Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Tulioshuhudia vituko kwenye mabasi ya mikoani tukutane hapa!

Kuna siku mm nlikuwa naenda Dar bwana, nilikaa pekee yangu kufika Moshi akaingia mdada akakaa kwenye siti yangu, halaf mjuavyo wadada na mapozi yao hakunisalimia nkasema sio inshu tumeenda weee kufika Makanya akaanza kusinzia na kusinzia kwenyewe akawa ananilalia nkavumilia, tumeenda weee c akaanza kukoroma bwana halafu bahati mbaya kumbe katoa maudelele yamenimwagia mm, nlimuwasha kofi nkamwambia unifute uliponichafua nkamwita Konda nkamwambia muhamishe huyu siti au mm nihame tutapigana njia nzima watu walicheka Konda akanitoa nkakaa kwingine, alinikera kishenzi ,haya siku nyingine nilikuwa naenda Mwanza nilikosa basi la kuanzia Arusha ikabidi nisubiri zinazotoka Moshi nkapanda Mghamba zile za zamani bwana 3/2 weeeee sitasahau mbaba alikuwa na watoto sijui watano wengine wamesimama tumebanana halaf walivyokuwa wanakula jamani khaaa kila kituo mkisimama wanasimama, kufika pale Tinde mtoto mmoja si akaanza kuendesha acha achafue hadi siti nilokaa ikabidi nisimame tu
 
Yani acha tu balaaaaa
 
Mm nina kituko changu kwenye natoka arusha kuna dar yaan sitaki kukumbuka
 
Acha kabisaa alafu nina bahat mbaya nikijambaa ushuzi unapita kwenye papuchi unasikia kama tetemeko la ardhi prprrprrpapaapaparapapraa
Hahaha hahaha,umenikumbusha mdada mmoja wa kizanzibar nilisoma nae primary ndio ilikuwa michezo yako,kipindi kile cha utoto ilikuwa kama anatukera but baada ya kukua unatamani upate atakaekuwa vitimbi kama hivyo,sababu ina raha yake
 
Habari zenu wakuu

Leo ningependa kila mtu aweke tukio lake alilowahi kuliona kwenye mabasi ya mikoani.
Nikianza na mim mwenyew,
Mwezi wa 1 nlkua natoka Dar naenda Moro ndani ya Alsaedy bus full kiyoyozi nimeulamba kila kitu na chini nna kiatu changu kipyaaaaa!
Pemben amekaa binti ambaya kwa kwel ni mrembo sana,hapa niweke wazi...kwenye safari zangu mkoa cjawahi kukaa seat moja na demu mkali...siku hii ikawa kama neema ivi imeshuka!
Baada ya kutoka Ruvu pale kwenye misosi na kuchimba dawa tukawa tumekaa tunapiga story za hapa na pale na yule demu...
Daah,sijakaa sawa naanza kuckia harufu za ajabu ajabu kama matapishi ivi..daah kweli bhana jamaa moja alikuwa amekaa siti ya mbele yangu mambo yalikuwa sio mambo matapishi yamejaa kwenye siti yake kote harufu karbia basi zima inasikika
Siku hii japo nilikuwa na furaha kukaa na mtoto mzuri sehemu moja ila nilichukia sana...maana yale matapishi yalishuka hadi chini kwenye kiti na kuanza kuingia kwenye viatu vyangu...maana akili yote ilikuwa kwa mtoto mzuri hata yalivoingia ingia hayo matapishi skuweza kujua....
Daah kucheki vizuri jamaa alikuwa anapiga chips yai zile za take away na ndo zilizosababisha zahama yote hii...Siwezi sahau hii siku maana viatu vyangu na miguu yote ilkuwa matapishi 2..sema nlitembea na body spray kwenye begi....jamaa akanipa tambaa nikajifutia na spray yangu ndo ikawa mtetezi nilipofika msamvu sina harufu tena...hahahah

Wakuu tupieni vimbwanga mlivyoona kwenye mabasi huko ya mikoani.
kwahiyo umekaa tu na mtt mzuri hujafanya lolote?
haina maana kuingizia kati ulikuwa na mtt mkali kumbe ulikuwa bubu.
 
kwahiyo umekaa tu na mtt mzuri hujafanya lolote?
haina maana kuingizia kati ulikuwa na mtt mkali kumbe ulikuwa bubu.
Mkuu ningeandika vitu vingi hapo nimefanya kaufupisho tu kwa sababu lengo kuu lilikuwa ni kuelezea jinsi jamaa alivonitapikia miguuni tu..ningeanza kusema na demu nkachukua namba na tulvofika moro tukakutana sehem fulani baada ya siku kadhaa....mastory yangekuwa marefu mno mkuu
 
endelea basi kutusimulia vingine vituko
 
Hawa masista duu was kwenye mabasi ni wa hovyo sana.
Mwaka Jana mwezi wa sita natoka Dodoma kuja dar siti ya pembeni yangu alikuua demu flani mweupe kisu kinyama nikasema saaafi, leo Nina bahati. Sasa bwana picha linaanza ndani ya gari Luna joto lakini yeye kapigilia jacket la mvua Kubwa kinoma, hadi nikawa namuonea huruma, nikamwambia si uvue Tu hilo dude,akalivua.
Tumefika Moro kanunua mahindi ya kuchemsha akanigawia na Mimi, ile napeleka mdomoni, yakikuwa yamechacha nikaacha kula lakini yeye alikuwa anayapeleka balaa, sasa nikakawa najiuliza yeye hahisi kuwa yameharibika?
Sasa alikuja kuniua mbavu kuna jamaa alikuwa anauza mbuzi (ya kukunia Nazi) akaniuliza ile nini nikamwambia kuwa hicho ni kifaa cha kukunia Nazi, eti akanijibu mbona kimekaa kama msalaba eti anakiogopa.

