Tuliokurupukia kuanzisha biashara baadaye tukajua hatujui tukutane hapa

Dah Mkuu nipe mkopo hata wa laki 5 aisee, demand naiona but mtaji mdogo
 
Biashara yoyote ni rahisi kwa mtu anayeifanya. Ukisikia biashara fulani ni nzuri inanipa faida jua mtu yule katumia muda na yuko na Wateja hadi kufika hapo.

Ukiingia kichwa lazima mbavu ziwake moto, niliwai jaribu biashara moja yaani ikafika kipindi bora niuze kwa bei yoyote wateja huoni kudadek
 
Nilienda ilala kununua mitumba nije niuze mkoa dakika ya mwisho hizi nguo nazivaa mwenyewe za kike nilimpa demu wang
Nacheka kama mazuri pole mkuu, ila sababu ni wateja hamna ama hukufanya jitihada zaidi za kuwatafuta au pia ulizitamani uzivae mwenyewe 😛
 
Nacheka kama mazuri pole mkuu, ila sababu ni wateja hamna ama hukufanya jitihada zaidi za kuwatafuta au pia ulizitamani uzivae mwenyewe [emoji14]
Sema ht hivyo changamoto zinafahamika.kwanza nilinunua mzigo wa laki nne Tena za kupoint mwenyewe sio balo...majeje,makoti,ma t shirt na vigauni vya kike...ishu ya kwanza NI kuzinguana kwenye frem na aliyenipangisha nilitaka anifanyie marekebisho akashindwa.pili NI pointer Wangu niliyetaka aniuzie alianza kuingiza tamaa tukazinguana urafiki Hadi leo ukawa umepungua..niliamua kuanza kuzungusha mwenyewe nikitoka job saa tisa naweka kwenye bag ila ndo wateja sijapata nikaishia kuuza nguo zisizozidi 10 kwenye nguo zaidi ya 200...nikaona isiwe case demu Wangu mpya nikampa Kama nguo 20 Mimi navaa zozote Hadi Sasa Niko nazo sema TU Niko busy nataka nikitulia nitafute wauza mitumba niwauzie Bei ya chini... biashara sio mchezo.now ninawaza nimfungulie demu Wangu genge la matunda yaani mtaji wa kawaida around laki ili hata ukipotea nisiumie sana
 
Baada ya kuingia kibaruani na kusave miaka 3 niliona watu wenye bus barabaran wanafaidi sana 😃😃😃
Nikawa na ham ya hiyo biz nikanunua bus used kwa mtu daah hakuna rangi niliacha kuona
 
Umenikumbusha kipindi Corona inaingia wakawa wanasema watu wengi watakufa
Mwanaume nikaingia bank kukopa kama 7m hivi ili nipanue mradi wangu wa majeneza nikiamini ndo mwaka wangu wa kutoboa lakini cha ajabu mambo yakaenda tofauti mpaka ikafikia nakosa hata hela ya marejesho!
Kuna jamaangu ana gereji yake Dar akanishauri nichukue mzigo wa majeneza kiasi nikaweke branch Dar maana hapa Dom biashara iligoma kabisa ikabidi huyo rafiki yangu anitafutie eneo zuri Dar nikapeleka mzigo wa majeneza kama pc 250 hivi lakini huko ndo hali iligoma sana kiasi kwamba lile eneo nilipokuwa misiba mingi ni waislamu hawatumii majeneza yaani ilikuwa mpaka namaliza week nimeuza jeneza moja wakati mwingine namaliza week bila kuuza ikabidi nifunge maana hata hela ya kulipia eneo nilishindwa kulipa ikabidi nirudi Dom kuendelea na kijiwe changu cha huko.
Yaani kifupi nililazimika kuuza kagari kangu( kama ka Mr Bean) ili nipunguze deni la mkopo sintosahau mpaka nazeeka
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mkuu nimecheka Sana kudadeki
 
Umenikumbusha jamaa yangu mmoja baada ya kutoka ulaya na dollar zake kadhaa, akasema anataka akalime ni akang’ang’ania kulima vitunguu.

Kwa ufupi ile hasara aliyoipata hataki hata kusikia neno KILIMO,

  • Moja, shambani hakuvuna kama alivyotarajia
  • Pili, vile vitunguu alivyovuna alitegea eti soko lipande kumbe vitunguu vinakawaida ya kuoza

Milioni zake kadhaa ziliteketea kule na alijutavni bora angefuga ng’ombe wa maziwa kama mimi tu.
 
Dah dah nmecheka kama mazuri Dah kwahyo mkuu ulitaka watu wafe wengi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Dah Mkuu nipe mkopo hata wa laki 5 aisee, demand naiona but mtaji mdogo
Tafuta unachoweza kufanya kwa mtaji ulionao au ingiza pesa kwa njia nyingine usave ufike kiwango unachotaka. Kiwango hiki cha pesa kinapatikana kirahisi kwa njia hizo mbili si lazima kukopa.

Pia njiani hapo utajifunza kitu kitachokusaidia katika safari yako mbeleni.
 
Yeah Mkuu, polepole nasonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…