Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Hao watu wa chini wengi ni watu wa kuburuzwa tu hawana uelewa wowote. Wengi Magufuli aliwapata maana aliua Uhuru wa vyombo vya habari, na kubaki kuwatangazia alichokitaka. Lakini watu hao hao wa chini wakipata upande wa pili wa shilingi watabadilika na watajiuliza waliwezaje kuongozwa na mtu muovu na mwizi wa aina hiyo. Kama kweli Magufuli alikuwa anakubalika na hao watu wa chini angeheshimu box la kura. Kwakuwa mikutano ya wazi imezuiliwa ndio maana unaamini kuna kundi la chini kubwa tiifu kwa Magufuli. Watu watakapoanza kwenda kwenye mikutano ndio utajua hawana msimamo wowote.

Propaganda alizimudu
 
Kama mtu kakosea, asemwe tu.

Bila kujali wafuasi wake ni wengi ama la.

Bila kujali mzima ana kafa.

Huo ndio uongozi.

Uongozi ni kuonesha watu hapa mlikosea, bila kujali kama utaudhi wengi ama wachache.

Ukianza kuangalia nani ana wafuasi wachache ili umnange, unachanganya siasa na uongozi.

Tatizo ninaloliona ni huu ujinga wa mtu leo akiwa Tanzania anasema "Mimi na Magufuli ni kitu kimoja", akienda Marekani anasema "Tulitofautiana sana na Magufuli"

😀😀😀😀

Unafiki ndio Siasa za Waafrika
 
Kwema Wakuu!

Hakuna atakayemsema Hayatti Magufuli akapata Faida yoyote Ile, zaidi nawaona wanaomkosoa hasa viongozi wakipata uharibifu mkubwa na kujenga chuki mioyoni mwa wananchi wa chini.

Nimemsikia Mhe. Zito Kabwe akimshambulia JPM Kwa namna mbalimbali, nataka kumhakikishia Zitto kuwa anachokifanya ni kujikorogea sumu na kuinywa ambayo itamuua POLEPOLE pasipo yeye kujua.

Magufuli anamabaya yake mengi mno, lakini pia hatuwezi kujidanganya kuwa anamazuri yake pia mengi tuu.

Hayo mazuri aliwafanyia kina man? Kisha hayo mabaya aliwatendea kina Nani?
Hapo ndipo tunaweza kukokotoa mlinganyo huo, ili Wale wakosoaji na wanaomtukana Magufuli waone Kama watafaidika au laah!

Tabaka la juu la wasomi, Wataalamu, matajiri, na wafanyabiashara, wanasiasa wa Vyama vya upinzani Kwa kweli walionja joto la jiwe. Wapo waliolia kuhusu Ajira, wapo waliolalamika kutekwa na kupotezwa, wapo waliotiwa Korokoroni Kwa kesi za uhujumu uchumi, wapo waliofunguliwa kesi za ugaidi, wapo waliofunga biashara zao n.k. kundi hili sio watu wengi ukilinganisha na Kundi la Tabaka la chini.

Tabaka la chini, la watu wasiosoma, Masikini hohehahe, wasio na Vyama, vibarua, Machinga na Mama ntilie, na watifua udongo(Wakulima wadogo) hawa walimpenda Magufuli Kwa sababu mbili kuu, mosi walimuona Kama mtetezi wao; pili, Kwa kuleta kilio Kwa Tabaka la juu.

Masikini wengi sio kama maisha yao yalibadilishwa na JPM, hilo halikutokea Ila walifurahia jinsi jpm alivyokuwa akiwahenyesha mavi matajiri, wafanyabiashara na akiwafokea na kuwadhalilisha wasomi na Wataalamu. Unajua Masikini anamsemo wake usemao; msiba wa wengi ni sherehe, hivyo awamu ya JPM ilikuwa ni sherehe Kwa masikini kwani sio wao tuu waliokuwa wakiteseka bali haya matajiri walikuwa wakiteseka Kwa namna Yao.

Sasa kitendo cha JPM kufariki, kilikuwa ni huzuni Kwa Tabaka la chini kwani mtetezi wao na kuumiza tabaka la juu hayupo tena. Sasa msiba umebakia tabaka la chini, tabaka la juu limeanza kuneemeka Kwa Kula asali ya nchi.

