Tulinde maadili hasa ya vijana wa kiume-Rc Simiyu,Kenan Kihongosi

Tulinde maadili hasa ya vijana wa kiume-Rc Simiyu,Kenan Kihongosi

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Ulinzi wa maadili hasa kwa vijana wa kiume dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia,ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vitendo vya kulawitiwa ni suala nyeti linalohitaji hatua madhubuti kutoka kwa jamii,serikali na taasisi mbalimbali.

Hayo yameelezwa ,April 3,2025 na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Kenan Kihongosi wakati akizungumza na ofisi kwake juu ya kulinda maadili hasa kwa vijana wa kiume kutoingiliwa kinyume na maumbile.
Amesema kuwa uhalisia wa tatizo hilo katika jamii watoto wa kiume ni waathirika wa ukatili wa kijinsia lakini mara nyingi tatizo hili halizungumzwi kwa kina.

Amesema kuwa mara nyingi wanaofanya vitendo hivyo ni watu wa karibu kama wanafamilia,walimu na majirani na watoto hao wamekuwa waoga wa aibu hivyo huwafanya waathirika wengi washindwe kutoa taarifa.

“Nazidi kusisitiza tulinde maadili hasa kwa vijana wa kiume kutoingiliwa kinyume na maumbile,tuwalinde watoto wa kiume,”amesema.

Amesema kuwa licha ya vitendo hivyo kutoripotiwa kuwepo katika mkoa huo lakini ni vizuri kwa jamii kuelezwa ili iweze kuchukua hatua kwa kuimarisha malezi mema kwa vijana wao hasa wa kiume.
“Katika nchi yetu haya mambo yanakatazwa na kifungu cha 154 cha kanuni ya adhabu kinakataza vitendo vya sodomia na adhabu yake ni kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani,”amesema.
 
Ameyasema hayo leo tarehe 4 april,2025, je ni ukweli kuwa mkuu wa mkoa alikuwa na kikao kuhusu maadili usiku wa leo au hyo tarehe imefka ...
NABETT: kati yangu na mtoa uzi kuna mmoja kachanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom