Kwema Wakuu!
Hakuna atakayemsema Hayatti Magufuli akapata Faida yoyote Ile, zaidi nawaona wanaomkosoa hasa viongozi wakipata uharibifu mkubwa na kujenga chuki mioyoni mwa wananchi wa chini.
Nimemsikia Mhe. Zito Kabwe akimshambulia JPM Kwa namna mbalimbali, nataka kumhakikishia Zitto kuwa anachokifanya ni kujikorogea sumu na kuinywa ambayo itamuua POLEPOLE pasipo yeye kujua.
Magufuli anamabaya yake mengi mno, lakini pia hatuwezi kujidanganya kuwa anamazuri yake pia mengi tuu.
Hayo mazuri aliwafanyia kina man? Kisha hayo mabaya aliwatendea kina Nani?
Hapo ndipo tunaweza kukokotoa mlinganyo huo, ili Wale wakosoaji na wanaomtukana Magufuli waone Kama watafaidika au laah!
Tabaka la juu la wasomi, Wataalamu, matajiri, na wafanyabiashara, wanasiasa wa Vyama vya upinzani Kwa kweli walionja joto la jiwe. Wapo waliolia kuhusu Ajira, wapo waliolalamika kutekwa na kupotezwa, wapo waliotiwa Korokoroni Kwa kesi za uhujumu uchumi, wapo waliofunguliwa kesi za ugaidi, wapo waliofunga biashara zao n.k. kundi hili sio watu wengi ukilinganisha na Kundi la Tabaka la chini.
Tabaka la chini, la watu wasiosoma, Masikini hohehahe, wasio na Vyama, vibarua, Machinga na Mama ntilie, na watifua udongo(Wakulima wadogo) hawa walimpenda Magufuli Kwa sababu mbili kuu, mosi walimuona Kama mtetezi wao; pili, Kwa kuleta kilio Kwa Tabaka la juu.
Masikini wengi sio kama maisha yao yalibadilishwa na JPM, hilo halikutokea Ila walifurahia jinsi jpm alivyokuwa akiwahenyesha mavi matajiri, wafanyabiashara na akiwafokea na kuwadhalilisha wasomi na Wataalamu. Unajua Masikini anamsemo wake usemao; msiba wa wengi ni sherehe, hivyo awamu ya JPM ilikuwa ni sherehe Kwa masikini kwani sio wao tuu waliokuwa wakiteseka bali haya matajiri walikuwa wakiteseka Kwa namna Yao.
Sasa kitendo cha JPM kufariki, kilikuwa ni huzuni Kwa Tabaka la chini kwani mtetezi wao na kuumiza tabaka la juu hayupo tena. Sasa msiba umebakia tabaka la chini, tabaka la juu limeanza kuneemeka Kwa Kula asali ya nchi.
Ukweli ni kuwa Nchi hii zaidi ya 80% ni Tabaka la chini. Hivyo kumshambulia Magufuli ni kushambulia Watanzania waliowengi. Kuwazomea, kuwakashfu, JPM Kwa tabaka la chini ni Kama Mtume au Nabii wao aliyekuja kuwakomboa lakini ungejiuliza kuwakomboa na kitu gani? Maana Kama ni umasikini bado wanao na hawana Mabadiliko yoyote yale, ndipo hapo nikakuambia kuwa labda ni Kwa sababu alifanya Tabaka la juu lihenyeke na hiyo ni sherehe Kwa tabaka la watu masikini.
Wengine tulimkosoa Magufuli akiwa hai tukiwa na Nia nzuri tuu, wala hatukuwa na chuki naye isipokuwa kuwekana Sawa. Lakini ameshakufa tunamuwekaje Sawa marehemu aliyekwisha kufa na kuzikwa. Kama ni chuki nafikiri ingekuwa imeisha ndani ya miezi sita tangu alipozikwa lakini kinachoendelea sasa hivi kinashangaza.
Hakuna sababu ya kuendelea kumshambulia mtu ambaye hana lolote la kufanya katika ulimwengu wa waliohai.
Zitto Kabwe na wengine wote mnaomshambulia JPM hakuna faaida yoyote mtakayoipata katika Jambo Hilo, zaidi Sana mnapoteza kukubalika Kwa Watanzania waliowengi ambao ni Wafuasi wa jpm waliomuona Kama mtetezi wao na mpiganaji wa matajiri ambao masikini huwaona Kama mafisadi na wezi wa Mali za nchi. Ambao masikini huwaona matajiri ndio wanaowasababishia umasikini wao
Huwaona matajiri ndio waliowasababishia wasisome
Ambao huwaona matajiri ndio wanaowatesa viwandani Kwa kuwalipa mishahara midogo.