Ukweli ni kuwa Nchi hii zaidi ya 80% ni Tabaka la chini. Hivyo kumshambulia Magufuli ni kushambulia Watanzania waliowengi. Kuwazomea, kuwakashfu, JPM Kwa tabaka la chini ni Kama Mtume au Nabii wao aliyekuja kuwakomboa lakini ungejiuliza kuwakomboa na kitu gani? Maana Kama ni umasikini bado wanao na hawana Mabadiliko yoyote yale, ndipo hapo nikakuambia kuwa labda ni Kwa sababu alifanya Tabaka la juu lihenyeke na hiyo ni sherehe Kwa tabaka la watu masikini.

Wengine tulimkosoa Magufuli akiwa hai tukiwa na Nia nzuri tuu, wala hatukuwa na chuki naye isipokuwa kuwekana Sawa. Lakini ameshakufa tunamuwekaje Sawa marehemu aliyekwisha kufa na kuzikwa. Kama ni chuki nafikiri ingekuwa imeisha ndani ya miezi sita tangu alipozikwa lakini kinachoendelea sasa hivi kinashangaza.

Hakuna sababu ya kuendelea kumshambulia mtu ambaye hana lolote la kufanya katika ulimwengu wa waliohai.

Zitto Kabwe na wengine wote mnaomshambulia JPM hakuna faaida yoyote mtakayoipata katika Jambo Hilo, zaidi Sana mnapoteza kukubalika Kwa Watanzania waliowengi ambao ni Wafuasi wa jpm waliomuona Kama mtetezi wao na mpiganaji wa matajiri ambao masikini huwaona Kama mafisadi na wezi wa Mali za nchi. Ambao masikini huwaona matajiri ndio wanaowasababishia umasikini wao

Huwaona matajiri ndio waliowasababishia wasisome
Ambao huwaona matajiri ndio wanaowatesa viwandani Kwa kuwalipa mishahara midogo.

Taikon Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Twangoma.
Huku ni kufikiria kienyeji zaidi. Nchi bila kujua historia yake haiwezi kupanga ya mbele. Historia ni muhimu sana kwani inatufunza mengi na kutufanya kutorudia makosa tuliyofanya nyuma. Wananchi na viongozi wote wako sahihi kusema mabaya na mazuri yaliyofanywa na viongozi wa nyuma. Wewe unadhani kusema mabaya yake nia yake ni kumrekebisha tu wakati mabaya yake yanatumika kuongoza viongozi wajao ili wasirudie makosa.
 
Hao watu wa chini wengi ni watu wa kuburuzwa tu hawana uelewa wowote. Wengi Magufuli aliwapata maana aliua Uhuru wa vyombo vya habari, na kubaki kuwatangazia alichokitaka. Lakini watu hao hao wa chini wakipata upande wa pili wa shilingi watabadilika na watajiuliza waliwezaje kuongozwa na mtu muovu na mwizi wa aina hiyo. Kama kweli Magufuli alikuwa anakubalika na hao watu wa chini angeheshimu box la kura. Kwakuwa mikutano ya wazi imezuiliwa ndio maana unaamini kuna kundi la chini kubwa tiifu kwa Magufuli. Watu watakapoanza kwenda kwenye mikutano ndio utajua hawana msimamo wowote.
Sema tena na tena. Mimi kila siku huwa nawaambia watu waache kutufanyia illussion zao za kijinga. Hivi kweli kama alipendwa sana na watu wa hali ya chini ambao ndiyo wengi kabisa kwenye nchi yetu, kwa nini aliogopa kuacha uchaguzi ufanyike na badala yake akafanya uporaji ambao haujawahi kushuhudia? Angeachia walau watu wapige kura wakishamaliza ndiyo apore ili ajue anakubalika kiasi gani, kama ilivyotokea Zanzibar kipindi cha Jecha!
 
Mtoa mada ROBERT HERIEL uliwahi kuleta mada ukihusisha "umasikini na shetani" kwamba masikini ni mashetani yanayoishi, huku ukisema "matajiri ni wa Mungu maana Mungu naye ni tajiri.

Na ukasema utajiri ni Siri maana hata Mungu hajawahi kuonekana japo anamiliki mbingu na ardhi.

