Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Aliyepataga faida kubwa kwenye kilimo ni Sir Jeff aka Ontario! Nakumbuka alipiga 39M Kwa msimu mmoja na alikuwa anafanya kuwalimia watu!

Yaliyomkuta sasa!!!!
 
Ukiweka gharama za ww kwenda Na kurudi pamoja na Chakula hakuna faida
 
Government naona sasa imeshaanza kuamka kidogo:-

"Kuna malalamiko huko Watu wanasema mbona bei ya unga imepanda hamtengenezi bei elekezi, unatengenezaje bei elekezi wakati alipokuwa analima hakuna aliyekwenda?,

Hatupangi bei elekezi, ukiona mahindi yamepanda bei kanunue mchele, huwezi basi usile"-HASUNGA http://
 
Mwingine aliwahi kusema kama hauna nauli ya kupanda pantoni piga mbizi.

 
Mwingine aliwahi kusema kama hauna nauli ya kupanda pantoni piga mbizi.
Kiukweli kaka serikali imewatia wakulima wengi kwenye wimbi kubwa la umaskin kwa habari za bei elekezi kumjali mlaji pasipo kujali gharama alizotumia mkulima pamoja na mateso ya shambani,ni vyema sasa mkulima akawa na haki ya kujipangia bei anayoona inafaa kwendana na gharama zake alizotumia pamoja na faida ambavyo soko huru litaamua na siyo serikali;serikali isaidie pembejeo,miundombinu nk. na kuweka minimum price sokoni na siyo kutuwekea maximum price
 

Katika kilimo mkulima hana sauti ktk soko. Soko linatawaliwa na madalali pamoja na wafanyabiashara. faida ni nusu kwa nusu wakati mwingine mpaka zaidi ya robo tatu. Mfano ukiona tenga la nyanya linauzwa elf 70 sokoni basi ujue mkulima kauza elfu 20. Serikali inatakiwa iingilie kati hapa katikati ya mkulima na mfanyabiashara
 
Ila ndugu habari yako sijaikubali haileti mashiko kwangu, mimi ni mkulima miaka sita mfululizo, ni kweli kuna hasara huwa inapatikana kwenye kilimo ila sio kwa kiwango hicho unachokizungumzia kiasi kwamba unakatisha watu tamaa ya kupambana na maisha unless hilo ndio lengo lako kukwamisha watu kupambana.

Kilimo kina hasara na hasara take huja kwa Maana ya kupishana na malengo tunayo jiwekea hasa ikiwa tumehamasika kulima kupitia social media na tukaamua kuanza kilimo bila kujua uhalisia was ABC zilizopo kwenye kilimo.

Halafu jua kuwa Roma haikujengwa kwa siku moja/mafanikio hayawezi kuja ndani ya misimu miwili mitatu ya kulima, uvumilivu ndio nguzo ya kilimo.
 
Mie sijamkatisha mtu tamaa nimeelezea real experience niliyokutana nayo. na bahati nzuri wengine nao wameshare experience walizokutana nazo kama ambavyo mada inasema.

Fuatilia comment za watu wamefunguka hasa uhalisia waliokutana nao. kuna wengine hata kwenye mavuno hawakufikia, wengine waliingiliwa na ng"ombe nk.

Lengo la kuweka changamoto ni watu wajifunze kugeuza changamoto kua fursa na si kuwakatisha tamaa. ndo maana kuna wengine wameamua kua walanguzi tu nk.

Mara nyingi tunapenda kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa bila kuelezea ukweli wa changamoto ili watu wajipange. Nimekutana na changamoto zaidi ya hizo nilizoshare
 
Hapa nakubaliana na wewe 100%
Inabidi mtu aanze kidogo kidogo
 

Mie sijamkatisha mtu tamaa nimeelezea real experience niliyokutana nayo. na bahati nzuri wengine nao wameshare experience walizokutana nazo kama ambavyo mada inasema. Fuatilia comment za watu wamefunguka hasa uhalisia waliokutana nao. kuna wengine hata kwenye mavuno hawakufikia, wengine waliingiliwa na ng"ombe nk.

Lengo la kuweka changamoto ni watu wajifunze kugeuza changamoto kua fursa na si kuwakatisha tamaa. ndo maana kuna wengine wameamua kua walanguzi tu nk. Mara nyingi tunapenda kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa bila kuelezea ukweli wa changamoto ili watu wajipange. Nimekutana na changamoto zaidi ya hizo nilizoshare
 
Usikate tamaa hata mimi mwaka Jana sikuvuna mahindi vizuri ila nilipata chakula na mpaka sasa bei ya mahindi imepanda mi nachekelea tu maana ni stock ya kula miaka 2 na mpunga ninao sisi wa kanda ya kati bado tuna butter trade kipindi cha mavuno nilibadilisha mpunga gunia kwa gunia nikaweka gunia zangu kumi Niko dar huwa napiga Simu tu home pakia debe mbili zinakuja wakati wengine wanamlaumu mangi kupandisha bei ya mchele na unga Mimi kimyaaa
 
Duh! Tutafika kweli
 
Nendeni Same kuna kilimo cha mpunga cha umwagiliaji uhakika wa mazao mkubwa na mpunga hauharibiki unaweka stoo unasubiria bei ipande
Same sehemu gani...tuambie zaidi, je wewe umefanya au unamfahamu mtu alie au anaefanya na matokeo yake ...
 
Milioni 28 zilirudi ngapi?
 
Aliyepataga faida kubwa kwenye kilimo ni Sir Jeff aka Ontario! Nakumbuka alipiga 39M Kwa msimu mmoja na alikuwa anafanya kuwalimia watu!

Yaliyomkuta sasa!!!!
Yapi yaliyomkuta mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…