#COVID19 Tuliopitiwa na wimbi la 3 Mwenyezi Mungu akatuokoa tukutane hapa

#COVID19 Tuliopitiwa na wimbi la 3 Mwenyezi Mungu akatuokoa tukutane hapa

Niliugua kichwa kisichopona, homa na baridi. Nilipima Typhoid, malaria, UTI na nikafanya kipimo cha BS lakini majibu yakaonyesha nipo sawa (hakuna tatizo).. Then nikaongea na daktari mmoja kwa simu akaniandikia hizi dawa ambazo zilinisaidia sana
1.Azuma
2. Ped zinc
3. Vitamin C
3. Junior Asprin
 
A
Azuma hiyohiyo ya mg500 ila sio peke yake maana Virus vimeanza kuijua hivyo inakaribia kudunda
Duuh kwa hio mtumiaji mpya nae itadunda? Na je wataalamu wanajipanga kutumia dawa gani fragili, piroxam, penvil, ampicloxin, au nini hasa maana anticipation ndio muhimu kwa sasa, na azuma ina content zipi na waliwezaje kutambua na dawa mtambuka zenye muelekeo kama azuma ni zipi?
 
Kwa wale ndugu zangu wenye presha tujitahidi
1.kula korosho Ili kuongeza kiwango Cha zinc mwilini
2.Kula Kitunguu swaumu kwani Ni ant virus moja nzuri.
3.Tukae katika jua japo kwa Dk 15 tu kwa siku ili kuongeza Vitamin D ambayo Ni muhimu sana kwa afya zetu.
 
Duuh kwa hio mtumiaji mpya nae itadunda? Na je wataalamu wanajipanga kutumia dawa gani fragili, piroxam, penvil, ampicloxin, au nini hasa maana anticipation ndio muhimu kwa sasa, na azuma ina content zipi na waliwezaje kutambua na dawa mtambuka zenye muelekeo kama azuma ni zipi?
Mkuu Kikawaida hakuna dawa ya Covid ila kuna dawa za kutibu dalili za Covid, kutegemea na unavyoumwa ndio mtu anakunywa Tangawizi, Paracetamol, na michanganyo mengine.
 
Habari Wana JF wenzangu.Kama kichwa kinavyo jieleza.

Kwa wale tuliopitiwa na wimbi la 3 na Mwenyezi Mungu akatuokoa tubadilishane mapito na Aina ya tiba tulizotumia na zika tusaidia .
Binafsi nililala kitandani kwa takribani wiki 3.
Lambda kishaingia USA kwa hiyo sasa Delta na Lambda wanakinukisha, kesho sijui kitakuwa kirusi gani.....
 
Therapy Ni nini?
Mimi mwenyewe nipo kwenye dozi ya dawa pedilisolin na ceraphin
Nilipita huko kabla na baada ya tiba mkuu NA SASA NINA TUMIA THERAPY KWA AJILI YA KUSAFISHA MAPAFU MKUU NA KUJUA YAPO NJEMA TENA NINA WEZA TEMBEA 5 KM KILA SIKU MARA 2 MKUU.
 
Nliugua kwa wiki mbili, homa Kali kifua kikohozi mafua na mwili kuchoka.Nilitumia azuma pedzink asprin na hizi tiba za asili.Nikamwambia Mungu unajua wazi mimi ndo mzazi pekee wa wanangu nilobaki na bado ni wadogo.Niponye niweze kuwatunza wakue vyema.MUNGU MWEMA AFYA IMEIMARIKA NIMEREJEA KWENYE MAJUKUM YANGU.
 
Pole sana, Mungu ni mwema sana.

Mimi hapo kabla nilikua kati ya wale wabishi, kwamba hili gonjwa halipo kwanza haliwezi kunipata kijana [emoji23][emoji23]

Aisee kwa muda wa wiki moja lilinigeuza binu binu homa kali, kichwa kama kipo jikoni, koo linawasha, kifua, kikohozi, pumzi kubana etc

Kuna muda unaogopa kulala, nikawa naogopa kupitiliza aisee.

Nikawaza tu hii kitu ikimpata mzee, basi ngumu sana kutoboa.

Tuchukue tahadhari, Corona ipo.
 
Asante mkuu,tahadhari ni muhimu sana.
 
Mungu kweli katuonekania... Mimi nlianza mafua, kifua wik 2 dodi za kifua siponi,,, kuchoka kichwa kuuma, kukosa ladha wala kutohisi harufu yoyote na kuharisha wk ya 3 hiyoo... Ktk kusoma makala nkakutana na dalili za uviko 19, kujiangalia ndizoo... Nkampogia dr mmoja akaniambia ndizo wahi Azuma kwa siku 6,pedzink, vitamin c, aspen.... Ndio nikafufuka ila nomelala siku sio chini ya 30 hapo kuna wik 3 za hofu, homa kali, mateso makubwaa...

"Kweli Mungu kwetu kimbilio na Nguvu"
 
Back
Top Bottom