Tulionya umeme wa maji sio wa kutegemewa, Hayati Magufuli akatia kiburi, leo tuna mgao

Tulionya umeme wa maji sio wa kutegemewa, Hayati Magufuli akatia kiburi, leo tuna mgao

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Tulionya umeme wa maji sio wa uhakika kwa sababu mvua hazitabiriki siku hizi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Umeme wa uhakika ungekuwa ule wa gesi kule kusini.

Lakini watu wakatia pamba masikioni na kutekelekeza mradi wa gesi uliokuwa umegharimu mabilioni tayari.

Hayo matrilioni kwenye bwawa la Nyerere ni kama yanapotea tu sababu ni ya kutegemea mvua hizi hizi za kubahatisha.
 
Tulihoji sana huo uhuni. Kundi lilelile lililotuimbisha umeme wa gas, na kuwa umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Ndio kundi hilo hilo lililosofia umeme wa maji!

Unashangaa inakuwaje 7t+ ziwekwe kwenye umeme wa maji, wakati tungeweza kuweka chini ya 3t na tukapata umeme mwingi wa gas kuliko hizi 2115mg za kwenye maji.

Ukiuliza hili hakuna majibu bali unaambiwa ww sio mzalendo! Usishangae akija rais mwingine akishajua kwenye nishati ndio kuna 10% nzuri akasema umeme wa joto ardhi ndio mzuri, na kundi lilelile likapiga debe la kufa mtu.
 
Dunia ilishaachana na Technologia ya umeme wa maji miaka nenda rudi ila sisi Tanzania karne ya 22 bado tunarudi kule kule ambako mpini ulibaki shoka likaungua.

Haya ndiyo madhara ya kutokuwa na mikakatiya kitaifa ya muda mfupi na mrefu.

Tungepata umeme wa uhakika wa muda mfupi tena kwa bei nafuu kwa kutumia
Upepo
Jua

Muda mrefu kwa kutumia
Makaa ya mawe,
Gesi - LNG
Uranium.
 
Na sasa mmeletewa vitimbi vya Bashiru na kuupiga mwingi ili mhamishie magoli huko muachane na shida ya maji na umeme.
 
Tulionya umeme wa maji sio wa uhakika kwa sababu mvua hazitabiriki siku hizi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani...
Unajua hiyo gas inamirikiwa na nani? Unafikiri ni ya watz? Ni ya wazungu mkuu itarudi kumilikiwa na watz baada ya miaka 50. Hivyo usiitegemee sana hiyo gas tulipigwa sana tu wakati wakusaini mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa gas hiyo. Ilitumika njia ya BOT yaani Build, Operate and Transfer hivyo tulipigwa kwenye ku Operate for 50 years.

Wataalamu wetu hawaku bargan sawa sawa. Na kwa sasa tena tumeruhusu gas yetu kupelekwa Mombasa ili ikapakiwe kwenye Meli na kupelekwa Ulaya bado tena tumepigwa kwa mara nyingine afadhali ingepakiwa Mtwara ili tuambulie hata vikodi na wafanyakazi wa kupakia hapo Bandarini Mtwara hivyo hata mzunguko wa pesa ungeongezeka kwa watz wa Mtwara sasa tumewapelekea Wakenya tena!! Sijui nani katuroga!
 
Tulionya umeme wa maji sio wa uhakika kwa sababu mvua hazitabiriki siku hizi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani...
Kati ya maji na gesi, kipi renewable? Kwanini mkiambiwa, hamchanganyi na za kwenu?

Isitoshe, tunaweza kulinda vyanzo vyetu vya maji lakini tunaweza kulazimisha geology itututengenezee gesi?

Kama ni ukame, umekuwepo toka enzi za kina Baba wa Mataifa Ibrahim(Abraham), Isaka, Nuhu, Yakobo etc.
Acheni kutumia masaburi kufikiri.
 
