Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Aliyepataga faida kubwa kwenye kilimo ni Sir Jeff aka Ontario! Nakumbuka alipiga 39M Kwa msimu mmoja na alikuwa anafanya kuwalimia watu!

Yaliyomkuta sasa!!!!
 
Kuna mwaka niliweka ndani KARANGA maeneo ya Mpwapwa, niliwekeza 5m! Baada ya miezi 8, nakuja kuiProcess na kuuza! Kutoa gharama zote ikiwemo wabebaji, ushuru wa gate, transport! Shabash! Nlipata faida 350k na mind you storage ilikuwa bure! Km ningelipia storage manake ningeliwa!
Ukiweka gharama za ww kwenda Na kurudi pamoja na Chakula hakuna faida
 
Government naona sasa imeshaanza kuamka kidogo:-

"Kuna malalamiko huko Watu wanasema mbona bei ya unga imepanda hamtengenezi bei elekezi, unatengenezaje bei elekezi wakati alipokuwa analima hakuna aliyekwenda?,

Hatupangi bei elekezi, ukiona mahindi yamepanda bei kanunue mchele, huwezi basi usile"-HASUNGA http://
 
Mwingine aliwahi kusema kama hauna nauli ya kupanda pantoni piga mbizi.

Government naona sasa imeshaanza kuamka kidogo:-
"Kuna malalamiko huko Watu wanasema mbona bei ya unga imepanda hamtengenezi bei elekezi, unatengenezaje bei elekezi wakati alipokuwa analima hakuna aliyekwenda?, hatupangi bei elekezi, ukiona mahindi yamepanda bei kanunue mchele, huwezi basi usile"-HASUNGA http://
 
Mwingine aliwahi kusema kama hauna nauli ya kupanda pantoni piga mbizi.
Kiukweli kaka serikali imewatia wakulima wengi kwenye wimbi kubwa la umaskin kwa habari za bei elekezi kumjali mlaji pasipo kujali gharama alizotumia mkulima pamoja na mateso ya shambani,ni vyema sasa mkulima akawa na haki ya kujipangia bei anayoona inafaa kwendana na gharama zake alizotumia pamoja na faida ambavyo soko huru litaamua na siyo serikali;serikali isaidie pembejeo,miundombinu nk. na kuweka minimum price sokoni na siyo kutuwekea maximum price
 
Katika kilimo mkulima hana sauti ktk soko. Soko linatawaliwa na madalali pamoja na wafanyabiashara. faida ni nusu kwa nusu wakati mwingine mpaka zaidi ya robo tatu. Mfano ukiona tenga la nyanya linauzwa elf 70 sokoni basi ujue mkulima kauza elfu 20. Serikali inatakiwa iingilie kati hapa katikati ya mkulima na mfanyabiashara
 
Naanza kwa kutoa experience yangu.

Niliingia kwenye kilimo baada ya kushawishika na vipindi vya Clouds Media kuhusiana na fursa. Presenters walishawishi sana kuwa vijana hatujitumi na hatutumii brain zetu vizuri.

Nikajitosa kwenye kilimo cha tikiti Migoli Iringa na milioni zangu 2. Nikaingia front mwenyewe sikutaka kilimo cha simu. Nilikutana na changamoto katika kulima nikapambana nazo nilikuwa nalala shamba kwenye vibanda vya nyasi, vibarua wanazingua balaa na changamoto ya madawa. Baadae nikafanikiwa kuvuna na yalikubali sana.

Mziki ukaja kwenye soko sasa. Unatoka mjini na mfanyabiashara kuja shamba kununua mzigo, mjini umeacha bei ya tikiti 1 ni elfu 4. Mfanyabiashara shamba anataka kununua tikiti 1 sh 500, nikaamua kwenda nayo mwenyewe sokoni Dodoma. Kufika pale, dah! washaambizana wafanyabiashara wao hawanunui direct kutoka kwa mkulima; wananunua kupitia madalali, ikanibidi niwakabidhi madalali mzigo. Hapo nilichoka nilirudi nyumbani na laki 4.

