Tulioajiriwa ni kwamba tumeamua kupata hela mara 12 tu kwa mwaka

Siyo kila mtu lazima ajiajiri ,division of labour ,kuna wengine wana vipawa vya kujiajiri na kutengeneza ajira ,kuna wengine hawana hivyo vipawa ,kuna jamaa mmoja alipata mafao mazuri tu baada ya mkataba wake kuisha ,akaingia kufanya biashara hadi za china ,kapiga miaka kadhaa akaona bora arudishe mpira kwa kipa ,kaajiriwa tena....Jamaa alikuwa na mtaji mkubwa sana lakini biashara ilimshinda lakini kuna wengine walikuwa na mtaji mdogo tena robo ya jamaa lakini wamefanikiwa na wanaendeleza biashara mpaka leo.
Yes -Exactly bro. Maisha hayana fixed Formulae. Kupanga ni kuchagua. Ukiona upande huu imebuma unaenda alt. B.
 
Ji
Hatari sana. Unapoajiriwa unakuwa unamuuzia mwajiri wako muda wako. Kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Mwajiri hukulipa kutokana na wewe kutumia sehemu yake ya kazi kumzalishia mali.

Kwa mwaka utapewa hela mara kumi na mbili tu. Dah kweli kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini. Ndio maana waajiriwa wengi ni wezi
Jiwe gizani
 
Mtu anakwambia ajira mbaya wakati huo huo anamtafutia connection mtoto wake apate ajira sehemu X
Ni Ukweli mtupu..Yan huyo ana roho ya Korosho(?) anapakazia Ajira lakini yeye mwenyewe ameikumbatia na hataki wengine angalau wayaonje mema ya nchi isipokuwa mtoto wake.
 
Hatari sana. Unapoajiriwa unakuwa unamuuzia mwajiri wako muda wako. Kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Mwajiri hukulipa kutokana na wewe kutumia sehemu yake ya kazi kumzalishia mali.

Kwa mwaka utapewa hela mara kumi na mbili tu. Dah kweli kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini. Ndio maana waajiriwa wengi ni wezi
Na nawaambia tulieni hukohuko mnakolipwa mara12 sisi huku hatulipwi kabisa
 
Hatari sana. Unapoajiriwa unakuwa unamuuzia mwajiri wako muda wako. Kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Mwajiri hukulipa kutokana na wewe kutumia sehemu yake ya kazi kumzalishia mali.

Kwa mwaka utapewa hela mara kumi na mbili tu. Dah kweli kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini. Ndio maana waajiriwa wengi ni wezi
Hoja kwamba “kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini” ni hoja ya jumla, ya kivivu kiakili na isiyo na msingi wa kiuchumi. Kuajiriwa ni njia mojawapo ya kubadilisha ujuzi, muda, uzoefu na uwezo wa kutatua matatizo kuwa kipato. Biashara nayo ni kubadilisha bidhaa, huduma, mtaji na uwezo wa kubeba hatari kuwa kipato. Hakuna mfumo unaomfanya kila mtu awe tajiri au maskini moja kwa moja.

Kwanza, si kweli kwamba waajiriwa wote ni maskini. Group CEO wa CRDB Bank ni Dkt. Abdulmajid Nsekela, na Managing Director/CEO wa NMB Bank ni Ruth Zaipuna. Hawa ni waajiriwa wanaoongoza taasisi kubwa za kifedha. Kwa hiyo, kuwaita maskini kwa sababu tu wana mikataba ya ajira na kupokea mishahara ni kushindwa kutofautisha employment status na economic status.

Duniani, Satya Nadella wa Microsoft alipata jumla ya takribani USD 96.5 milioni kama malipo ya mwaka wa fedha 2025; Tim Cook wa Apple takribani USD 74.3 milioni; na Jensen Huang wa NVIDIA takribani USD 49.9 milioni. Hawa wote wanapokea malipo kupitia nafasi zao za kiuongozi katika kampuni. Kwa hiyo, payslip si cheti cha umasikini.

Pili, kusema mtu analipwa “mara 12 tu kwa mwaka” si hoja ya maana. Utajiri haupimwi kwa idadi ya mara unazolipwa, bali kwa kiasi unachopata, unachobakiza, unachowekeza na mali unazojenga. Mtu anayelipwa milioni 20 kila mwezi anaweza kuwa na hali bora zaidi kuliko mfanyabiashara anayepokea fedha kila siku lakini mwisho wa mwezi ana madeni, gharama kubwa na hasara. Zaidi ya mshahara, baadhi ya ajira huwa na bonasi, hisa, pensheni, bima ya afya, posho, mafunzo na likizo yenye malipo.

