Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Moja Kati ya kitu siwaelewi hawa wakosowaji ukiwafuatilia comment zao wenyewe wanasema Magufuli anapendwa na watu wengi wasio na elimu na Masikini na kweli ipo hivyo lakini hao hao wanasema Uchaguzi wa mwisho Magufuli aliiba kura na hakustahili kushinda kwasababu wananchi walimkataa but kiuhalisia hao watu wanasema Wanaompenda Magufuli ndio wapo wengi inchini kuliko hata wasomi hapo ndio wanajitekenya na kucheka wenyewe kiufupi hata siwaelewi vizuri
Si lazima duniani uelewe vyote, vikikushinda vingine unakaa kimya.
 
Ndugu yangu kiongozi bora anapimwa kwa vitu vitatu tu. Kusikiliza, kuheshimu na kuwatii wale anaowaongoza. Bahati mbaya sana Magufuli hakuwa na sifa hata moja katika hizo. Magufuli alikuwa mbabe, mkatili na mjuaji kwenye kila kitu.

Magufuli hakupendwa na watu bali alilazimisha aonekane anapendwa na kila mtu, ndio maana baada ya kufa kwake hata wale wasaidizi wake wa karibu wameamua kumgeuka na kumkana, maana wanajua hakupendwa kiuhalisia.

Kuhusu wamachinga na mama ntilie kutetewa na Magufuli wafanye biashara holela ule ulikuwa ni uhuni wa kiongozi kuvunja sheria ili aonekane anawajali. Sio kipimo sahihi cha uongozi bora.
Hao viongozi waliowaheshimu, kuwasikiliza na kuwatii walifanya nini kipindi chote cha uhuru wa TZ kabla ya JPM kukamata madaraka ya Urais 2015?

Ngozi nyeusi ni ngumu sana kuipeleka kilelemama lelemama, ndiyomaana tunaendelea kuwa maskini tukipumbazwa na democracy ilihali maisha yetu ni ya kipumbavu sana.

Nature yetu ngozi nyeusi ni kupata maendeleo kwa njia fupi tu za dili ilihali namna ya kudumisha hayo maendeleo ni 0.

JPM alikuwa anaujua sana udhaifu wa wafanyakazi wengi serikalini na taasisi binafsi hasa ikiwa alishakaa katika uongozi wa ubunge na uwaziri zaidi ya miaka 20 kabla ya kuwa Rais wa TZ.

Kwa namna hiyo utamdanganya nini sasa kuhusu kuinyoosha hii nchi kiuongozi?
 
Magufuli alishakufa.
Tuachane naye, hana jipya au jema la kuja kutufanyia sasa. Chuki dhidi ya Magufuli na wapambe wake zitaendelea milele maana Magufuli alizipandikiza na kuzikuza mpaka kumea. Kwa sasa tunavuna chuki alizozipanda yeye mwenyewe.

Ni kama ilivyokuwa kwa Hitler kule Ujerumani, mpaka leo hii kumbukumbu za ukatili wake zipo japokuwa ni mtu aliyeacha Legacy kubwa kwa wajerumani.
Mzanzibar kaongea. 😅 anamzungumzia magufuli kwa mfano wa hitler 😆😆 ama kweli akili ni mali. Unazungumzia ukali wa mbwa kwa kutolea mfano wa chui.
 
Hao viongozi waliowaheshimu, kuwasikiliza na kuwatii walifanya nini kipindi chote cha uhuru wa TZ kabla ya JPM kukamata madaraka ya Urais 2015?

Ngozi nyeusi ni ngumu sana kuipeleka kilelemama lelemama, ndiyomaana tunaendelea kuwa maskini tukipumbazwa na democracy ilihali maisha yetu ni ya kipumbavu sana.

Nature yetu ngozi nyeusi ni kupata maendeleo kwa njia fupi tu za dili ilihali namna ya kudumisha hayo maendeleo ni 0.

JPM alikuwa anaujua sana udhaifu wa wafanyakazi wengi serikalini na taasisi binafsi hasa ikiwa alishakaa katika uongozi wa ubunge na uwaziri zaidi ya miaka 20 kabla ya kuwa Rais wa TZ.

