Daaah hatari Sana , Mwamba Baada ya kumaliza chuo ,mambo hayakuenda Viral kama nilivyotegemea , nikiwa sina hili wala lile , mara paap nikapata hot news toka kwa Wana , wakanitonya kuwa biashara ya kukausha samaki aina ya furu imeburst na inalipa kinoma ... samaki hawa watu wa kanda ya ziwa wanawaelewa , samaki hukaushwa kwenye mchanga wa ufukwe mwambao wa ziwa, baada ya kukaushwa husafrishwa kuuzwa na soko kuu ni nyanda za juu kusini , hasa Tunduma mpak nchi ya Zambia ,
Mhuni nikajichanga , nikachumpa maeneo ya Fukwe za Kayenze Mkoani Mwanza , nikiwa na matumaini lukuki...!!
Asikwambie mtu maisha ya ziwani ni tough na ya kuogofya, mostly watu wanaishi in a deadliest way , magonjwa kama Amiba, Typhoid , Malaria , na magonjwa yote yanayosababishwa na ngono zembe pamoja na ushirikina wa kutosha ziwani ndo mahali pake...
Aisee katika hii biashara nilikula vitasa vya uso mpak sio poa , baada ya miezi mitatu ya hasara niliamua kutimua...!!