Tulioishi Dodoma miaka ya 90's mpaka miaka ya 2000 tukutane hapa tujikumbushe

Watoto wa gwasa na uchamwinoni mlikua mnakuja sana kushinda Area C
 
Umenikumbusha enzi za NK maisha yalikuwa murua sana
 
Dah umenikumbusha mbali sana mkuu..... nimesoma primary chamwino enzi ya mwalimu mkuu Amani, utotoni na utundu ule na marafiki wa mtaani tulishapanda mlima wa mlimwa kwa waziri mkuu pale mpaka juu kabisa, kilima cha magereza pale na chenyewe tulikipanda... kuanzia pale ilipo shule ya Al hijra kulikuwa pori tu la mitunduru, ila nimezimiss sana embe mwaka hivi bado zinapatikana? Na furu, ngweru zabibu za msalato kulikuwa na mashamba makubwa tu kule ni kwenda kujichumia tu.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Enzi hizo kupanda daladala ni anasa tulikuwa full kutembea vijana wa zamam ndo maana tulikuwa na afya njema
 
Kwahiyo tulikuwa tunapishana, sie kipindi hicho tunakatiza uwanja wa ndege kwenda Dodoma Secondary, mlinzi akijipindua tunakatiza uwanja na kama amekaza tunapitia chini ya daraja lilikuwa karavati mnapita huku mmeinama.

Ikija ndege ya Rais wakati unataka kuondoka mnaenda kukaa nyuma pale upande huu wa shule ya Jamhuri wakati inatoa ule upepo ikianza ku-take off. Area D tumewinda sana ndege kipindi naishi area C kipindi hicho kulikuwa Kuna lami ila nyumba za kuhesabu na vichaka kibao
 
Kama dodoma ya sasa iko hoi hivi hiyo ya 2000 ilikuaje ? Sio fisi tu walikuwa wanazunguka kote kama mapori yao ?
Ilikuwa ukifika Uzungunguni na pale Railway kifuatacho ni pori tu mpaka Chimwaga alafu njia ya Iringa ukifika Maghorofani mpaka Mazengo Secondari kwingine kote vichaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…