Bradha
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 8,787
- 45,257
Mwaka Jana mwezi wa 10 nilikua nasafiri kutoka Manyoni kuelekea Bunda.
Kama kawaida nilipanda Bunda bus, kutokana na hali ilivyo barabarani kwa sasa askari wengi jamaa alikua anatembea mwendo wa kawaida tu.
Nyegezi tukaingia mida ya saa kumi na moja jioni lakini gari ilizimika ghafla kumbe iliishiwa mafuta.
Wahusika wakafanya jitihada wakajaza mafuta ishu ikawa uwakaji wa gari maana ilikua imevuta upepo.
Baada kama ya nusu saa mambo yakakubali tuenda ofisini kwao then tukaanza safari ya kuelekea Buzuruga ili ashushe abiria wengine na apakie wengine tuendelee na safari yetu.
Kufika Buzuruga bus ikaharibika this time iliua compressor ya upepo.
Mafundi wakaanza kuhangaika, abiria wakapaniki wakaenda kumuita traffic, afande akapiga mikwara kibao pale wahusika wakaomba msamaha na ishu ikaisha.
Baada kama ya saa limoja gari ikapona tukaanza safari ya kuelekea Bunda.
Kiukweli Dereva alikua anatembea mwendo wa kawaida tu, kama 70km/h ila kutokana na ile barabara kua na mawimbi mawimbi bus ikawa kama inakimbia sana.
Abiria wakapaniki wengine walisikika wakisema Dereva tuna familia zinatutegemea Punguza mwendo.
Dereva akasema mwendo ninao tembea ni wa kawaida mbona abiria wakatulia baada kama ya dakika kumi hivi akasimama mama mmoja akamfuata dereva na kumwambia apunguze mwendo.
Basi kwenye gari ukaibuka ubishi wapo walio kua wana msapoti suka wakisema dereva aachwe atimize wajibu wake wapo walio kua wameanza kutoa vitambulisho vyao huku wakitoa kauli kama " unajua mimi ni nani ".
Dereva akaona isiwe tabu akapunguza spidi mpaka kama 10km/h.
Yani tulikua tunapitwa hadi na baiskeli.
Watu kumwambia dereva aongeze spidi wanashindwa wakaanza kulalamika tunachelewa bhana... Dereva alivyo na kiburi akasema haongezi mwendo kama huko Bunda tutafika kesho yeye hajali.
Baada ya kuona hii hali Ikabidi nishuke kituo kinaitwa masanza kona nipumzike.
Sasa sijui waliishia wapi lakini hali ilikua tete ndani ya basi.
Hii iliwahi kunipata zamani nikienda shule from Arusha to Dar.Nilikua ndani ya Ngorika.Kuna abiria akapiga simu kuwa basi linakimbia sana.Kufika mahali tukasimamishwa na polisi na hapo ndipo polisi walipomwambia dereva kuna abiria yako ametoa taarifa kuwa unakimbiza gari na akapewa onyo.Sasa tulipoondoka hapo dereva akasema hajui aliyepiga simu ni nani ila akasisitiza alikua hakimbii na akajikita ktk kigezo kuwa tulikua tumeongozana na mabasi mengine kwa mda mrefu tuu(ambao ulikua ni ukweli).Baada ya hapo alienda 50km/hr hadi Dar(kuanzia mitaa ya Tanga).Watu walimind hadi tukamjua na aliyepiga simu.
Kila basi lililotukuta lilidhani basi letu ni bovu na kutaka kutoa msaada....