Taikon Acha nipumzike sasa!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Twangoma.
Kwanza napingana na wewe kuwa JPM alishambulia matajiri, mimi nadhani JPM alipambana na wale wote wanaokwepa kodi awe tajir awe masikini, sasa jiulize masikini anakwepa vipi kodi hapo ndipo utakuta matajiri wasiolipa kadi ipasavyo walikutana na JPM uso kwa uso.
Pili unaposema kuwa JPM aliwakomesha wasomi wa elimu ya juu na wataalamu hili nalo nalipinga sababu kama kuna kipindi wasomi wetu wenye elimu kubwa wametamba basi ni kipindi cha JPM, ilifikia wakati mpaka akalalamiwa kuwa anamaliza wahadhiri wa UDSM kwa kuwapa vyeo. Kuhusu kukemea wasomi kweli alikemea sana hasa pale alipokuta kuna uzembe umefanyika au kuna ufisadi sasa hapo hata wewe ungekuwa ni kiongozi ungecheka? Uzur wa JPM alikuwa muwazi akichukia utamjua akifurahi utamjua.
Swala la ajira kuwa hakuajiri hili nalo halina ukweli sana nakumbuka jamaa zangu wamehudhuria interview nyingi sana kipindi cha utawala wa JPM wako walipata kazi na wengine walikosa sasa hizo ajira alitoa nani? Na ikumbukwe wakati JPM anaingia madarakani kulikuwa na tatizo kubwa la ajira kwa vijana na hii ilikuwa ni agenda kubwa ya siasa hasa kwa mzee wetu Lowasa kipindi yupo ccm aliwahi kusema ajira kwa vijana ni bomu linalosubiria kulipuka.
Kuhusu upinzani, JPM alihitaji watu wapige kazi hakuhitaji siasa za maneno matupu zitakazozuia kufikia adhma yake, mfano wewe umekamata mchanga wa madini alafu wanaibiku wapinzani wanapinga angeshirikiana nao kivipi? Alitaka kushirikiana nao kujenga nchi kwa bahati mbaya upinzani walionekana kumpinga kwa kila hatua aliyochukua kwa ajili ya kulinda maslahi ya watanzania, hasa kaka hata ingekuwa wewe ni JPM ungeshirikiana na mtu ambaye hataki wewe hufanikiwe.
Kuhusu masikini kumpenda, hii ni logic ya kawaida tu, sio kwamba walimpeda kwa kuwa aliwatesa matajiri hii sio kweli, masikini wengi walimpenda kwakuwa aliwagusa wao moja kwa moja kitu ambacho viongozi wengi hawakuwahi kufanya hivyo. Kwa mfano JPM alisimamisha msafara wake popote pale alipowakuta wananchi na aliwauliza wanashida gani , wakisema shida yao ni zahanati basi atachangisha pesa hapo atawaachia zahanati, wakisema ni barabara alijibu hapo hapo kwa itajengwa lini au haijengwi, kifupi alikuwa ni mtu mwenye majibu ya maswali magumu ya wananchi papo kwa papo hakupenda michakato, kwamba hili nalibeba talifanyia kazi yeye alimaliza palepale hichi ni kitu wananchi wengi walihisi huyu ni mtu wao.
Machinga waliachwa wafanye biashara popote bila bugudha, wachimbaji wadogo wadogo nao hawakufukuzwa na wewekezaji sasa hapo haya makundi kwa nini yasimpende? yanahaja gani yampepende mpka atese matajiri?
Kingine kilichofanya JPM apendwe na wengi ni kutekeleza ahadi zake kwa wakati, mfano JPM alikuta Dar ya foleni miaka nenda rudi lakini ndani ya mda mfupi aliikomesha foleni Dar.
Alikuta Dar kila mwaka anikipindupindu lakini ndani ya utawala wake kipindupindu kilibaki historia
Alikuta Dar inapanya Road akawamaliza.
Alikuta vijana wanashinda kunywa viroba na madawa ya kulevya lakini ndani ya utawala wake haya mambo yalipungua sana.
Kifupi JPM alionekana kwa wengi kama ni kiongozi wa tofauti kutokana na kufanya mambo magumu ambayo kwa miaka mingi yalionekana kuwa hayawezekani hivyo hizi sifa zilimfanya apendwe na wengi hasa wale wenye mapenzi mema na nchi.