#COVID19 Tuliochanjwa chanjo ya COVID-19 Karibuni tutoe mrejesho

#COVID19 Tuliochanjwa chanjo ya COVID-19 Karibuni tutoe mrejesho

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,385
Reaction score
10,659
Leo nimefika kituoni kwangu nikiwa na kitambulisho changu cha Taifa, nimesita kidogo kufika RCH station kwa ajiri ya kupata chanjo as bado nilikua sijaamua.

Nimefungua Computer yangu, nikapitia some notes on Chanjo then nikaamka fasta nikanyoosha RCH. Hakukua na folen, we were only about watu 7. Moyo ulikuwa unadunda duu duu duuuu, but hiari ikaishinda hofu. Ilipofika zamu yangu nilionesha kitambulisho, nikamaliza issues za usajili nikaenda mpaka kwa mdungaji, nikapekenya shati langu, nikakinga bega, akanipaka alcoholic cotton then akazamisha sindano na kusukuma kimiminika cha Johnson n Johnson!

After that nikasaini form ya kiapo, hapa nasubiria cheti changu tu cha kudhibitisha kuwa Nami ni mchanjwa!

Sijasikia chochote zaidi ya maumivu kidogo ya sindano (binafsi ni mwoga wa sindano) I am completely OK.

Je, wengine mlijisikiaje? Mlipata side effects gani?

Please, usinywe ulabu ndani ya masaa 72 baada ya chanjo!

Nawahimiza na wengine mkachanje maana Kinga ni bora kuliko tiba.


UPDATE: Jana usiku nilidevelop Homa kali na kuvibrate kama simu ya Nokia tochi (Homa ni kawaida unapochanjwa as inaashiria mwili unajenga Kinga)
Asubuhi hii nipo ok na nipo job napambana kutafuta mkate wa kila siku.

TUKACHANJE!
 
Kwanini wengi wenu mliochanjwa mnazungumzia madhara ya chanjo ya muda mfupi..? Mkishachomwa mnasema hamjaona mabadiliko yoyote!.

Ukichanjwa leo haimaanishi mabadiliko lazima uyaone leo inaweza chukua miaka!. Wengine wanakuja na hoja ati mbona tulichanjwa utotoni! Hawajifikirii ile chanjo ya utotoni zilipitia hatua nyingi mpk kukubaliwa tofauti na hizi za uviko 19 ambazo ni for your own risk even your government inaogopa kutiwa hatia na madhara utakayoyapata halafu wanakushawishi choma..😅

Hii statement ni ya kuangalia Sana tena sana. Kuna mahali huko nimeandika "dunia inahitaji strong people na intelligent" Kama taifa tunahitaji kuwa na wataalum wenye ujuzi wa kutosha na wenye uhakika na ujuzi wao,viongozi pia wawe na maamuzi yenye utimamu na uhakika wa muelekeo stahiki kwa staili hii ya kudungwa kimiminika toka nchi za nje ambacho hata serikali yako inakusainisha mkataba wa kutohusika kwa litakolokupata!,hili tayari ni doa kubwa sana hata huko marekani mpk wanapeana dollar mia ili ukubali kuchanjwa..😂

Mkuu chanja chanjo ya uviko kwa manufaa yako mwenyewe huu ugonjwa unakasumba nyingi sana kusema kweli.
 
Kwanini wengi wenu mliochanjwa mnazungumzia madhara ya chanjo ya muda mfupi..? Mkishachomwa mnasema hamjaona mabadiliko yoyote!.
Ukichanjwa leo haimaanishi mabadiliko lazima uyaone leo inaweza chukua miaka!...
Unajua chanjo ya Mumps ilichukua muda mfupi kuliko hii ya COVID19? Kachanje ndg yangu!
 
Back
Top Bottom