Yes -Exactly bro. Maisha hayana fixed Formulae. Kupanga ni kuchagua. Ukiona upande huu imebuma unaenda alt. B.Siyo kila mtu lazima ajiajiri ,division of labour ,kuna wengine wana vipawa vya kujiajiri na kutengeneza ajira ,kuna wengine hawana hivyo vipawa ,kuna jamaa mmoja alipata mafao mazuri tu baada ya mkataba wake kuisha ,akaingia kufanya biashara hadi za china ,kapiga miaka kadhaa akaona bora arudishe mpira kwa kipa ,kaajiriwa tena....Jamaa alikuwa na mtaji mkubwa sana lakini biashara ilimshinda lakini kuna wengine walikuwa na mtaji mdogo tena robo ya jamaa lakini wamefanikiwa na wanaendeleza biashara mpaka leo.
Na kuacha hawataki wakati milango iko wazi, ni wazi waajiri hawajali kuondoka kwao. Hapo ndo unajua yeye anaihitaji ajira kuliko inavyomhitaji yeye.Ajira this, ajira that. As if ajira ilikufata nyumbani, kumbe we ndio uliitafuta 😁
Kwani wamefungiwa kwa minyororo hapo walipoajiriwa? Si waondoke?Piga hao
Bado wanapumua.
Nyumbu wengine watasingizia mfumo wa elimu ndio umewafanya watafute ajira.
Sio lazimaKatika maisha lazima uajiriwe ili upate capital na experience kwa sisi tuliotoka familia za kimasikini.
Naam; Ndo mana "wale jamaa" wana kamsemo kao kanakosema "Kujitafuta".Sio lazima
Mwajiri na Mwajiriwa wote ni WEZI kwa hiyo hapo ni ngoma droo. Hoja inakuja ni nani atamzidi mwenzake?Usipokuwa mwizi unasubiria nn? Huwezi tobowa
Mtu anakwambia ajira mbaya wakati huo huo anamtafutia connection mtoto wake apate ajira sehemu XKwani wamefungiwa kwa minyororo hapo walipoajiriwa? Si waondoke?
Jiwe gizaniHatari sana. Unapoajiriwa unakuwa unamuuzia mwajiri wako muda wako. Kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.
Mwajiri hukulipa kutokana na wewe kutumia sehemu yake ya kazi kumzalishia mali.
Kwa mwaka utapewa hela mara kumi na mbili tu. Dah kweli kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini. Ndio maana waajiriwa wengi ni wezi
Ni Ukweli mtupu..Yan huyo ana roho ya Korosho(?) anapakazia Ajira lakini yeye mwenyewe ameikumbatia na hataki wengine angalau wayaonje mema ya nchi isipokuwa mtoto wake.Mtu anakwambia ajira mbaya wakati huo huo anamtafutia connection mtoto wake apate ajira sehemu X
SwadaktaKatika maisha lazima uajiriwe ili upate capital na experience kwa sisi tuliotoka familia za kimasikini.
Na nawaambia tulieni hukohuko mnakolipwa mara12 sisi huku hatulipwi kabisaHatari sana. Unapoajiriwa unakuwa unamuuzia mwajiri wako muda wako. Kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.
Mwajiri hukulipa kutokana na wewe kutumia sehemu yake ya kazi kumzalishia mali.
Kwa mwaka utapewa hela mara kumi na mbili tu. Dah kweli kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini. Ndio maana waajiriwa wengi ni wezi
Hoja kwamba “kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini” ni hoja ya jumla, ya kivivu kiakili na isiyo na msingi wa kiuchumi. Kuajiriwa ni njia mojawapo ya kubadilisha ujuzi, muda, uzoefu na uwezo wa kutatua matatizo kuwa kipato. Biashara nayo ni kubadilisha bidhaa, huduma, mtaji na uwezo wa kubeba hatari kuwa kipato. Hakuna mfumo unaomfanya kila mtu awe tajiri au maskini moja kwa moja.Hatari sana. Unapoajiriwa unakuwa unamuuzia mwajiri wako muda wako. Kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.
Mwajiri hukulipa kutokana na wewe kutumia sehemu yake ya kazi kumzalishia mali.
