#COVID19 Tuliochanjwa chanjo ya COVID-19 Karibuni tutoe mrejesho

Mwendazake alifanikiwa kuwafanya watanzania kuhofia kuhusu chanjo na vita vya uchumi , kuwa wazungu wanataka kutuua na chanjo.
Wajinga ndio waliwao...[emoji1787][emoji1787]
Nenda kachanje wewe mdanganyika, chanjo kwa afya na usalama wako.
 
Naona unayatafuta majanga yasiyo ya lazima.
Ukigeuka zombie tunakupiga risasi ya kichwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sitakubali mnishuti.

Hivi nyinyi mnajiamini na washambuliaji mlio nao?
 
Nenda kituo kingine waambie una HIV au una Sickle cell au Pumu kali watakuchoma bila janjajanja
 
siku ya3 leo, maumivu kwa mbaali pale nilipo dungwa sindano kwenye bega la kushoto, hopeful by tomorrow kila kitu kitakaa sawaa………….
 
Mimi nilichanja jana, niliwaambia ni diabetic 2, wakasema unatumia dawa za kukohozi nikasema ndio, wakaziagalia zile dawa wakasema hakuna shida ni za allergy tu....ila wakashauri madaktari wawambie wachanjwaji kama unatumia dawa za kikohozi usichanje kwanza.....sikutoa kitambulisho wala nini, nilijaza tu fomu..yenye maelekezo ya kujua ninaishi mtaa gani na other normal details, kisha nisaini mwaka wa kuzaliwa below 50! nikadungwa ..bado sijaona shida sana!
 
Nilichanja leo saa nne asubuhi chanjo ya Jahnson & johnson,sasa hivi ni saa kumi na mbili jioni nasikia homa kwa mbali na joto linapanda.
 
Congratulations rafiki.
 
Homa ni normal. Hapo Kinga inajijenga. Hongera
Mkuu usiku nimechakazwa kwelikweli.Kichwa kilikuja kuuma,misuli ikauma na joto kupanda sana ila sasa hivi joto limeshuka,misuli haiumi tena.Kimebakia kichwa tu.
 
Mimi nimepiga leo..sikuwa na mpango wa kuchoma kabisaaa!!
Ila nilipeleka aunt wangu na bibi tena walikuwa hawataki kusikia habari za chanjo kabisa..
Nikawapiga somo vizuri wakaelewa nikawapeleka!!
Sijui wazo gani liliniingia.chap chap nikaweka booking nikachoma.ajabu tulikuwa sisi tuu.naona mwitikio wa chanjo bado upo chini sana.
Nimechoma kiukweli sijahisi chchote zaidi ya hofu tuu!!
 
Hebu nipe heads up za utaratibu wa kufuata kwa tunaotaka kupiga Chanjo mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…