mbongo_halisi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 7,074
- 5,486
Mwaka 2010 wakati nakwenda Arusha toka Dar. Nilikuja Dar vizuri tu toka Dom kujiandaa na safari yangu ya Arusha, siku tunatoka Dar kuna Mama alikuwa na watoto wawili wadogo waroho sana maana kila wakati wanataka kula. Huyu Mama alikaa siti moja na mimi huku akimpakata mtoto wake mkubwa, mdogo alimbeba. Kwa kumuonea huruma yule Mama nikamwambia nimpakate mwanaye mkubwa ili kumpa nafasi ya kupumua yule Mama. Kwa mshangao wangu, yule dogo alikuja kunitapikia toka kifuani mpaka kwenye siti nzima....yaani nilionekana kama nimejinyea maana nilikalia yale matapishi. Kwa haibu yule Mama alinipa kanga nifiche ile taswira ya kulowa makalio na akajaribu kunifuta lakini wapi, nilikuwa nanuka kama mtu anayelala jalalani.