Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Mwaka Jana mwezi wa 10 nilikua nasafiri kutoka Manyoni kuelekea Bunda.

Kama kawaida nilipanda Bunda bus, kutokana na hali ilivyo barabarani kwa sasa askari wengi jamaa alikua anatembea mwendo wa kawaida tu.
Nyegezi tukaingia mida ya saa kumi na moja jioni lakini gari ilizimika ghafla kumbe iliishiwa mafuta.
Wahusika wakafanya jitihada wakajaza mafuta ishu ikawa uwakaji wa gari maana ilikua imevuta upepo.
Baada kama ya nusu saa mambo yakakubali tuenda ofisini kwao then tukaanza safari ya kuelekea Buzuruga ili ashushe abiria wengine na apakie wengine tuendelee na safari yetu.
Kufika Buzuruga bus ikaharibika this time iliua compressor ya upepo.
Mafundi wakaanza kuhangaika, abiria wakapaniki wakaenda kumuita traffic, afande akapiga mikwara kibao pale wahusika wakaomba msamaha na ishu ikaisha.
Baada kama ya saa limoja gari ikapona tukaanza safari ya kuelekea Bunda.

Kiukweli Dereva alikua anatembea mwendo wa kawaida tu, kama 70km/h ila kutokana na ile barabara kua na mawimbi mawimbi bus ikawa kama inakimbia sana.
Abiria wakapaniki wengine walisikika wakisema Dereva tuna familia zinatutegemea Punguza mwendo.
Dereva akasema mwendo ninao tembea ni wa kawaida mbona abiria wakatulia baada kama ya dakika kumi hivi akasimama mama mmoja akamfuata dereva na kumwambia apunguze mwendo.
Basi kwenye gari ukaibuka ubishi wapo walio kua wana msapoti suka wakisema dereva aachwe atimize wajibu wake wapo walio kua wameanza kutoa vitambulisho vyao huku wakitoa kauli kama " unajua mimi ni nani ".
Dereva akaona isiwe tabu akapunguza spidi mpaka kama 10km/h.
Yani tulikua tunapitwa hadi na baiskeli.
Watu kumwambia dereva aongeze spidi wanashindwa wakaanza kulalamika tunachelewa bhana... Dereva alivyo na kiburi akasema haongezi mwendo kama huko Bunda tutafika kesho yeye hajali.
Baada ya kuona hii hali Ikabidi nishuke kituo kinaitwa masanza kona nipumzike.
Sasa sijui waliishia wapi lakini hali ilikua tete ndani ya basi.

Hii iliwahi kunipata zamani nikienda shule from Arusha to Dar.Nilikua ndani ya Ngorika.Kuna abiria akapiga simu kuwa basi linakimbia sana.Kufika mahali tukasimamishwa na polisi na hapo ndipo polisi walipomwambia dereva kuna abiria yako ametoa taarifa kuwa unakimbiza gari na akapewa onyo.Sasa tulipoondoka hapo dereva akasema hajui aliyepiga simu ni nani ila akasisitiza alikua hakimbii na akajikita ktk kigezo kuwa tulikua tumeongozana na mabasi mengine kwa mda mrefu tuu(ambao ulikua ni ukweli).Baada ya hapo alienda 50km/hr hadi Dar(kuanzia mitaa ya Tanga).Watu walimind hadi tukamjua na aliyepiga simu.

Kila basi lililotukuta lilidhani basi letu ni bovu na kutaka kutoa msaada....
 
Hahahaha

Daaaah vituko vingi sana...
-Kuna siku tuko moro tumelala zetu kwenye gari lidogo limoja likaharisha kwenye Dust bin hafu likubwa kama 14 yrs, mle ndani tulikua ni mwendo wa kutema mate kama tumenasa mimba.

-Nilishuka stendi nikakuta begi langu limebadirishwa mtu kachukua kaacha lake lenye vikama vya mtoto tu nililia sana hafu nilikua naenda kufanya field somewhere begi ndo lilikua linavyeti.hiyo ilikua Nyehunge bus
Mkuu vyeti ulipata?
 
Nilitoka Tanga kipindi cha mfungo wa ramadhan. Ndani ya Tahmeed ya kutoka Mombasa. Sasa rafiki yangu niliketi karibu na ustaadh mmoja alikuwa kwenye mfungo ananuka mdomo balaa. Nilifika Dar nikiwa hoi na harufu ya mdomo wa mshikaji
 
Nakumbuka nilikuwa natoka kilombero ndan ya basi kuna mtu alibeba kuku kwenye mfuko ,basi bhana yule kuku kumbe kafulukuta kwenye mfuko mle si akatoka lkn mfuko umemnasa mguu balaa likaanza ,kuku kaleta purukushan akarukia mbele kwa dereva anarukaruka na mfuko wake mguuni mara kwenye dashbodi mara kaingia miguuni dereva kataharuki barabara yote yake nyuma huku tukaanza unatuua wewe akaritia machakan pemben ya barabara anafoka mtoeni kuku wenu kum.........e tutakufa kisa kuku ,tukamtupa kuku nje alafu tukammaindi mwenyewe kinoma alikuwa mama mtu mzima daaah alinywea kinoma bac mpaka tunafika dar ikawa ndio stor bac zima
Hahahahahahahahahahaha eti tutakufa kisa kuku.
 
