Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Mwaka 2010 wakati nakwenda Arusha toka Dar. Nilikuja Dar vizuri tu toka Dom kujiandaa na safari yangu ya Arusha, siku tunatoka Dar kuna Mama alikuwa na watoto wawili wadogo waroho sana maana kila wakati wanataka kula. Huyu Mama alikaa siti moja na mimi huku akimpakata mtoto wake mkubwa, mdogo alimbeba. Kwa kumuonea huruma yule Mama nikamwambia nimpakate mwanaye mkubwa ili kumpa nafasi ya kupumua yule Mama. Kwa mshangao wangu, yule dogo alikuja kunitapikia toka kifuani mpaka kwenye siti nzima....yaani nilionekana kama nimejinyea maana nilikalia yale matapishi. Kwa haibu yule Mama alinipa kanga nifiche ile taswira ya kulowa makalio na akajaribu kunifuta lakini wapi, nilikuwa nanuka kama mtu anayelala jalalani.
 
Nakumbuka nilisafiri na abiria mmoja alafu inaonyesha ndio mara yake kuja Dar, alikuwa na kisimu chake cha tochi alafu kajiunga na bando la dakika nyingi. Yaani mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari alikuwa anapiga kilugha na kuongea na watu wa ukoo wake wote! Wengine anarudia rudia kwa vicheko. Inaonekana kuwa alikiwa akiwataarifu na kuwakoga kuwa anaenda mjini.


nahisi huyo mtu kama si Muhaya basi ni Muha wa Kigoma.
 
Mwaka 2010 wakati nakwenda Arusha toka Dar. Nilikuja Dar vizuri tu toka Dom kujiandaa na safari yangu ya Arusha, siku tunatoka Dar kuna Mama alikuwa na watoto wawili wadogo waroho sana maana kila wakati wanataka kula. Huyu Mama alikaa siti moja na mimi huku akimpakata mtoto wake mkubwa, mdogo alimbeba. Kwa kumuonea huruma yule Mama nikamwambia nimpakate mwanaye mkubwa ili kumpa nafasi ya kupumua yule Mama. Kwa mshangao wangu, yule dogo alikuja kunitapikia toka kifuani mpaka kwenye siti nzima....yaani nilionekana kama nimejinyea maana nilikalia yale matapishi. Kwa haibu yule Mama alinipa kanga nifiche ile taswira ya kulowa makalio na akajaribu kunifuta lakini wapi, nilikuwa nanuka kama mtu anayelala jalalani.
Alikukomeshaa ahahha,sipendi kukaa siti za hivyo na watu wenye watoto maana atakuomba tu umsaidie au utapatwa na huruma
 
Daaaah vituko vingi sana...
-Kuna siku tuko moro tumelala zetu kwenye gari lidogo limoja likaharisha kwenye Dust bin hafu likubwa kama 14 yrs, mle ndani tulikua ni mwendo wa kutema mate kama tumenasa mimba.

-Nilishuka stendi nikakuta begi langu limebadirishwa mtu kachukua kaacha lake lenye vikama vya mtoto tu nililia sana hafu nilikua naenda kufanya field somewhere begi ndo lilikua linavyeti.hiyo ilikua Nyehunge bus
Mm nikisafiri vyeti vyangu navipakatia, siwez kubwaga begi langu lenye vyet kweny bus hovyo
 
Mwaka2005 unanifanya niwe na kumbukumbu sna katk suala zima la safari, tokea kipindi hicho hata nisafiri kutwa nzima siwez kula kitu zaidi ya biscuit na soda tuuu.
Kilichonitokea mwaka huo nakijua na nitaendelea kikumbuka sna
 
Juzi kati hapa mwezi wa tatu nilikua na safari kutoka Dar kwenda Arusha, basi jana yake nilikuwa kariakoo nikanunua tende kufika home nikatengeneza juice ya tende na mtindi nikanywa ikabaki alafu asubuhi safari.

Nikaona nisiiache niibebe nitakunywa njiani maana ghetto kutakuwa hamna mtu na nakaa siku nyingi itaharibika nikiiacha. Basi nikaiweka kwenye chupa ya maji nikaiweka kwenye begi kimfuko chapembeni chakuwekea chupa. Safari imekolea nikasinzia nimejisahau kumbe kitu kinajichochea pressure na ile mitikisiko ndio noma zaidi.

Nimeshtuliwa na kelele na sauti ya mlipuko mkubwa nikajua twafaaa tyre limepasuka, abiria wote kelele wengine wanasali sala za mwisho ikabidi basi lisimamishwe kuja kuangalia kumbe ile chupa yenye juice mixa mtindi ili burst na kutoa mlio wa ajabu. Watu wakaanza kuuliza begi la nani nikanyamaza nikajidai nimesinzia ikabidi safari iendelee, baadhi ya abiria na mabegi ya wengine kwenye carrier yamechafuka.

