Tulioishi Dodoma miaka ya 90's mpaka miaka ya 2000 tukutane hapa tujikumbushe

aka2030

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
2,657
Reaction score
3,679
Enzi hizo Dodoma washua wote wanaishi uzunguni
Watoto wa kishua wanasoma stockley
Kina sie tunasoma amani, na mlimwa ambazo ndio zilikuwa shule bora mjini
Club ilikuwa ni NK pamoja na shilla disco mitaa ya iringa road
Picnic tunajichanga tunaenda pnde za mkalama kule ma miyuji kwenye ile swimming juu ya jiwe ama weekend swimming pool ya kule mirembe mixture na kucheza basketball
Zunny ice cream ilikuwa chimbo hatari sana watoto wa mjini lazima tukutane hapo
Enzi hizo nyerere square ndio lilikuwa soko kuu la Dodoma kabla halijavunjwa baada ya kujengwa la majengo
Mnadani ilikuwa veyula
Watoto wa mailimbi,chang'ombe tuliwaogopa hasa
 
Umesahau majengo kulikuwa na kilabu Cha masonyeni zinauzwa pombe za komoni na bia kidogo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama dodoma ya sasa iko hoi hivi hiyo ya 2000 ilikuaje ? Sio fisi tu walikuwa wanazunguka kote kama mapori yao ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…