Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Nakumbuka nilikuwa natoka kilombero ndan ya basi kuna mtu alibeba kuku kwenye mfuko ,basi bhana yule kuku kumbe kafulukuta kwenye mfuko mle si akatoka lkn mfuko umemnasa mguu balaa likaanza ,kuku kaleta purukushan akarukia mbele kwa dereva anarukaruka na mfuko wake mguuni mara kwenye dashbodi mara kaingia miguuni dereva kataharuki barabara yote yake nyuma huku tukaanza unatuua wewe akaritia machakan pemben ya barabara anafoka mtoeni kuku wenu kum.........e tutakufa kisa kuku ,tukamtupa kuku nje alafu tukammaindi mwenyewe kinoma alikuwa mama mtu mzima daaah alinywea kinoma bac mpaka tunafika dar ikawa ndio stor bac zima
 
Hahhqhahqhq inàonekana mwenye kuku alikasirika sanaaa.
Ndo shida ya kusàfiri na makukuuuuu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu umenivunja mbavu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nimelala kitandani ninaumwa lakini nimecheka mpaka machozi [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
[emoji12] [emoji12] [emoji13] [emoji13] kuku angewatoa nishai
Mimi nilibeba fenesi kwenye basi watu walivimba matumbo ndani ya dakika chache ..kilichotokea dereva alisimamisha basi na kulitupa nje fasta ..nilinyamaza kama sio langu

 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
hhh waoga wa kuku kumbe[emoji23] [emoji23]
 
[emoji12] [emoji12] [emoji13] [emoji13] kuku angewatoa nishai
Mimi nilibeba fenesi kwenye basi watu walivimba matumbo ndani ya dakika chache ..kilichotokea dereva alisimamisha basi na kulitupa nje fasta ..nilinyamaza kama sio langu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119] [emoji119] [emoji119] [emoji119]
 
Sitasahau nilivyotapika kwenye Bombadier. Usiku wa kabla ya safari nilienda mitaa fulani pale Kigoma nikala kuku wa kuchoma wa kienyeji kama nusu hivi. Sasa wakati nasafiri nilikuwa naumwa Malaria kali. Basi nikawa najisikia vibaya sana kama kutapika. Tuko angani juu ya Tabora nikabanwa. Ikabidi nikimbilie chooni kutapika kwenye sinki. Nimetapika ile mbaya yule air hostes akaniambia nitapikie kwenye sinki la choo. Ile kutapika matapishi yakatoka kama bomba mvua. Choo chote cha kwenye Bombadier kikawa kimechafuka sana. Ikabidi baada ya kumaliza nianze kupiga deki choo cha kwenye Bombadier. Nikaosha kuanzia sinki la kunawia mpaka sinki la choo na ile sakafu maana niliona aibu kuwaachia wale wahudumu wafanye ile kazi.
Kwa kweli, I had a very terrible flight.
 
Jamani mbona mna vituko hivii
 
Hao kuku wawe wanawekwa kwenye bodi
 
[emoji12] [emoji12] [emoji13] [emoji13] kuku angewatoa nishai
Mimi nilibeba fenesi kwenye basi watu walivimba matumbo ndani ya dakika chache ..kilichotokea dereva alisimamisha basi na kulitupa nje fasta ..nilinyamaza kama sio langu
Kivipi walivimba?
 
Mwaka Jana mwezi wa 10 nilikua nasafiri kutoka Manyoni kuelekea Bunda.

Kama kawaida nilipanda Bunda bus, kutokana na hali ilivyo barabarani kwa sasa askari wengi jamaa alikua anatembea mwendo wa kawaida tu.
Nyegezi tukaingia mida ya saa kumi na moja jioni lakini gari ilizimika ghafla kumbe iliishiwa mafuta.
Wahusika wakafanya jitihada wakajaza mafuta ishu ikawa uwakaji wa gari maana ilikua imevuta upepo.
Baada kama ya nusu saa mambo yakakubali tuenda ofisini kwao then tukaanza safari ya kuelekea Buzuruga ili ashushe abiria wengine na apakie wengine tuendelee na safari yetu.
Kufika Buzuruga bus ikaharibika this time iliua compressor ya upepo.
Mafundi wakaanza kuhangaika, abiria wakapaniki wakaenda kumuita traffic, afande akapiga mikwara kibao pale wahusika wakaomba msamaha na ishu ikaisha.
Baada kama ya saa limoja gari ikapona tukaanza safari ya kuelekea Bunda.

Kiukweli Dereva alikua anatembea mwendo wa kawaida tu, kama 70km/h ila kutokana na ile barabara kua na mawimbi mawimbi bus ikawa kama inakimbia sana.
Abiria wakapaniki wengine walisikika wakisema Dereva tuna familia zinatutegemea Punguza mwendo.
Dereva akasema mwendo ninao tembea ni wa kawaida mbona abiria wakatulia baada kama ya dakika kumi hivi akasimama mama mmoja akamfuata dereva na kumwambia apunguze mwendo.
Basi kwenye gari ukaibuka ubishi wapo walio kua wana msapoti suka wakisema dereva aachwe atimize wajibu wake wapo walio kua wameanza kutoa vitambulisho vyao huku wakitoa kauli kama " unajua mimi ni nani ".
Dereva akaona isiwe tabu akapunguza spidi mpaka kama 10km/h.
Yani tulikua tunapitwa hadi na baiskeli.
Watu kumwambia dereva aongeze spidi wanashindwa wakaanza kulalamika tunachelewa bhana... Dereva alivyo na kiburi akasema haongezi mwendo kama huko Bunda tutafika kesho yeye hajali.
Baada ya kuona hii hali Ikabidi nishuke kituo kinaitwa masanza kona nipumzike.
Sasa sijui waliishia wapi lakini hali ilikua tete ndani ya basi.
 
duuuu!!!! Unabalaa wewe
 
[emoji12] [emoji12] [emoji13] [emoji13] kuku angewatoa nishai
Mimi nilibeba fenesi kwenye basi watu walivimba matumbo ndani ya dakika chache ..kilichotokea dereva alisimamisha basi na kulitupa nje fasta ..nilinyamaza kama sio langu
hahahahahahahaha mzee uliacha mzigo wako ukatupwa Hahahahaha kama nakuona vile ulivo jikausha kwa bus Hahahahaha Daaah nimecheka sana
 
Ndomana kabla sijasafiri lazima nimeze flagyly a subuhi silikitu ikifka mida ni mwendo wa bites bites tuu clips au biskut na juic had nafika [emoji4] [emoji4] [emoji4] sjawah haribu safarini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…