Sasa basi, kwa kuwa masikini ni shetani (kwa mujibu wako) je, jiwe alikuwa anayatetea mashetani (masikini) na kuwasulubu matajiri (Mungu)?, And aftermath, ni kipi kimejiri?

Sasa kwa kuwa Zitto hapati faida kwa kukosoa mtetezi wa shetani, je, jiwe alipata ni nini kwa kuwatetea masikini dhidi ya matajiri?
Hahaha!! "USISAIDIE MASIKINI WACHA WAFE" bonge la heading la kikatili kabisa.
 
Mtoa mada ROBERT HERIEL uliwahi kuleta mada ukihusisha "umasikini na shetani" kwamba masikini ni mashetani yanayoishi, huku ukisema "matajiri ni wa Mungu maana Mungu naye ni tajiri.

Na ukasema utajiri ni Siri maana hata Mungu hajawahi kuonekana japo anamiliki mbingu na ardhi.

Sasa basi, kwa kuwa masikini ni shetani (kwa mujibu wako) je, jiwe alikuwa anayatetea mashetani (masikini) na kuwasulubu matajiri (Mungu)?, And aftermath, ni kipi kimejiri?

Sasa kwa kuwa Zitto hapati faida kwa kukosoa mtetezi wa shetani, je, jiwe alipata ni nini kwa kuwatetea masikini dhidi ya matajiri?

😊😊

MKUU msimamo wangu upo palepale. Huwezi pambana na Mungu ukashinda!

Kupambana na Utajiri ni kuukataa uzima
 
Sema tena na tena. Mimi kila siku huwa nawaambia watu waache kutufanyia illussion zao za kijinga. Hivi kweli kama alipendwa sana na watu wa hali ya chini ambao ndiyo wengi kabisa kwenye nchi yetu, kwa nini aliogopa kuacha uchaguzi ufanyike na badala yake akafanya uporaji ambao haujawahi kushuhudia? Angeachia walau watu wapige kura wakishamaliza ndiyo apore ili ajue anakubalika kiasi gani, kama ilivyotokea Zanzibar kipindi cha Jecha!

Alitarajia anapendwa kweli kutokana na kupiga propaganda na kuziamini. Lisu alipoanza kampeni na kuona mwitikio aliokuwa anapata, tena akiwa hana bango hata moja nchi nzima, wala matangazo kwenye televisheni, akajua anakwenda kukutana na ukweli utakaomsononesha kwenye box la kura. Akaona isiwe tabu bora apore uchaguzi. Na alijua kabisa mwenendo wake kwenye demokrasia ya nchi yetu ndio ulishusha idadi ya wapiga kura. Hivyo ili kukwepa lawama toka kwa chama chake kuwa ndio kaharibu demokrasia, ikabidi apore uchaguzi na kutangaza matokeo yasiyo na uhalisia wowote.

Alivyoona haikai vizuri akasema hakuna kushangilia ushindi bali watu wachape kazi. Lakini katika hali ya kushangaza hasa kuanzia wakati wa kampeni, ni kama alipata msongo wa mawazo kwa kuona aliyemchafua kwa kumuita msaliti muda wote anapata uungwaji mkono mkubwa. Hali ile ya msongo wa mawazo iliendelea kumuandama na hakuwa na furaha tena hadi mauti yanamkuta, kutokana na ukweli aliopewa na hasimu wake mkubwa Tundu Lisu wakati wa kampeni. Na Lisu asingefanikiwa kuondoka baada ya uchaguzi chini ya mabalozi angemuua, maana alikuwa ameshachanganyikiwa na hakuwa na busara ya kiuongozi au kimaamuzi.
 
Magufuli alibrainwash watu, kazi ya kuwa"unbrainwash" ni muhimu iendelee japo kelele zitakuwa nyingi.
Hatuwezi kujenga jamii iliyostaaribika ambayo majority bado Wana sumu Kauli ya ujinga waliyopandikizwa na Mtu.
Tumestruggle sana kufuta propaganda za zidumu fikra za Mwenyekiti Sasa tunastruggle kufuta propaganda na ujinga alioupandikiza mwendazake. Hii ni kazi muhimu lazima ifanywe.
 