Tangu uhuru tumechimba mabwawa zaidi ya 4 nyumba ya Mungu, Hale, Mtera, Kidatu lakini shida ya umebaki pale pale maana chanzo cha maji kwenye mabwawa haya ni mvua hivyo wakati wa kiangazi kina cha maji kinapungua shida inarudi bado Tena tunarudi kuchimba bwawa tukitegemea mvua ijaze mito ili kujaza bwawa. Maana yake kama kuna uhaba wa mvua mambo ni yale yale.
 
Gas ni ya kwetu maana iko kwetu. Kama kuna mikataba michafu tulitaka kama kweli Magufuli alikuwa anapambana na mafisadi awachukulie hatua. Sio kudeal na wezi vidagaa wakati kuna wezi wa kweli hakuthubutu kuwagusa.
Kuna mikataba ukiigusa tu lazima nchi ifirisike! Hata CDM akiingia hawezi kuibadirisha ni siasa tu.
 
Tulionya umeme wa maji sio wa uhakika kwa sababu mvua hazitabiriki siku hizi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani...
Ethiopia wamezindua lao na sasa wanauza umeme Kenya! Hivi kweli sisi tushindwe namna ya kuhakikisha bwawa halikauki?

Unajua toka JPM aingie madarakani mabwawa yaliyokuwa yanakauka kila uchao hayakuwahi kukauka? We are not stupid!
 
Tulionya umeme wa maji sio wa uhakika kwa sababu mvua hazitabiriki siku hizi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Umeme wa uhakika ungekuwa ule wa gesi kule kusini.

Lakini watu wakatia pamba masikioni na kutekelekeza mradi wa gesi uliokuwa umegharimu mabilioni tayari.

Hayo matrilioni kwenye bwawa la Nyerere ni kama yanapotea tu sababu ni ya kutegemea mvua hizi hizi za kubahatisha.

Mkuu marekani umeme wao asilimia kubwa unatokana na chanzo gani...

Ulishawahi kwenda ice land ukakuta barafu imekata wanalima bustani?!

Ebu tusaidie wananchi maana mnatuchanganya kweli kweli...

Kiangazi kipo miaka yote...ni wakati wa Magufuli tu tulikuwa hatuna mgao wa maji na umeme...unataka kusema mabadiliko ya hewa yanabalika kutokana na aina ya uongozi...
 
Haujafanya utafiti wa kutosha kuhusu ulichoandika. Umeme unapaswa kutoka kwenye sources tofauti, haiwezi kuwa gesi tu na haiwezi kuwa maji tu.

Lakini pia umeme unaozalishwa Tanzania kwa asilimia kubwa ni umeme wa gesi 65%, huo umeme ww maji ni 32% tu. Wala kwa hilo usipate shida, bado tunategemea sana gesi kuliko maji

Mwisho; umeme wa gesi sio renewable hivyo sio sustainable. Umeme wa maji ni renewable hivyo ni sustainable. Hapa ndio mnapaswa wengi muelewe hii kitu.
 
Gas ni ya kwetu maana iko kwetu. Kama kuna mikataba michafu tulitaka kama kweli Magufuli alikuwa anapambana na mafisadi awachukulie hatua. Sio kudeal na wezi vidagaa wakati kuna wezi wa kweli hakuthubutu kuwagusa.
Hili la gesi ya kwetu au si ya kwetu ni mada ambazo hujadiliwa na wasio na ufahamu.

Gesi kuwa kwetu haimaanishi ni ya kwetu, lakini pia haimaanishi haiwezi kuwa ya kwetu.

Issue nzima ni pesa. Hatukua na pesa ya kuchimba gesi, hivyo waliowekeza pesa zao ni haki yao kuivuna na kutuuzia. Yes gesi tunainunua kutoka kwa wawekezaji ili tuzalishe umeme.

Gesi huisha, kabla hatujalaumu kuwa kwa nn gesi ipo kwetu lakini sio yetu tulipaswa kujiuliza je tuna pesa za kuchimba hiyo gesi? Mradi mpya tu unahitaji trillion 90, tunazo?
 
Back
Top Bottom