Nikaingia kwenye kilimo cha vitunguu Ruaha Mbuyuni. Nikapambana nacho; jani lilikubali balaa kila siku nikawa napiga picha narusha social media. Wakati wa kuvuna kuja kuchimba chini chenga tu nikaishia kuuza reja reja nikatoka na laki 7.

Nikaja kulima mahindi ya kuchoma maarufu kama Gobo. Nilipambana nayo mpaka mwisho kwenye soko tena changamoto. Mfanyabiashara anakuja kuchagua mahindi shamba anataka kununua muhindi mmoja kwa sh 120 ilihali mjini muhindi mmoja sh 500, nikaghairi kuuza nikasubiri yakauke bahati nzuri bei ya mahindi nzuri.

My take: Katika kilimo madalali na wafanyabiashara ndiyo wanaonufaika sana kuliko wakulima.
Ila ndugu habari yako sijaikubali haileti mashiko kwangu, mimi ni mkulima miaka sita mfululizo, ni kweli kuna hasara huwa inapatikana kwenye kilimo ila sio kwa kiwango hicho unachokizungumzia kiasi kwamba unakatisha watu tamaa ya kupambana na maisha unless hilo ndio lengo lako kukwamisha watu kupambana.

Kilimo kina hasara na hasara take huja kwa Maana ya kupishana na malengo tunayo jiwekea hasa ikiwa tumehamasika kulima kupitia social media na tukaamua kuanza kilimo bila kujua uhalisia was ABC zilizopo kwenye kilimo.

Halafu jua kuwa Roma haikujengwa kwa siku moja/mafanikio hayawezi kuja ndani ya misimu miwili mitatu ya kulima, uvumilivu ndio nguzo ya kilimo.
 
Mie sijamkatisha mtu tamaa nimeelezea real experience niliyokutana nayo. na bahati nzuri wengine nao wameshare experience walizokutana nazo kama ambavyo mada inasema.

Fuatilia comment za watu wamefunguka hasa uhalisia waliokutana nao. kuna wengine hata kwenye mavuno hawakufikia, wengine waliingiliwa na ng"ombe nk.

Lengo la kuweka changamoto ni watu wajifunze kugeuza changamoto kua fursa na si kuwakatisha tamaa. ndo maana kuna wengine wameamua kua walanguzi tu nk.

Mara nyingi tunapenda kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa bila kuelezea ukweli wa changamoto ili watu wajipange. Nimekutana na changamoto zaidi ya hizo nilizoshare
 
Hata hiyo ya kununua mazao usiingie kwa pupa anza taratibu ikiwa kama sehem ya kujifunza. Mkiambiwaga kua gunia moja unapata faida elf 50 basi kwa tamaa mtu anatupia million 10 ili apige 30. Kuna changamoto ya kuuziwa mpunga ambao sokon hauna wateja ukaja baki Na mzigo stoo au ukauza kwa hasara
Hapa nakubaliana na wewe 100%
Inabidi mtu aanze kidogo kidogo
 
Ila ndugu habari yako sijaikubali haileti mashiko kwangu, mimi ni mkulima miaka sita mfululizo, ni kweli kuna hasara huwa inapatikana kwenye kilimo ila sio kwa kiwango hicho unachokizungumzia kiasi kwamba unakatisha watu tamaa ya kupambana na maisha unless hilo ndio lengo lako kukwamisha watu kupambana.

Kilimo kina hasara na hasara take huja kwa Maana ya kupishana na malengo tunayo jiwekea hasa ikiwa tumehamasika kulima kupitia social media na tukaamua kuanza kilimo bila kujua uhalisia was ABC zilizopo kwenye kilimo.

Halafu jua kuwa Roma haikujengwa kwa siku moja/mafanikio hayawezi kuja ndani ya misimu miwili mitatu ya kulima, uvumilivu ndio nguzo ya kilimo.