Ndio maana nawashauri viongozi Kama kina Zitto Kabwe wawaachie watu wa mitandaoni mambo haya kwani wao hawana chakupoteza Ila Kwa Viongozi Kama wao haiwezi kuwa nzuri kwao Kisiasa
Mtu analipwa kwa kazi hiyo, hawezi kuacha. Zitto yeye aongee tu lakini ataacha tu, wengine nao wataongea pia. Wanapambana na marehemu.
 
Kwema Wakuu!

Hakuna atakayemsema Hayatti Magufuli akapata Faida yoyote Ile, zaidi nawaona wanaomkosoa hasa viongozi wakipata uharibifu mkubwa na kujenga chuki mioyoni mwa wananchi wa chini.

Nimemsikia Mhe. Zito Kabwe akimshambulia JPM Kwa namna mbalimbali, nataka kumhakikishia Zitto kuwa anachokifanya ni kujikorogea sumu na kuinywa ambayo itamuua POLEPOLE pasipo yeye kujua.

Magufuli anamabaya yake mengi mno, lakini pia hatuwezi kujidanganya kuwa anamazuri yake pia mengi tuu.

Hayo mazuri aliwafanyia kina man? Kisha hayo mabaya aliwatendea kina Nani?
Hapo ndipo tunaweza kukokotoa mlinganyo huo, ili Wale wakosoaji na wanaomtukana Magufuli waone Kama watafaidika au laah!

Tabaka la juu la wasomi, Wataalamu, matajiri, na wafanyabiashara, wanasiasa wa Vyama vya upinzani Kwa kweli walionja joto la jiwe. Wapo waliolia kuhusu Ajira, wapo waliolalamika kutekwa na kupotezwa, wapo waliotiwa Korokoroni Kwa kesi za uhujumu uchumi, wapo waliofunguliwa kesi za ugaidi, wapo waliofunga biashara zao n.k. kundi hili sio watu wengi ukilinganisha na Kundi la Tabaka la chini.

Tabaka la chini, la watu wasiosoma, Masikini hohehahe, wasio na Vyama, vibarua, Machinga na Mama ntilie, na watifua udongo(Wakulima wadogo) hawa walimpenda Magufuli Kwa sababu mbili kuu, mosi walimuona Kama mtetezi wao; pili, Kwa kuleta kilio Kwa Tabaka la juu.

Masikini wengi sio kama maisha yao yalibadilishwa na JPM, hilo halikutokea Ila walifurahia jinsi jpm alivyokuwa akiwahenyesha mavi matajiri, wafanyabiashara na akiwafokea na kuwadhalilisha wasomi na Wataalamu. Unajua Masikini anamsemo wake usemao; msiba wa wengi ni sherehe, hivyo awamu ya JPM ilikuwa ni sherehe Kwa masikini kwani sio wao tuu waliokuwa wakiteseka bali haya matajiri walikuwa wakiteseka Kwa namna Yao.

Sasa kitendo cha JPM kufariki, kilikuwa ni huzuni Kwa Tabaka la chini kwani mtetezi wao na kuumiza tabaka la juu hayupo tena. Sasa msiba umebakia tabaka la chini, tabaka la juu limeanza kuneemeka Kwa Kula asali ya nchi.

Ukweli ni kuwa Nchi hii zaidi ya 80% ni Tabaka la chini. Hivyo kumshambulia Magufuli ni kushambulia Watanzania waliowengi. Kuwazomea, kuwakashfu, JPM Kwa tabaka la chini ni Kama Mtume au Nabii wao aliyekuja kuwakomboa lakini ungejiuliza kuwakomboa na kitu gani? Maana Kama ni umasikini bado wanao na hawana Mabadiliko yoyote yale, ndipo hapo nikakuambia kuwa labda ni Kwa sababu alifanya Tabaka la juu lihenyeke na hiyo ni sherehe Kwa tabaka la watu masikini.

Wengine tulimkosoa Magufuli akiwa hai tukiwa na Nia nzuri tuu, wala hatukuwa na chuki naye isipokuwa kuwekana Sawa. Lakini ameshakufa tunamuwekaje Sawa marehemu aliyekwisha kufa na kuzikwa. Kama ni chuki nafikiri ingekuwa imeisha ndani ya miezi sita tangu alipozikwa lakini kinachoendelea sasa hivi kinashangaza.

