Tuliokuwa tunamponda Magufuli akiwa hai, sasa tutamtetea akiwa Amekufa!

Kuna watu humu akili hamna ndio maana mnamshabikia mgonjwa wa akili.

Magufuli hakufanya kampeni mikoa yote ya kusini alikuwa anaogopa uchawi halafu uchaguzi alishaumaliza kwenye kikao chake na watendaji wa Tanzania nzima kilichofanyika ikulu baada tv zote zilizokuwa live zilikata matangazo na kuanza kikao cha wizi wa kura ambao ni wa kishamba mno, unaiba kura hadi Pemba hata wasiokuwa na akili wanaelewa kwamba hapa kuna namna.

Dhulma za namna Mungu anakuadhibu mapema sana kwa sababu matokeo yake leo hakuna bunge la wananchi, mtu mmoja amedhulumu haki za mamilioni kuachaguwa wawakilishi wao.

Huyu mwehu wenu angekuwa anajitambuwa angeaiba kura zake za Urais na majimboni unaacha watu wapambane.

Ukitaka kujuwa washindi halali wa uchaguzi ule na nani alipata kura ngapi basi angalia kura za mbunge aliyeshinda wa ccm ana kura ngapi halafu ondowa kura 3000 kwa kila kata ya jimbo ndio utapata kura halisi nani alishinda wapi na kwa kura ngapi.
 
Sawa Chawa wa Nape ,
Ila ukwl mchungu.

Habari tunazo kwamba hata kwenye kampeni zako ulizomewa jimboni.

Sasa ungeshindaje Kama sio Magufuli kuiba Kura?
 
Kwanza napingana na wewe kuwa JPM alishambulia matajiri, mimi nadhani JPM alipambana na wale wote wanaokwepa kodi awe tajir awe masikini, sasa jiulize masikini anakwepa vipi kodi hapo ndipo utakuta matajiri wasiolipa kadi ipasavyo walikutana na JPM uso kwa uso.

Pili unaposema kuwa JPM aliwakomesha wasomi wa elimu ya juu na wataalamu hili nalo nalipinga sababu kama kuna kipindi wasomi wetu wenye elimu kubwa wametamba basi ni kipindi cha JPM, ilifikia wakati mpaka akalalamiwa kuwa anamaliza wahadhiri wa UDSM kwa kuwapa vyeo. Kuhusu kukemea wasomi kweli alikemea sana hasa pale alipokuta kuna uzembe umefanyika au kuna ufisadi sasa hapo hata wewe ungekuwa ni kiongozi ungecheka? Uzur wa JPM alikuwa muwazi akichukia utamjua akifurahi utamjua.

Swala la ajira kuwa hakuajiri hili nalo halina ukweli sana nakumbuka jamaa zangu wamehudhuria interview nyingi sana kipindi cha utawala wa JPM wako walipata kazi na wengine walikosa sasa hizo ajira alitoa nani? Na ikumbukwe wakati JPM anaingia madarakani kulikuwa na tatizo kubwa la ajira kwa vijana na hii ilikuwa ni agenda kubwa ya siasa hasa kwa mzee wetu Lowasa kipindi yupo ccm aliwahi kusema ajira kwa vijana ni bomu linalosubiria kulipuka.

Kuhusu upinzani, JPM alihitaji watu wapige kazi hakuhitaji siasa za maneno matupu zitakazozuia kufikia adhma yake, mfano wewe umekamata mchanga wa madini alafu wanaibiku wapinzani wanapinga angeshirikiana nao kivipi? Alitaka kushirikiana nao kujenga nchi kwa bahati mbaya upinzani walionekana kumpinga kwa kila hatua aliyochukua kwa ajili ya kulinda maslahi ya watanzania, hasa kaka hata ingekuwa wewe ni JPM ungeshirikiana na mtu ambaye hataki wewe hufanikiwe.

Kuhusu masikini kumpenda, hii ni logic ya kawaida tu, sio kwamba walimpeda kwa kuwa aliwatesa matajiri hii sio kweli, masikini wengi walimpenda kwakuwa aliwagusa wao moja kwa moja kitu ambacho viongozi wengi hawakuwahi kufanya hivyo. Kwa mfano JPM alisimamisha msafara wake popote pale alipowakuta wananchi na aliwauliza wanashida gani , wakisema shida yao ni zahanati basi atachangisha pesa hapo atawaachia zahanati, wakisema ni barabara alijibu hapo hapo kwa itajengwa lini au haijengwi, kifupi alikuwa ni mtu mwenye majibu ya maswali magumu ya wananchi papo kwa papo hakupenda michakato, kwamba hili nalibeba talifanyia kazi yeye alimaliza palepale hichi ni kitu wananchi wengi walihisi huyu ni mtu wao.

Machinga waliachwa wafanye biashara popote bila bugudha, wachimbaji wadogo wadogo nao hawakufukuzwa na wewekezaji sasa hapo haya makundi kwa nini yasimpende? yanahaja gani yampepende mpka atese matajiri?

Kingine kilichofanya JPM apendwe na wengi ni kutekeleza ahadi zake kwa wakati, mfano JPM alikuta Dar ya foleni miaka nenda rudi lakini ndani ya mda mfupi aliikomesha foleni Dar.
Alikuta Dar kila mwaka anikipindupindu lakini ndani ya utawala wake kipindupindu kilibaki historia
Alikuta Dar inapanya Road akawamaliza.
Alikuta vijana wanashinda kunywa viroba na madawa ya kulevya lakini ndani ya utawala wake haya mambo yalipungua sana.

Kifupi JPM alionekana kwa wengi kama ni kiongozi wa tofauti kutokana na kufanya mambo magumu ambayo kwa miaka mingi yalionekana kuwa hayawezekani hivyo hizi sifa zilimfanya apendwe na wengi hasa wale wenye mapenzi mema na nchi.
 
Miundombinu gani?
 
Hivyo ndio unavyojidanganya?

Eti Magufuli hakuiba kura 2020!

Bora hata huo ubunge au udiwani huenda wizi wa kura ulifanywa kwa aibu, lakini kwenye Urais ilikuwa ni lazima wizi ufanyike kwa kiwango cha SGR ili Magufuli abakie madarakani.
Wewe kweli ni amnazo,kweli ulitegemea lissu amshide magufuri kwenye box la kura,watanganyika kweli tunavituko
 
Miaka mitatu baada ya kuondoka bado unatikisa Tanzania,kila mtu anakutaja kwa namna yake Ili kujipambanua mbele ya Watanzania,wengine sababu wao wezi basi wanakusingizia na wewe ulikuwa mwizi ilimradi wafanikishe wizi wao,RIP Mwamba.
 

Attachments

  • IMG-20230808-WA0128.jpg
    96.7 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…