Tatu, mwajiriwa bora anatakiwa kuwa na entrepreneurial mindset. Kwa namna fulani, kila professional ni mfanyabiashara: anauza ujuzi, uwezo wa kufanya maamuzi, muda, ubunifu na matokeo yake kwa mwajiri anayevihitaji. Anatakiwa ajiulize kila siku:

Ninaongeza thamani gani? Ujuzi wangu unahitajika kiasi gani sokoni? Ninawezaje kuwa bora, adimu na mwenye kulipwa zaidi?

Tatizo si ajira. Tatizo ni kuwa seat warmer: kufika kazini, kusubiri mwisho wa mwezi, kutokujifunza, kutokuongeza ujuzi na kutotafuta majukumu makubwa zaidi. Mtu anaweza kufanya kazi Tanzania, Afrika au kwenye soko la kimataifa. Mtanzania si lazima auze ujuzi wake ndani ya mipaka ya Tanzania pekee. Kwa mfano, Elsie Kanza aliwahi kushika nafasi za juu katika World Economic Forum. Dkt. Bahati Sanga, Mtanzania mwingine, ameshika nafasi ya juu ya uongozi wa teknolojia katika African Development Bank. Hii inaonyesha kuwa kujenga ujuzi unaohitajika kimataifa kunaweza kumwezesha mwajiriwa kupata nafasi, kipato na ushawishi unaovuka mipaka ya nchi.

Nne, ajira inaweza kuwa shule na msingi wa ujasiriamali. Kupitia ajira mtu anaweza kujifunza kuendesha mifumo, kusimamia fedha, kuongoza watu, kuhudumia wateja, kufanya maamuzi, kujenga mtandao na kupata mtaji wa kuwekeza.

Reginald Mengi hakuruka moja kwa moja kutoka shuleni na kujikuta mmiliki wa IPP. Alifanya kazi Coopers & Lybrand Tanzania, akapanda hadi kuwa Managing Partner na Mwenyekiti, kisha akaacha ajira na kuelekeza nguvu kwenye biashara zake. Strive Masiyiwa pia alifanya kazi kama mhandisi wa mawasiliano kabla ya kuanzisha biashara yake ya kwanza. Ajira haikuwazuia kuwa wafanyabiashara; iliwaongezea ujuzi, uzoefu na uwezo wa kutekeleza.

Na ukweli mwingine usiopendeza ni huu: mtu mvivu, asiyeaminika na asiye na nidhamu akiwa mwajiriwa ana uwezekano mkubwa wa kubeba tabia hizo hizo kwenye biashara yake. Biashara haibadilishi tabia kimiujiza. Kama huwezi kuheshimu muda, fedha, wateja na majukumu ya mtu mwingine, huenda ukashindwa kufanya hivyo hata kwenye kampuni yako mwenyewe.

Mwisho, kusema “waajiriwa wengi ni wezi” ni tuhuma nzito, isiyo na ushahidi na inayodhalilisha mamilioni ya watu waaminifu wanaoendesha hospitali, benki, viwanda, shule, mashirika na serikali. Kama waajiriwa wengi wangekuwa wezi, taasisi nyingi zisingeweza hata kuendelea kufanya kazi.

Ajira inaweza kumfanya mtu abaki maskini, awe na maisha mazuri, awe mwekezaji au hata awe tajiri. Biashara nayo inaweza kumtajirisha mtu, kumweka kwenye madeni au kumfilisi. Kinachoamua si jina “mwajiriwa” au “mfanyabiashara”; ni thamani anayozalisha, uwezo anaoujenga, nidhamu ya fedha, maamuzi anayofanya na namna anavyotumia fursa zake.
 
Baada ya hapa mnapiga simu kuwakopa pesa kwa kisingizio biashara hazijakaa vizuri. ... Ajira sio mbaya kwa watu wa below 40, maana ni chanzo cha mitaji ila kuanzia 40 above ni fedhea kama hujawekeza popote.
Mkuu; Unawekeza kwenye lipi kwa kiasi unacholipwa kama mshahara wako? Ungelisema kwamba mshahara wako unakuwa ni collateral inayoaminika ili ukope bank na huo mkopo ndo utakaowekeza mahali fulani. Vinginevyo mshahara unabaki ni from hand to mouth huwezi ku-invest kwenye lolote.
 
