Tulionya umeme wa maji sio wa kutegemewa, Hayati Magufuli akatia kiburi, leo tuna mgao

Tunataka tujue hiyo mikataba na kwanini haigusiki. Sio wahuni watambe kwa mikataba isiyo na tija na bado waachwe.
Mikataba ukiivunja lazima ufirisi nchi mkuu ni kusubiri tu mpaka hiyo miaka ikamilike na ubaya zaidi hata wataalamu wetu hawaajiriwi huko kwenye mitambo ya gas hivyo itamalizika hiyo miaka hatutakuwa na wataalamu wa kuendesha mitambo hiyo ya uchimbaji wa gas itabidi tuendelea kurenew mikataba hiyo tena mpaka gas iishe kabisa huko ardhini. Ni shida sana.
 

Ndio tunasema ukweli uwekwe hadharani tujue nani katufikisha hapa, sio kutuambia mikataba haigusiki kisha ndio iishe.
 
Sio kweli, umeme lazima uwe kutoka vyanzo mbalimbali renewable na non renewable

Gesi ni non renewable hivyo sio sustainable. Lakini hata hivyo bado tunategemea gesi kwa asilimia kubwa kuzalisha umeme hapa kwetu 65%. Hii story ya kwamba tunategemea sana maji kuzaisha umeme sio ya kweli, umeme wa maji ni 33% tu.

Tatizo kubwa ni gesi hii ya kuzalisha umeme tunainunua kutoka kwa wawekezaji, tukisema tuachane na vyanzo vingine ambavyo ni renewable basi huko mbeleni kutaakua na shida kubwa na crisis. Ingekua tumewekeza kwenye gesi kwa pesa zetu wenyewe basi unayosema yangekua sawa kabisa
 
Huyu jama inatakiwa afufuliwe kisha auliwe au tuchape maiti yake viboko 12 kila siku asubuhi.
 
Ndio tunasema ukweli uwekwe hadharani tujue nani katufikisha hapa, sio kutuambia mikataba haigusiki kisha ndio iishe.
Hapa wala hakuna wa kulaumiwa, tujadili hili bila mhemko. Twende taratibu tu

Sisi tuna gesi Ila hatuna pesa, inatubidi kwenda kutafuta wawekezaji. Hawa wawekezaji moja ya vipengele vyao ni mikataba hii kutokua wazi. Je ilipaswa tukatae na kuwalazimisha mikataba hii kuwa open??

Mfano hivi karibuni tulirudi mezani na mwekezaji kwenye gesi asilia mradi wa trillion 90. Mwekezaji ana kipengele Cha mkataba kutokua wazi. Je ilipaswa serikali iachane nae sababu mkataba hautaakua open? Hiyo trillion 90 sisi tutaipata wapi?
 
Huyu jama inatakiwa afufuliwe kisha auliwe au tuchape maiti yake viboko 12 kila siku asubuhi.
Mara kadhaa nimesema humu sasa hivi jamii forums Kuna watu wengi wameanza kuwa low

Umeme tunategemea hadi Sasa ni umeme wa gesi tena kwa 65%, hatutegemei umeme wa maji. Umeme wa maji ni kwa asilimia ndogo sana 33%.

Lakini umeme unapaswa kuzalishwa kwa vyanzo tofauti, ukisema tutegemee tu gesi kwa 100%. Basi jua tutaanguka moja kwa moja, kwa kuwa gesi hii tunainunua kutoka kwa wawekezaji. Pili gesi sio renawable energy hivyo haipo sustainable.
 
Ndio tunasema ukweli uwekwe hadharani tujue nani katufikisha hapa, sio kutuambia mikataba haigusiki kisha ndio iishe.
Kaiombe usome ipo Bungeni na Wizarani. Unaruhusiwa kuiomba na kuisoma lakini hairuhusiwi kuwekwa Public kwa sababu ya ushindani wa kibiashara duniani. Siyo TZ tu bali duniani kote.
 
Hakuna kazi ngumu Kama kumshauri Lord Lofa
 
Labda jamaa anafikiri tutaichimba hiyo gesi kwa kutumia koleo halafu tutuikusanya na ndoo; ha ha ha.
 
mshaanza propaganda wananchi wanasubiri kwa hamu BWAWA LA NYERERE likamilike la sivyo hapatatosha
 
Magufuri acha apumzike, alikuwa mtu na nusu hakuna aliempiku mpaka sasa, tuendelee na waliopo..washauri cha kufanya
 

Sometimes tuheshim mawazo ya viongozi wetu

Wao wanaona zaidi na kuelewa zaidi kuliko sisi

Do you think ges ingekuwa na faida that big kwenye umeme wetu Jpm angeacha kutumia?

Mpaka aliacha na kwenda kwenye bwawa ujue kuna mambo hayakuwa sawa
 
Sasa Kama sio yetu mbona unasema tumeruhusu kupelekwa Kenya, tungeruhusu vip Kama hatuimiliki?
 
Nchi ya Qatar ipo jangwani kwa asilimia 100% rasilimali yao ni gesi tu ambayo sio renewable, na ni moja ya nchi tajiri zaidi ulimwenguni

Usijikwamishe kwenye kigezo Cha renewable, Kama gesi ipo ya kutosha..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…