Kwa namna hiyo utamdanganya nini sasa kuhusu kuinyoosha hii nchi kiuongozi?
Kama lile bwawa lililokula mamia ya mamilioni juzi tu hapa. 😂😂
 
Ushasema Alikua na mabaya yake mengi Sana, usipoukemea ubaya wake atakuja kuibuka mwingine akifuata nyayo zake akijua ndio wengi wanapenda rais anaetafuta kiki kuliko usawa wa haki.
Huyu wa sasa hana mabaya? Au mnasubiri afe ndo mkemee 😂😂
 
Ni kweli mkuu magufuli alifanikiwa kirahisi kabisa kuwadanganya watu wajinga ambao kwa Tanzania ndio wengi kuwa alikua mtetezi wa wanyonge na mpaka leo wanaamini kuwa asingekufa mpaka leo nchi ingekuwa haina haya matatizo iliyo nayo kama kupanda kwa bei za mafuta,nauli nk
 
Ni kweli mkuu magufuli alifanikiwa kirahisi kabisa kuwadanganya watu wajinga ambao kwa Tanzania ndio wengi kuwa alikua mtetezi wa wanyonge na mpaka leo wanaamini kuwa asingekufa mpaka leo nchi ingekuwa haina haya matatizo iliyo nayo kama kupanda kwa bei za mafuta,nauli nk
Na tozo zisingekuwepo. Mafuta gharama isingekuwa kubwa kuliko wanaopitishia bandarini kwetu, waziri mdogo angekuwa hatembelei helicopta
 
Hakuna kupumzika, JPM lazima anangwe tu na Mtanzania anayeipenda Nchi yake. Yule baradhuli alikuwa anatuharibia nchi vibaya sana. Tushukuru Mungu tu aliiingilia kati akamchukua kumpeleka jehanam
Na atakuchukua na wewe kukupeleka huko huko. Yeye amepumzika unajichosha tu na mikelele yako.
 
😀😀😀😀

Unafiki ndio Siasa za Waafrika
Aliyepo hawaoni km anakosea sehemu, ye sa hv ni malaika. Au wanasubiri awe marehemu ndo wamuamshie oooh alimkalisha flan rumande miezi kadhaa, mara alishindwa kutupa tenda ya kushuti royal tour n.k
 
Chama tawala wameamua kucheza ngoma ya wapinzani bila kujua, taratibu wanapoteza wafuasi wao (pro Magufuli). Kwa maana nyingine chama tawala wanashambuliana wenyewe kwa wenyewe, wakisaidiwa na wapinzani.

Kama jina lile lisingekuwa na nguvu, wasingesimama kujitetea kila siku kuwa watamaliza miradi iliyoachwa. Kama jina lisingekuwa na nguvu wasingekusanyika chart kuazimisha. The best choice ni kukaa kimya.
 
Chuki ni chukizo. [emoji16] hata lile la kusema fagilia simba siyo jema? Huyu aliyepo hebu nae mmwambie mabaya yake mapema ili baadae tukwepe kuwatuhumu marehemu
Hapa tunaongelea Jiwe habari za wengine hizo fungulia uzi wake.
Jiwe hakuna alichokifanya chenye neema kwa watanzani.
 
Na tozo zisingekuwepo. Mafuta gharama isingekuwa kubwa kuliko wanaopitishia bandarini kwetu, waziri mdogo angekuwa hatembelei helicopta
Huu ni wivu wa kijinga kabisa
 
Kwema Wakuu!

Hakuna atakayemsema Hayatti Magufuli akapata Faida yoyote Ile, zaidi nawaona wanaomkosoa hasa viongozi wakipata uharibifu mkubwa na kujenga chuki mioyoni mwa wananchi wa chini.

Nimemsikia Mhe. Zito Kabwe akimshambulia JPM Kwa namna mbalimbali, nataka kumhakikishia Zitto kuwa anachokifanya ni kujikorogea sumu na kuinywa ambayo itamuua POLEPOLE pasipo yeye kujua.

Magufuli anamabaya yake mengi mno, lakini pia hatuwezi kujidanganya kuwa anamazuri yake pia mengi tuu.

Hayo mazuri aliwafanyia kina man? Kisha hayo mabaya aliwatendea kina Nani?
Hapo ndipo tunaweza kukokotoa mlinganyo huo, ili Wale wakosoaji na wanaomtukana Magufuli waone Kama watafaidika au laah!

Tabaka la juu la wasomi, Wataalamu, matajiri, na wafanyabiashara, wanasiasa wa Vyama vya upinzani Kwa kweli walionja joto la jiwe. Wapo waliolia kuhusu Ajira, wapo waliolalamika kutekwa na kupotezwa, wapo waliotiwa Korokoroni Kwa kesi za uhujumu uchumi, wapo waliofunguliwa kesi za ugaidi, wapo waliofunga biashara zao n.k. kundi hili sio watu wengi ukilinganisha na Kundi la Tabaka la chini.