Nanukuu para hii:
Mwisho, kusema “waajiriwa wengi ni wezi” ni tuhuma nzito, isiyo na ushahidi na inayodhalilisha mamilioni ya watu waaminifu wanaoendesha hospitali, benki, viwanda, shule, mashirika na serikali. Kama waajiriwa wengi wangekuwa wezi, taasisi nyingi zisingeweza hata kuendelea kufanya kazi."
Sehemu niliyonukuu ni ukweli usiopingika kwa mantiki kwamba wizi sio lazima iwe ni fedha cash. Kwa mfano ukienda kwenye maeneo ya kutolea huduma(Maofisini) unakuta wahudumu(Watumishi/waajiriwa hawapo japokuwa ni muda wa kuwahudumia wateja. Wengine wameinamia simu zao -wanachati. Vipo visingizio vingi-ametoka kidogo, yupo kwa chai n.k.n.k. huo nao ni WIZI wa muda kwani mtumishi huyo atalipwa kwa muda huo ambao hajaufanyia kazi. Mtumishi anadai eti anakwenda Field kikazi lakini huko field alikoenda hana cha maana alichokifanyia kazi zaidi ya kufuatilia mambo yake personal (Mwajiri na Mwajiriwa wote sawa)na hata Serikali imeshindwa kudhibiti hilo japokuwa kuna kipindi Serikali iliweka kipimio cha Perfomance (OPRAS)lakini ilishindwa kwani udanganyifu ulikuwa ni mwingi. Kwa mantiki hiyo wizi uliendelea kutamalaki na hadi leo hii hayo mambo yapo yanaendelea.
 
Mkuu; Unawekeza kwenye lipi kwa kiasi unacholipwa kama mshahara wako? Ungelisema kwamba mshahara wako unakuwa ni collateral inayoaminika ili ukope bank na huo mkopo ndo utakaowekeza mahali fulani. Vinginevyo mshahara unabaki ni from hand to mouth huwezi ku-invest kwenye lolote.
Zingatia neno Ajira; kama hukuwahi kupitia msoto huwezi elewa umuhimu wa Ajira.
Kama Ajira ni mbaya hakuna mtu angeilaumu serkali kwa kukosa aajira

~Mshahar Ni sehemu ya Ajira, Unaweza kuwa mdogo lakini kule tu kuwa nayo kunapunguza stress nyingi za maisha
~Unapata mikopo sababu una ajira
~Bima ya afya sababu una ajira
~Unakopesheka mitaani sababu una ajira
~Unachukua kiwanja na kulipia kidogokidogo sababu una ajira
~Watu wana kuheshimu mtaa sababu una ajira

N.k

vyote hapo juu ni kukusaidia kupata utulivu wa akili ukose visingizio vya kutoboa kimaisha.

Swala la kuishi maisha ya kifahari kwa mshahara wa milioni alafu unakuja kuisalimu JF kwa kutoa laana za kuajiriwa ni ulimbukeni.
 
Kwa nyongeza: Halafu bado kama mwajiri wako ni lezafeya na hobela-hobela unaweza "kujitwalia" muda (kutega)wa kufanya mambo yako (Private projects nyingi)na bado mwisho wa mwezi ukalipwa sawa kana kwamba ulikuwa full time kazini.
Dah umenikumbusha taasisi fulani ya serikali staff anaingia saa mbili then anakunywa chai saa zima huku akijadili simba na yanga then anasoma gazeti saa moja then anatoka anaenda kusalimia staff wa idara nyingine saa tano kwa kujivuuuta ndiyo anaanza kazi, the saa saba anaenda lunch, saa nane na nusu ndiyo anarudi then anafanya kazi nusu saa then saa tisa anatoka kurudi nyumbani.
 
Huo ndo wizi uliokubuhu katika ubora wake na Mwajiri wala hastuki ila ni anastuka tu pale CAG anapopita na kutoa ripoti yake na bado hata hivyo yatatafutwa majibu ya hoja hizo za CAG. -Unaona kazi hiyo?
 
Sio kweli.

Tarehe 23: Mshahara wenye koma tatu
Tarehe 28: Posho ya nyumba na usafiri
Tarehe 30: Malipo ya kazi za muda wa ziada
Tarehe 02: Safari ya kikazi ya wiki mbili Arusha
Tarehe 25: Malipo ya posho ya sikukuu
Tarehe 15: Malipo ya posho ya mavazi
Tarehe 30: Mafunzo maalum ya uendeshaji wa mitambo ya kusafisha "bidhaa ghafi" baada ya usimikaji, miezi mitatu, Soul Korea

Naomba niishie hapo
 
Back
Top Bottom