Tuliofunga gesi kwenye magari njooni tupongezane, bajeti ya mafuta kutoka 900,000/= hadi 200,000/= kwa mwezi

Tuliofunga gesi kwenye magari njooni tupongezane, bajeti ya mafuta kutoka 900,000/= hadi 200,000/= kwa mwezi

BINAFSI NILIWASIKIA HAO DIT WAKIHOJIWA CLOUDS FM NA WALISEMA KWASASA WANABADILISHA MAGARI YANAYOTUMIA TU PETROL YA UKUBWA WA AINA YOYOTE KWA GHARAMA YA TSH, MILIONI MOJA NA LAKI NANE (1,800,000) WAKASEMA VIFAA VYA KUFUNGA MAGARI YANAYOTUMIA DIESEL WAMESHALETA ILA BADO HAWAJAANZA KUFUNGA ILA SOON WATAANZA PIA YA DIESEL.
PIA WALISEMA KWENYE DASH BOdi KUTAKUA NA ALAMA INAYOONESHA KIWANGO CHA GESI KILUCHOPO KAMA TU INAVYOONYESHA MAFUTA, PIA KUTAKUWA NA BUTON MAALUM YENYE UWEZO WA KUSWICH OFF UPANDE WA GESI KAMA IMEKWISHA NA KURUDI UPANDE WA MATUMIZI YA PETROL.
NA WALISEMA KWASASA KILO MOJA YA GESI NI TSH, 1500 NA KWA GARI DOGO INA UWEZO WA KUTEMBEA MPAKA KM 27 KWA KG, 1 NAFIKIRI KIDOGO NIMEELEWEKA.
Umeelewka kuliko hata aliyeleta Uzi... Ila heruf kubwa zinabooooooa....
 
Ni modification ndogo tu wanafanya kwenye dashboard, kuna kuwa na zile reserve port za kufunga extra switch pale pembeni ya ignition, wataalam wanaelewa zaidi. Na pia kuna slave ECU inayounganishwa na master ECU / computer ili zishirikiane kwenye seamless/smooth changerover ya gesi kwenda mafuta and vice-versa. Na slave computer ikihisi gas pressure imeshuka sana basi automatically infyatua switch na kuirudisha kwenye mafuta, just incase umejisahau.
Gharama zake zikoje?
 
Sasa mkuu kama unalazimika kubonyeza switch utasemaje kwamba inarudi kwenye mafuta automatically? Fafanua hapo.
Incase umenotice wewe mwenyewe kwamba gesi imepungua basi unaweza ukajisalimisha kwa kubonyeza switch, ila kama umejisahau kuna computer ambayo wanaifunga na inauwezo wa kudect low gas pressure na kufyatua ile switch automatically.
 
Hiyo garama 1.8M si bora kama una gari inakula sana mafuta uuze af ununue ka terios kid au gari yoyote yenye cc ndogo lita moja km 20 sasa ya nn gharama kubwa na akat mafuta yapo nunua hata tata nano full tank unatumia mwezi mzima maaana kana piston 2 tuu
Mnataka tununue hivyo vitoy halafu baadae mtunange kwamba tunatembelea gari za kuongea michepuko si ndio? Hapana aisee, nunua wewe kwanza hiyo terios kid..
 
Ingefaa ifungulie Uri maalum wa hili suala, mtu aandike kirefu na afafanue zaidi, ni wapi unaweza kufunga huo mtungi na kwa gharama gani, na mtungi huo ni wa lita ngapi na utakupeleka km ngap, na hiyo gesi ni ya bei gani. Na je kama nitanunua gari linalotumia gesi kama ya huku ulaya je nitaweza kutumia huko TZ..
Watu wengi watanufaika hapo.
Kwenye gas hawatumii vipimo vya Lita mkuu ila wanatumia vipimo vya kg.
 
Iyo kitu nimeeilewa sana mabebru wasije kutuchonganisha tu km Libya maana biashara yao ya mafuta inaingia doa.
Gesi yetu ya Mtwara ianze sasa kuchakatwa mahsusi kwa ajili ya soko la ndani la magari, maana ni mengi mno, ni muda wetu sasa kuokoa fedha za kigeni zinazotumika kuagiza nishati nje ya nchi, tutumie nishati yetu wenyewe, kama tunavyofanya kule Kinyerezi.
 
Back
Top Bottom