dadaake
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,125
- 1,108
Kununua mawe kunapotezaje hela mkuu,tupe darasa kdgBila shaka dhahabu kununua mawe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kununua mawe kunapotezaje hela mkuu,tupe darasa kdgBila shaka dhahabu kununua mawe?
Dah Mkuu nipe mkopo hata wa laki 5 aisee, demand naiona but mtaji mdogoBiashara na ujasirimali kiujumla ni safari ya mafunzo na mafanikio. Mafunzo ni sehemu ambazo unashindwa, unakosea, unapata hasara. Inabidi kufanya tathmini hili linapotokea ili mara zijazo uwe na somo litalokusaidia mbeleni hata kama ni vitu kama uvumilivu na bidii.
Nishawahi fanya biashara zaidi ya 20 hadi sasa na ni biashara 5 tu zilipata faida na mbili tu zilizoniingizia zaidi ya milioni 100. Kila moja ilikuwa na funzo katika hatua moja au nyingine. Naamini nisingefika hapa bila kupitia biashara ambazo zilifeli.
Sasa HV uko na product gani [emoji16][emoji16][emoji16]Nilifanya Mchele nikachezea vitasa, nikafanya Vitunguu nikachezea vitasa at least sasahivi naona Pesa kidogo
Nikiwa mmoja wao pia😂hongera sana mkuu ila navyowajua wabongo wakisoma comment yako hapa kitu pekee watachokielewa ni "zilizoniingizia zaidi ya milioni 100"[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Nacheka kama mazuri pole mkuu, ila sababu ni wateja hamna ama hukufanya jitihada zaidi za kuwatafuta au pia ulizitamani uzivae mwenyewe 😛Nilienda ilala kununua mitumba nije niuze mkoa dakika ya mwisho hizi nguo nazivaa mwenyewe za kike nilimpa demu wang
Sema ht hivyo changamoto zinafahamika.kwanza nilinunua mzigo wa laki nne Tena za kupoint mwenyewe sio balo...majeje,makoti,ma t shirt na vigauni vya kike...ishu ya kwanza NI kuzinguana kwenye frem na aliyenipangisha nilitaka anifanyie marekebisho akashindwa.pili NI pointer Wangu niliyetaka aniuzie alianza kuingiza tamaa tukazinguana urafiki Hadi leo ukawa umepungua..niliamua kuanza kuzungusha mwenyewe nikitoka job saa tisa naweka kwenye bag ila ndo wateja sijapata nikaishia kuuza nguo zisizozidi 10 kwenye nguo zaidi ya 200...nikaona isiwe case demu Wangu mpya nikampa Kama nguo 20 Mimi navaa zozote Hadi Sasa Niko nazo sema TU Niko busy nataka nikitulia nitafute wauza mitumba niwauzie Bei ya chini... biashara sio mchezo.now ninawaza nimfungulie demu Wangu genge la matunda yaani mtaji wa kawaida around laki ili hata ukipotea nisiumie sanaNacheka kama mazuri pole mkuu, ila sababu ni wateja hamna ama hukufanya jitihada zaidi za kuwatafuta au pia ulizitamani uzivae mwenyewe [emoji14]
Nazunguka minadani Mkuu vyupi, taiti mixer boxer huko hakuna sijui huyu anaenda kunununua kwa nani n.kSasa HV uko na product gani [emoji16][emoji16][emoji16]
Biashara ya kukaa na kusubiri wateja nimechezea vitasa sanaSasa HV uko na product gani [emoji16][emoji16][emoji16]
Umenikumbusha kipindi Corona inaingia wakawa wanasema watu wengi watakufaNilipojua kua sijui yangu ilikua katika biashara ya nafaka
Ilikua mwaka 2011 baada ya kufanya vibarua vya hapa na pale nikawa nimesave pesa kiasi cha tsh 750,000 nilikua na shauku sana ya kujiingiza katika biashara yoyote ya halali ili niachane na vibarua vya kutokua na uhakika wa kukipata kila siku
Sasa katika tafuta tafuta ushauri nikakutana na jamaa mmoja zamani alikua anafanya biashara ya nafaka lakini aliacha kwa kufilisika aliwekewa dawa za usingizi kwenye pombe na wahuni wakatoroka na pesa zake zote
basi jamaa hakuwa mchoyo akanipa muongozo wote wa jinsigani gani alikua anafata mahindi huko porini akanipa na mawasiliano ya rafiki yake mmoja ni mkazi wa hicho kijiji pale ambapo jamaa alipokua anafikia analala hapo kwa huyo jamaa
jamaa anafamilia mke na watoto wengi kiasi huyu mshikaji akaniambia kua kule wanahitaji mboga tu sababu ugali wanao basi nikaenda soko kuu pale mwanza nikanunua dagaa visado viwili nyanya na vitunguu
