Tulioitika Wito Kuhamia Burundi, Tumefarijika Sana Kumuona Former First Lady, Mama Salma Kikwete. Kumbe Rais Akiwa Mwanamke, Nchi Haina First Lady!

Unaladha fulani jinsi unavyofikisha ujumbe ktk maandiko yako, wee jamaa ni shule kabisa yaani...
Ubarikiwe!!
 
Ni ushauri tu, p mayala mara nyingi Sana mm huwa nafuatilia Sana mawazo yako lakin huwezi kutumia kiswahili fasaha unapenda kuchanganya na kingereza,Kwa nn usitumie kiswahili tu? Maana ukiweka meno LA kingereza tyari unampotosha anayekufutilia😁😁😁😁
 
Kwanini asiende Mama Janet Magufuli, Siti Mwinyi ama Anna Mkapa?
 
Mkuu, umeleta hii hoja lakini itaonekana ni chonganishi kwa wenyewe wa kule kilimani.

Na hapo Bujumbura hizo safari ni mwamvuli wa yale mambo yale, maana saa hivi karibuni pamekuwapo wahudhuriaji wengi sana.

Yaani yale mambo yale.
 
Kama kulikuwa na ulazima wa mke wa rais Mstaafu basi hata mjane wa JPM alipaswa kuwa ndiye chaguo la kwanza.

Hapa ni wazi Mungu anatufungua macho kuwa nani ana veto kubwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…