Kwa mwaka utapewa hela mara kumi na mbili tu. Dah kweli kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini. Ndio maana waajiriwa wengi ni wezi
Mkuu; Unawekeza kwenye lipi kwa kiasi unacholipwa kama mshahara wako? Ungelisema kwamba mshahara wako unakuwa ni collateral inayoaminika ili ukope bank na huo mkopo ndo utakaowekeza mahali fulani. Vinginevyo mshahara unabaki ni from hand to mouth huwezi ku-invest kwenye lolote.Baada ya hapa mnapiga simu kuwakopa pesa kwa kisingizio biashara hazijakaa vizuri. ... Ajira sio mbaya kwa watu wa below 40, maana ni chanzo cha mitaji ila kuanzia 40 above ni fedhea kama hujawekeza popote.
Nanukuu para hii:Hoja kwamba “kuajiriwa ni mtego rasmi wa umasikini” ni hoja ya jumla, ya kivivu kiakili na isiyo na msingi wa kiuchumi. Kuajiriwa ni njia mojawapo ya kubadilisha ujuzi, muda, uzoefu na uwezo wa kutatua matatizo kuwa kipato. Biashara nayo ni kubadilisha bidhaa, huduma, mtaji na uwezo wa kubeba hatari kuwa kipato. Hakuna mfumo unaomfanya kila mtu awe tajiri au maskini moja kwa moja.
Kwanza, si kweli kwamba waajiriwa wote ni maskini. Group CEO wa CRDB Bank ni Dkt. Abdulmajid Nsekela, na Managing Director/CEO wa NMB Bank ni Ruth Zaipuna. Hawa ni waajiriwa wanaoongoza taasisi kubwa za kifedha. Kwa hiyo, kuwaita maskini kwa sababu tu wana mikataba ya ajira na kupokea mishahara ni kushindwa kutofautisha employment status na economic status.
Duniani, Satya Nadella wa Microsoft alipata jumla ya takribani USD 96.5 milioni kama malipo ya mwaka wa fedha 2025; Tim Cook wa Apple takribani USD 74.3 milioni; na Jensen Huang wa NVIDIA takribani USD 49.9 milioni. Hawa wote wanapokea malipo kupitia nafasi zao za kiuongozi katika kampuni. Kwa hiyo, payslip si cheti cha umasikini.
Pili, kusema mtu analipwa “mara 12 tu kwa mwaka” si hoja ya maana. Utajiri haupimwi kwa idadi ya mara unazolipwa, bali kwa kiasi unachopata, unachobakiza, unachowekeza na mali unazojenga. Mtu anayelipwa milioni 20 kila mwezi anaweza kuwa na hali bora zaidi kuliko mfanyabiashara anayepokea fedha kila siku lakini mwisho wa mwezi ana madeni, gharama kubwa na hasara. Zaidi ya mshahara, baadhi ya ajira huwa na bonasi, hisa, pensheni, bima ya afya, posho, mafunzo na likizo yenye malipo.
Tatu, mwajiriwa bora anatakiwa kuwa na entrepreneurial mindset. Kwa namna fulani, kila professional ni mfanyabiashara: anauza ujuzi, uwezo wa kufanya maamuzi, muda, ubunifu na matokeo yake kwa mwajiri anayevihitaji. Anatakiwa ajiulize kila siku:
Ninaongeza thamani gani? Ujuzi wangu unahitajika kiasi gani sokoni? Ninawezaje kuwa bora, adimu na mwenye kulipwa zaidi?
Tatizo si ajira. Tatizo ni kuwa seat warmer: kufika kazini, kusubiri mwisho wa mwezi, kutokujifunza, kutokuongeza ujuzi na kutotafuta majukumu makubwa zaidi. Mtu anaweza kufanya kazi Tanzania, Afrika au kwenye soko la kimataifa. Mtanzania si lazima auze ujuzi wake ndani ya mipaka ya Tanzania pekee. Kwa mfano, Elsie Kanza aliwahi kushika nafasi za juu katika World Economic Forum. Dkt. Bahati Sanga, Mtanzania mwingine, ameshika nafasi ya juu ya uongozi wa teknolojia katika African Development Bank. Hii inaonyesha kuwa kujenga ujuzi unaohitajika kimataifa kunaweza kumwezesha mwajiriwa kupata nafasi, kipato na ushawishi unaovuka mipaka ya nchi.
