Tuliodumu miaka 20+ kwenye ndoa zetu tukutane hapa tupeane na kubadilishana uzoefu

Kuna mwingine atajisifu ndoa yake imetulia,lakini akishafika home atafua chupi za mkewe,ataogesha watoto na kupika msosi. Ndoa zina siri nyingi na ni vema siri zibaki kuwa siri.
Sasa mkuu kupika msosi au kuogesha watoto nalo ni kosa? Hizi ndizo taabu za ndoa kujifanya kuna majukumu ya wanawake na wanaume. Siku hizi kuna hizi mambo za unpaid care work mwanangu inabidi tugawane tu majukumu.
 
Wewe una umri gani hata ushangae ndoa kudumu miaka 20?

Means una miaka chini ya 20 kwamba hata wazazi wako hawajaifikia hiyo 20 nadhani ila 20 ni michache wapo watu wamegonga 50 years pamoja.
pamoja mkuu ndoa ni kuvumiliana.
 
Hongereni sana, ndoa ni kuchukuliana madhaifu na kukubali kusameheana na kujishusha pale inapobidi.
 
😅😅😅 wahenga hawaamini!
 
Mwenyewe Nina miaka 10 ivi. Iko very interesting bana, meza yangu imepinduka so imebidi nisimamie kila kitu. Nimeelewa kwanini mnaenda bar kunywa, kumbe sometimes sio kwamba mnapenda ni kupunguza mawazo tu maana kuna wakati nasikia kuchizi. Home enyewe ukirudi hata nguvu ya shoo hamna kabisa. Huko kwenyewe kwenye kupambana, unakutana na Zaddy's, viBen10, watu wa kila aina😶 very interesting aisee.
Kwakweli mwanaume hakikisha unatafuta pesa na kulea familia, na pia nawapa pongezi wanaume wote wapambanaji na akirudi home anatoa shoo ya kufa mtu. Mbarikiwe. Si rahisi kabisa, ila nashukuru Mungu kwa yote!
 
Kipindi cha korona Mzee, nilikuwa naingia bar nashangaa wadau hawapo bar.
 
Kuna mwingine atajisifu ndoa yake imetulia,lakini akishafika home atafua chupi za mkewe,ataogesha watoto na kupika msosi. Ndoa zina siri nyingi na ni vema siri zibaki kuwa siri.
Mbona hakuna Tatizo hapo!
1.kufua chupi za mkewe hayo ni mahaba!
2.kuogesha watoto anatengeneza bond
3.kupika anasaidia majukumu pia ni sehemu ya kuonesha upendo!
 
Maisha yanachangamoto sana ,maisha yana majaribu sana ,tumepoteza marafiki ,wengine wamefungwa katika kupambania mkate...lakini hakuna jinsi life inabidi liendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…