Hakuna sababu ya kuendelea kumshambulia mtu ambaye hana lolote la kufanya katika ulimwengu wa waliohai.

Zitto Kabwe na wengine wote mnaomshambulia JPM hakuna faaida yoyote mtakayoipata katika Jambo Hilo, zaidi Sana mnapoteza kukubalika Kwa Watanzania waliowengi ambao ni Wafuasi wa jpm waliomuona Kama mtetezi wao na mpiganaji wa matajiri ambao masikini huwaona Kama mafisadi na wezi wa Mali za nchi. Ambao masikini huwaona matajiri ndio wanaowasababishia umasikini wao

Huwaona matajiri ndio waliowasababishia wasisome
Ambao huwaona matajiri ndio wanaowatesa viwandani Kwa kuwalipa mishahara midogo.

Taikon Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Twangoma.
Mbona hata maza naye anamsema vibaya na wakati ndiyo alikuwa msaidizi wake no 1?
 
Magufuli alibrainwash watu, kazi ya kuwa"unbrainwash" ni muhimu iendelee japo kelele zitakuwa nyingi.
Hatuwezi kujenga jamii iliyostaaribika ambayo majority bado Wana sumu Kauli ya ujinga waliyopandikizwa na Mtu.
Tumestruggle sana kufuta propaganda za zidumu fikra za Mwenyekiti Sasa tunastruggle kufuta propaganda na ujinga alioupandikiza mwendazake. Hii ni kazi muhimu lazima ifanywe.
Kweli tupu
 
Lisu alikuwa mpigaji wa nini?Ben Saanane alikuwa mpigaji wa nini?Mbowe alikuwa mpigaji wa nini?Acheni upimbi nyie.******** alikuwa mnywa damu za watu.Halafu;Miundo mbinu aliyoijenga ******** ni ipi?Mradi gani aliuanzisha na kuumaliza?Acheni kuendeleza propaganda,Sasa hivi nchi haiendeshwi kwa propaganda,inaendeshwa kwa uhalisia .Kiuhalisia Mama Samia kwa muda mchache tu amejenga miundombinu mingi kuliko ******** wenu.
Ukiwa na chuki, hata mtu akiwa mwema kiasi gani utamuona muovu.
 
Magufuli this Magufuli that.

Kwanini wasingemwambia mbele ya uso wake akiwa hai ili awajibu. Hapo wanatudhihirishia kuwa hao jamaa ni waoga mno.

Maana wanasubiri mtu amefariki ndio wanamsema. Kama kweli wao ni watu wangemwambia akiwa hai tuone umwamba wao.

A bunch of cowards that we have and hypocrites too. Maana waliishi nae ila kinafiki.

Mtu mnafiki ni mbaya zaidi kuliko hata muuaji.
 
Mtu mnafiki anakuua akiwa amekufunga kitambaa usoni ili usimuone
 
HAYATI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI;MWAMBA UNAOTIKISA UKIWA UMELALA.

Leo 10:15pm 18/04/2022

Hayati Rais Magufuli anaendelea kutikisa kwa sababu moja tu hakuna mtu mwenye sifa kama zake kiutawala,hili nalisema kama mbobezi katika masuala ya Uongozi,Rais John Pombe Magufuli alikuwa Champion katika mambo mengi na kila mwananchi analijua hilo,hii inawapa wakati mgumu viongozi wengi wanapokuwa mbele za Wananchi hivi sasa,useme nini wananchi wakuelewe,maana tayari Wananchi wana mfano wao wa kiongozi bora,wana performance appraisal ya kiongozi wao bora,nae ni John Pombe Magufuli,Mtu ambae amefanya kazi na watanzania bara miaka zaidi ya 20 akiwa ni Field Public Leader tangu akiwa Naibu Waziri miaka ya 1995 kisha Waziri kamili katika wizara zaidi ya tano kwa miaka ishirini na baadaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Je tunatenda haki kumtukana kiongozi wetu huyu aliyelala milele!? Je mtu huyu atukanwe hadharani,utakuwa unamuumiza nani kama si Watanzania,leo Zitto anatufundisha sisi kuhusu Utendaji wake wakati kazi zake zipo wazi nchi nzima,alikuwa ni mmoja wa Viongozi wachache sana Wazalendo wa kweli kwa Wananchi wanyonge Nchi nzima ya Tanzania,sasa viongozi tunafeli hapa,tunapokuwa mbele ya Watanzania,Mimi kama kiongozi nifanyeje ili nami wanione bora kama Rais John Pombe Magufuli au niwe bora zaidi yake,je nimtukane au nitende kama yeye,kwa hivyo basi Rais Magufuli amefanyika kuwa kipimio cha wengi kwa kihaya wanasema Rais Magufuli amefanyika kuwa ( Measuring stick) kila kiongozi lazima atamtaja Rais Magufuli ili kufikisha ujumbe wake,kila kiongozi anaetaka kukanekti na wananchi basi lazima amtaje Rais Magufuli ili kujiweka sawa kwenye uongozi na Wananchi waweze kumuelewa,bila kutaja jina la Rais Magufuli basi Wananchi hawawezi kukuelewa,

