#COVID19 Tuliochanjwa chanjo ya COVID-19 Karibuni tutoe mrejesho

#COVID19 Tuliochanjwa chanjo ya COVID-19 Karibuni tutoe mrejesho

Inaonekana wewe ni mmoja wapo wa wale wanaopinga chanjo lakini umechanjwa bro,ngojeni micro chip za neurolink zianze kazi mtakavyokuwa controled na computer kama ma robot ndio mtajua.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
Ha ha haaaa, Hawa kenge wa kizungu wakitaka kutuua Wana njia Mingi. Hii haiwezi kuwa njia ya kutuvuruga
 
Watanzania tulipata chanjo za polio, pepo punda, ndui, kifua kikuu etc, mbona tuko normal tu kama binadamu wengine!?
Hayo mabadiliko yatakuja baada ya miaka 200!?
Mkuu Tuendelee kuelimisha
 
UVIKO-19 kwa kuwa unatibika sina sababu ya kupata chanjo.

Isitoshe nikizingatia ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi sina sababu ya kuchanjwa.

Na kwamba hachanjwi mtu mwenye matatizo ya kiafya ni sababu tosha ya mimi kutokuchanjwa.
Mtazamo huu si Sahihi. Ukipata hii makitu u may end up kuusambaza kwa wengine. Ukiambukiza wasio na Kinga nzuri they end up die
 
Sawa tupo sawa lakini hii chanjo ya Sasa watu wanaigopa maana yaonyesha hofu kwa watu hasa ukizingatia zimekuja kwa emergency na baadhi ya nchi walisitisha baadhi ya chanjo kutokana na kuleta tafrani baada ya kusababisha some cases na hata kupelekea vifo.
Mi sidhani chanjo hizi za uviko 19 zinathibitishwa na chanjo tulizopata huko awali!,mkuu watu huiamini serikali yao lakini kwa hili la serikali kuchukua chanjo toka nje(sio kosa lakini Kama ikiwa salama kwa watu) lakini swala la kusainishwa ka mkataba ka for your own risk,inaleta mashaka sana maana hata government inaonyesha inahofu juu ya chanjo husika na inajiepusha na lawama juu ya chochote kitakachokukuta kutokana na chanjo husika!.. what this..??
Serikali zetu chenga Sana. Wamechukua hii chanjo for just kufuata mkumbo
 
Suala la chanjo ni la binafsi na hiari. Kila mtu apambanie afya yake kwa namna anayoona inafaa. NIMECHANJA
Mkuu Safi Sana. Kila mtu na ahiari but kwa mtazamo wangu Kuchanja ni bora kuliko kutochanja
 
Ha ha haaaa, Hawa kenge wa kizungu wakitaka kutuua Wana njia Mingi. Hii haiwezi kuwa njia ya kutuvuruga
true,na tujue pia Sisi ndiyo wateja wao wakubwa.sidhani kama kuna mangi anaweza ua mteja,halafu atauza kwa nani? ni wateja wa kuanzia hizo chanjo zenyewe.kinachofanyika hapa ni kulinda wateja wao
 
true,na tujue pia Sisi ndiyo wateja wao wakubwa.sidhani kama kuna mangi anaweza ua mteja,halafu atauza kwa nani? ni wateja wa kuanzia hizo chanjo zenyewe.kinachofanyika hapa ni kulinda wateja wao
We jamaa umeongea bonge la point. Kunywa mtori wa buku 3 nakuja kulipia. Thumb up!!
 
Kwanini wengi wenu mliochanjwa mnazungumzia madhara ya chanjo ya muda mfupi..? Mkishachomwa mnasema hamjaona mabadiliko yoyote!.

Ukichanjwa leo haimaanishi mabadiliko lazima uyaone leo inaweza chukua miaka!. Wengine wanakuja na hoja ati mbona tulichanjwa utotoni! Hawajifikirii ile chanjo ya utotoni zilipitia hatua nyingi mpk kukubaliwa tofauti na hizi za uviko 19 ambazo ni for your own risk even your government inaogopa kutiwa hatia na madhara utakayoyapata halafu wanakushawishi choma..[emoji28]

Hii statement ni ya kuangalia Sana tena sana. Kuna mahali huko nimeandika "dunia inahitaji strong people na intelligent" Kama taifa tunahitaji kuwa na wataalum wenye ujuzi wa kutosha na wenye uhakika na ujuzi wao,viongozi pia wawe na maamuzi yenye utimamu na uhakika wa muelekeo stahiki kwa staili hii ya kudungwa kimiminika toka nchi za nje ambacho hata serikali yako inakusainisha mkataba wa kutohusika kwa litakolokupata!,hili tayari ni doa kubwa sana hata huko marekani mpk wanapeana dollar mia ili ukubali kuchanjwa..[emoji23]

Mkuu chanja chanjo ya uviko kwa manufaa yako mwenyewe huu ugonjwa unakasumba nyingi sana kusema kweli.
Side effect ya chanjo kama ipo mara nyingi ni immediate, within one week tayari utaona madhara kama ina madhara, kama hutaona any changes within one week to one month then hyo chanjo haina side effect.
 
Mkuu mleta mada.....naomba nieleze kuhusu hicho kiapo.......una sign kiapo cha namna gani?? Yani inasemaje hiyo form ya kiapo
 
Sawa tupo sawa lakini hii chanjo ya Sasa watu wanaigopa maana yaonyesha hofu kwa watu hasa ukizingatia zimekuja kwa emergency na baadhi ya nchi walisitisha baadhi ya chanjo kutokana na kuleta tafrani baada ya kusababisha some cases na hata kupelekea vifo.
Mi sidhani chanjo hizi za uviko 19 zinathibitishwa na chanjo tulizopata huko awali!,mkuu watu huiamini serikali yao lakini kwa hili la serikali kuchukua chanjo toka nje(sio kosa lakini Kama ikiwa salama kwa watu) lakini swala la kusainishwa ka mkataba ka for your own risk,inaleta mashaka sana maana hata government inaonyesha inahofu juu ya chanjo husika na inajiepusha na lawama juu ya chochote kitakachokukuta kutokana na chanjo husika!.. what this..??
Mkuu hilo la kuhusu kusaini lisikutie shaka ni nchi zote wanafanya hivyo hiyo ni kama formality tu.
 
Mnaopinga chanjo tuleteeni mbadala maana Delta Force amekamatia chini mapmb huku kitaa na hamna majibu ya kueleweka nini kifanyike!
 
Mkuu mleta mada.....naomba nieleze kuhusu hicho kiapo.......una sign kiapo cha namna gani?? Yani inasemaje hiyo form ya kiapo
Ni form tu ya kukubali kuchanjwa na kutoilaumu/kui-hold responsible Serikali.

Ni kawaida as hata ukiingizwa thietre hasa kwa major operation unasaini
 
Mtazamo huu si Sahihi. Ukipata hii makitu u may end up kuusambaza kwa wengine. Ukiambukiza wasio na Kinga nzuri they end up die
Kama kila mmoja wetu atazingatia kanuni za kujikinga UVIKOZ-19 utatoweka. Lakini, kwa asili ya binadamu na tabia mbalimbali tutaishi nao kama magonjwa mengine.

Kwa kuwa tutaishi nao, ukweli ni kwamba kila mtu ajali afya yake kwa jinsi ya ushauri wa wataalamu wa afya
 
Shida ni kuwa most of people are careless, kwa hiyo Tunahitaji chanjo. Hilo la kuchukua tahadhali ni zuri ila wengi hawajali. Angalia hapo ulipo wenye barakoa ni wangapi?
 
Back
Top Bottom