Nne, ajira inaweza kuwa shule na msingi wa ujasiriamali. Kupitia ajira mtu anaweza kujifunza kuendesha mifumo, kusimamia fedha, kuongoza watu, kuhudumia wateja, kufanya maamuzi, kujenga mtandao na kupata mtaji wa kuwekeza.
Reginald Mengi hakuruka moja kwa moja kutoka shuleni na kujikuta mmiliki wa IPP. Alifanya kazi Coopers & Lybrand Tanzania, akapanda hadi kuwa Managing Partner na Mwenyekiti, kisha akaacha ajira na kuelekeza nguvu kwenye biashara zake. Strive Masiyiwa pia alifanya kazi kama mhandisi wa mawasiliano kabla ya kuanzisha biashara yake ya kwanza. Ajira haikuwazuia kuwa wafanyabiashara; iliwaongezea ujuzi, uzoefu na uwezo wa kutekeleza.
Na ukweli mwingine usiopendeza ni huu: mtu mvivu, asiyeaminika na asiye na nidhamu akiwa mwajiriwa ana uwezekano mkubwa wa kubeba tabia hizo hizo kwenye biashara yake. Biashara haibadilishi tabia kimiujiza. Kama huwezi kuheshimu muda, fedha, wateja na majukumu ya mtu mwingine, huenda ukashindwa kufanya hivyo hata kwenye kampuni yako mwenyewe.
Mwisho, kusema “waajiriwa wengi ni wezi” ni tuhuma nzito, isiyo na ushahidi na inayodhalilisha mamilioni ya watu waaminifu wanaoendesha hospitali, benki, viwanda, shule, mashirika na serikali. Kama waajiriwa wengi wangekuwa wezi, taasisi nyingi zisingeweza hata kuendelea kufanya kazi.
Ajira inaweza kumfanya mtu abaki maskini, awe na maisha mazuri, awe mwekezaji au hata awe tajiri. Biashara nayo inaweza kumtajirisha mtu, kumweka kwenye madeni au kumfilisi. Kinachoamua si jina “mwajiriwa” au “mfanyabiashara”; ni thamani anayozalisha, uwezo anaoujenga, nidhamu ya fedha, maamuzi anayofanya na namna anavyotumia fursa zake.
Zingatia neno Ajira; kama hukuwahi kupitia msoto huwezi elewa umuhimu wa Ajira.Mkuu; Unawekeza kwenye lipi kwa kiasi unacholipwa kama mshahara wako? Ungelisema kwamba mshahara wako unakuwa ni collateral inayoaminika ili ukope bank na huo mkopo ndo utakaowekeza mahali fulani. Vinginevyo mshahara unabaki ni from hand to mouth huwezi ku-invest kwenye lolote.
Dah umenikumbusha taasisi fulani ya serikali staff anaingia saa mbili then anakunywa chai saa zima huku akijadili simba na yanga then anasoma gazeti saa moja then anatoka anaenda kusalimia staff wa idara nyingine saa tano kwa kujivuuuta ndiyo anaanza kazi, the saa saba anaenda lunch, saa nane na nusu ndiyo anarudi then anafanya kazi nusu saa then saa tisa anatoka kurudi nyumbani.Kwa nyongeza: Halafu bado kama mwajiri wako ni lezafeya na hobela-hobela unaweza "kujitwalia" muda (kutega)wa kufanya mambo yako (Private projects nyingi)na bado mwisho wa mwezi ukalipwa sawa kana kwamba ulikuwa full time kazini.
Huo ndo wizi uliokubuhu katika ubora wake na Mwajiri wala hastuki ila ni anastuka tu pale CAG anapopita na kutoa ripoti yake na bado hata hivyo yatatafutwa majibu ya hoja hizo za CAG. -Unaona kazi hiyo?Dah umenikumbusha taasisi fulani ya serikali staff anaingia saa mbili then anakunywa chai saa zima huku akijadili simba na yanga then anasoma gazeti saa moja then anatoka anaenda kusalimia staff wa idara nyingine saa tano kwa kujivuuuta ndiyo anaanza kazi, the saa saba anaenda lunch, saa nane na nusu ndiyo anarudi then anafanya kazi nusu saa then saa tisa anatoka kurudi nyumbani.