-Faida na hasara za kulitaja jina la Rais Magufuli.

1.Faida

Katika Uongozi wa Rais Magufuli tulishuhudia improvements kubwa sana katika huduma za kijamii na miundo mbinu ambayo kimsingi Watanzania wengi walikuwa wahanga wa huduma mbovu kabla yake, hivyo basi utakapo fanya jambo jema kwenye huduma za jamii au miundo mbinu na ukalitaja jina la Rais Magufuli basi Wananchi watakuelewa sana.

Hayati Rais Magufuli alileta elimu bure,aliwasaidia Watanzania wengi sana. Takwimu zinathibitisha hili baada ya wanafunzi wengi sana kuongezeka sasa,hii ni faida aliyoleta Rais Magufuli.Rais Magufuli alitatua kero za wanyonge na walioonewa ambao walishaomba msaada kwa wasaidizi wake karibu wote bila kusaidiwa,na wakakata tamaa,Wananchi walifurahi Rais Magufuli alipokwenda na kutatua matatizo yao pale pale,hiyo ilikuwa ni karama ya Uongozi aliyokuwa nayo Rais Magufuli.

Magufuli alilinda rasilimali za nchi,tulifikia wakati hadi twiga wanapanda ndege,unatarajia Watanzania wengi tungemchukia,jibu ni hapana, Watanzania walimpenda Rais Magufuli kwa sababu Wanyama waliongezeka mbugani badala ya kupungua na takwimu zinaonyesha,Rais Magufuli alijenga ukuta Mererani kuzuia kuibiwa kwa madini ya Tanzanite,hii hakuifanya kwa ajili yake bali aliifanya kwa ajili ya Watanzania,je unatarajia Watanzania wamchukie!?

Rais Magufuli aliwatetea machinga na mama ntilie, nao wakawa walau na uhuru wa kufanya biashara zao halali kwa amani ili kupata vipato vya kusaidia familia zao.je unatarajia Watanzania wangemchukia Watanzania walimpenda kwa kuwa alikuwa kiongozi bora, not kwa kuwa aliwahenyesha matajiri hapana Rais Magufuli hakuhenyesha matajiri, alihenyesha wapigaji,wala rushwa,waonea wanyonge, Mafisadi na walanchi.

-Hasara

Unapotaja jina la Rais Magufuli kwa chuki binafsi za udini,ukabila au itikadi hii ni hasara kwako,adui yako si Magufuli,kwa wapinzani adui yenu ni CCM kama itafanya vibaya mbele za Wananchi,Kosa hilohilo lilifanywa na Chadema ambao waligombana na Zitto na Dkt Slaa huku adui yao akiwa ni CCM ambayo ilionekana kuanza kukataliwa kwa Wananchi,kwa sasa tuna tatizo kubwa la mfumuko wa bei vitu vinavyowagusa Wananchi moja kwa moja badala yake Zitto Mambo ya mwaka 2017 na anamtaja mtu aliyekufa!! Sasa ataamka aje akurekebishie mfumuko wa bei uliopo hii leo!!?

