Hongera sanaHuyu ndio mwanamke alikuja getto kwangu kunitembelea, ikabidi nitoke nikamchukulie chochote kitu, mfukoni nilikuwa na buku tu ambayo nilikuwa na mpango ndio nitakula mchana, kwa kuogopa aibu nikasema ngoja nimfatie soda ya miasita na biscuit za mia nne, basi nikatoka.
Ile nafika ndani nikampa, akaniuliza wewe mbona hauli? Nikamwambia umekuta ndio nimetoka kula kwa mama ntilie, bado nimeshiba, ila kiukweli nilikuwa na njaa sana.
Akaniambia naomba unisaidie kunifatia vocha hata ya buku nataka niongee na mama, daah moyoni nikajisemea hii sasa ndio balaa, nikatoka kama naenda dukani halafu nikazunguka nikaenda kukaa mlango wa nyuma kimyaa, kama baada ya dakika 3 nikarudi, nikamwambia vocha wameishiwa, hawako serious wauzaji wa mtaani hapa, nitakutumia baadae nikienda mjini wala usijali, hilo likapita.
Ikafika muda akawa anaondoka, nimemsindikiza, akaniambia "Ukweli humuweka mtu huru" hilo neno ni dogo lakini lina maana katika maisha.
Nikamwambia sijaelewa labda ufafanue, akasema siwezi kufafanua mi nishamaliza. Basi akaondoka,
Ile narudi home sina hili wala lile, nikaja kukuta 20k chini ya mto wa kulalia, sikuamini macho yangu, maana nilikuwa naenda kulala njaa kabisa, nilishukuru sana Mungu, nikamtafuta kwa simu kumuuliza akasema ni mimi nimeziacha maana nilikuona ulivyozunguka kukaa nyuma ya nyumba. Daah nilipata hisia fulani hivi, anyway to make a story short huyo mwanamke ndio mke wangu kwa sasa, na tunaishi vizuri tu, shetani tunazidi kumkemea kwa nguvu zote. 😀
Miaka 20 iliyopita vocha zilikuwepo?Huyu ndio mwanamke alikuja getto kwangu kunitembelea, ikabidi nitoke nikamchukulie chochote kitu, mfukoni nilikuwa na buku tu ambayo nilikuwa na mpango ndio nitakula mchana, kwa kuogopa aibu nikasema ngoja nimfatie soda ya miasita na biscuit za mia nne, basi nikatoka.