Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umenikumbusha enzi za NK maisha yalikuwa murua sanaEnzi hizo Dodoma washua wote wanaishi uzunguni
Watoto wa kishua wanasoma stockley
Kina sie tunasoma amani, na mlimwa ambazo ndio zilikuwa shule bora mjini
Club ilikuwa ni NK pamoja na shilla disco mitaa ya iringa road
Picnic tunajichanga tunaenda pnde za mkalama kule ma miyuji kwenye ile swimming juu ya jiwe ama weekend swimming pool ya kule mirembe mixture na kucheza basketball
Zunny ice cream ilikuwa chimbo hatari sana watoto wa mjini lazima tukutane hapo
Enzi hizo nyerere square ndio lilikuwa soko kuu la Dodoma kabla halijavunjwa baada ya kujengwa la majengo
Mnadani ilikuwa veyula
Watoto wa mailimbi,chang'ombe tuliwaogopa hasa
Ile gari kipindi cha mvua kuloa kutu ilikuwa kawaida tu . HahahahaaMabasi enzi hizo ni kingcross
Enzi hizo kupanda daladala ni anasa tulikuwa full kutembea vijana wa zamam ndo maana tulikuwa na afya njemaDah umenikumbusha mbali sana mkuu..... nimesoma primary chamwino enzi ya mwalimu mkuu Amani, utotoni na utundu ule na marafiki wa mtaani tulishapanda mlima wa mlimwa kwa waziri mkuu pale mpaka juu kabisa, kilima cha magereza pale na chenyewe tulikipanda... kuanzia pale ilipo shule ya Al hijra kulikuwa pori tu la mitunduru, ila nimezimiss sana embe mwaka hivi bado zinapatikana? Na furu, ngweru zabibu za msalato kulikuwa na mashamba makubwa tu kule ni kwenda kujichumia tu.
Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
Mpaka Kesho, Vumbi Maji ChumviDODOMA YA VUMBIIIIII TU PUMBAFU.
HaaNgoja waje...
Masonyeni hadi 2015 kilikuwepoUmesahau majengo kulikuwa na kilabu Cha masonyeni zinauzwa pombe za komoni na bia kidogo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwahiyo tulikuwa tunapishana, sie kipindi hicho tunakatiza uwanja wa ndege kwenda Dodoma Secondary, mlinzi akijipindua tunakatiza uwanja na kama amekaza tunapitia chini ya daraja lilikuwa karavati mnapita huku mmeinama.Kitambo sana Dodoma. Toka Makole Primary nakatisha kiwanja cha Ndege kati navuka naenda twisheni kwa Mwal. Kikanya hapo K/Ndege shule ya msingi. Area C walikuwa wanakaa watoto wa matajiri, enzi hizo Area D ndo inaanza chipukia. Dah nimekumbuka mengi sana Dodoma. Matajiri walikuwa wakina Mzee Chove wa mabasi ya Urafiki. Bunge enzi hizo lipo mjini huku karibu na Hospitali ya General. Kwa leo ngoja niishie hapo.
Ilikuwa ukifika Uzungunguni na pale Railway kifuatacho ni pori tu mpaka Chimwaga alafu njia ya Iringa ukifika Maghorofani mpaka Mazengo Secondari kwingine kote vichakaKama dodoma ya sasa iko hoi hivi hiyo ya 2000 ilikuaje ? Sio fisi tu walikuwa wanazunguka kote kama mapori yao ?
Umenikumbusha Omax, Yohana baunsa wa N.K pamoja na Dj Kessy.
Acha bangiBai ni manyoni