Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Bibi yangu ilikuwa akiwa kijijini analalamika kutelekezwa, akiletwa mjini analalamika mara kuna joto sana, mara tumemleta huku mjini kwenye joto tumemtelekeza mumewe anapigwa na baridi kule kijijini(hapo mumewe alishafariki hivyo hilo baridi anapigwa kaburini).

Mkimtembelea kijijini atawafurahia siku mbili tu ya tatu anawaambia mrudi msijefukuzwa kazi mkakosa pesa za kumtumia. Mkiondoka analalamika tena.
 
Bibi yangu alikua anapika hatari, sijui mikate ya kumimina sijui kalmat, hiyo michuz ya nazi ndio usipime kabisaaaa. Huwa anawatania na anawashangaa wajukuu zake wa kike eti toka aje akae hapo nyumban hajawahi ona wamekuja chukuliwa na gari wakat yeye miaka ya 1970's huko alikua anafuatwa na magari mpk kijijini kwao huko halafu anapelekwa sinema
 
Bibi yangu ana fix hatari nikikaa-ga naye haishiwi story. Eti kuna siku alilazwa hosp mimi nilikuwa mdogo sikumbuki ila huwa ananiambia tulikuwa wote namuuguza.

Sasa siku akazidiwa akakata kuja kustuka akajikuta anatembea kwenye kakamba kadogo kembamba anaelekea juu mawinguni. Akawakuta watu watatu huko mbinguni mmoja boss wengine nyokaa wake.

Bibi hakusemeshwa, akasikia wanaambiana vipi moyo wake bado upo? Hahaha mmoja akajibu sijui..boss akamkaripia nenda kaangalie. Jamaa akaenda akarudi akamwambia upo.

Boss akaamuru basi mshushe. Bibi akashushwa bwana. Kwa speculations zake anakuambia eti juu kuna moyo wa kila mtu umetundikwa kama drip so ukipotea kule na huku duniani umepotea.. na ndiyo maana hao jamaa waliangalia wake.

Ukimbishia ukamwambia bibi labda ulikuwa unaota hahaha anakununia week nzima. Bibi nimemisa story zake inakadiriwa anafikisha 115+ sasa.
Na vya kurithi huwa vinazidi.
Kumbeeeeee!!!
 
Bibi yangu ilikuwa akiwa kijijini analalamika kitelekezwa, akiletwa mjini analalamika mara kuna joto sana, mara tumemleta huku mjini kwenye joto tumemtelekeza mumewe anapigwa na baridi kule kijijini(hapo mumewe alishafariki hivyo hilo baridi anapigwa kaburini).

Mkimtembelea kijijini atawafurahia siku mbili tu ya tatu anawaambia mrudi msijefukuzwa kazi mkakosa pesa za kumtumia. Mkiondoka analalamika tena.

Ama kweli maji hufuata mkondo [emoji23] [emoji23]
 
Bibi yangu alikua anapika hatari, sijui mikate ya kumimina sijui kalmat, hiyo michuz ya nazi ndio usipime kabisaaaa. Huwa anawatania na anawashangaa wajukuu zake wa kike eti toka aje akae hapo nyumban hajawahi ona wamekuja chukuliwa na gari wakat yeye miaka ya 1970's huko alikua anafuatwa na magari mpk kijijini kwao huko halafu anapelekwa sinema
Alikuwa anakuja kuchukuliwa na wachuchu?
 
Babu yangu aisee, akinywa akilewa anakuwa mkali balaa...
Anapiga kiingereza hatari, halafu anaanza fix kuwa kiingereza alijifunzia uholanzi...
Bibi mpole sana...
 
Bibi yangu alikuwa ananiita mme wangu na mimi ndo nilikuwa nanyoa nywele zake nyeupe mara zote...alikuwa mzushi mkimuukliza bibi una umri gani utasikia sasa hivi nina miaka kama 300 hivi...hahaha lakini haikuwa hivo bibi etu alifariki akiwa na miaka 98 hakika tulihuzunika japo alipaswa apuzike tu.
 
Hahahaha
 
Yah wachuchu, na anajisifia alikua mzuri balaa (Ofcourse anaonekana alikua mzuri). Halafu anaonekana alijaaliwa nyonga hatar, maana akianzaga kucheza hapo na uzee wake lakini unaona kabisa huyu alikuwa nuksi. Ni mtu wa pwani halafu ni mweupe pe
Haha..aseeh mwenyewe bibi yangu anajisifia hatari.

Huwa anamsema saana sister(dogo) utaskia anasema nyie mnajifanya wanawake sasa hivi? Enzi zangu nilikuwa sitoki mchana nashinda ndani akiwa na namaana atasababisha tafurani.
 
Hizi fix huwa za wabibi wengi.
 
Back
Top Bottom