Mie sijamkatisha mtu tamaa nimeelezea real experience niliyokutana nayo. na bahati nzuri wengine nao wameshare experience walizokutana nazo kama ambavyo mada inasema. Fuatilia comment za watu wamefunguka hasa uhalisia waliokutana nao. kuna wengine hata kwenye mavuno hawakufikia, wengine waliingiliwa na ng"ombe nk.

Lengo la kuweka changamoto ni watu wajifunze kugeuza changamoto kua fursa na si kuwakatisha tamaa. ndo maana kuna wengine wameamua kua walanguzi tu nk. Mara nyingi tunapenda kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa bila kuelezea ukweli wa changamoto ili watu wajipange. Nimekutana na changamoto zaidi ya hizo nilizoshare
 
Mwaka jana nimelima eka tatu za mpunga, mnvua ikagoma mwanzoni ikaja mwishoni, nikapata matumaini, ulivoanza kukauka ikanyesha mvua ya mawe,ikapukutisha wote uliokuwa umekauka.
Niliambulia gunia 13, sijaziuza nasubiri bei ipande
Sijakata tamaa, mwaka huu nalima tena. Mungu atie baraka zake
Usikate tamaa hata mimi mwaka Jana sikuvuna mahindi vizuri ila nilipata chakula na mpaka sasa bei ya mahindi imepanda mi nachekelea tu maana ni stock ya kula miaka 2 na mpunga ninao sisi wa kanda ya kati bado tuna butter trade kipindi cha mavuno nilibadilisha mpunga gunia kwa gunia nikaweka gunia zangu kumi Niko dar huwa napiga Simu tu home pakia debe mbili zinakuja wakati wengine wanamlaumu mangi kupandisha bei ya mchele na unga Mimi kimyaaa
 
Government naona sasa imeshaanza kuamka kidogo:-
"Kuna malalamiko huko Watu wanasema mbona bei ya unga imepanda hamtengenezi bei elekezi, unatengenezaje bei elekezi wakati alipokuwa analima hakuna aliyekwenda?, hatupangi bei elekezi, ukiona mahindi yamepanda bei kanunue mchele, huwezi basi usile"-HASUNGA http://
Duh! Tutafika kweli
 
Nendeni Same kuna kilimo cha mpunga cha umwagiliaji uhakika wa mazao mkubwa na mpunga hauharibiki unaweka stoo unasubiria bei ipande
Same sehemu gani...tuambie zaidi, je wewe umefanya au unamfahamu mtu alie au anaefanya na matokeo yake ...
 
Mimi niliwekeza mkuranga kama 28 mil nikachimba Visima nk, Nikaweka Wafanyakazi wawili, Siku ya kwanza tukapanda Embe ekari nane, asubuhi miche yote imeibiwa ! Niliagiza miche SUA kila mche elfu 3... Roho iliuma hatari..

Nilisikitika mno, nikaanza mboga mboga, mpunga, basi bwana si nikaanza kilimo cha simu, sikuambulia hata shilingi moja ! Nikastop...

Nikahamia kwa broilers, île nataka kuwatoa soko likaharibika hata tuliyekubaliana awe anachukua akashindwa maana naye alikua anapeleka mahala, nikafanya batch nne nikaona sasa huu Msala... Nikastop...

Ila sasa Nimerudi tena kivingine, Nimepata mikataba ya broilers tumesaini ndo nimeanza, nitakua natoa broilers elfu moja kila Wiki, nilichojifunza Ni kutokukata tamaa na kufanyia kazi zile changamoto zilizokukuta, usiache.. Jitafakari anza tena !
Milioni 28 zilirudi ngapi?
 
Aliyepataga faida kubwa kwenye kilimo ni Sir Jeff aka Ontario! Nakumbuka alipiga 39M Kwa msimu mmoja na alikuwa anafanya kuwalimia watu!

Yaliyomkuta sasa!!!!
Yapi yaliyomkuta mkuu
 
Back
Top Bottom