nikanunua na mifuko ile ya debe 6 na kamba na sindano ya kushonea magunia akaniambia pia nitafute debe la plastic na kisado nivichemshie maji ya moto alafu vikiisha pata moto nijaze mchanga huku naushindilia ili hilo debe na kisado vitanuke ili niweze kupata mahindi mengi kutoka kwa wanakijiji
alafu inahitajika niwe na chenji noti ndogo ndogo ili iwe rahisi maana kule nako chenji ni tabu nikaenda bank kuu pale mwanza karibu na keep left nikawaambia shida yangu wakachukua pesa zangu 750,000 wakaziweka katika mashine ya kuhakiki noti kama ni bandia
zote zilikua safi basi wakanipa chenji za vibunda vipyaaa vya 2,000 na 1,000 na 500 bila vikwazo vyovyote basi asubuhi nikaenda stendi ya mabasi nyegezi nikapanda vi HIACE vya kwenda MISUNGWI MISASI
nikashuka misasi kuna baiskeli za kwenda huko porini kijijini panaitwa NKUNGUHUMULU nauli ya baiskeli ni 500
ni kipande kirefu aisee wasukuma wanapiga pedeli baiskeli inapanda mlima kama inatelemka unapigwa na upepo tu kama umepanda bodaboda
nilifika pale kijijini jamaa mwenyeji akanipokea nikamuelezea basi akawajulisha wanakijiji kuwa kwake kuna mnunuzi wa mahindi basi wana kijiji wakaanza kuniletea mahindi mwenye kisado mwenye debe moja mwenye gunia sawa ilinichukua kama siku 3 kukamilisha gunia 21
nikawa nimebakiwa na akiba ya 80,000 nikasema hapa inatosha sasa nirudi maana mjini nimeeacha mahindi gunia wanauziwa 38,000 mpaka 40,000 kwa bei ya jumla na mimi nimemenunua kila gunia 27,000 mpaka 28,000 nikawa napiga hesabu za kwenda kukunja 200,000 kama faida
sasa kipengele kilikua usafiri kumbe kule porini fuso haiji kama hauna gunia 100 maana wale wenye fuso wanabeba kila gunia moja kwa bei ya 1,000 basi nilisota huko porini maji ya kunywa yenyewe wanachota kwenye bwawa ambalo wanako kunywa maji ng'ombe na punda wanyeji wenyewe wanayatwanga hawaoni tatizo mimi ndio siwezi yaani maji ukiyaangalia hunywi mpaka uangalie juu ndio unywe
nimekaa kama siku sita nika mpigia tena jamaa alie nielekeza, kaka vipi natokaje huku jamaa akawapigia wadau wenzake wa zamani kama wapo vijiji jirani ili anionganishe nao ili fuso lije lituchukue wadau wanasema bado mzigo wao hawaja maliza wako mjini bado
dah nimeka jamaa kampigia mdau mwingine na yeye akawa ana gunia 25 na yeye kakwama porini
basi kuna fuso moja inaitwa MAMBO YA CHINGA ilikua imeleta wamachinga vijijini sasa wanatafuta mzigo wa chap wapeleke mjini ili jioni wawarudie machinga wao hio ndio ikawa ponapona yangu ya kutoka porini
tukapakia mzigo tukafika sehemu kuna watu wa ushuru tukalipa ushuru kila gunia moja 1,000 jumla gunia moja likawa limesimamia 30,000 tumeenda mpaka sehemu moja inaitwa bugarika kuna masine ya kuuza mahindi nikapiga mzigo wangu pale kwa kua jamaa mwenyeji alikua ana kijiwe pale basi mzigo nikawa naulaza bure
tatizo likawa hapa katikati kipindi nilipokua polini kumbe kuna watu wenye mitaji mikubwa wamemwaga mahindi pale mwanza kila mtu ana mahindi basi na bei ikaanza ku drop ikashuka mpaka 34,000 kwa kila gunia da nikazidi kuvurugwa nikasemaa niki kaa sana hapa mahindi yanaweza yakashuka zaidi nikapata hasara basi mimi nikashusha bei maradufu nikayauza 32,000 mengine nikawakopesha wanao uza lejaleja lakini walinilipa kila walipo maliza mzigo
dah nikaja piga mahesabu faida niliyo pata ni 40,000 na hela yenyewe ya faida nimeshaila kuangalia mkononi mtaji wangu umebaki kiasi gani najikuta nina 690,000 kati ya 750,000 kwahio nikawa nimepoteza muda na pesa yangu kama 60,000 imepungua wanaosema biashara ni mtaji hawakukosea kipindi hicho ningekua nina mtaji kama 3,500,000 hata kama kwa kila gunia ningekua napata faida ya 2,000 bado ningekua na faida nzuri tu
BIASHARA NI MTAJI
Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mkuu nimecheka Sana kudadekiUmenikumbusha kipindi Corona inaingia wakawa wanasema watu wengi watakufa
Mwanaume nikaingia bank kukopa kama 7m hivi ili nipanue mradi wangu wa majeneza nikiamini ndo mwaka wangu wa kutoboa lakini cha ajabu mambo yakaenda tofauti mpaka ikafikia nakosa hata hela ya marejesho!
