Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

Mimi niliwekeza mkuranga kama 28 mil nikachimba Visima nk, Nikaweka Wafanyakazi wawili, Siku ya kwanza tukapanda Embe ekari nane, asubuhi miche yote imeibiwa ! Niliagiza miche SUA kila mche elfu 3... Roho iliuma hatari..

Nilisikitika mno, nikaanza mboga mboga, mpunga, basi bwana si nikaanza kilimo cha simu, sikuambulia hata shilingi moja ! Nikastop...

Nikahamia kwa broilers, île nataka kuwatoa soko likaharibika hata tuliyekubaliana awe anachukua akashindwa maana naye alikua anapeleka mahala, nikafanya batch nne nikaona sasa huu Msala... Nikastop...

Ila sasa Nimerudi tena kivingine, Nimepata mikataba ya broilers tumesaini ndo nimeanza, nitakua natoa broilers elfu moja kila Wiki, nilichojifunza Ni kutokukata tamaa na kufanyia kazi zile changamoto zilizokukuta, usiache.. Jitafakari anza tena !
 
Unapata wapi mda wa kuuza reja reja akat mzigo shamban unaharibika, dereva na ww inabidi mle ,mlale n.k
 
Strawberries unapandeje milima
 
Hapa polisi unacheza nao vp mkuu mana wakikudaka si wanasumbua sana....na awamu hii kila mtu anataka kuonekana anafanya kaz vzur bas lazma alupeleke jela
 
Halafu hii miraa kule Kenya si imehalalishwa au?
 
Walimfanyia hivi mdogo wangu huko tabora daah kumbe mwanajeshi akachukua wana wake watatu wakala full beto alafu kila mtu ana pikipiki kuingia kijijini wanakijiji wote mbio alafu mvua ilikataa kipindi hiko basi wakachukua ng'ombe wote au millioni kumi daah dogo ndipo alipopatia faida hapo otherwise ilikua matherloss
Wasukuma wasumbufu sana
 
Miche ya maembe iliibwaje sasa??? Itakuwa ndugu zako hao walikuzungukaa
Kama alilima kwa sm miche wanaiuza wanakwambia imeibiwa. Ukiwatumia dawa waweke shamban wanawauzia wenye mashamba ya jiran. Jamaa yangu alikua analima vitunguu kwa sim yeye akawa anaibuka jumapili tu kutokana na kubanwa na kazi. Kwa wiki ilitakiwa kumwagilia Mara 3. Jamaa walikua wanamwagilia jumamosi shamba linaloa balaa jumapili akifika anakuta shamba limeloa safi. Mafuta ya siku zingine wanawauzia bodaboda
 
Mtu akija na story za kulima huwa nacheka sana, maana mziki wake naujua, ngumu sana kufanikiwa kwenye kilimo, ndio maana wenye mashamba hawalimi wanaona bora wayakodishe!
Nikiwaonaga viongozi wanawashambulia vijana kua hawajiajili fursa zimejaa kwenye kilimo na kilimo kinalipa hua napata sana hasira
 

Mkuu naomba nije PM kama hautojali
 
unapata wapi mda wa kuuza reja reja akat mzigo shamban unaharibika, dereva na ww inabidi mle ,mlale n.k
Alishafika na mzigo mjini,wakati anapambana na masoko ilitakiwa kujiongeza na plan b,unatafuta ata daywaka wanakupigia Debe mdogo mdogo jioni unampa chake
 
Kama unataka Kulima wewe Lima.
Ila zile hesabu za wajasiliamali usizifuate zitakupoteza.
Maana wao hawajui kutoa na kugawanya.
Wanajua Mara na jumlisha.
Sasa utakapoweka matumaini makubwa alafu ukakuta mambo tofauti unaweza ukadata.
Namimi ndio nataka nianze ila mnanivunja moyo
 
Mzee umepambana kweli kweli. Ila haina kulaza damu.
 
Daaha Mchele kitumbo.
Umenikumbusha Mbali sanaa.
Enzi ya utoto.
Mama alikuwa ananipa sh 400 nikanunue kilo Moja.
Ila lazma niutafune njia nzima mpaka home.
Unafanana na mchele kitumbo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…