Tulimchukia Hayati Magufuli bila sababu za msingi, sasa tumetambua kuwa alikuwa sahihi, yanayofanyika sasa ni aibu

Tatizo letu sisi kama wananchi hatuna tunachofanya ili kubadili au kupata tunayo yataka, kazi yetu kuishia kuongea tu humu mitandaoni basi. Hivi kama kweli Magufuli alikuwa antesa na kuuwa watu ndio tuseme hayo yalikuwa mapungufu yake hivyo tuliacha tu kwa sababu kila mtu ana mapungufu yake na sasa tunasema Samia anauza nchi bado tunaacha na kuishia kulalamika na kuyapokea kama mapungufu yake?
 
Magu alikuwa Rais mzuri na mwenye vision kwa kiasi fulani kosa alilolifanya ni kuminya haki na uhuru wa watu ikiwa ni pamoja na kuteua baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao walikuwa wanafanya kazi kama viongozi wa genge la mamafia
Ndio ilitakiwa iwe hivyo,na hata mimi ningekuwa rais ningefanya hivyo.watanzania hatuna utii wa sheria,ili kuwanyoosha watanzania,ni lazima utumie nguvu.china ilijengwa kwa nguvu,singapole,malaysia,urusi,ufaransa.zimejengwa na viongozi wagumu na wenye misimamo migumu.democrasia na maendeleo ni mbingu na nchi.huwezi kupata maendeleo kwa kutumia democrasia,hata wewe leo lete democrasia kwenye familia yako,uwape uhuru wa kila mtu afanye kila analotaka,utaona! Familia itakushinda.
Anzisha kiwanda leo,halafu ruhusu democrasi,utafilisika.

Nchi ni familia,nchi ni kama kiwanda,mipango ya mkuu wa familia ndio itaiinua famila na taifa.
 
Werevu wake umelifikisha Taifa hapa na hatuna wa kumlilia maana yeye alishamaliza kazi yake acha Mama Samiah na timu yake wafurahie kuisambaratisha nchi kama kitabu.Alianza na mbuga ya Ngorongoro akafanikiwa,akaja na Bonde la Usangu akashindwa,amekuja na la Bandari ameshinda 100% kwa hiyo tusubiri mengine katika nchi ya mababu zetu waje watu from nowhere kuja kutuendesha na kututawala.
 

Mfumo wetu wa sasa Inategemea sana utashi, vision, mikakati, ufuatialiaji wake, na vipaumbele vyake, vitendo vyake, maneno yake hata akili zake.

Ukiongeza yuko juu ya Bunge, mahakama, katiba, anachagua, kuteua watu wote wa maana, ana kinga ya kutoshitakiwa ni mungu katika hii nchi.

Tunahitaji katiba mpya kujenga msingi mzuri.
 
Ujinga ni mzigo,wala hujishughurishi na kujua kile mwenzio amesema,weww unalipuka tu kama kichaa amekata kamba.changia maada baada ya kuisoma na kuelewa.
 
Sasa si kila mtu anawaza familia yake. Mtatoboa vipi? 🤣 Ukianzisha movement wewe ndio utaonekana kituko mbele ya watanzania wenzio hao hao ambao wanalalamikaga🤣🤣🤣 ubinafsi, chuki na unafiki ndio kitu watanzania wanakiweza kwa 100%
 
Umetambua wewe na nani? Mbona mi mpaka Leo namchukia kwa sababua alinifanya kuwa maskini Leo ndo angalau najikongoja
 
Lipi alifanya jpm lika umiza wananchi?. Mimi silioni.nionyeshe wewe jamba alilofanya jpm la kujinufaisha yeye binafsu na kuwa umiza wananchi.

Tofautisha wanachi ns magenge ya kipigaji na uporaji alyokuwa akipambana nayo jpm.
 
Hebu nitajie jambo moja ambalo upinzani umewahi kuzuia bugeni?,hoja ngapi za hovyo zimepitishwa bungeni kipindi cha kikwete na upinzani ukiwemo?. Acheni upumbavu.
 
Magu alikuwa Rais mzuri na mwenye vision kwa kiasi fulani kosa alilolifanya ni kuminya haki na uhuru wa watu ikiwa ni pamoja na kuteua baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao walikuwa wanafanya kazi kama viongozi wa genge la mamafia
Sasa Leo tumeteua genge la kimafia lakiarabu,
kipi bora?
Bakora za muarabu au bakora za Mswahili?
Tatizo tumejaa unafki na hatujui tunachokitaka
 
Ni huzuni kubwa na haya yanayotukuta nadhani ni masikitiko yake huko aliko.ila linalomipa moyo ni kuwa uwepo wake ulifungua akili za watanzania. Only what is needed is to go extra mile ,kuchukua hatua. Hilo ndo linakosekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…