Kuomba radhi bila kujua kosa lako ni jambo baya sana, hasa mtu anapotoa kauli ya jumla kuwa fulani yuko ndani kwa sababu hana heshima, ni heshima gani hiyo aliyoikosa inayomgharimu kukaa jela zaidi ya miezi minne? ni vyema aijue ili kama akitolewa asijekurudia kosa bila kujua.
Habari ya Kabendera kuachiwa baada ya vikao hamsini na akaridhika hata bila kujua kosa lake hilo ni uamuzi wake, unaheshimiwa; anasema anapaogopa jela, lakini kama akitokea mwenzake akaamua kukaa jela hata kama akipewa nafasi ya kuomba msamaha mpaka atakapojua kosa lake nae pia anastahili kusikilizwa.
Kwenye maisha kila mmoja wetu hupitia njia zake kufikia malengo aliyojiwekea maishani, tusilazimishane njia aliyopitia fulani na wengine wote waifuate, huo sio ustaarabu, kila mmoja wetu abakie na uhuru wake wa kuchagua muhimu asivunje sheria.