Tabaka la chini, la watu wasiosoma, Masikini hohehahe, wasio na Vyama, vibarua, Machinga na Mama ntilie, na watifua udongo(Wakulima wadogo) hawa walimpenda Magufuli Kwa sababu mbili kuu, mosi walimuona Kama mtetezi wao; pili, Kwa kuleta kilio Kwa Tabaka la juu.

Masikini wengi sio kama maisha yao yalibadilishwa na JPM, hilo halikutokea Ila walifurahia jinsi jpm alivyokuwa akiwahenyesha mavi matajiri, wafanyabiashara na akiwafokea na kuwadhalilisha wasomi na Wataalamu. Unajua Masikini anamsemo wake usemao; msiba wa wengi ni sherehe, hivyo awamu ya JPM ilikuwa ni sherehe Kwa masikini kwani sio wao tuu waliokuwa wakiteseka bali haya matajiri walikuwa wakiteseka Kwa namna Yao.

Sasa kitendo cha JPM kufariki, kilikuwa ni huzuni Kwa Tabaka la chini kwani mtetezi wao na kuumiza tabaka la juu hayupo tena. Sasa msiba umebakia tabaka la chini, tabaka la juu limeanza kuneemeka Kwa Kula asali ya nchi.

Ukweli ni kuwa Nchi hii zaidi ya 80% ni Tabaka la chini. Hivyo kumshambulia Magufuli ni kushambulia Watanzania waliowengi. Kuwazomea, kuwakashfu, JPM Kwa tabaka la chini ni Kama Mtume au Nabii wao aliyekuja kuwakomboa lakini ungejiuliza kuwakomboa na kitu gani? Maana Kama ni umasikini bado wanao na hawana Mabadiliko yoyote yale, ndipo hapo nikakuambia kuwa labda ni Kwa sababu alifanya Tabaka la juu lihenyeke na hiyo ni sherehe Kwa tabaka la watu masikini.

Wengine tulimkosoa Magufuli akiwa hai tukiwa na Nia nzuri tuu, wala hatukuwa na chuki naye isipokuwa kuwekana Sawa. Lakini ameshakufa tunamuwekaje Sawa marehemu aliyekwisha kufa na kuzikwa. Kama ni chuki nafikiri ingekuwa imeisha ndani ya miezi sita tangu alipozikwa lakini kinachoendelea sasa hivi kinashangaza.

Hakuna sababu ya kuendelea kumshambulia mtu ambaye hana lolote la kufanya katika ulimwengu wa waliohai.

Zitto Kabwe na wengine wote mnaomshambulia JPM hakuna faaida yoyote mtakayoipata katika Jambo Hilo, zaidi Sana mnapoteza kukubalika Kwa Watanzania waliowengi ambao ni Wafuasi wa jpm waliomuona Kama mtetezi wao na mpiganaji wa matajiri ambao masikini huwaona Kama mafisadi na wezi wa Mali za nchi. Ambao masikini huwaona matajiri ndio wanaowasababishia umasikini wao

Huwaona matajiri ndio waliowasababishia wasisome
Ambao huwaona matajiri ndio wanaowatesa viwandani Kwa kuwalipa mishahara midogo.

Taikon Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Twangoma.
Ukisikia mtu anakwmabia historia itakuhukumu ndio hivyo.

Mambo ndivyo yalivyo. Wewe uliyetendewa mazuri ila hujali watu walioumizwa hongera.
 
Unaongea ukweli mkuu,kuna watu Magufuli aliwaumiza moja kwa moja kama kuwafungia biashara,kuwaweka ndani,kuvunja nyumba zao,kuwatumbua e.t.c hao hata uwaambie nini hawawezi kuona mazuri ya Magufuli na kuna watu wa hali ya chini ambao wameona ujenzi wa miundo mbinu nao huwezi kuwaambia kitu,so mwisho wa siku tutaishia kuingia kwenye mgogoro ili hali muhusika ameshafariki.Sijui watu wanajaribu kuachieve nini kumsema Magufuli daily.
Alitutisha tusimseme akiwa hai, sasa hayupo, acha asemwe, asiyetaka kumsema pia akae kimya, ni uamuzi wake.

Magufuli ndio kaweka historia yake ya kusemwa au kutosemwa ama kwa mazuri au kwa mabaya
 
Back
Top Bottom