Kuna jamaangu ana gereji yake Dar akanishauri nichukue mzigo wa majeneza kiasi nikaweke branch Dar maana hapa Dom biashara iligoma kabisa ikabidi huyo rafiki yangu anitafutie eneo zuri Dar nikapeleka mzigo wa majeneza kama pc 250 hivi lakini huko ndo hali iligoma sana kiasi kwamba lile eneo nilipokuwa misiba mingi ni waislamu hawatumii majeneza yaani ilikuwa mpaka namaliza week nimeuza jeneza moja wakati mwingine namaliza week bila kuuza ikabidi nifunge maana hata hela ya kulipia eneo nilishindwa kulipa ikabidi nirudi Dom kuendelea na kijiwe changu cha huko.
Yaani kifupi nililazimika kuuza kagari kangu( kama ka Mr Bean) ili nipunguze deni la mkopo sintosahau mpaka nazeeka
Hahahaha shukran mkuu...hongera sana mkuu ila navyowajua wabongo wakisoma comment yako hapa kitu pekee watachokielewa ni "zilizoniingizia zaidi ya milioni 100"[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Dah dah nmecheka kama mazuri Dah kwahyo mkuu ulitaka watu wafe wengi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Umenikumbusha kipindi Corona inaingia wakawa wanasema watu wengi watakufa
Mwanaume nikaingia bank kukopa kama 7m hivi ili nipanue mradi wangu wa majeneza nikiamini ndo mwaka wangu wa kutoboa lakini cha ajabu mambo yakaenda tofauti mpaka ikafikia nakosa hata hela ya marejesho!
Kuna jamaangu ana gereji yake Dar akanishauri nichukue mzigo wa majeneza kiasi nikaweke branch Dar maana hapa Dom biashara iligoma kabisa ikabidi huyo rafiki yangu anitafutie eneo zuri Dar nikapeleka mzigo wa majeneza kama pc 250 hivi lakini huko ndo hali iligoma sana kiasi kwamba lile eneo nilipokuwa misiba mingi ni waislamu hawatumii majeneza yaani ilikuwa mpaka namaliza week nimeuza jeneza moja wakati mwingine namaliza week bila kuuza ikabidi nifunge maana hata hela ya kulipia eneo nilishindwa kulipa ikabidi nirudi Dom kuendelea na kijiwe changu cha huko.
Yaani kifupi nililazimika kuuza kagari kangu( kama ka Mr Bean) ili nipunguze deni la mkopo sintosahau mpaka nazeeka
Tafuta unachoweza kufanya kwa mtaji ulionao au ingiza pesa kwa njia nyingine usave ufike kiwango unachotaka. Kiwango hiki cha pesa kinapatikana kirahisi kwa njia hizo mbili si lazima kukopa.Dah Mkuu nipe mkopo hata wa laki 5 aisee, demand naiona but mtaji mdogo
Yeah Mkuu, polepole nasonga.Tafuta unachoweza kufanya kwa mtaji ulionao au ingiza pesa kwa njia nyingine usave ufike kiwango unachotaka. Kiwango hiki cha pesa kinapatikana kirahisi kwa njia hizo mbili si lazima kukopa.
Pia njiani hapo utajifunza kitu kitachokusaidia katika safari yako mbeleni.