Tulimsingizia na kumhukumu Hayati Magufuli juu ya utekaji, Je leo tutamsingizia nani? Magufuli hayupo

Tulimsingizia na kumhukumu Hayati Magufuli juu ya utekaji, Je leo tutamsingizia nani? Magufuli hayupo

Vyombo tulivyoviamini visipofanya kazi zake kwa weledi wataendelea tuu kusingiziwa "kama ni kweli" tuliowapa dhamana ya kusimamia ulinzi wa uhai na mali zetu,mbona hili ni rahisi sana.
 
Kwa hiyo mtekaji ni nani sasa? Manake polisi hawahusiki, TISS hawahusiki, JW security unit hawahusiki. Mkuu wa nchi ambaye ndiyo sauti ya mwisho nchi hii naye anasema hii kitu ni drama. Kama ni vyama vya upinzani mbona hawakamatwi? Shida Iko wapi?
utatafuta majibu hapa hautapata vitu kama hivi huwa ni siri labda tu apatikane mtu anaejua aamue kushusha mambo hadharani ila wao wanajua ni nani,kwanini,wapi na sangapi!.

na hata mtu akiweza kujibu yote hayo watakutafuta!!, usionyeshe kipaji chako kwa kuandika isipokuwa kipaji chako ndio kinatakiwa kiandike!.
 
Msaidizi wa Mwenyekiti Mbowe,alivyopotea tukasema Magufuli kamteka eti msaidizi wa Mbowe alikuwa anapinga PhD ya Magufuli,Leo kapotea Msaidizi wa katibu Mkuu Mnyika,Je tutamsingizia nani wakati Magufuli hayupo!?

Soma Pia: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Magufuli hakusingiziwa. Kama ilikuwa haki kumsifu kwa zuri lolote lililofanyika, hali kadhalika ni haki kumlaumu kwa baya lolote lililofanyika. Na kwa principal ya M/Mungu ilivyo lazima atawajibika hamna namna. Labda kama alitubu, lakini kwa kiburi kile sidhani.
 
Baada ya hapo tukashuhudia Chadema wakimsifu sana SSH kuwa ameleta maridhiano katika nchi, wakamualika na kumpa tuzo kama sikosei; huku CHADEMA hao wakifanya mikutano ya hadhara maeneo mbalimbali nchini nankumsema vibaya sana kwa kejeli na matusi shujaa Hayati JPM ambaye alikuwa boss wa SSH; huku wakisema 'mama' amerejesha haki na utawala bora
Kwamba ameiponya nchi na pamoja na Mbowe kufunguliwa wakati wa Samia lakini wakadai oda ilikuwa imetolewa kabla Magu hajafa.

Mungu Fundi sana naona aliyekuwa anaponya nchi ana haki ya kuagiza raia wake wauawe.

Ni kweli hata Magu alifanya makosa makubwa sana kuruhusu utekaji uwe mwingi kiasi kile. Lakini kwa sasa utekaji unatisha mwanzo tulijifanya hatuoni lakini mambo ndo yanazidi kuwa mambo. Hili linchi kwa sasa linajiendea tu halina mwenyewe, rasilimali za nchi zinaporwa na kupewa wageni huku tena tunauliwa jama kuku. Eti tuna usalama wa taifa, huo sio usalama wa taifa ni usalama wa ccm na viongozi wake.
 
Huwa bado nawaza sana balozi Simoni Sirro enzi akiwa IGP aliwahi kusema kuwa Polisi wana ushahidi kamili kuhusu mashitaka dhidi ya Freeman Mbowe katika kesi yake ya 'ugaidi' iliyokuwa inahusisha pia utekaji na mipango ya mauaji kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa na tuliona kina Kingai wakienfa mahakamani kutoa matokeo ya upelelezi wao, ambapo mahakama ilimkuta Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu; mara ghafla bin vuu tukaona DPP amesita kuendelea na kesi, Mbowe akatoka jela yeye na washtakiwa wenzake, siku hiyo hiyo akaenda Ikulu kuonana na Samia, mara ghafla tukaambiwa maridhiano, Kisha IGP Sirro anatolewa U-IGP na kuteuliwa kuwa balozi Zimbabwe;....
Unauzungumziaje hii ya Mzee kibao kutekwa mchana kweupe kwenye bus nani unazani atakuwa muhusika
 
1. Kuna uwezekano ilifanyika kuonesha JPM ndo alikuwa mbaya ili kupata uungwaji mkono dhidi ya upinzani na mahasimu wa JPM kwenye chama kwa wakati huo
2. Sasa inawezekana reverse is true. Mahasimu wa Her Excellence ndani ya chama wameungana na wapinzani kuonesha kutokuwa na uwezo wa kuwa comfort in chief Kwa kushindwa kidhibiti uhalifu nchini hata kama unafanywa na genge la wahuni wakitokea walikotokea
3. Mama anahitaji kupata washauri wazuri asije akavurugwa halafu wahuni waseme ameshindwa kazi, hafai kuendelea 2025
 
Walimchafua Magufuli ili watimize malengo na walifanikiwa kwakua uelewa wa watu wengi sio mkubwa.

Anyways Yanga Bingwa tena.
 
Kosa la mzee wetu hayati lilikuwa sio kuteka, bali kukaa kimya na watu waka-assume yy ndio anayetoa order. Isemwe tu kama kuna kikosi rogue kimetengenezwa tujue moja
Upumbavu mwingine! Unajua nguvu alizonazo rais? Unajua vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko chini yake? Unajua kuwa ana uwezo wa kuomba hata Scotland Yard waje kusaidia? Yule mpumbavu Magufuli alikuwa muuaji na kipindi chake utekaji ndiyo ulizidi.
 
Sawa.
 
Back
Top Bottom