Uzuri nilikua nashuka mwisho wa safari na tumefika usiku nikawa mtu wa mwisho kushuka nikapanda toyo hadi maskani
 
Mwaka juzi nilikuwa natoka zangu dar naenda moro, na pale moro nikapanda bus la kwenda maeneo ya matombo_mvuha, sasa kuna mama mmoja hivi alikuwa anakula vitu mchanganyiko vitu venyew ni mahind mchemsho, karanga mchemsho, ndiz mbivu,mwisho kamalizia keki flan hiv za mia mia na juice yakusaga. Kwakwel yule mama nikamtafakar sijapata jibu kuhusu ule mseto (mchangnyiko) aliopiga.
Safari ikaaza ya kwenda matombo_mvuha, kama mwendo wa lisaa hivi, aiseeee yule mama alikuwa anajamba gari zima linanuka, licha ya upepo mkali lakini wapi gari zima linanuka, sasa abiria wengi walikuwa wanapiga kelele mpka kuna mmoja kasema yupo tayari kumrudishia nauli huyo mtu kma atajitokeza maaan angalau watu wapate auheni ya safari
 
Mimi nilichokuwa nafanya siku moja kabla ya safari ilikuwa naingia zangu shoprite pale kamata najaza apples, zabibu na matunda mengine kadri navyoweza, nanunua na kisu kabisaaaa kosha vizuri. Kwenye basi ni mwendo wa matunda tu mpaka kufika, wengi niliowahi kukaa nao siti moja waliipenda sana hio style
Sio ile ya lete wali maharage, mayai ya kuchemsha na muhindi wa kuchoma. Plus Pespi. Ukitoka hapo, unakuwa unatembea na bomu la ushuzi wa maangamizi
 
the same story imewahi kutokea waalii 12 walienda kisiwani kutalii, walivyorudi mmoja wao alinunua mtoto wa mamba kwa ajili ya kufuga, akamvesha kwenye kamfuko, airport hawaruhusu kupita na live animal, mtalii kahonga security wa airport kapita. Kamamba kakaanza kuhangaika kujaribu kutoka kwenye kamfuko.... Kakafanikiwa, jamaa kapiga usingizi abiria kuangalia miguuni mamba mamba weee, kuhangaika kule na huku, ndege ika loose centre of gravity, abiria wote 12 pamoja na rubani kwisha.
Hiyo story nani amekusimulia wakati wote walikuwemo kwenye ndege wote walikufa au Black box ilikuambia kuwa mwenye kamamba kake alipitiwa na usingizi?
 
Yani kweli abiria wote mnamwagiwa mkojo mnakubali??angeshuka njiani huyo
yaani nimewashangaa kwa huo uvumilivu, yaani angeshukia njiani akiwa taabani zaidi kwa kipigo.
 
Hiyo story nani amekusimulia wakati wote walikuwemo kwenye ndege wote walikufa au Black box ilikuambia kuwa mwenye kamamba kake alipitiwa na usingizi?

Mkuu labda nikupe stori ingine tajiri mmmoja aliekuwa ana dil na biashara za nyumba na ardhi alipigiwa simu aende ku sign contract ya multi millions project ya kujenga headquarter za kampuni flani kubwa. Akaamua ili kuwahi safari option ni kukodi chopper kama wanavyofanya wanasiasa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ili kuwahi, haukuwa mji wa mbali sana. Akaelekea airport yeye na ujumbe wake wa watu 2, baada ya kumaliza taratibu zote safari ikaanza. Ndani ya saa moja na nusu wakiwa angani chopper ikapata hitilafu, taarifa zilizopatikana baadae abiria wote waliokuwemo mule wamefariki. Nini kilisababisha ajali ile wakati kampuni husika ni kampuni kubwa na yenye credentials zote? Pilot wa chopper ile pia ni mzoefu wa more than 22 yrs? Baada ya uchunguzi wa miaka miwili uliosimamiwa na wanafamilia wa tajiri yule, waligundua chanzo ni simu ya mkononi aka cellphone. Ni story ndefu lakini chunguzi hizi za ajali za ndege kaka sio kama simple brain yako inavyokutuma Kwamba kwa vile watu wote wamekufa ndio haitajuilikana chanzo, kwamba kutakuwa hakuna watu wa kusimulia. Moja kati ya kazi za Black box ni kurekodi sauti za watu wakati wa tukio pamoja na rubani wa chombo husika.
 
Alikukomeshaa ahahha,sipendi kukaa siti za hivyo na watu wenye watoto maana atakuomba tu umsaidie au utapatwa na huruma


Very true ila kuanzia siku hii sitaki tena kukaa na kina Mama wenyewe watoto. In short, huruma wangu ndio uliniponza.
 
Back
Top Bottom