Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Mmoja wa waasisi wa kundi mashuhuri la Wabunge 55 (G55) na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kyela, Lumuli Alipipi Kasyupa, amefunguka kuhusu ujasiri waliokuwa nao wa kumpinga Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, huku akibainisha kuwa tofauti na zama za sasa, mazingira ya kisiasa ya kipindi hicho yaliruhusu kushindanisha hoja bila hofu ya kuteswa au kutekwa.
Kasyupa, ambaye alikuwa mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka 2015, ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Sasa Live, akifafanua msukumo uliowafanya wasimame kidete kudai kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya muundo wa Muungano.
"Kipindi kile Mungu alishikilia moyo wa Mwalimu kutokuingia kwenye ujana wa nguvu; alikwenda kwa hoja. Tulitaka kusahihisha muundo alioasisi ili tuwe na Serikali ya Tanganyika kama ilivyo ya Zanzibar, kisha ibaki ya Muungano. Mwalimu hakutaka kutumia rungu kuponda kichwani au kututorosha—tuliitwa mara nyingi Msasani, tunazungumza naye kwa hoja na kurudi nyumbani salama," alisema Kasyupa.
Akimtaja Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba kama kiungo na mpatanishi muhimu katika mzozo huo wa kisiasa, Kasyupa ameeleza kuwa ingawa Warioba alitetea mfumo wa Serikali Mbili, hakuwazuia wao kuwasilisha msimamo wao mbele ya Nyerere.
"Aliyekuwa na ujasiri wa kwenda kule ni Joseph Sinde Warioba. Yeye tangu mwanzo alikuwa na Mwalimu na hakutaka kabisa tuwe na Serikali Tatu, akisema zilizopo zinatosha. Hatukukubaliana naye kwa sababu 'logic' ya hoja yetu ya kutaka Tanganyika ilikuwa na nguvu zaidi, lakini mijadala iliendeshwa kwa kuheshimiana," aliongeza Kasyupa.