ChoiceVariable "take zako" huwa ni vihoja na mihemko sana kwa sababu ya uelewa wako finyu wa mambo, nikikumbuka ulivyoandika uzi mrefu kuwazodoa "machedema" kwamba Tanzania ina sheria nzuri za Madini kuliko Botswana nacheka sana.
Kinachokuchekesha ni kipi? Kwani ni uongo?
 
Nchi haiwezi kuwa inaongozwa kwa one-man show akaja kiongozi kugeuza na kufanya iongozwe kitaasisi?

Taasisi haziyumbi, kuanguka au kufa kabisa??
Sio kwa Marekani ndugu zangu, hiyo nchi na nchi nyingine ambazo mnaona zinaendelea Karne hii sio kwasababu ya "one man show" bali kwasababu ya taasisi imara

Trump ni populist, yaani angekuwa nchi hizi zetu zenye taasisi legelege yeye na Mobutu wangekuwa na tofauti kidogo sana ila kitu kama hicho hakiwezi kutokea Marekani kwasababu tangu hiyo nchi inaanza misingi ya Katiba kufuatwa strictly imesimikwa na kujichimbia kabisa kwenye taasisi zake

Chochote afanyacho Trump atakifanya ndani ya Katiba ambayo imempa mamlaka ya kufanya hivyo, na vile vile ndani ya mamlaka yake hiyo hiyo Kuna "handbreak" ambazo zinafanya kazi (mabunge ya Congress na Senate, bila kusahau Judiciary ambayo nayo sio ngeni "kumsawazisha rais")

Kwa ufupi: Hamna kitu Trump atafanikiwa kufanya ambacho kitakuwa nje ya katiba
 

" ......MBONA MIMI......"

☝️☝️☝️☝️☝️
 
Kuna kitu unashindwa kuadmit, hizi show si ni kama executive orders za jpm? Ukizigeuza zikatolewa tokea afrika inakuwa udikteta
 
Basi katiba yao ni mbovu sana kama zetu tu.

Kama mtu anajiamkia tu asubuhi anasema futa kile, leta hili.
Tujitoe kule, tuingie kule hapo maana ya taasisi haipo
Wabongo watabisha na walokole wao huwaambii kitu kuhusu hilo taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…