[emoji12] [emoji12] [emoji13] [emoji13] kuku angewatoa nishai
Mimi nilibeba fenesi kwenye basi watu walivimba matumbo ndani ya dakika chache ..kilichotokea dereva alisimamisha basi na kulitupa nje fasta ..nilinyamaza kama sio langu
Mkuu, kubeba fenesi na kuvimba matumbo kunahusiana vipi, embu tupe darasa.
 
Sitasahau nilivyotapika kwenye Bombadier. Usiku wa kabla ya safari nilienda mitaa fulani pale Kigoma nikala kuku wa kuchoma wa kienyeji kama nusu hivi. Sasa wakati nasafiri nilikuwa naumwa Malaria kali. Basi nikawa najisikia vibaya sana kama kutapika. Tuko angani juu ya Tabora nikabanwa. Ikabidi nikimbilie chooni kutapika kwenye sinki. Nimetapika ile mbaya yule air hostes akaniambia nitapikie kwenye sinki la choo. Ile kutapika matapishi yakatoka kama bomba mvua. Choo chote cha kwenye Bombadier kikawa kimechafuka sana. Ikabidi baada ya kumaliza nianze kupiga deki choo cha kwenye Bombadier. Nikaosha kuanzia sinki la kunawia mpaka sinki la choo na ile sakafu maana niliona aibu kuwaachia wale wahudumu wafanye ile kazi.
Kwa kweli, I had a very terrible flight.
Pole sana Mkuu ila nna swali la kukuuliza, kuku wa kienyeji na wa kisasa yupi mzuri kwa kumchoma?
 
Hii iliwahi kunipata zamani nikienda shule from Arusha to Dar.Nilikua ndani ya Ngorika.Kuna abiria akapiga simu kuwa basi linakimbia sana.Kufika mahali tukasimamishwa na polisi na hapo ndipo polisi walipomwambia dereva kuna abiria yako ametoa taarifa kuwa unakimbiza gari na akapewa onyo.Sasa tulipoondoka hapo dereva akasema hajui aliyepiga simu ni nani ila akasisitiza alikua hakimbii na akajikita ktk kigezo kuwa tulikua tumeongozana na mabasi mengine kwa mda mrefu tuu(ambao ulikua ni ukweli).Baada ya hapo alienda 50km/hr hadi Dar(kuanzia mitaa ya Tanga).Watu walimind hadi tukamjua na aliyepiga simu.

Kila basi lililotukuta lilidhani basi letu ni bovu na kutaka kutoa msaada....
hhhaaaa mlivojua mlimfanyaje
 
hhhaaaa mlivojua mlimfanyaje
Hakufanywa kitu chochote.
Abiria waligawanyika makundi mawili, wanaosema lilikua linakimbia na wengine wakipinga.So watu wakaishia kubishana tuu na kutukanana.

Binafsi nilipanda lile basi ili niwahi Dar na nilichelewa vilivyo.
 
Hahahahaha yaan kuna siku tulipanda basi ilikuwa ugomvi dereva na abiria wee huwa nafurahi sana mimi
 
Hahahahaha yaan kuna siku tulipanda basi ilikuwa ugomvi dereva na abiria wee huwa nafurahi sana mimi
Hapo kwenye ugomvi wa driver na abiria nnaogopa asije akawamwaga 😀😀.

Case yetu baada ya driver kusema msimamo hakuongea tena.Watu walimwomba aongeze mwendo lkn wapi, kama vile hawasikii hadi na waliotaka apunguze mwendo nao wakaboreka.
 
Hawa masista duu was kwenye mabasi ni wa hovyo sana.
Mwaka Jana mwezi wa sita natoka Dodoma kuja dar siti ya pembeni yangu alikuua demu flani mweupe kisu kinyama nikasema saaafi, leo Nina bahati. Sasa bwana picha linaanza ndani ya gari Luna joto lakini yeye kapigilia jacket la mvua Kubwa kinoma, hadi nikawa namuonea huruma, nikamwambia si uvue Tu hilo dude,akalivua.
Tumefika Moro kanunua mahindi ya kuchemsha akanigawia na Mimi, ile napeleka mdomoni, yakikuwa yamechacha nikaacha kula lakini yeye alikuwa anayapeleka balaa, sasa nikakawa najiuliza yeye hahisi kuwa yameharibika?
Sasa alikuja kuniua mbavu kuna jamaa alikuwa anauza mbuzi (ya kukunia Nazi) akaniuliza ile nini nikamwambia kuwa hicho ni kifaa cha kukunia Nazi, eti akanijibu mbona kimekaa kama msalaba eti anakiogopa.

Nikavaa headphones nikalala.
Wewe mwenyewe ngweshu tu,h tu,hatuna headphones tuna earphones
 
Mapungufu memgi mbona ya wadada hamna ya wanaume washamba na wenye kero kwenye mabasi?!
 
Hahahaha naomba nikupongeze kwa kutoka maeneo hayo.
Kuna watu wakarimu sana aisee.
Asante sanaaa mkuu,yeah ni watu wakarimu sanaa aiseee sio kama dar ,dar wanakwambia utapambana na hali yako kule mwanza hata ukiwa mgeni wa jiji utakuwa huru sanaa tatzo dar ukiwa mgeni lazma wakukaribishe kwa aina yakeee mpaka uisome namba..
 
Kama walikufa wote we ulijuaje kama hiyo ndio sababu au kulikua na cctv zilizobaki kwenye ndege
Black box na uchunguzi mwa miezi 18 ulionyesha kwa ushahidi usio na pingamizi kuwa mamba ndio chanzo cha ajali.
 
Back
Top Bottom