Tukiwa kwenye mfumuko wa bei hakuna atakayemsema Hayati Rais Magufuli akapata Faida yoyote Ile, zaidi nawaona wanaomkosoa hasa viongozi kama akina Zitto wakipata uharibifu mkubwa na kujenga chuki mioyoni mwa wananchi wa hali ya chini,masikini ambao daima walimuona Rais Magufuli mkombozi wao,wakati huu wa maisha magumu vitu vinapanda bei ukimshambulia Rais Magufuli, Kwa namna mbalimbali,ni kujimaliza kisiasa,kifikra,kiutamaduni na kimaendeleo.

Kundi la Wananchi masikini walioneemeka au kupata ahueni kijamii,kiuchumi na kisiasa katika awamu ya Rais Magufuli daima watamchukia mtu ambae anamsema Rais Magufuli ambae kwao alikuwa mkombozi,Kitendo cha Rais Magufuli kuleta nidhamu serikalini tayari ni neema maana watu watahudumiwa ipasavyo na hakika watu walihudumiwa ipasavyo,Umeme ulikuwa stable na Umeme usipokatika unatumika na watu wote na ukiwa stable faida twapata sote,Aliwaachia wamachinga uhuru wa kutengeneza vipato vyao vya halali na wakapata hela kwa kazi za halali kwa hakika Wamachinga walimpenda Rais Magufuli kwa hilo,na kwa ujumla hatuwezi kusema hakuna alieneemeka kiuchumi!.Rais Magufuli alijenga Reli ya Umeme kwa faida ya Watanzania,Rais Magufuli alijenga masoko Kila Wilaya Tanzania mzima kwa faida ya Watanzania,sio kwa faida yake,Rais Magufuli alijenga Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere kwa faida ya Watanzania,Rais Magufuli alihamisha makao makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa faida ya Watanzania.

Leo atanangwa juu ya covid lakini twende ndani turudi nje mzee alifanya maamuzi sahihi juu ya lile suala,hilo gonjwa la corona tutaishinalo kama mafua na ukimwi tu hata huko nje sasa wanaishinalo,Rais Magufuli hakukataa chanjo ila alitaka uhakika wa chanjo hizo kama ni salama kwanza,hii ni kwa faida ya Watanzania,yeye kama mkemia nae alitaka kujiridhisha,sio kupokea tu,Kinachofanyika sasa ni kutoa ile imani ya utendaji wa Rais Magufuli ndani ya akili za Watanzania!,maana watu wanaamini ule utendaji wake kama ndio kiongozi anavyopaswa kuwa na waliusubiri uongozi kama huo kwa muda mrefu,sasa viongozi wa sasa wanajua tutawahukumu kwa kumtumia magufuli kama mfano!..Mfano suala la upatikanaji wa umeme lilivyoanza kusuasua ni mashahidi tosha watu walianza kupiga kelele!,na hii ni kwa sababu tulishazoeshwa huduma hii kutokuwa ya kusuasua katika Uongozi wa Rais Magufuli.

Nimalizie kwa ushauri kwa viongozi wetu,hakuna sababu ya kuendelea kumshambulia mtu ambaye hana lolote la kufanya katika ulimwengu wa waliohai,Zitto na wengine wote mnaomshambulia Rais Magufuli hakuna faida yoyote mtakayoipata katika Jambo hilo,zaidi sana mnapoteza kukubalika kwa Watanzania waliowengi ambao ni wafuasi wa JPM waliomuona Kama mtetezi wao na mpiganaji wao mbele ya sauti za matajiri ambao masikini huwaona matajiri kama mafisadi na wezi wa mali ya Umma,Ningemshauri Zitto aanze kuondoa dhana ya kuwa matajiri ni mafisadi na awaonyeshe kwa vitendo kuwa matajiri ni wakombozi na Wananchi waelewe,unapoteza muda kupambana na mtu aliyelala milele.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Ndio maana nawashauri viongozi Kama kina Zitto Kabwe wawaachie watu wa mitandaoni mambo haya kwani wao hawana chakupoteza Ila Kwa Viongozi Kama wao haiwezi kuwa nzuri kwao Kisiasa
Jitu lishakula chake kimya kimya ili kuichafua legacy ya JPM litakuelewa nakati ndiyo kwaaanza limeanza kushupalia shingo na hivi lina udini kibao kichwani mwake, sijui [emoji848][emoji2960]
 
Back
Top Bottom