Nikavaa headphones nikalala.
 
Nakumbuka nilisafiri na abiria mmoja alafu inaonyesha ndio mara yake kuja Dar, alikuwa na kisimu chake cha tochi alafu kajiunga na bando la dakika nyingi. Yaani mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari alikuwa anapiga kilugha na kuongea na watu wa ukoo wake wote! Wengine anarudia rudia kwa vicheko. Inaonekana kuwa alikiwa akiwataarifu na kuwakoga kuwa anaenda mjini.
Huyo lazma alitokea kanda ya ziwa kama sio Iringa na Mbeya
 
Nakumbuka nilikuwa natoka Mwanza naenda Kigoma nimepanda basi la Adventure. Limejaa watu na mizigo kibao, kama kawaida ya gari za shamba. Siti zimejaa na watu kibao wamesimama pembeni yangu kaja kasimama mama mmoja hivi na mizigo yake mingine kaibeba kichwani kwake..sasa yule mama alipandia njiani na alikuwa anashukia njiani sasa hivyo mizigo yake akajitwisha ilhali kapanda gari..sasa Konda kaja kuandika tiketi achukue na nauli ikiwemo ya mizigo...weee! Mama anakwambia nailipiaje mizigo wakati nimeibeba kichwani kwangu? Ahahaha!! Mizigo niibebe Mimi na kuilipia niilipie tena? Silipi. Kwa lafudhi yao ya kiha...aisee siku hiyo nilicheka sana. Kweli mama akakomaa hadi Konda akafyta mkia akachukua nauli yake tu ya mizigo maza kamkazia.

Waha kwa ubishi na ubahili wanatisha sana.
 
Nakumbuka nilikuwa natoka arusha - dar nilishuhudia mrembo sista duu kwelikweli mweupeee..akiaribu ndani ya basi
maskini ya mungu sijui alikuwa amepata tumbo la kuhara yule bahati nzuri aliharibu karbu na mombo hotel, ikabidi basi liingie hotel pale, ndo akaenda kujiswafi pia kuna mwanadada alijitolea kumuazima skirt nyingine.
Jeans aliyokuwa amevaa sijui aliitupia wapi maana alivyorudi kwenye bus hakuibeba. Akajiinamia kwenye kiti mpaka tunafika kimara,. Yani hadi huruma

Dah ilikuwa ni aibu kwelikweli
Arusha to kimara bas gani hilo mkuu
 
Nakumbuka nilikuwa natoka kilombero ndan ya basi kuna mtu alibeba kuku kwenye mfuko ,basi bhana yule kuku kumbe kafulukuta kwenye mfuko mle si akatoka lkn mfuko umemnasa mguu balaa likaanza ,kuku kaleta purukushan akarukia mbele kwa dereva anarukaruka na mfuko wake mguuni mara kwenye dashbodi mara kaingia miguuni dereva kataharuki barabara yote yake nyuma huku tukaanza unatuua wewe akaritia machakan pemben ya barabara anafoka mtoeni kuku wenu kum.........e tutakufa kisa kuku ,tukamtupa kuku nje alafu tukammaindi mwenyewe kinoma alikuwa mama mtu mzima daaah alinywea kinoma bac mpaka tunafika dar ikawa ndio stor bac zima
Basi zima kulikua hakuna mwenye kisu duh
 
the same story imewahi kutokea waalii 12 walienda kisiwani kutalii, walivyorudi mmoja wao alinunua mtoto wa mamba kwa ajili ya kufuga, akamvesha kwenye kamfuko, airport hawaruhusu kupita na live animal, mtalii kahonga security wa airport kapita. Kamamba kakaanza kuhangaika kujaribu kutoka kwenye kamfuko.... Kakafanikiwa, jamaa kapiga usingizi abiria kuangalia miguuni mamba mamba weee, kuhangaika kule na huku, ndege ika loose centre of gravity, abiria wote 12 pamoja na rubani kwisha.
Kama walikufa wote we ulijuaje kama hiyo ndio sababu au kulikua na cctv zilizobaki kwenye ndege
 
Nakumbuka nilikuwa natoka Mwanza naenda Kigoma nimepanda basi la Adventure. Limejaa watu na mizigo kibao, kama kawaida ya gari za shamba. Siti zimejaa na watu kibao wamesimama pembeni yangu kaja kasimama mama mmoja hivi na mizigo yake mingine kaibeba kichwani kwake..sasa yule mama alipandia njiani na alikuwa anashukia njiani sasa hivyo mizigo yake akajitwisha ilhali kapanda gari..sasa Konda kaja kuandika tiketi achukue na nauli ikiwemo ya mizigo...weee! Mama anakwambia nailipiaje mizigo wakati nimeibeba kichwani kwangu? Ahahaha!! Mizigo niibebe Mimi na kuilipia niilipie tena? Silipi. Kwa lafudhi yao ya kiha...aisee siku hiyo nilicheka sana. Kweli mama akakomaa hadi Konda akafyta mkia akachukua nauli yake tu ya mizigo maza kamkazia.

Waha kwa ubishi na ubahili wanatisha sana.
Mkuu noma saba
 
Back
Top Bottom